Mtoto kuoa mama yake mzazi. Kwa mtazamo wangu, ni kwa sababu tu kesi hii imetoka katika vyombo vya habari kutokana na maendeleo ya habari. Lakini, kesi hizi zipo na huenda ni nyingi Tanzania. Hii ni toto yake tuu. Mfano-kuna makabila ambapo baba akifariki na akiwa na wake wengi, mtoto wa kiume wa kwanza anamrithi mke mdogo (wa mwisho wa baba) ambaye si mama yake (Hehe, Bena etc). Wapo wale ambao mke hurithiwa na ndugu wa mume apende asipende bila ya kuangalia tahadhari ya maambukizi ya ukimwi na other hereditary diseases zenye kuleta uendelezo wa vilema. Zipo mila za makabila ya kumsafisha mume au mke mfiwa ili aweze kuoa au kuendelea na ngono katika jamii. Pamoja na elimu ya afya inayotolewa pamoja na Ukimwi kuwepo watu wanausugu na tamaa. Kuoana binamu kwa baadhi ya makabila kunaendelea. Mtoto wa baba mkubwa na mdogo au shangazi na mjomba na udugu mwingine wa karibu kwa baadhi ya African tribes, wahindi na Waarabu waliomo nchini. Unaweza ukakuta mfarakano wa ndoa lakini ukakuta wazee hao bado wapo pamoja kwa sababu ni binamu wapo pamoja wanatunzwa na watoto na wajukuu na ndugu wengine kwa sababu hana pa kwenda bado hapo ni kwao anyway. Tunakuta kesi hizi katika tafiti mbali mbali nchini. Cha kushangaza nilichokiona kijiji kikubwa kimojawapo cha South Pare, kijana Graduate wa Engineering UDSM aliyelelewa na kaka yake baba mmoja na mama mmoja kaka huyo alikuwa ameoa. Kaka alifariki ghafla ktk ajali ya gari lakini alikuwa na maduka, mashine za kusaga, mashamba, nyumba nzuri nyingine kapangiza na mali nyingine-magari. Kijana aliitwa kusimamia mali za kaka yake na kutakiwa kumrithi huyo shemeji yake ambaye hasa ni mama yake kwa kumlea toka awe mdogo mpaka anamaliza chuo kikuu uinjinia. Shinikizo la ndugu wa mke kuwa mama huyo akubali kurithiwa na mtoto aliyemlea lilitokana na kuwa mali hiyo ataikosa akikataa kurithiwa. Ndugu wa mume walikataa mali kugawiwa wakitaka mke arithiwe mali ibaki kwao. Mfiwa alirithiwa bila ridhaa yake kwa lazima alilia kilio ambacho hakikusikilizwa akarithiwa. Mara baada ya kurithiwa akazaa nae mtoto wa uzeeni (middle age) kijana wake ambaye alikuwa ahami nyumba ya mke huyo (Shemeji yake) akiwa na wivu wa kupindukia. Story zao za kijana kufagia uwanja na kumlinda huyo mama kwa wivu wa hali ya juu zilitufanya watafiti tuitembelee nyumba hiyo wakati wa utafiti wa 'Maisha ya wanawake wa Tanzania wa umri wakati (40-55 yrs The Female Life Cycle- WRDP Study funded by SAREC). Utafiti ulianzia kuhoji watoto wa kike na kiume ili kulinganisha wa umri wa miaka 9-13; 14-19; 20-24; 25-39; 40-55; 56-64; 65+. Tumekuta pia vijijini akina mama lea (watu wazima, vibibi) ambao wanaishi na vijana wadogo waliochetuka kwa bangi maisha yakawashinda. Prostitutes wakishindwa maisha mijini na yupaisha mijini na wanaumwa hoi wakirudi kijijini hudakwa na vibabu ambao wana nyumba, miji na mashambamba ambapo yeye hupana nafuu ya maisha lakini vibabu vinamalizika kwa maambukizo. Yeye anaona kapata ndogodogo wa kujionyesha naye. Utafiti wetu ulihoji watu mambo mengi ya maisha pamoja na walianzaje ngono na mtu wa aina gani, maisha yao ya ndoa na malezi ya watoto na changamoto wazipatazo. Utafiti huu kwa old age women 65+ years, ulionyesha vituko ambavyo sitaki nimalize kurasa hapa ila ni kusema, kuwa-kuna mengi katika jamii yetu hatuyachunguzi au hatuyaelewi na kukubali kuwa yapo yanatokea hata kama tunayaona. Hizi mila za mibaba wa umri wa miaka 40-90years+ kuoa katoto ka miaka 12-15 ni kitu gani hiki ambacho bado kinaendelea huyu si mwanae. Bado akina mama walioolewa nae wanayatazama. Hii ni kuongeza matatizo ya Cancer za vagina (Vulva) na cervix kwa akina mama kwa hizo fungus na virus za kupeana. Yapo mengi yasiyofaa pamoja na masuala yasukumwayo na ushirikina ya zinaa batili. Bado hayo ya ushoga ambayo yapo karne nyingi. Watu na akili zao, elimu na fedha zao wam, wameoa, wanafamilia, wanasali sana katika mahekalu lakini wamewapangia chumba/nyumba shoga (mwanaume mwenzie kama mkewe) . Ipo inaendelea humu bongoland. Hii ya Songea ya mama na mtoto kuoana kutokana na Wosia wa Baba ni mtoto tu wa tukio. --- On Wed, 8/29/12, Avitt Riwa <avittr@yahoo.com> wrote:
|
Sunday, 9 September 2012
Re: [wanabidii] Fw: MTOTO AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI - SONGEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment