Tuesday, 30 October 2012

Re: [wanabidii] UKWELI KUHUSU RIDHWANI KIKWETE KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA

Tony, 

I  agree with you more! I don't care about the authenticity of whether dr. Slaa said this or not. I will dwell on the general issue of patriotism, values and moral stand of issues that matters to our country.

Nchi yetu haiwezi kuendelea kama hatutahoji wale tuwapendao kisiasa, tunakuwa washabiki zaidi badala ya kuunganishwa na sera na mambo tunayoaamini.. Hii sio timu ya mpira, huu ni mustakabali  wa taifa. mapenzi kwa nchi yetu kwanza.. Wengi wetu hatuyaoni.

Na huu ndio ugonjwa wa CCM, na kuna rafiki yangu wa CCM alisema kuwa "Watanzania ndio hawa hawa" ie CHADEMA and CCM kwenye rushwa ni sawa, alisema nikambishia,  Sikumuelewa sasa naanza kuelewa hoja yake kidogo kidogo.

 Ni vema chama hiki cha upinzanj Kiki prove hiyo theory wrong, watu wamekosa Imani na system, siasa na hawajali nani anakuwa kiongozi, ili mradi katoa hela.

Mabadiliko hayaji kwa kuwa na watu Kama mh.Zitto ambao wanatuonyesha  sisi watazamaji kuwa kuna shida aidha kwenye chama au kwake yeye. For the love of God, why would you behave like that? Score what? political points, make your colleagues offended and  overreact? Come on! Have you expelled from the party and prove your opponents right?

I stand to be corrected but I have a bad feeling about Zitto and his political belief and if he really want his party to grow. His utterance are proving wrong, of what he tells us to be his true values and genuine commitment about bringing change to this country.

I have similar disagreement with hon. Sitta, if you disagree with your party move out, if you can't stand heat get out of the kitchen, but you can't be senior and seasoned politician like Mr. Sitta and remain an opposition in the cabinet. It's like retiring and stay in the office.

My 50 cent

From LR

On 30 Okt 2012, at 8:14, "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

Emma,

Slaa aliona taarifa iliyoanikwa hapa naye bila kujiongeza, kaitoa laivu huko tabora (uyui) kwenye mkutano wa kampeni! Msitetee bila kuwa na ushahidi kama alisema au la! Ugonjwa wa kupenda ndo naona unawasumbueni! Ningeelewa mtu angesema mpenda ya mtandaoni, kapatikana! Ndio zake huyo na naona kambi zinazosigana kwenye chadema zimempata laivu huyooo!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
Date: Mon, 29 Oct 2012 05:57:52 -0400
Subject: Re: [wanabidii] UKWELI KUHUSU RIDHWANI KIKWETE KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA

Bariki,
Kuna mantiki. Aliyeandika ripoti hiyo amejitaja kuwa alikuwemo kwenye msafara.
Na kama alikuwemo basi lazima awe afisa mwandamizi Ikulu aka usalama wa taifa.
Sijui Slaa amehusishwaje na ripoti hii.
em

2012/10/29 Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
Mimi sioni mantiki ya kuhusisha kilichoandikwa na Afisa Mwandamisi wa Usalama wa Taifa. Jambo la msingi ni kupata maelezo ya Dkt Slaa kama yapo kwani aliyeandika anaweza kuwa hata ni mwendawazimu tu wala sio mtumishi wa Serikali.

2012/10/29 Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
Abdallah,
Kabla ya kumhukumu Dr. Slaa nakushauri uangalie uwezekano kwamba hii story kama imetungwa, basi imetungwa na afisa mwandamizi katika idara ya usalama wa taifa. Hapo ndipo ninaona kuna tatizo. Ndio maana nimeuliza katika bandiko
langu la awali, watu wenye akili watujulishe, ilikuwaje wakati Ikulu inaungua, kilichochukuliwa ni mafaili kuhusu biashara za Mkapa ambayo yalikuja kutumiwa na Kikwete na Rostum kumshinikiza Mkapa ampitishe Kikwete mwaka 2005. The problem is bigger than shutuma zako kuhusu uwongo wa Mheshimiwa Slaa.
em

2012/10/29 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa.  Huyu kwa umri wake, kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli. Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.

Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.

Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi.  Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:

Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka  kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi  alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote.  Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

0 comments:

Post a Comment