Friday, 28 September 2012

[wanabidii] Kitabu cha lazima kwa Walimu, Watunga sera , Waandishi wa vitabu, Wahariri na Wanaithibati.

Kitabu cha lazima kwa Walimu, Watunga sera , Waandishi wa vitabu, Wahariri na Wanaithibati.

Lipi ni jina sahihi la chombo kinachosimamia maendeleo katika ngazi ya kata? Je, ni KAMATI YA MAENDELEO YA KATA (Ward Development Committee) au "HALMASHAURI" YA MAENDELEO YA KATA -Ward Development Council? Je, ni kweli katika mfumo wa serikali za mitaa Tanzania kuna halmashauri katika ngazi ya kata? kama haipo kwanini inafundishwa mashuleni?

Je, ni kweli cheo cha Katibu Tarafa (Divisional Secretary) bado kipo au kilibadilishwa? na kama kilibadilishwa ni toka lini na kwa nini? Je, sasa kinaitwaje? Je, Hansard za Bunge na hata sheria zinasemaje juu ya cheo hiki? je, vitabu vya kiada vinaendana na mabadiliko haya?

Je, ni kweli Wenyeviti wa vijiji ni wajumbe kwenye vikao vya Baraza la Madiwani (FULL COUNCIL) kama ambavyo inafundishwa katika shule za msingi na sekondari?

Je, unajua kuwa shirika la Umoja wa Mataifa la GATT - General Agreement on Tariffs and Trade liliuliwa na kuzikwa tangu mwaka 1995 na nafasi yake kuchukuliwa na WTO- Ward Trade Organization? je, kwanini hadi sasa karibu miaka 20 waandishi wa vitabu vya kiada na ziada nchini Tanzania bado wanalitaja katika orodha ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kama shirika hai wakati ni mfu?

Hivi ni kweli UNICEF ni kifupisho cha United Nations "International" Children "Education" Fund kama ambavyo vitabu vyetu vya kiada vinatuelekeza?

Je, nembo yetu ya taifa inafundishwa kwa usahihi? yale mazao mawili chini ya bibi na bwana vipi, mbona kuna hadithi nyingi tofauti tofauti kwenye vitabu vya kiada? mara Chai na Kahawa, mara Kahawa na Pamba mara Karafuu na Pamba na vyote vinaithibati. Loo! hadi unachoka. Mpiga Chapa wa serikali ambaye ndiye mwenye dhamana ya nembo yetu tukufu anaiondoaje hii sintofahamu? Soma barua aliyomwandikia mtafiti: Huruma K. Joseph (0768590418)
Haya na mengine mengi yanapatikana kwenye kitabu cha ajabu kinachoitwa - 40 BIG LIES IN CIVICS FOR TANZANIA SCHOOLS ambacho kipo madukani na kinapatikana kirahisi sana amazon kwa kubofya kiunganishi hiki hapa chini.

http://www.amazon.com/dp/B009GDDBJY

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment