DC Korogwe awajibishwe kwa udhalilishaji
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), tumesikitishwa sana na kauli
iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Ndugu Mrisho
Gambo, kwa mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bi. Najum Tekka, kuhusu
uhalali wa shahada aliyonayo hususan kuihusisha shahada hiyo na
vitendo vya ngono! Kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari ikiwepo
gazeti la Majira Augosti 29,2012 Uk.3
Kauli hii ni udhalilishaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za wanawake na
inaenda kinyume na misingi ya kuzingatia usawa sanjari na Katiba ya
nchi ; Uwezeshaji wa wanawake na utekelezaji wa Maazimio ya Haki na
Usawa katika ngazi za Kimataifa Kikanda na Nchini Tanzania.
Aidha kauli hii, inalenga kupotosha na kukatisha tamaa juhudi kubwa
wanazofanya wanawake na wasichana katika kupata elimu na mafanikio
mbalimbali nchini Tanzania. Zaidi ya hapo, kauli hii inadhalilisha na
kushusha hadhi ya vyuo vya elimu ya juu vinavyofanya kazi kubwa ya
kutoa elimu kwa Watanzania.
Kutokana na kauli hiyo DC amekiuka maadili ya uongozi wa umma na
kukidhalilisha kiti cha ukuu wa wilaya na kiongozi Mkuu wa nchi
aliyemteua kushika wadhifa huo. Aidha kauli ya kiongozi huyo ya
kutimia mahakama kutetea hoja yake , kunaashiria ubabe , ujeuri,
vitisho, kiburi na dharau ya kutaka kuingilia uhuru wa mahakama na
ajenda binafsi isiyokuwa na maslahi kwa wanawake na umma wa Watanzania
Kutokana na kauli hiyo ya udhalilishwaji ,sisi wanaharakati wa
ukombozi wa wanawake Kimapinduzi, usawa wa kijinsia, haki za
kibinadamu demokrasia tunalaani vikali kauli za DC na kutoa Rai
ifuatayo:
1. Mkuu wa Wilaya Ndugu Mrisho: amwombe radhi Mwanasheria Bi.
Najum Tekka, kwa kosa la kumdhalilisha kijinsia
2. Tume ya maadili ya utumishi wa umma, na Mamlaka nyingine za
kinidhamu zimchukulie hatua za kinidhamu Ndugu Gambo kwa kutumia lugha
ya kudhalilisha watumishi kinyume na maadili.
3. Wanawake wote, wanaume, vijana wa kike na kiume kuendelea na
mapambano dhidi ya mfumo dume na mifumo yote kandamizi, kushikamana
katika kudai misingi ya kisheria, uwajibikaji inayozingatia usawa na
haki na kukataa kudhalilishwa katika ngazi binasfi na za umma !.
Imetolewa
Dar es salaam leo 31/08/2012 na:
Usu Mallya
Mkrugenzi Mtendaji TGNP
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment