Wednesday, 28 November 2012

[wanabidii] Tukubaliane Kutokubaliana - Tupige Kura

Ndugu Lwegasira, naona umegoma kunielewa. Umegoma kumuelewa mwalimu wa Kiingereza na mtaalamu wa lugha, Mabala. Pia umegoma kumuelewa mwalimu wa Kiingereza na ufundishaji wa lugha za kigeni, Dakta Qorro. Hatujatumia lugha ngumu isiyoeleweka kulieleza hili suala ndio maana nachelea kusema hujaelewa - nasema umegoma kuelewa. Sote - sisi na ninyi - tuna nia njema: Kuhakikisha Mtanzania wa kawaida anajua Kiswahili na Kiingereza pia ikiwezekana na Kichina, Kifaransa n.k. Nasisitiza kuwa wote tuna nia moja labda kama kweli mpo ambao mna nia mbaya ya kuwafanya walio wengi wasijue hizo lugha zingine. Tofauti yetu kuu, na hilo Mabala na Qorro wamelisisitiza sana, ni mbinu ya kufundisha Kiingereza kwa walio wengi ili wakijue vizuri. Sisi tunasema mbinu bora ni kukifundisha kama kinavyofundishwa huko Ujerumani, Uchina, Uswidi n.k. - kama lugha ngeni. Ninyi mnasema mbinu bora ni kukitumia kama lugha ya kufundishia masomo.

Ushahidi mlio nao ni hizi shule binafsi zilizoibuka ambazo zinatumia Kiingereza kufundishia masomo. Dakta Rukoma anatoa mfano wa mtoto wake aliyejiunga na shule hizo katikati na sasa anajua Kiingereza vizuri na yule aliyeanza mwanzo ndio anakijua vilivyo. LKK ana ushahidi wa kufundishwa enzi hizo kulipokuwa na walimu wazuri wa Kiingereza wa kuwatosha wanafunzi wachache waliokuwepo. Na anashuhudia kuwa watu wamemsifia kuwa anakijua Kiingereza hasa. Nyoni anasisitiza kuwa yeye aliweza kujua pia Kiingereza kwa kufundishiwa kwa lugha hiyo sekondari japo alianza shule kijijini ambako hawakufundishwa kwa Kiingereza na anasisitiza kuwa hadi tujiandae ndio tutaweza kutumia Kiswahili ila kwa sasa hatuwezi. Mtana yeye ana uchungu sana na jinsi ambavyo kutojua Kiingereza kunawanyima ajira vijana hivyo anaona ni heri kabisa kama jamii tuanze kuongea Kiingereza na kukitumia kufundishia ili tukijue - anaamini ndivyo ilivyo Kenya.

Katika kundi letu ushahidi tulio nao ni wa hali ambayo walimu wa Kiingereza wameiona kwa wanafunzi wao darasani na ambao sisi tuliofundishwa katika mfumo huo tumeiishi wenyewe na imetuathiri katika kujifunza Kiingereza, Kiswahili na kupata maarifa. Pia tuna ushahidi wa tafiti na takwimu mbalimbali zinazoonesha kwa nini kufundishia kwa Kiingereza Tanzania sio njia bora ya kujifunza lugha hiyo ya Kiingereza achilia mbali kutoa maarifa. Ishara zote za namna tunavyotumia Kiswahili nchini zinatuonyesha kuwa hii ndio lugha bora ya kufundishana na kutoa maarifa Tanzania na wala haikinzani na mbinu ya kufundisha lugha ya Kiingereza.

Tunabishana, tunalaumiana na tunahubiriana. Wapo watakaobadilisha mtazamo kutokana na nguvu za hoja za upande mwingine. Lakini makundi yataendelea kutokubaliana. Na kila moja litaona hoja zake ndio ziko sahihi na ndio zinazofaa kufikia lengo kuu - kujifunza lugha (Kiingereza, Kiswahili n.k.) na kupata maarifa. Hivyo, ni heri tukubaliane kutokubaliana kwa kupiga kura kama taifa na sote kukubali matokeo. Hiyo ndio demokrasia.
 
From: Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, November 28, 2012 5:35 AM
Subject: Re: [Mabadiliko] Tujikumbushe: Alichosema Mama Lwakatare kuhusu Kiingereza

Chachage,

Hiyo siyo maana ya LKK. Unapotosha kwa nini? Kwa nini watanzania wasijue lugha zote mbili na ikiwezekana na nyingine??? Kwa nini kiswahili tu???? Tunachokisema ni kwamba kiingereza kitumike kufundishia kuanzia chini mpaka chuo kikuu na watu wakitumie, wakizoee, wakipende kwa sababu kitawasaidia zaidi. Wewe unataka wajue kiswahili tu. Kwa nini? Waendelee kuwa maskini siyo???!!

From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, November 28, 2012 9:39 AM
Subject: Re: [Mabadiliko] Tujikumbushe: Alichosema Mama Lwakatare kuhusu Kiingereza

LKK, hata mimi ningekuwa wewe ningekubali kubaki kuwa mteule na kuwarithisha wajukuu zangu uteule - hakika wengi wameitwa (kwenye shule zinazotumia sera ndumilakuwili na katili) ila wachache wameteuliwa!
 
From: Lutgard Kokulinda Kagaruki <lutgardkokulinda@gmail.com>
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, November 28, 2012 1:30 AM
Subject: Re: [Mabadiliko] Tujikumbushe: Alichosema Mama Lwakatare kuhusu Kiingereza

Augustine,

Nakuunga mkono mia kwa mia! Nyie semeni tuuuu, miye wala SIDANGANYIKI!! Nshakubali utumwa!! LKK.

Sent from my iPad

On 28 Nov 2012, at 7:34 asubuhi, Augustine Rukoma <arukoma66@gmail.com> wrote:

Chambi mambo yanaeleweka tu, sema tuongeze idadi ya masomo. haya ya sasa yafundishwe kwa kiingereza mwanzo mwisho, alafu tunaweza kuanzisha masomo mengine ya kwetu kama ngoma za utamaduni, ufundi asili ambapo wanafunzi watafundishwa uchongaji wa vinyago, usukaji wa mikeka, kujenga nyumba imara za tope na kinyesi cha ng'ombe, kutengeneza mikokotene ya mbao n.k tukafundisha kwa kiswahili mwanzo mwisho, tukajenga hata chuo kikuu huko bagamoyo, lakini haya mengine tutumie elimu ya tuliopoyaiga

2012/11/27 Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
Bariki, inawezekana Dakta Rukoma yuko kwenye mchakato wa kusahau Kiswahili ndio maana kashindwa kumuelewa mheshimiwa (nasikia wamekataza kutumia neno hili) mama mchungaji mbunge, sitashangaa baada ya muda Rukoma akija na hoja ya kubadili hili kundi liitwe Change Tanzania baadala ya Mabadiliko Tanzania maana inawezekana kabisa dhana ya kisosholojia ya social change haiwezi kueleweka kwa lugha yetu maskini!
 
From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, November 27, 2012 8:35 AM

Subject: Re: [Mabadiliko] Tujikumbushe: Alichosema Mama Lwakatare kuhusu Kiingereza

Ha hahahha mahokaaaa!

Nashukuru Dokta, tupo pamoja

2012/11/27 Richard Mabala <rmabala@gmail.com>
Dokta R ha ha ha
Pole sana.  Hebu jitahidi kutafuta dawa ya allergy maana mwisho
utajikuna hadi utoe ngozi.  Kama tunataka kuondoa magamba, jambo la
kwanza, uchambuzi.

On 27/11/2012, Augustine Rukoma <arukoma66@gmail.com> wrote:
> Bariki, nimekupata, tatizo ni allergy tuliyo nayo wengi dhidi ya magamba
> inatufanya basi tu
>
>
> 2012/11/27 Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
>
>> Rukoma katika hii ya mama Lwakatare umedandia treni tena la mizigo. Mama
>> Lwakatare hakuwa akichangia bungeni kwamba kitumike Kiswahili. Naomba
>> usome
>> neno baada ya neno. Alisisitiza kwamba watoto wanapoongea Kiingereza
>> wasikatishwe tamaa, watiwe moyo ili wawe na ujasiri. Naomba urudie kusoma
>> neno baada ya neno. Ni vibaya kumwona mtu ni mnafiki kabla ya kuelewa
>> kile
>> anachokisema.
>>
>>
>> 2012/11/27 Augustine Rukoma <arukoma66@gmail.com>
>>
>>> Sasa chambi uone unafiki huo, huyo mama mishule yake yote kuanzia
>>> chekechea mpaka form six ni kiingereza tu, ilala sasa walimu kutoka
>>> kenya
>>> wameanza kumkimbia maana mkoloni ndio anafikiri kiswahili sasa ili
>>> awadhrumu waswahili. Huyo ndio andeufyata kabisa
>>>
>>>
>>>
>>> 2012/11/27 Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
>>>
>>>> "Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mwenyewe ni shuhuda, nilienda kule kwetu,
>>>> nilikuwa napita nikasikia Mwalimu anasema *"this is a kinife"*
>>>>  anamaanisha *knife*. Nikaingia darasani, kuingia darasani, nikamsaidia
>>>> nikamwambia hii inatwa *knife* ("naifu"), usiseme "kinife". Au mtoto wa
>>>> *Form Six *anakwambia *"my phone is crying". Your phone is not crying,
>>>> is ringing!* Ni kwa sababu ya vitu vidogo, kwa sababu hatuko *fluent*,
>>>> tujitahidi, tusione aibu" - Mama Lwakatare Bungeni kama alivyonukuliwa
>>>> kwenye hiyo makala hapo chini:
>>>>
>>>> *Laiti Tungejifunza Kwa Lugha Zetu*
>>>>
>>>> Je, unakumbuka neno hili 'Tujifunze Lugha Yetu'? Hilo ndilo lililokuwa
>>>> jina la vitabu vya kiada tulivyovitumia kujifunza Kiswahili enzi za
>>>> Ujamaa.
>>>> Kwa hakika lilikuwa andiko la kizalendo.
>>>>
>>>> Siku hizi kuna msisitizo mkubwa wa kujifunza kwa lugha ya kigeni. Na si
>>>> kujifunza tu kwa lugha hiyo, bali pia kuitumia kufundishia. Lo, shule
>>>> za
>>>> Kiingereza imekuwa biashara nono mno!
>>>>
>>>> Wataalamu wa 'nadharia ya baada ya ukoloni', au 'postcolonial theory'
>>>> kama wanavyoiita kwa Kiingereza, wanadai lugha ya kikoloni si ya kigeni
>>>> tena. Eti sasa ni lugha yetu maana tumechangia kwa kiasi kikubwa
>>>> kuibadili
>>>> na kuikuza. Hata maneno ya Kiswahili kama 'Safari' na 'Uhuru' leo yapo
>>>> kwenye Kamusi ya Kiingereza. Eti nayo yamekuwa maneno ya Kiingereza.
>>>>
>>>> Naam ni kweli kabisa tumechangia - kwa lazima au hiari - kukiendeleza
>>>> Kiingereza. Tena Afrika inajivunia kuwa na waandishi mahiri wa lugha
>>>> hiyo.
>>>> Wapo Wole Soyinka, John Cortzee na Nardine Gordimer waliopata mpaka Tuzo
>>>> ya
>>>> Nobeli ya Fasihi kutokana na maandishi yao kwa Kiingereza. Pia kuna
>>>> kina
>>>> Chinua Achebe na Ngugi wa Thiong'o wavumao katika medani hiyo.
>>>>
>>>> Kwa nini basi, wanahoji waumini wa Kiingereza, tusitumie lugha hiyo ya
>>>> kitandawazi kufundishia kwenye ngazi zote za elimu nchini? Kwa nini
>>>> tung'ang'anie kutumia Kiswahili na hata tudai kitumike kabisa kuanzia
>>>> Chekechea hadi Chuo Kikuu? Hatuoni kuwa tutapoteza fursa ya kutumia
>>>> lugha
>>>> inayotambulika zaidi duniani? Au hatutambui kuwa Kiingereza ndio lugha
>>>> ya
>>>> soko huria - chombo cha mawasiliano kwenye uchumi na biashara ya
>>>> ushindani
>>>> ulimwenguni?
>>>>
>>>> Wakati mjadala huu mkali ukiendelea, juma lililopita tulibahatika
>>>> kupata
>>>> ujio wa mmoja wa waandishi waliotajwa hapo juu. Ngugi alikuja kwenye
>>>> 'Kongamano la 6 la Umajumui wa Afrika la Usomaji kwa Wote'. Kaulimbiu
>>>> ya
>>>> Kongamano hilo lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam lilikuwa
>>>> 'Usomaji
>>>> kwa ajili ya Kuleta Mageuzi na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.'
>>>>
>>>> Mwandishi huyu alitumia fursa hii kutukumbusha umuhimu wa kutumia lugha
>>>> zetu kutunza kumbukumbu na kukuza maarifa ya jamii zetu. Katika
>>>> mhadhara
>>>> mkuu wa Kongamano hilo alioupa kichwa kinachoweza kutafsiriwa kama
>>>> 'Dhidi
>>>> ya Ukabaila wa Lugha na Udarwini: Mazingira ya Kujenga Utamaduni wa
>>>> Kusoma', Ngugi alisisitiza umuhimu wa uelewa/kuelewa.
>>>>
>>>> Hakika huwezi kuleta maendeleo ya kijamii bila kuvirithisha uelewa wa
>>>> kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi wa jamii hiyo vizazi vyake. 'Je
>>>> umeelewa?'
>>>> Hilo ndilo swali ambalo mama yake Ngugi alikuwa akimuuliza kila baada
>>>> ya
>>>> maelekezo aliyokuwa akimpa kila alipokuwa akimtuma kwa ndugu zake enzi
>>>> za
>>>> utoto wake. 'Yule mzazi asiyewajibika tu', anatukumbusha Ngugi, 'ndiye
>>>> anaweza kutoa maelekezo kwa kutumia maneno na lugha ambayo mtoto wake
>>>> haielewi.'
>>>>
>>>> Lakini hivyo ndivyo tunavyofanya kwa kuanza ghafla kufundishia kwa
>>>> Kiingereza baada ya kufundishia kwa Kiswahili shuleni. Tunafanya hivyo
>>>> japo
>>>> tunajua fika kuwa hatuna walimu wa kutosha wanaojua hata kufundisha
>>>> Kiingereza kama lugha ya pili licha ya kukifundishia. Mfano wa
>>>> kuaibisha
>>>> kuhusu mkanganyiko huu ulitolewa hivi karibuni Bungeni na Gertrude
>>>> Lwakatare.
>>>>
>>>> Mbunge huyo alisema: "Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mwenyewe ni shuhuda,
>>>> nilienda kule kwetu, nilikuwa napita nikasikia Mwalimu anasema *"this
>>>> is a kinife"* anamaanisha *knife*. Nikaingia darasani, kuingia
>>>> darasani, nikamsaidia nikamwambia hii inatwa *knife* ("naifu"), usiseme
>>>> "kinife". Au mtoto wa *Form Six*anakwambia *"my phone is crying". Your
>>>> phone is not crying, is ringing!* Ni kwa sababu ya vitu vidogo, kwa
>>>> sababu hatuko *fluent*, tujitahidi, tusione aibu." Wabunge wakacheka.
>>>> Na kupiga makofi. Mjadala ukaisha. Sera ya lugha ikabaki vilevile.
>>>>
>>>> Hili ni suala zito la kisera. Si jambo la kulifanyia mzaha. Wala
>>>> kulichekea. Limetugharimu sana kama nchi. Na linatupoteza kama jamii.
>>>> Ni
>>>> kitu cha kustaajabisha. Tena hakifanyiki katika nchi zingine. Eti
>>>> kuwafundishia watoto kwa lugha wanayoielewa kwa miaka saba bila
>>>> kuwafundisha vizuri lugha wasiyoielewa. Kisha kuanza ghafla
>>>> kuwafundishia
>>>> kwa lugha hiyo wasiyoielewa!
>>>>
>>>> Laiti tungeweka pembeni kasumba na kutambua kuwa suala hili si suala la
>>>> uzalendo tu. Ni suala la ubinadamu. Unapomnyima mtu fursa ya kujifunza
>>>> kwa
>>>> lugha yake anayoitumia na kuielewa zaidi unamnyang'anya utu wake. Tena
>>>> unamuibia uhuru wake wa kufikiri, kuhoji na kuvumbua katika muktadha wa
>>>> mazingira ya jamii yake. Unamfanya mtumwa katika nchi yake mwenyewe.
>>>>
>>>> Ndio maana kuna umuhimu wa kuzitafakari kwa makini hoja alizozitoa
>>>> Ngugi
>>>> katika huo mhadhara wake. Na kuna hitaji la kuzingatia hoja kuu ya
>>>> kitabu
>>>> chake kipya cha 'Re-membering Africa'. Jina la kitabu hicho lina maana
>>>> ya
>>>> kuwa Afrika imevunjwavunjwa kwa ukoloni na ubeberu wa lugha za kigeni
>>>> na
>>>> inahitaji kuungwa tena kwa kutumia kumbukumbu za lugha zetu.
>>>>
>>>> Tukitaka kuendeleza maarifa na kujiletea maendeleo yetu wenyewe tuenzi
>>>> lugha zetu. Tujifunze lugha zetu. Tufundishe kwa lugha zetu. Tutafiti
>>>> kwa
>>>> lugha zetu. Tuvumbue kwa lugha zetu zote.
>>>>
>>>> Kama anavyoghani Malenga 'Issa Bin Mariam':
>>>>
>>>> *Amkeni, Waafrika.*
>>>> *Uafrika ni Umajumui wa Afrika.*
>>>> *Oteni ndoto, Kizaramo,*
>>>> *Fikra, Kiswahili; mawazo Kigikuyu.*
>>>>
>>>> *© **Chambi Chachage – Mwananchi (18 Agosti 2009)*
>>>>
>>>> *-------*
>>>> *My mission is to acquire, produce and disseminate knowledge on and
>>>> about humanity as well as divinity, especially as it relates to Africa,
>>>> in
>>>> a constructive and liberating manner to people wherever they may be.*
>>>>
>>>> *Address:* 41 Banks Street # 1, Cambridge, MA 02138 USA
>>>> *Cellphone:* US = +1 (857) 413 - 9521/TZ = +255754771763
>>>> *Skype:* chambi100
>>>> *Twitter:* @Udadisi
>>>> *Facebook: *http://www.facebook.com/chambi78
>>>> *Blogs:* http://udadisi.blogspot.com  <http://udadisi.blogspot.com/>&
>>>> http://ufunuo.blogspot.com
>>>> *Group:* http://groups.yahoo.com/group/wanazuoni
>>>>
>>>> --
>>>> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
>>>> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii:
>>>> mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>>>
>>>> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
>>>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
>>>> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>>>>
>>>> TEMBELEA Facebook yetu:
>>>> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>>>>
>>>> For more options, visit this group at:
>>>> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>>>>
>>>> ---
>>>> You received this message because you are subscribed to the Google
>>>> Groups "Mabadiliko Forums" group.
>>>> To unsubscribe from this group, send email to
>>>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
>>>>
>>>>
>>>>
>>>
>>>  --
>>> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
>>> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii:
>>> mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>>
>>> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
>>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
>>> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>>>
>>> TEMBELEA Facebook yetu:
>>> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>>>
>>> For more options, visit this group at:
>>> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>>>
>>> ---
>>> You received this message because you are subscribed to the Google
>>> Groups
>>> "Mabadiliko Forums" group.
>>> To unsubscribe from this group, send email to
>>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
>>>
>>>
>>>
>>
>>
>>
>> --
>> Bariki G. Mwasaga,
>> P.O. Box 3021,
>> Dar es Salaam, Tanzania
>> +255 754 812 387
>>
>>  --
>> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
>> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
>> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>>
>> TEMBELEA Facebook yetu:
>> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>>
>> For more options, visit this group at:
>> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>>
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Mabadiliko Forums" group.
>> To unsubscribe from this group, send email to
>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
>>
>>
>>
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
>  http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group, send email to
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
>
>
>

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.

TEMBELEA Facebook yetu:
 http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl

For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en

---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group, send email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.

--
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

0 comments:

Post a Comment