Thursday, 2 August 2012

[wanabidii] Re: MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA

Nilipomwona Zitto anachakarika kutafuta sahihi za kumwondoa WM Pinda
madarakani wakati yeye kama Waziri Mkuu hakuwa na kosa nikadhani hali
kama hiyo ikimtokea Zitto atajiuzulu mara moja bila kusubiri ushahidi
unaothibitika! Kumbe Zitto mwenyewe hayuko hivo. Kuna nini cha mno
kwenye uenyekiti wa POAC? Kiongozi wa UMRI wa Zitto hapaswi
kung'ang'ania madaraka ambayo ni ya kupewa tu.

On Aug 2, 10:45 am, Felix Mwakyembe <fkye...@gmail.com> wrote:
> Neville,
>
> Nakushukuru sana kwa uchambuzi wako wa kina, unaotokana na uelewa wako uso
> shaka wa mambo ya Bungeni, wengi tunajadili kishabiki, tena kwa maslahi ya
> itikadi ya vyama na sio maslahi ya mapana ya taifa!!
>
> Tangu awali natoa angalizo hapa kuhusu mjadala huu unavyoelekezwa watu
> tuamini kwamba Zitto yuko innocent ila kina Prof Muhongo ndio wakosefu.
>
> Katika suala la chanzo chake cha taarifa, niulize, ni mwandishi gani wa
> habari anaye mu expose source wake!!!!
>
> Tuvute subira mambo yote yataeleweka!!!
>
> 2012/8/1 Neville Meena <nevill...@gmail.com>
>
>
>
>
>
>
>
> > Wakuu,
> > Kwanza kuna mambo ambayo sikubaliani na Zitto katika taarifa yake.
>
> > 1. Kwamba Zitto aliwatafuta Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
> > Muhongo na Katibu Mkuu,    Eliakimu Maswi akawakosa zinatia shaka. Zitto
> > akiwa Mbunge, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na zaidi ya yote,
> > Mwenyekiti wa POAC hawezi kushindwa kuonana watu hao, ikiwa kweli
> > aliwahitaji. Nimekuwa mwandishi wa habari pale Bungeni,
> > mawaziri wanapatikana kwa urahisi, si kwa wabunge wenzao tu hata kwa watu
> > wengine wanaowahitaji wakiwamo waandishi wa habari. Labda awe wazi kwa
> > kusema kwamba wamekuwa wakimkimbia.
>
> > 2. Suala kwamba alitaka kuwauliza kuhusu taarifa alizopata kwa mwandishi
> > wa habari aliyemfuata kumhoji kuhusu tuhuma za rushwa, nalo linatia shaka.
> > Kama taarifa alizipata kwa mwandishi huyo, basi alipaswa kuwatafuta
> > wahusika (Muhongo na Maswi) kwa gharama zozote kabla ya kwenda kwenye media
> > na kuwataja. Zitto alitumia kigezo gani kuamini kwamba mwandishi
> > aliyemfuata kweli aliambiwa na Maswi na Muhongo kwamba yeye amehongwa? Kama
> > yeye anavyolalamika kwamba anasingiziwa au anatuhumiwa bure, basi naye
> > ameingia katika mtego wa kuwatuhumu watu wengine bila hata kusikia kutoka
> > kwao (kwa maneno ya kuambiwa).
>
> > 3. Nimekuwa Dodoma kwa wiki sita nikiripoti habari za Bunge (bunge la
> > bajeti), na wakati suala hili likishika kasi nilikuwa huko bado. Kwamba
> > baadhi ya wabunge walihongwa, siyo suala la uzushi, ni kweli walihongwa
> > hata kama hakuna ushahidi wa kuwapeleka mahakamani. Kwamba wawakilishi wa
> > kampuni za mafuta waliotumia fedha, ni kweli walikuwapo na fedha
> > zilimwagwa. Kama walikuwa na haki ya kisheria (na wanaamini hivyo) kwanini
> > walikuwa wanamwaga fedha kiasi hicho?
>
> > 4. Kinachosababisha Zitto na POAC yake kutuhumiwa ni uharaka waliokuwa nao
> > kutaka kuihoji Bodi ya Tanesco baada ya Mhando kusimamishwa kazi. Kwamba
> > kamati ya Kisekta ya Nishati na Madini ndiyo ilipaswa kuwa ya kwanza
> > kuguswa na hatua hiyo, lakini POAC wakawa wa kwanza kiasi cha kuomba idhini
> > ya Spika kushughulikia suala ambalo kwa mtizamo wa haraka halikuwa lao bali
> > la kamati nyingine.
> > Lakini pia, Mhando alisimamishwa kazi wala hakufukuzwa, uchunguzi
> > unaendelea, kwanini POAC wasisubiri uchunguzi ufanywe ili matokeo yaonekane
> > na badala yake wanataka kuingilia kazi ya Serikali inapomshughulikia mtu
> > wake?
>
> > 5. Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imepewa wajibu wa
> > kulifanyia jambo hili. Na pili kuna watu ambao Mbunge wa Singida Mashariki,
> > Tudu Lissu aliwataja kwa majina (Zitto si mmoja wao). Ni kitu gani
> > kinachomsukuma Zitto kutoa maelezo mengi kuhusu tuhuma ambazo kimsingi
> > hazijajadiliwa wala kufikishwa na kusikilizwa katika chombo chochote rasmi?
>
> > 6. Mwisho niseme wazi kwamba, mimi nikiwa mwandishi wa habari za Bunge
> > POAC ni moja ya kamati ambazo mara kadhaa zimetuhumiwa kwa rushwa, si sasa
> > katika sakata la Tanesco pekee, bali hata siku zilizopita. Tofauti ya sasa
> > ni kwamba tuhuma hizi zimevuma sana kuliko ilivyokuwa awali. Inawezekana
> > tuhuma hizi si za kweli au ni za kweli. Huu ni wakati mzuri wa POAC
> > kujisafisha baada ya uchunguzi kufanywa, wasubiri matokeo.
>
> > 2012/8/1 RICHARD MGAMBA <rmgamba2...@yahoo.com>
>
> >> Rugambwa nakubaliana nawewe asilimia mia—lakini hata wanao mtuhumu watoe
> >> ushahidi pia ikiwemo mali zake alizopata kwa wizi au jinsi alivyohongwa na
> >> makampuni ya mafuta yaliyokoswa tenda siyo ngojera za hapa na pale.
>
> >> In this case the burden of proof lies to Zitto's accusers. They should
> >> come with concrete evidence above just mere allegations or wishful thinking.
>
> >> --- On *Wed, 8/1/12, Chacha Mairi <chachama...@gmail.com>* wrote:
>
> >> From: Chacha Mairi <chachama...@gmail.com>
>
> >> Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI
> >> YA TUHUMA ZA RUSHWA
> >> To: wanabidii@googlegroups.com
> >> Date: Wednesday, August 1, 2012, 3:20 AM
>
> >> Pole kijana Zitto! Nakutakia safari njema katika kutetea rasilmali za
> >> Taifa letu dhidi ya wachumia tumbo. Namfahamisha Dada Monica Malle
> >> kuwa; Kijana alikuwa anamfuta Waziri Mohongo na Katibu Mkuu wake Maswi
> >> kwa njia ya simu ili wathibitishe tuhuma dhidi yake ama kukanusha, na
> >> bila maelezo yao yangekuwa recorded kupitia simu ya Kijana Zitto au
> >> control room ya mtandao husika na hivyo kuleta ushahidi usiotia shaka
> >> mbele ya jamii.
>
> >> Na bila shaka Waheshimiwa hao waliibaini mbinu hiyo ndo maana
> >> wakakwepa kuwasiliana naye! Hata mimi naamini katika kweli, na kweli
> >> siku zote hubaki kweli na kuendelea kujitetea kama kweli daima.
>
> >> Bila shaka Watanzania wenye nia njema na mapenzi mema na nchi
> >> wataendelea kushikamana kwa kuomba dua ili wachumia tumbo washindwe na
> >> kulegea milele; Amina.
>
> >> On 8/1/12, Laurean Rugambwa <rugam...@hotmail.com<http://mc/compose?to=rugam...@hotmail.com>>
> >> wrote:
>
> >> > Dear Richard,Nikuunge mkono wewe  kwa maelezo yako hapo chini..Ila
> >> nitoe tu
> >> > angalizo:lazima hapa wote tuwe sober, nchi hii mimi nimeisha kosa imani
> >> na
> >> > kila mtu. Maana ufisadi uko kila kona hata huwezi jua umwamini nani, sio
> >> > hata rafiki yako!! kwahiyo tuwe makini na kuwaunga watu mikono bila
> >> kuwa na
> >> > facts.  Mh. Zitto Kabwe, amekuwa "akitajwa tajwa" mtaani na tuhuma za
> >> rushwa
> >> > na ukwasi usiolingana na umri wake sio tu kwenye hili la TANESCO.
> >> > Inawezekana sio kweli kama alivyobainisha hapo chini. Lakini, he need to
> >> > come clean, what is his business interest? what does he own and how he
> >> owned
> >> > them/it..  Maana yeye ni public figure na ana ushawishi mkubwa sana wa
> >> > kisiasa. He need to have impeccable integrity. I am also aware of the
> >> > conspiracy theories which might have been planted to taint him.
> >> Everything
> >> > and anything is possible. We are not out of the woods yet. Kuna
> >> waanasiasa
> >> > wa chama pinzani na chake  na Zitto waliwahi kusema watampa vitu
> >> anapenda
> >> > ili wamteke bila yeye kujua.  Hilo nalo tuliangalie kwa makini. Monica:
> >> > Maswi ni katibu mkuu sio naibu waziri. Kwenye hii horror movie,
> >> tutayajua
> >> > mengi! we are staying tuned,kila la heri,LR
>
> >> >  Date: Wed, 1 Aug 2012 05:05:55 -0700
> >> > From: rmgamba2...@yahoo.com<http://mc/compose?to=rmgamba2...@yahoo.com>
>
> >> > Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE
> >> DHIDI YA
> >> > TUHUMA ZA RUSHWA
> >> > To: wanabidii@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com>
>
> >> > Mambo,
> >> > I like your quote, "Time is the best judge".
>
> >> > --- On Tue, 7/31/12, flano mambo <flei...@yahoo.com<http://mc/compose?to=flei...@yahoo.com>>
> >> wrote:
>
> >> > From: flano mambo <flei...@yahoo.com<http://mc/compose?to=flei...@yahoo.com>
>
> >> > Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE
> >> DHIDI YA
> >> > TUHUMA ZA RUSHWA
> >> > To: "wanabidii@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com>"
> >> <wanabidii@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com>
>
> >> > Date: Tuesday, July 31, 2012, 11:44 PM
>
> >> > Mh Zitto maelezo yako yanashawishi kuaminiwa, la muhimu kazeni kamba tu
> >> > maana kama ni njama mbona ni muda kitambo tu mambo yote yatakua
> >> hadharani
> >> > maana "time is
> >> >  the best judge"
>
> >> >         From: Monica Malle <monina...@hotmail.com<http://mc/compose?to=monina...@hotmail.com>
>
> >> >  To: Wanabidii googlegroup <wanabidii@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com>
>
> >> >  Sent: Wednesday, August 1, 2012 2:30 PM
>
> >> >  Subject: RE: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE
> >> DHIDI
> >> > YA TUHUMA ZA RUSHWA
>
> >> > Pole Mh. Zito nimekupata na kukuelewa maelezo yako.
>
> >> > Ila nasikitika wewe kushindwa kuwasiliana na Mh. waziri Mhongo na naibu
> >> wake
> >> > Mh. Maswi.
>
> >> > Umesema umewatafuta kwenye simu hawapatikani kwani si mko wote hapo
> >> Dodoma?
> >> > kwanini usiwatafute mkaongea uso kwa uso? ili wakupe jibu la uhakikika
> >> kama
> >> > wao ndio walisema wewe ndio unahusika na rushwa?
>
> >> > From: kerezesia_mukaluga...@hotmail.com<http://mc/compose?to=kerezesia_mukaluga...@hotmail.com>
> >> > To: wanabidii@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com>
>
> >> > Subject: RE: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE
> >> DHIDI YA
> >> > TUHUMA ZA RUSHWA
> >> > Date: Wed, 1 Aug 2012 10:38:55 +0000
>
> >> > Pole mwanangu Zito. Lakini songa mbele hadi kieleweke! Husikatishwe
> >> tamaa
> >> > kamwe! Mimi,  hata kabla sijakutana nawe uso kwa uso  jana asubuhi  hapa
> >> > Dodoma na kupata maelezo yako yaliyoniridhisha kabisa, niliisha kuwa na
> >> > hisia kuwa  kuna mchezo ulikuwa unachezwa  wenye lengo la kuwaaminisha
> >> > Watanzania  kuwa eti CCM na Chadema vyote ni vyama vya wachumia
> >> tumboni  kwa
> >> > sawa sawa kabisa. Juhudi  zilikuwa zinafanywa kuwaaminisha  Watanzania
> >> kuwa
> >> > walikuwa wanaangaika bure kutafuta uongozi mbadala wa nchi yetu kutoka
> >> > kwenye safu ya viongozi wa kitaifa wa Chadema kama wewe. Lengo pana
> >> > limekuwa
> >> >  kuwakatisha
> >> >  tamaa   Watanzania, hasa vijana wa rika lako na rika  chini yako, kwa
> >> > kuwaonesha   kuwa eti CCM walau ilikuwa ina akina
>
> ...
>
> read more »

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment