Friday, 28 September 2012

Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!

Kuna haki na uhuru wa kufanya jambo, halafu kuna busara ya kufanya jambo. Nina uhakika kabisa kuwa Zitto ametumia haki na uhuru wake wa kikatiba (katiba ya Jamhuri ya Tanzania na katiba ya chama) lakini nahisi hakutumia busara.
 
Bado nashikilia kauli ya Mwalimu, mtu anayeutaka sana Urais -------------, ni wa kumwogopa kama ukoma. Nafurahia sana utaratibu wa FRELIMO wa vikao vya chama kumpendekeza mtu wanayedhani anafaa kuwa mgombea wa kiti cha Urais badla ya mtu kujipendekeza mwenyewe. Ni kwa kupitia utaratibu huu, haishangazi kuona Joachim Chisana alitangazwa kuwa Rais bora mstaafu.
 
Pamoja na CHADEMA kuungwa mkono na Watanzania walio wengi lakini ni ukweli pia kuwa bado ni kichanga. Na sidhani kama kina uwezo mkubwa wa kuhimili migawanyiko ya makundi ambayo yanaweza kuundwa na viongozi wake wakuu (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, n.k.) kwa nia ya kuutaka Urais. Lililo muhimu kwa sasa ni kwa viongozi wa juu wa CHADEMA kushikamana ili watakapomtoa mgombea kupitia CHADEMA awe ni mwakilishi halisi wa CHADEMA, na siyo mwakilishi wa kundi ndani ya CHADEMA.
 
CCM, pamoja na ukongwe wake, makundi ya Urais yamekidhoofisha kwa kiasi kikubwa. Kigwangala na wengineo wa CCM watafurahia sana wakiona kuna makundi yanajengeka ndani ya CHADEMA.Ni lini Kigwangala alisifia jambo jema ndani ya CHADEMA? Kwa nini leo watu wa kwanza kuisifia kauli ya Zitto wawe ni CCM?
 
CHADEMA kikitaka kupata mafanikio katika uchaguzi Mkuu, kwa sasa viongozi wake wajishughulishe zaidi kujenga chama, kutoa elimu kwa wapiga kura, na kujenga mfumo imara na wa kidemokrasia ndani ya chama. Kiongozi yeyote ambaye atajishughulisha zaidi kujenga makundi ya Urais badala ya jukumu la msingi, ni adui wa maendeleo ya harakati za kuleta mabadiliko. CHADEMA ikifanya kosa la kuwaacha viongozi wake kuufikiria Urais zaidi kuleta harakati za utoaji Elimu kwa wapiga kura, hata wakipata dola, hawatakuwa tofauti na CCM, watalazimika kuyahudumia makundi badala ya Watanzania, na kwetu sisi kilicho muhimu siyo Zitto, Dr. Slaa, Mh. Mbowe, n.k. kuwaona mmojawapo akiwa Rais, bali ni kujiuliza kuwa huyo atakayekuja kuwa Rais ataleta kitu gani kipya kiutawala, kimfumo, kisera, kiutendaji na katika usimamizi wa majukumu ya serikali. Na kama tunataka hilo, ni lazima tofauti yake ianze kuonekana kuanzia kwenye mfumo wa upatikanaji wa wagombea wenyewe. Taratibu wanazozishabikia akina Kigwangala ndiyo zilizotuzalishia viongozi wa namna ya sasa, viongozi ambao wameshindwa kutoa matumaini kwa watanzania, na kubakia kuwa watumwa wa makundi yaliyowapeleka kwenye utawala.
 
Sina tatizo na Zitto kuwa mgombea wa CHADEMA au mwananchi yeyote lakini siungi mkono nguvu kubwa anayotumia kuwaaminisha watu kuwa yeye ndiye pekee mwenye uwezo huo. Tamaa yake kubwa inanipa mashaka makubwa. Je, tamaa hiyo yote dhamira yake ni kuwatumikia Watanzania au ni nia ya kufikia tamaa yake ya kimaisha. Angalizo ni kuwa watu wanaoyapenda sana madaraka, hawajawahi kuwa viongozi bora, na kuna wakati walipoyapata waligeuka kuwa madikteta, kiasi cha kukataa kuondoka madarakani baada ya muda wao kwisha.
 
Naikumbuka hotuba ya Hayati Mwalimu Nyerere pale UDSM kwenye kongamano la "Hatma ya Uongozi wa Afrika', akimjibu aliyemwuliza, 'ni nini sifa za kiongozi mzuri', mwalimu alimjibu akinukuu maneno ya Mwanafasafa mmoja, 'kiongozi mzuri ni mwanafalsafa lakini tatizo la wanafalsafa ni kuwa hawapendi kuwa viongozi mpaka walazimishwe, matokeo yake ni kuwa wengi wa wanaoutaka uongozi huwa ni wale wasiofaa'. Kwetu Watanzania, baada ya kupitia kwenye uongozi wa kila aina ambao umeshindwa kuleta tija, inabidi tujiulize, 'Je, ni nani miongoni mwetu afaaye kuwa kiongozi, hata kama hataki kuwa kiongozi, tumwombe/tumlazimishe awe kiongozi wetu', maana wengi wa hawa wautakao uongozi wanautaka kwaajili ya utukufu wao. Na tumewaona wengine wakitamka wazi kuwa Urais ni wa kwao na familia zao, na katika hilo hawana ubia na mtu mwingine, maana yake ni kuwa hawana ubia na Watanzania, wakati ukweli ni kuwa uongozi unastahili kuwa wa Umma, siyo wa mtu au kikundi cha watu, wabia wakuu wa uongozi wowote ulio makini lazima wawe wale unaowaongoza.
 
Bart

From: RICHARD MGAMBA <rmgamba2000@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, September 29, 2012 8:01 AM
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
Nadhani ndugu zangu ama mnamuonea Zitto au mna matatizo naye binafsi. Kuna tatizo ghani katika chama na nchi ambayo watu wanaheshimu demokrasia kwa Mbunge kutangaza mapema kwamba hatawania ubunge tena? Napata shaka na maneno muda muafaka, maana yanatumika vibaya.

Hakuna muda maalumu kwa mtu kutangaza kwamba atagombea au hatagombea ubunge au urais wa nchi. Huu ni uoga ambao Chadema na wafuasi wake wameurithi kwa chama tawala ambacho kwa hofu ya kumeguka hasa baada ya vyama vingi kuingia, kikaweka vikwazo.

Mfano hapa Kenya, wagombea wa Urais wanajulikana hata miaka minne kabla ya uchaguzi mkuu na hakuna shida maana inatoa Mwanya kwa umma kuwachunguza kwa kina ili kuona kama wanafaa au la. Hata ubunge ni hivyo hivyo, sasa unashangaa sana hapa Tanzania, Zitto kutangaza kwamba hatagombea tena, inakuwa karopoka au katenda dhambi.

 Okay tuamini kwamba anayo nia ya kugombea urais kupitia chama chake kama umri utakuwa unaruhusu, kwani tatizo ni nini? Si mumuache aweke jina ili apambane na akina Dr Sla katika mchakato wa urais, akishindwa basi na kama akishinda yote heri. Ni kwa nini chama kama Chadema ambacho kinaamini katika demokrasia ya kweli, wafuasi wake wahofie na hata kumchukia mwanachama anayetaka kutumia haki yake ya kikatiba kugombea nafasi fulani katika chama?

Mgombea urais wa Chadema anapatikanaje? 

Kuweni wakweli. Zitto siyo malaika, na ni kiongozi kijana toka upinzani ambaye hata kupanda kwake pia kulikinufaisha Chadema hivyo inatia shaka kuona anatukanwa, kubezwa na kubambikizwa tuhuma bila ushahidi eti kwa sababu tu katangaza kwamba hatagombea tena ubunge? Wasi wasi wenu ni nini?

Kama ana mpango wa kuhama kwani yeye ndiye Chadema? Akihama Chadema inakufa? 

Chadema walikataa kumtambua rais wa Tanzania, Zitto akamtambua, akalaaniwa lakini baadaye wabunge wa Chadema wakatinga ikulu kuzungumza na mtu wasiyemtambua kuhusu katiba ya nchi na hatimaye wakampelekea majina ya kuchagua watu watakaokuwa katika tume ya katiba mtu yule yule ambaye hawajawahi kumtambua!

Chadema ni chama kinachokua kwa kasi lakini kinakoswa umakini katika mikakati yake na mwishowe utakuwa ni kama vyama vilivyotangulia. Chukulia mfano wa Mwanza, ambako sasa chama kinapoteza nafasi muhimu sana na huenda ikawa ndiyo Mwanzo wa kutoa mwanya tena kwa CCM iliyokuwa imekufa huko kujijenga upya.

Muacheni Zitto afanye siasa zake na watu wake wa Kigoma...Kama hagombei, Chadema waanza mkakati wa kuchagua mtu wa kutetea jimbo mapema.

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, September 28, 2012 10:29 PM
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
Nimeipokea kisawasawa. Mimi nkokotoa tangu huyu jamaa apande chati baada ya kuadhibiwa na Bunge kwa sababu alifaya kosa kweli lakini kwa kuwa watu walishaichoka serikali wakaamua kumshangila mhalifu. Afterall alifanya kosa akitetea UKWELI. Hii ilimpandisha chati kiasi CHADEMA nikafikiri lazima iende naye kwa tahadhari maana watu wamemshangilia kama waJerumani walivyombeba Hilrer. Mtu aliyemuelewa Hitre mapema angekuwa na busara kunyamaza kuliko kusema. Zito ni mbunge mzuri nami naamini sitashangaa asipopewa wizara 2015 kama CHADEMA itashinda. N awakitaka kumpa lazima wapate ushauri kutoka TAKUKURU.

--- On Fri, 9/28/12, gm26may@gmail.com <gm26may@gmail.com> wrote:

From: gm26may@gmail.com <gm26may@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, September 28, 2012, 12:18 PM

ElisaPokea Saluti yangu nikiwa mguu sawa
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Fri, 28 Sep 2012 12:15:35 -0700 (PDT)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
 
Nanukuu kutoka Zanzibar Kwetu  '------Tuliwahi kusema huko nyuma na tunasema tena na leo pia, kuwa…"Chadema inabidi iyakabili kijitu kizima matatizo ya huyu kijana, bila ya Zitto kudhibiti mdomo wake, chama ambacho kinategemewa na wengi to form the next government in the country will slowly and surely bleed again to an ignominous defeat in 2015!".
 
Kwa muda mrefu mimi naamini CHADEMA wanajitahidi kujitenga ka tabia za Zitto. Kila mtu anajua aliyeropoka ni Zitto si CHADEMA. Angekuwa Slaa, Mbowe hata Tundu Lisu ingekuwa rahisi kufikiri CHADEMA imeropoka. Ila kwa Zitto, labda zamani zile.
 
Nafikiri kwa muda mrefu hisia kuwa Zitto kanunuliwa zinaweza kuwa zimewaingia 'wapangaji' wa CHADEMA. Na kama bado nitafikiri basi sio chama makini. Kama tayari basi ni kweli pia wanakwenda naye kwa tahadhari wakijitofautisha na upuuzi anaoweza kuufanya. Yesu aliwazuia wahudumu wa shamba kuwa magugu mengine wasiyang'oe yasije yakang'oka na Ngano. Sijasema Zito ni Gugu. Atakayesema sitapinga.  --- On Fri, 9/28/12, John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com> wrote:

From: John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, September 28, 2012, 11:18 AM

"Ni kweli kuwa hakuna makosa kwa mwanachama wa chama chochote kile kutangaza nia ya kugombea 
nafasi yoyote ya chama hata ya urais, lakini unapotangaza kuwa na ubunge pia hutogombea wakati hujui 
kama chama chako kitakuchagua wewe au vipi, inatia shaka sana kuwa kuna kitu nyuma ya pazia".   
http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/09/mhe-zitto-aropokwa-tena_7278.html
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment