Sunday, 30 September 2012

Re: [wanabidii] FLASH DISK KAMA KIFAA CHA KUTENDA UHALIFU

Asante kwa kutujuza.
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 29 Sep 2012 08:51:55 -0700
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>; <wanakenya@googlegroups.com>; Wanazuoni<wanazuoni@yahoogroups.com>; <kenyaonline@yahoogroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] FLASH DISK KAMA KIFAA CHA KUTENDA UHALIFU

FLASH DISK KAMA KIFAA CHA KUTENDA UHALIFU


Flash Disk au thumb drive kama wengine wanavyopenda kuita ni kifaa cha kuhifadhia vitu , kifaa hichi huja kwa ukubwa mbalimbali kuanzia mb 128 mpaka gb 32 na kuendelea na kwa sasa watu wengi wanacho angalau kimoja au zaidi kwa ajili ya kuhifadhia vitu vyake .


Flash disk kama kifaa cha kuhifadhia vitu inaweza kutumika katika kutekeleza uhalifu Fulani kwa mtumiaji kujua au kutokujua kutegemeana na mazingira na mtu mwenyewe au kundi la watu hao .


Hapa chini ni maelezo mafupi ya jinsi kifaa hiki kinavyoweza kutumika kutekeleza uhalifu wa aina mbalimbali .


KUENDESHA PROGRAMU

Kuna flash disk nyingi sasa hivi zinazokuja na programu za moja kwa moja ambazo zimeshaingizwa kwenye kifaa hicho , programu hizi zinakuwezesha kuweka password kwenye flash disk yako na ulinzi mwingine .


Lakini programu hizi zinaweza pia kutumika kukuibia wewe taarifa na kuzituma sehemu nyingine za mhalifu wako ambapo anaweza kutumia dhidi yako au maslahi yako .


PROGRAMU GANI ?

Programu zinazoweza kuendeshwa kutumia flashdisk kimya kimya ( Silent ) bila mtumiaji kujua ni kama


Keylog ambayo ni programu maalumu kwa ajili ya kuhifadhi kile unachofanya kutumia keyboard yako , vile unavyoandika na kuhifadhi .


Virus

Virus ni programu kama nyingine ambayo pia inauwezo wa kufanya kazi ndani ya flashdisk na kusambaa kwa kasi ndani ya ofisi yako au kompyuta husika , lakini hii inategemeana na aina ya virus .


Spyware

Hii ni kama Keylog tu lakini mara nyingi uhalifu wake unahusisha zaidi mitandao ,  haswa matangazo au kukulazimisha kutekeleza vitu bila wewe kujua au kwa kujua lakini bila kuelewa kile unachofanya .


Wahalifu wengi wanaoendesha uhalifu wao kutumia Internet Cafes wanatumia kifaa chao kikuu ni Flashdisk ingawa kuna uwezekano wa kutumia vingine kama CD , DVD na Mtandao wenyewe .


Ufanyaje ?

Nakushauri unapopata flashdisk mpya ni vizuri ufute programu zilizomo ( Format ) itaweza kuondoa zote , ingawa sio flash disk zote zinazokubali kufutwa .


Kama uko kwenye maofisi ni vizuri kuweka utaratibu na miongozo ya utumiaji wa flashdisk au vifaa vingine vya kuhifathia vitu ambavyo ni mali binafsi za watu au hata za ofisi lakini ambazo zinaweza kutumika nje ya ofisi husika .

Hii itaweza kuzuia au kupunguza uhalifu kama huu na zaidi ni kutoa elimu zaidi kwa watumiaji .


MASUALA MENGINE .

Pale unapobeba nyaraka ambazo sio zako ndani ya kifaa hiki ni uhalifu kwa njia moja au nyingine , nyaraka hizi zinaweza kuwa ni za serikali , mashirika , watu binafsi  na taasisi hapo utakuwa na kesi ya kujibu kwa sababu kidhibiti kimepatikana .


MWISHO

Pamoja na haya yote flash disk inaweza kutumika kama kifaa kizuri kwa ajili ya kuhifadhi vitu vyako na kuhamisha kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kazi bila shida yoyote lakini usiamini sana , vizuri ukaweka nakala ya kazi yako kama ni kwenye CD , DVD au Kifaa kingine maana inaweza kuharibika , kuibiwa au kuliwa na virus .


YONA F MARO

9/29/2012 8:50:05 AM

 

 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment