Monday, 29 October 2012

Re: [wanabidii] UKWELI KUHUSU RIDHWANI KIKWETE KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA

Magobe, lugha uliyotumia imekuwa ngumu kidogo kueleweka, naomba msaada Chief!

Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

-----Original Message-----
From: Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 29 Oct 2012 12:05:32
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] UKWELI KUHUSU RIDHWANI KIKWETE KUKAMATWA NA MADAWA YA
KULEVYA CHINA

Hata wewe unayesema haya ya Dk Slaa ni mwongo pia. Je, Mungu ambaye ni
mtakatifu aliwezaje kumwumba mtu mwongo kama wewe? Kwa vile umeumbwa
na Mungu aliyemtakatifu, inatia shaka/inaleta utata kuhusu utakatifu
wake kama it logically follows that what you are tells something about
who or what made/produced you!

On 10/29/12, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
> Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi
>
>
> WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na
> umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha
> Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa. Huyu kwa umri wake,
> kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya
> Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli.
> Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea
> kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya
> kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto
> katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.
>
>
> Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi
> kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo
> huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu
> watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena
> kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana
> Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua
> na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya
> Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong
> Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa
> alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.
>
>
> Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku
> hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
>
> Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako
> alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai
> 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya
> Burundi. Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa
> Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma
> ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam
> siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong
> Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa
> Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa
> Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa
> China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo
> sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa
> sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko
> wazi na siyo kificho.
>
>
> Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini
> Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka
> Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania
> Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo
> alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong
> kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba
> ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:
>
>
> Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi
> alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe
> za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya
> Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals
> Techonologies Group ambayo inataka kufungua viwanda cha madawa na mbolea
> nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa
> Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na
> Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano
> ya ZTE. Julai 5, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na
> Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika
> mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za
> Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa
> Rais kama siyo uongo?
>
>
> Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda
> wote. Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika
> maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea
> ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na
> Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama
> Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine
> ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya.
> Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya
> kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama
> vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa
> kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment