Ndugu zangu wanabidii,
Habari zenu? Natumaini mpo salama.
Naomba nitoe tahadhari juu ya kundi la matapeli wanaojipatia pesa kwa watu kwa ahadi za kuwapatia ajira kwenye taasisi zinazolipa vizuri. Rafiki yangu mmoja anaefanyakazi katika wizara moja amekuwa mmoja wa watu walioingia kwenye mikono ya matapeli hao. Dada huyo amekuwa akidanganywa kuwa atapatiwa ajira Vodacom, Tigo na sasa NSSF lakini kwa masharti kuwa atoe kwanza pesa ili hao wanaomsaidia 'wawaweke sawa wahusika' ili apatiwe position yenye pesa nzuri. Mwezi uliopita ndugu wa dada huyo walimkamata mmoja wa matapeli hao na kumpeleka polisi, lakini siku hiyohiyo huyo kaka alitoka na mpaka sasa anaendelea kumsumbua kuwa atamsaidia apate ajira.
Wiki chache zilizopita walimpigia simu na kumwambia apeleke salary slip yake ili akasign contract Vodacom. Aliponieleza niliogopa na kumkataza asipeleke kwani yawezekana matapeli hao wakaitumia kughushi other documentation wakaichukulia mkopo kwa jina lake. Hakuamini ushauri wangu. Kwa hili nina wasiwasi sana kwani nina rafiki kwenye moja ya taasisi zinazota mikopo aliwahi kunieleza kuwa she comes across utapeli wa aina hiyo regularly.
The worst part ni kwamba inaonekana kuwa kundi hili linishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu katika taasisi wanakofanyia kazi kwani wakati anapoitwa kwenye hizo interview Vodacom na Tigo huwa anakutanishwa na mtu ambaye anatambulishwa kuwa ni Director or Manager.
Ndugu zangu naomba mnisaidie kuwakomesha watu hawa kwani mbali na hasara anayopata rafiki yangu, I'm very concerned kwamba they might even harm her or do anything nasty to her manake wanamuita sehemu tofautitofauti awapelekee hela.
Nimefanikiwa kucopy namba anazowasiliana nazo:
0719077825
0652493425
0752027410
0752124250
0718353120
0767864471
Kwa wale wanaofanya kazi Vodacom, Tigo na NSSF humu kwenye forum, naomba mtambue kuwa kuna kundi la matapeli wanatumia majina ya taasisi hizi kufanya utapeli na mchukue hatua stahili.
Lissa Lauren
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
DELL LATITUDE D 620 & D30
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment