Saturday, 29 September 2012

[wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!?

----- Forwarded Message -----
From: Nico Eatlawe <eatlawe@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, 29 September 2012, 10:23
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!?
Kiongozi mzuri ana sifa yakuwa na ujasiri wa kusema anachokiamini maana ana maono ndani yake. Kama vile Mandela alivyohatarisha maisha yake akipinga ubaguzi vivyo hivyo kiongozi hawezi kuwa kamamcheza karata bali anakuwa tayari kukabiliana na vihunzi ili akishinda baadaye iwe shule kwa wengine. Inashangaza kuona jinsi watu wanavyokuwa na ukosoaji badala kumwuliza kwamba anataka anafanye nini kuboresha nchi yetu. Katiba yetu inampa kila mtu uhuru wa kutoa mawazo yake na ni pamoja kutangaza kugombea urais. Kuna dhambi gani au kosa la jinai hapo? Chama chake kikimpitisha basi atagombea na asipopitishwa atangoja kama JK alivyongojea wakati wake. I strongly believe in intrinsic motivaion than extrinsic one. Atambuaye hayo na afahamu. Kwa watu wa imani husema Mungu ndiye anatupa kiongozi na kama ni yeye basi kusudi la Mungu litasimama na kama siyo basi.  Kwa wale wa imani someni hii ili kupata jibu kwanini mambo yanaendaga kinyume na matarajio e.g. 1995, 2000, 2005, 2010:
 
I have observed something else under the sun. The fastest runner doesn't always win the race, and the strongest warrior doesn't always win the battle. The wise sometimes go hungry, and the skillful are not necessarily wealthy. And those who are educated don't always lead successful lives. It is all decided by chance, by being in the right place at the right time, Ecclesiastes 9:11 quoted from New Living Translation (©2007)

From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, 29 September 2012, 10:06
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!

Mgamba,
 
Nakushukuru sana kwa mchango wako katika hoja hii. Mimi nami nilichangia hoja hii hapo mwanzo lakini ikiwa na "heading"nyingine.
 
Kwanza nianze kwa kusema kwamba vijana msiwe kikwazo kwa vijana wenzenu. Mpeni ZITTO nafasi ya kutoa mawazo yake, kuna kitu mtakipata. Kumtukana na kumshambulia ZITTO kwa njia yoyote ile ni sawa na kujaribu kuzima nyota iliyoanza kung'ara miongoni mwa Watanzania. Na kwa mtizamo huo ni sawa na kufunikwa na wingu zito lisilotoa nafasi ya kuona upande wa pili wa shilingi. Na kwa hakika na kwa kusoma mawazo na michango mbalimbali hapa jukwaani ni wazi kwamba wingu hili zito limewafunika kiasi kwamba kwao ni usiku tu.
 
Zitto katamka rasmi kuwa hatagombea Ubunge katika jimbo lake. Sasa tatizo liko wapi. Woga huu unaojitokeza kwa yeye kutogombea ndio uliowapata hata watanzania wakati Mwl. JK Nyerere alipotangaza kuwa atang'atuka katika uongozi wa nchi. Watu walitaharuki lakini hatimae aliacha uongozi. Kwangu mimi naiona nafasi hii kama lulu kwa wanaKigoma na CDM kujiandaa sasa kuona ni yupi anayeweza kuziba kiatu cha ZITTO. Lakini kuendelea kumlaumu na kumwita msaliti, sioni kama hii ni kumtendea haki kwa sasa. Katumia haki yake ya kusema lolote atakalo bila kuvunja sheria za nchi, huenda sheria zao wao wenye mambo yao.
 
Jambo la pili ni kutangaza nia ya kugombea Urais ifikapo 2015. Hoja nyingi zimetolewa nyingine zikimnukuru Mwl. JK kwamba anayekimbilia urais ( japokuwa yeye alisema …Ikulu) ….. ni wa kuogopwa kama ukoma. Watu hawa nadhani aidha wanaacha kunukuru maneno mengine ya Mwl Jk kwa vile wanajua yatavuruga maana yao. Kimsingi hoja ya Mwl JK ilikuwa kwa wale waliokuwa wako tayari kuingia Ikulu kwa gharama yoyote hasa rushwa au kumwaga damu, na si kwa mtu kutangaza nia ya kugombea urais. Sioni kama kijana ZITTO ameonesha hali hiyo. Ninaloliona ni kwamba kuna watu hawataki kusikia kitu chochote kikisemwa kinyume kwa wateule wao. Wako tayari kufa ili kuzima sauti za upande wa pili. Na kwa bahati mbaya wanaiita hiyo ndiyo demokrasia. Nakumbuka Rais mmoja wa marekani aliwahi kusema wakati anatangaza nia ya kugombea kwamba sifa moja ya kuwa rais ni kuutaka Urais wenyewe. Hoja hii inapingana kwa nguvu zote na ile ilitajwa hapa ya kwa mtu lazima alazimishwe ndipo akubali. Hili naliona kama unafiki, kwamba mwanzoni hutaki lakini baadaye unashawishiwa unakubali. Hapana mimi siyo muumini wa hilo labda nielimishwe kwanza.
 
Huu msigano wa mawazo ni wa hatari sana. Sina hakika kama tukiendelea hivi tutafika. Picha ninayoipata hapa ni kwamba kama Watanzania wakiamua kuwapa ridhaa ya kuwatawala basi wote wenye mawazo tofauti (kama mimi) watafutiliwa mbali. Hili liko wazi na watanzania wanajua hili.
 
Kwa mtizamo wangu pamoja na kwamba ZITTO mnampiga madongo sana lakini uelewa wake wa mambo ni mkubwa sana kuliko hao mnaowaweka mbele (hata katika IQ zao – pingeni hili kwa hoja). Binafsi nimelipima hili kutoka na hoja zao kila siku kwenye majukwaa na kwenye matamko yao. Utamsikia mwingine hoja ni ile ile kila siku na kila sehemu, huenda akabadili mazingira au baadhi ya maneno lakini mantiki ni ileile, lakini ZITTO anatoa uchambuzi wa hoja zake kwa undani sana. Hebu rejeeni hoja yake ya kutetea vijana wapewe nafasi ya kugombea urais (japokuwa sikubaliani na msimamo huo) au ile ya Matajiri 30 wanavyonyonya Wananchi billioni 30sina hakika kama nimeiandika ilivyokuwa ikisomeka) Hata kama huzipendi lakini unaona kabisa kuwa kuna kitu (there is a substance in it) ndani yake cha kujishughulisha kutafuta kujua mambo na kutafuta ufumbuzi wake.
 
Historia ya CDM iko wazi, vurugu za kumchukia ZITTO ziko wazi mno kiasi kwamba wengine tunashangaa kuona kwamba ninyi wenzetu mlioko humo ndani ya CDM hamuoni. Binafsi sitaki kuamini kwamba hamuoni, lakini huenda kuna mbinu za kuzamisha mawazo yenye manufaa kwa watanzania ya vijana wetu. Vijana amkeni, leteni mawazo mapya yenye kujenga nchi. Acheni fitina na majungu, fueni vichwa vyenu kwa kusoma siyo kutegemea mawazo ya watu wengine. Chambueni hoja linganisheni na kuchambua kwa hoja pia. Fanyeni tafiti ili kupata "Critical thinking".
 
Mimi siyo mwana CDM, wanaonifahamu wananijua. Lakini nionavyo mimi ni kwamba nguvu za ziada zinazotumika kuzima mawazo ya ZITTO ni zile zile zilizokuwa zikitumika kuzima mawazo ya Marehemu Mhe. CHACHA WANGWE. Na siku wananchi watakapofahamu fika jinsi nguvu hizo zinavyofanya kazi ya kuingiza mawazo yasiyofaa vichwani mwao, hakuna atakayesamehewa. Mimi siyo nabii lakini kwa hili tuweni macho.
 
KEMS.
 
From: RICHARD MGAMBA <rmgamba2000@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, 29 September 2012, 0:41
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
Kwa bahati mbaya sana, ugonjwa ule ule wa CCM wa kutokutaka kuukubali ukweli nao unaanza kuingia katika Chadema. Mara ngapi wabunge vijana wa Chadema wamelazimishwa kukana matamshi yao juu ya Zitto Kabwe na mbio za urais?

Ninapowakosoa ninawasaidia kuyaona ambayo hamjayaona, lakini naona mnakuwa too defensive. Ilikuwaje wakati Zitto alipotangaza kugombea uenyekiti wa Chadema? Kama tunaamini katika demokrasia ni kwa nini tukimbilie kuona yule anayejitokeza kupambana na wakubwa kama katumwa? Hii ni kasumba ya CCM na siyo ya wanamageuzi kama Chadema.

Ilikuwaje Marehemu Chacha Wangwe alipotangaza kwamba anataka kugombea uenyekiti? Kama unakumbuka vizuri uhasama ulizuka. Huko CCM ndiyo kuna siasa kama hizo, lakini kama na Chadema wakizichukua, ipo kazi kubwa.

Mwanza ni matatizo yale yale. Kuna wakati unalazimika kutembea na mwiba mguuni hadi nyumbani ndiyo unauotoa maana ukisimama kati kati ya safari kuutoa, utaliwa na simba.

Chadema ilishachukua Jiji la Mwanza, hivyo wangevumilia wakaja kuyang'oa magugu 2015—hiyo ndiyo Siasa. Lakini wakafanya kinyume eti kusafisha chama, bila kujali matokeo yake. Kama ni hivyo mbona John Shibuda bado yumo kwenye chama?

 Katika siasa lazima upime matokeo ya hatua utakazo zichukua kabla ya kutenda. Leo hii Chadema imepoteza ngome muhimu kwa maamuzi ambayo hayakupimwa kwa kina kabla ya kufanywa.

Nayasema haya kwa dhati na wana-Chadema wasichukie, demokrasia ni pamoja na kukosoana.

From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, September 29, 2012 9:28 AM
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
Wewe Ni Anael Macha, mzee wa ANDA? Samahani nahisi kama anuani yako imeingiliwa.........................
2012/9/29 Anael Macha <kowiri@hotmail.com>
Kaka Mgamba,

- nampongeza Mhe Zitto kwa hatua yake ya kutangaza mapema kugombea. 

- wafuasi sie na chadema, wapi ambapo kiongozi yeyote alionyesha kukerwa na hatua ya Zitto? Ili useme chadema hakuna demokrasia? If happened basi lawama kubwa kwao. Please yasiwe ni maongezi binafsi na kiongozi mmojawapo then ukachukulia ndo kauli ya chadema.

- sijui mwanzo mwisho wa madiwani wa mwanza kama wale wa arusha lakini naamini hawaweze chukua maamuzi ya kukutupuka. Kind of changes we want sihitaji quantity but quality changes no matter how many years will take. I may not enjoy changes i want but my sob will do.

- ZItto go, wengine jitokezeni tena hata kwenye ubunge nk. 

Jumamosi njema

AM
Sent from my iPhone
On Sep 29, 2012, at 8:01, "RICHARD MGAMBA" <rmgamba2000@yahoo.com> wrote:
Nadhani ndugu zangu ama mnamuonea Zitto au mna matatizo naye binafsi. Kuna tatizo ghani katika chama na nchi ambayo watu wanaheshimu demokrasia kwa Mbunge kutangaza mapema kwamba hatawania ubunge tena? Napata shaka na maneno muda muafaka, maana yanatumika vibaya.

Hakuna muda maalumu kwa mtu kutangaza kwamba atagombea au hatagombea ubunge au urais wa nchi. Huu ni uoga ambao Chadema na wafuasi wake wameurithi kwa chama tawala ambacho kwa hofu ya kumeguka hasa baada ya vyama vingi kuingia, kikaweka vikwazo.

Mfano hapa Kenya, wagombea wa Urais wanajulikana hata miaka minne kabla ya uchaguzi mkuu na hakuna shida maana inatoa Mwanya kwa umma kuwachunguza kwa kina ili kuona kama wanafaa au la. Hata ubunge ni hivyo hivyo, sasa unashangaa sana hapa Tanzania, Zitto kutangaza kwamba hatagombea tena, inakuwa karopoka au katenda dhambi.

 Okay tuamini kwamba anayo nia ya kugombea urais kupitia chama chake kama umri utakuwa unaruhusu, kwani tatizo ni nini? Si mumuache aweke jina ili apambane na akina Dr Sla katika mchakato wa urais, akishindwa basi na kama akishinda yote heri. Ni kwa nini chama kama Chadema ambacho kinaamini katika demokrasia ya kweli, wafuasi wake wahofie na hata kumchukia mwanachama anayetaka kutumia haki yake ya kikatiba kugombea nafasi fulani katika chama?

Mgombea urais wa Chadema anapatikanaje? 

Kuweni wakweli. Zitto siyo malaika, na ni kiongozi kijana toka upinzani ambaye hata kupanda kwake pia kulikinufaisha Chadema hivyo inatia shaka kuona anatukanwa, kubezwa na kubambikizwa tuhuma bila ushahidi eti kwa sababu tu katangaza kwamba hatagombea tena ubunge? Wasi wasi wenu ni nini?

Kama ana mpango wa kuhama kwani yeye ndiye Chadema? Akihama Chadema inakufa? 

Chadema walikataa kumtambua rais wa Tanzania, Zitto akamtambua, akalaaniwa lakini baadaye wabunge wa Chadema wakatinga ikulu kuzungumza na mtu wasiyemtambua kuhusu katiba ya nchi na hatimaye wakampelekea majina ya kuchagua watu watakaokuwa katika tume ya katiba mtu yule yule ambaye hawajawahi kumtambua!

Chadema ni chama kinachokua kwa kasi lakini kinakoswa umakini katika mikakati yake na mwishowe utakuwa ni kama vyama vilivyotangulia. Chukulia mfano wa Mwanza, ambako sasa chama kinapoteza nafasi muhimu sana na huenda ikawa ndiyo Mwanzo wa kutoa mwanya tena kwa CCM iliyokuwa imekufa huko kujijenga upya.

Muacheni Zitto afanye siasa zake na watu wake wa Kigoma...Kama hagombei, Chadema waanza mkakati wa kuchagua mtu wa kutetea jimbo mapema.

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, September 28, 2012 10:29 PM
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
Nimeipokea kisawasawa. Mimi nkokotoa tangu huyu jamaa apande chati baada ya kuadhibiwa na Bunge kwa sababu alifaya kosa kweli lakini kwa kuwa watu walishaichoka serikali wakaamua kumshangila mhalifu. Afterall alifanya kosa akitetea UKWELI. Hii ilimpandisha chati kiasi CHADEMA nikafikiri lazima iende naye kwa tahadhari maana watu wamemshangilia kama waJerumani walivyombeba Hilrer. Mtu aliyemuelewa Hitre mapema angekuwa na busara kunyamaza kuliko kusema. Zito ni mbunge mzuri nami naamini sitashangaa asipopewa wizara 2015 kama CHADEMA itashinda. N awakitaka kumpa lazima wapate ushauri kutoka TAKUKURU.

--- On Fri, 9/28/12, gm26may@gmail.com <gm26may@gmail.com> wrote:

From: gm26may@gmail.com <gm26may@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, September 28, 2012, 12:18 PM

Elisa Pokea Saluti yangu nikiwa mguu sawa
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Date: Fri, 28 Sep 2012 12:15:35 -0700 (PDT)
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
 
Nanukuu kutoka Zanzibar Kwetu  '------Tuliwahi kusema huko nyuma na tunasema tena na leo pia, kuwa…"Chadema inabidi iyakabili kijitu kizima matatizo ya huyu kijana, bila ya Zitto kudhibiti mdomo wake, chama ambacho kinategemewa na wengi to form the next government in the country will slowly and surely bleed again to an ignominous defeat in 2015!".
 
Kwa muda mrefu mimi naamini CHADEMA wanajitahidi kujitenga ka tabia za Zitto. Kila mtu anajua aliyeropoka ni Zitto si CHADEMA. Angekuwa Slaa, Mbowe hata Tundu Lisu ingekuwa rahisi kufikiri CHADEMA imeropoka. Ila kwa Zitto, labda zamani zile.
 
Nafikiri kwa muda mrefu hisia kuwa Zitto kanunuliwa zinaweza kuwa zimewaingia 'wapangaji' wa CHADEMA. Na kama bado nitafikiri basi sio chama makini. Kama tayari basi ni kweli pia wanakwenda naye kwa tahadhari wakijitofautisha na upuuzi anaoweza kuufanya. Yesu aliwazuia wahudumu wa shamba kuwa magugu mengine wasiyang'oe yasije yakang'oka na Ngano. Sijasema Zito ni Gugu. Atakayesema sitapinga.   --- On Fri, 9/28/12, John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com> wrote:

From: John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, September 28, 2012, 11:18 AM

"Ni kweli kuwa hakuna makosa kwa mwanachama wa chama chochote kile kutangaza nia ya kugombea 
nafasi yoyote ya chama hata ya urais, lakini unapotangaza kuwa na ubunge pia hutogombea wakati hujui 
kama chama chako kitakuchagua wewe au vipi, inatia shaka sana kuwa kuna kitu nyuma ya pazia".   
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/ Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/ Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/   Kujiondoa Tuma Email kwenda mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
--
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment