Thursday, 2 August 2012

RE: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA

Mh. Dr. Kigwangallah,

Maelezo yako yamekaa vizuri.. Nimekuwa nifuatilia mchango wako hapa ukumbini, unajua kutoa hoja, unaona mbali na mimi ni mdau wa maendeleo kwenye jimbo lako wewe na Mh. Zedi.. Nyinyi ni tumaini la kuwakomboa wana Nzega. Fanya hilo kwa moyo wote bila kujali nani kaleta hoja.. maana lazima ujiulize ulienda bungeni kuwakilisha CCM au wana Nzega?

 

Kukiwa na wabunge kama ninyi, wasio waoga, wasio wachumia tumbo, wasiopokea rushwa za wapiga kura toka kwa wagombea wa Afrika mashariki, nchi itabadilika.

 

Nimependa umesema, ila endelea kusema, ulisemee bungeni hata kama wanakutoa kama rafiki yangu Mh.Faustine  Ngulile kwa kutetea wanyonge wa kigamboni.

 

Nyingi kama vijana, msiwazomee wenzenu wanaotetea maslahi ya wanyonge,  maana sisi wananchi tunawaona na kusema jamani, hawa vipi? Naomba tu msikate tamaa, msifanye siasa za maji taka, bado mna muda kwenye siasa, na wewe unajua kuliko wote kuwa kwa mwanasiasa, you dont need to prove anything just allege and it sticks!  throw any mud, it will stick, It is bad! Mathalani, waziri wa mambo ya ndani aende na helicopter ya polisi kwao Songea uonge vumbi lake, lakini IGP anaweza akaenda nayo shamba  au akaenda kuzika rafiki na jamaa na hakuna wa kumuuliza!!

 

Mzee hizo ndio siasa, na wala tusiseme ni za bongo, ni kote duniani.  When you are politician it is not what you have done, it is lying about what you have done. That is who gets what and when at work.

 

Shida mimi naona si vema kumchafua mtu makusudi, with aforethought malice, hiyo sio siasa ni character assassination. Si haki, si sawa, sio ustaarabu. Ni ushenzi wa kutokuwa na hoja. Na afanyaye hivo hafai kuwa kiongozi, ana hila, he is deceptive and conniving politician and usually corrupt! hana moral fiber and character.

 

Nyinyi hapa namaanisha vijana wote kuanzika 48 years hadi kwa yule wa 24 kijana wa NCCR Mageuzi kule Kibondo, tetea maslahi ya nchi., Tetea wafanyakazi juu hii sheria mpya ya kuwataka watu walipwe mafao yao ya hifadhi za jamii wakiwa na miaka 55 wote tukijua kuwa unemployment is hitting the roof. More people are into informal sectors ambazo hazilipi social securities.

 

Tuendelee kuona hii sinema inaishaje,mie niliibatiza horror movie!

 

kila la heri,

LR

 


 

Date: Thu, 2 Aug 2012 00:20:23 +0300
Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA
From: hkigwangalla@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Mimi nilitamani bajeti ya Nishati na Madini ipite kwa sababu binafsi nilikuwa nimejenga imani kubwa, na bado ninayo imani hiyo, kwa uongozi wa juu wa wizara hiyo, lakini kwa hakika sikupenda ipite at the peril of other's future ambitions...hatuwezi kuwa na kizazi cha viongozi makini kama tukiwa tunahukumiana bila kufuata misingi ya kidemokrasia na hata ha kutoa haki ya msingi kama kusikilizwa, kujitetea n.k. Kama ilivyokuwa nilivyohukumiwa mimi wakati wa sakata la madaktari, bila hata kusikilizwa, ndivyo leo hii kamati ya nishati na madini ilivyohukumiwa, ndivyo leo hii Ndg. yangu Selemani Jumanne Zedi (ambaye alianza vizuri kazi yake hiyo mpya) alivyopoteza matumaini ya kuonesha uwezo wake wa kiuongozi akiwa hata hajakaa vizuri kwenye kiti chake, ndivyo alivyohukumiwa ZZK, ndivyo alivyohukumiwa Sarah Msafiri, Munde Tambwe na wengine. Leo hii nilikuwa naongea na ndg yangu Yussuf Abdallah Nassir (Korogwe) akaniambia yeye wala hakuwa amehudhuria kikao hata kimoja tangu mgogoro huu uanze, lakini naye jana amechafuliwa na Mhe. Tundu Lissu...

Mara ya mwisho tuliwawajibisha mawaziri bila kuwapa fursa ya kusikilizwa. Nikakumbuka nilivyoshughulikiwa na wengi wa hao mawaziri (wakati wa sakata la madaktari) na jinsi walivyokuwa wakirukaruka na  kushangilia huku wakigonga meza kwamba eti adui yao namba moja amekamatwa leo, amebanwa, na wakipeana nafasi mmoja baada ya mwingine kunishughulikia...kinyume chake mimi sikufurahia wao ilipokuwa zamu yao kunyolewa badala yake niliandika barua kwa wakubwa kuomba watoe fursa ya mawaziri wetu kujitetea ili tuujue ukweli ndipo tuwatake wenye tuhuma watolewe...lakini sikusikilizwa, na mawaziri walimwaga unga! Bila shaka leo hii Mhongo na wenzake wanasherehekea ushindi, lakini najua siku si nyingi hawa hawa wanaowasherehekea leo ndiyo watakuwa watoaji na wasimamizi wa hoja ya kuwataka wawajibike! wanatakiwa wawe makini sana, ahadi nzuri walizotoa wazitekeleze na tuombe mungu alete mvua umeme usikatike, mgao usiwepo! 

Ubakaji wa haki za msingi za wenzetu umeendelea kushamiri na huku ukipigiwa vigelegele na makofi na wengi miongoni mwetu kwa kinga ya kile kinachoitwa uzalendo 

Mimi nasikitikia mfumo wetu wa kufanya maamuzi hususan ya kumchafua mtu! ama kummaliza mtu kisiasa!

Hiki ndi kilio changu...inatia kichefuchefu kabisa 

Wakatabahu,
HK.

2012/8/1 Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>
Wanabidii wenzangu

Kijana Zito kapatikana na sasa anaweweseka.  Mchecheto wote wa nini kama ni mtu safi?.  Mimi ni kati ya watu ambao ninaamini kuwa huwenda kijana Zito alishaonja asali na dalili zote zinaonyesha labda uchunguzi umuokoe lakini hata kama hatapatikana na hatia kutokana na uchunguzi ni kuwa suspicion tu peke yake ya mbunge muadilifu ni mwanzo wa kuwajibika. Ningekuwa mimi ni Zito ningechukua hatua za kujiuzulu kwani hana tena udhu wa kuwa mbunge. Kwa kifupi kachafuka na ninamuomba angalie dhamira yake na utu wake kwani siasa sio mwanzo na mwisho wa maisha.

Pole sana lakini kwa mazingira ya siasa zetu na bunge letu hakuna msafi hata mmoja.

Tutafakati

Herment


Date: Wed, 1 Aug 2012 21:53:38 +0300

Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA
From: nevilletz@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com


Wakuu,
Kwanza kuna mambo ambayo sikubaliani na Zitto katika taarifa yake.
 
1. Kwamba Zitto aliwatafuta Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu,    Eliakimu Maswi akawakosa zinatia shaka. Zitto akiwa Mbunge, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na zaidi ya yote, Mwenyekiti wa POAC hawezi kushindwa kuonana watu hao, ikiwa kweli aliwahitaji. Nimekuwa mwandishi wa habari pale Bungeni, mawaziri wanapatikana kwa urahisi, si kwa wabunge wenzao tu hata kwa watu wengine wanaowahitaji wakiwamo waandishi wa habari. Labda awe wazi kwa kusema kwamba wamekuwa wakimkimbia.
 
2. Suala kwamba alitaka kuwauliza kuhusu taarifa alizopata kwa mwandishi wa habari aliyemfuata kumhoji kuhusu tuhuma za rushwa, nalo linatia shaka. Kama taarifa alizipata kwa mwandishi huyo, basi alipaswa kuwatafuta wahusika (Muhongo na Maswi) kwa gharama zozote kabla ya kwenda kwenye media na kuwataja. Zitto alitumia kigezo gani kuamini kwamba mwandishi aliyemfuata kweli aliambiwa na Maswi na Muhongo kwamba yeye amehongwa? Kama yeye anavyolalamika kwamba anasingiziwa au anatuhumiwa bure, basi naye ameingia katika mtego wa kuwatuhumu watu wengine bila hata kusikia kutoka kwao (kwa maneno ya kuambiwa).
 
3. Nimekuwa Dodoma kwa wiki sita nikiripoti habari za Bunge (bunge la bajeti), na wakati suala hili likishika kasi nilikuwa huko bado. Kwamba baadhi ya wabunge walihongwa, siyo suala la uzushi, ni kweli walihongwa hata kama hakuna ushahidi wa kuwapeleka mahakamani. Kwamba wawakilishi wa kampuni za mafuta waliotumia fedha, ni kweli walikuwapo na fedha zilimwagwa. Kama walikuwa na haki ya kisheria (na wanaamini hivyo) kwanini walikuwa wanamwaga fedha kiasi hicho?
 
4. Kinachosababisha Zitto na POAC yake kutuhumiwa ni uharaka waliokuwa nao kutaka kuihoji Bodi ya Tanesco baada ya Mhando kusimamishwa kazi. Kwamba kamati ya Kisekta ya Nishati na Madini ndiyo ilipaswa kuwa ya kwanza kuguswa na hatua hiyo, lakini POAC wakawa wa kwanza kiasi cha kuomba idhini ya Spika kushughulikia suala ambalo kwa mtizamo wa haraka halikuwa lao bali la kamati nyingine.
Lakini pia, Mhando alisimamishwa kazi wala hakufukuzwa, uchunguzi unaendelea, kwanini POAC wasisubiri uchunguzi ufanywe ili matokeo yaonekane na badala yake wanataka kuingilia kazi ya Serikali inapomshughulikia mtu wake?
 
5. Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imepewa wajibu wa kulifanyia jambo hili. Na pili kuna watu ambao Mbunge wa Singida Mashariki, Tudu Lissu aliwataja kwa majina (Zitto si mmoja wao). Ni kitu gani kinachomsukuma Zitto kutoa maelezo mengi kuhusu tuhuma ambazo kimsingi hazijajadiliwa wala kufikishwa na kusikilizwa katika chombo chochote rasmi?
 
6. Mwisho niseme wazi kwamba, mimi nikiwa mwandishi wa habari za Bunge  POAC ni moja ya kamati ambazo mara kadhaa zimetuhumiwa kwa rushwa, si sasa katika sakata la Tanesco pekee, bali hata siku zilizopita. Tofauti ya sasa ni kwamba tuhuma hizi zimevuma sana kuliko ilivyokuwa awali. Inawezekana tuhuma hizi si za kweli au ni za kweli. Huu ni wakati mzuri wa POAC kujisafisha baada ya uchunguzi kufanywa, wasubiri matokeo.


2012/8/1 RICHARD MGAMBA <rmgamba2000@yahoo.com>
Rugambwa nakubaliana nawewe asilimia mia—lakini hata wanao mtuhumu watoe ushahidi pia ikiwemo mali zake alizopata kwa wizi au jinsi alivyohongwa na makampuni ya mafuta yaliyokoswa tenda siyo ngojera za hapa na pale.

In this case the burden of proof lies to Zitto's accusers. They should come with concrete evidence above just mere allegations or wishful thinking.

--- On Wed, 8/1/12, Chacha Mairi <chachamairi@gmail.com> wrote:

From: Chacha Mairi <chachamairi@gmail.com>

Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, August 1, 2012, 3:20 AM

Pole kijana Zitto! Nakutakia safari njema katika kutetea rasilmali za
Taifa letu dhidi ya wachumia tumbo. Namfahamisha Dada Monica Malle
kuwa; Kijana alikuwa anamfuta Waziri Mohongo na Katibu Mkuu wake Maswi
kwa njia ya simu ili wathibitishe tuhuma dhidi yake ama kukanusha, na
bila maelezo yao yangekuwa recorded kupitia simu ya Kijana Zitto au
control room ya mtandao husika na hivyo kuleta ushahidi usiotia shaka
mbele ya jamii.

Na bila shaka Waheshimiwa hao waliibaini mbinu hiyo ndo maana
wakakwepa kuwasiliana naye! Hata mimi naamini katika kweli, na kweli
siku zote hubaki kweli na kuendelea kujitetea kama kweli daima.

Bila shaka Watanzania wenye nia njema na mapenzi mema na nchi
wataendelea kushikamana kwa kuomba dua ili wachumia tumbo washindwe na
kulegea milele; Amina.

On 8/1/12, Laurean Rugambwa <rugambwa@hotmail.com> wrote:
>
> Dear Richard,Nikuunge mkono wewe  kwa maelezo yako hapo chini..Ila  nitoe tu
> angalizo:lazima hapa wote tuwe sober, nchi hii mimi nimeisha kosa imani na
> kila mtu. Maana ufisadi uko kila kona hata huwezi jua umwamini nani, sio
> hata rafiki yako!! kwahiyo tuwe makini na kuwaunga watu mikono bila kuwa na
> facts.  Mh. Zitto Kabwe, amekuwa "akitajwa tajwa" mtaani na tuhuma za rushwa
> na ukwasi usiolingana na umri wake sio tu kwenye hili la TANESCO.
> Inawezekana sio kweli kama alivyobainisha hapo chini. Lakini, he need to
> come clean, what is his business interest? what does he own and how he owned
> them/it..  Maana yeye ni public figure na ana ushawishi mkubwa sana wa
> kisiasa. He need to have impeccable integrity. I am also aware of the
> conspiracy theories which might have been planted to taint him. Everything
> and anything is possible. We are not out of the woods yet. Kuna waanasiasa
> wa chama pinzani na chake  na Zitto waliwahi kusema watampa vitu anapenda
> ili wamteke bila yeye kujua.  Hilo nalo tuliangalie kwa makini. Monica:
> Maswi ni katibu mkuu sio naibu waziri. Kwenye hii horror movie, tutayajua
> mengi! we are staying tuned,kila la heri,LR
>
>  Date: Wed, 1 Aug 2012 05:05:55 -0700
> From: rmgamba2000@yahoo.com

> Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA
> TUHUMA ZA RUSHWA
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Mambo,
> I like your quote, "Time is the best judge".
>
> --- On Tue, 7/31/12, flano mambo <flein47@yahoo.com> wrote:
>
> From: flano mambo <flein47@yahoo.com>

> Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA
> TUHUMA ZA RUSHWA
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Tuesday, July 31, 2012, 11:44 PM
>
> Mh Zitto maelezo yako yanashawishi kuaminiwa, la muhimu kazeni kamba tu
> maana kama ni njama mbona ni muda kitambo tu mambo yote yatakua hadharani
> maana "time is
>  the best judge"
>
>         From: Monica Malle <moninaike@hotmail.com>
>  To: Wanabidii googlegroup <wanabidii@googlegroups.com>
>  Sent: Wednesday, August 1, 2012 2:30 PM

>  Subject: RE: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI
> YA TUHUMA ZA RUSHWA
>
>
>
>
>
>
> Pole Mh. Zito nimekupata na kukuelewa maelezo yako.
>
> Ila nasikitika wewe kushindwa kuwasiliana na Mh. waziri Mhongo na naibu wake
> Mh. Maswi.
>
> Umesema umewatafuta kwenye simu hawapatikani kwani si mko wote hapo Dodoma?
> kwanini usiwatafute mkaongea uso kwa uso? ili wakupe jibu la uhakikika kama
> wao ndio walisema wewe ndio unahusika na rushwa?
>
>
>
>
>
>
>
> From: kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com

> Subject: RE: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA
> TUHUMA ZA RUSHWA
> Date: Wed, 1 Aug 2012 10:38:55 +0000

>
>
>
>
> Pole mwanangu Zito. Lakini songa mbele hadi kieleweke! Husikatishwe tamaa
> kamwe! Mimi,  hata kabla sijakutana nawe uso kwa uso  jana asubuhi  hapa
> Dodoma na kupata maelezo yako yaliyoniridhisha kabisa, niliisha kuwa na
> hisia kuwa  kuna mchezo ulikuwa unachezwa  wenye lengo la kuwaaminisha
> Watanzania  kuwa eti CCM na Chadema vyote ni vyama vya wachumia tumboni  kwa
> sawa sawa kabisa. Juhudi  zilikuwa zinafanywa kuwaaminisha  Watanzania kuwa
> walikuwa wanaangaika bure kutafuta uongozi mbadala wa nchi yetu kutoka
> kwenye safu ya viongozi wa kitaifa wa Chadema kama wewe. Lengo pana
> limekuwa
>  kuwakatisha
>  tamaa   Watanzania, hasa vijana wa rika lako na rika  chini yako, kwa
> kuwaonesha   kuwa eti CCM walau ilikuwa ina akina Mh Prof Tibaijuka,  Mh
> Magufuli na sasa Mh Prof Muhongo wenye kuwa wachapa kazi. Madudu kama ya
> mikataba ya mke wa bosi wa TANESCO aliyeondolewa na kampuni ya mke wake  na
> taarifa  za  bosi  huyo waliomteua juzi juzi wao wenyewe kuleta eti misumari
> toka Uingereza vilipenyezwa kwa mbwembwe  kubwa  katika mjadala wa bosi yule
> kukataa kuburuzwa kuhusu ufuataji wa sheria na kanuni za manunuzi  lengo
> likiwa  kuwapandisha hasira Watanzania na hivyo kuwaondolea bugudha ya
> kutafakari  kwa kina na kwa utulivu madudu makubwa  zaidi kama mabilioni
> yanayolipwa kwa kukodi mitambo ya Symbion aka Dowans aka Richmond n.k ..
>
> Hata pale viongozi wetu wapendwa wanapopindisha sheria na kanuni  Watanzania
> wanaimizwa kutowasumbua  kwa kuwauliza maswali maana tabia ya kuuliza
> maswali wapendwa wetu si tabia yenye staha na kukosa shukrani eti, ahaha!!!
> Hawa hawa waliokuzomea ulipodhubutu kusema tununue mitambo ya Dowans huko
> nyuma kuepuka kuingia giza leo wameinunua mitambo hiyo hiyo baada ya kuigia
> hasara maradufu  ya kesi ya tozo... Si mitambo hiyo hiyo ndiyo hii ya eti
> Symbion? ... Kama alivyosema Prof Goran Hyden Watanzania tulitakiwa kusema
> bila kufikiri sana kuwa heri zimwi tukujualo: yaani CCM daima, ahaha!!!Pole
> mwanangu Zito. Lakini songa mbele hadi kieleweke!!!Watanzania waongeze nguvu
>  katika juhudi zao za  kuagaika kutafuta uongozi mbadala wa nchi yetu kutoka
> kwenye safu ya viongozi wa kitaifa wa Chadema kama wewe. Na viongozi,
> wanachama, na wapenzi wa Chadema,  jahazi lililobaki  lenye uwezo
> wakuwavusha Watanzania kufanikisha ukombozi wa Watanzania awamu ya pili
> tuzidishe mshikamano!
> Mwl. Lwaitama
>
>
> Date: Wed, 1 Aug 2012 12:34:24 +0300
> Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA
> TUHUMA ZA RUSHWA
> From: mglady2@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> I Love this! Ukweli na Uhakika-Mungu yuko nawe Mhe Zitto na tunakuombea
> daima wale wenye nia mbaya na wewe Mungu atawadhihirisha mapema sana na
> kweupe bado giza Halijaingia!
>
>
>
>
> 2012/8/1 Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
>
>
> MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN
> KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
> Ndugu Waandishi,
> Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la
> kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika
> vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
> Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote
> zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.
> Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima
> imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi
> wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia
> zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu
> juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi
> yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya
> vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa.
> Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa
> kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:
>
>   Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na
> hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi
> wa rushwa;
>   Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya
> vyombo vya habari  zikidai ''Zitto kitanzini'' ama ''Zitto sawa na popo
> nundu''  zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na
>   Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi
> kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha
> iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.
> Ndugu Waandishi,
> Naomba kutoa ufafanuzi wa hicho kinachoelezwa kwamba nina ushiriki katika
> masuala ya rushwa hususan kwenye masuala yanayohusu sekta ya Nishati na
> Madini:-
>
> Mara baada ya bodi ya Wakurugenzi ya  Shirika la Usambazaji wa Umeme
> Tanzania (TANESCO) chini ya Uenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Robert
> Mboma kutangaza kwamba imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo,
> Nd. William Mhando ili kupisha uchunguzi wa baadhi ya vitendo/mwenendo wake,
> Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ambayo mimi ni Mwenyekiti wake
> ilimuandikia Mhe. Spika kumuomba aridhie ili Kamati iweze kuwaita Bodi ya
> TANESCO, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali  (CAG) na pia
> Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kujiridhisha na tuhuma zote
> zinazotajwa zinafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa;
> Kamati ya POAC ninayoiongoza ilimuomba Mhe. Spika kuwaita wahusika tajwa kwa
> kuwa zilikuwapo tetesi kuwa kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi huyo siku
> chache kabla ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kulikuwa na lengo la
> kufunika 'madudu' makubwa zaidi kwa kulichagiza Bunge na tukio hilo dogo,
> mkakati ambao naona umefanikiwa sana. Isitoshe, Kamati kutaka kujiridhisha
> na hatua za Bodi ni sehemu ya msingi ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati
> yaliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na pia Shirika la
> TANESCO ni moja kati ya mashirika ambayo yanawajibika kwetu kwa hesabu zake
> na pia ufanisi wake kwa ujumla. Tumefanya hivyo pia katika mashirika
> mengine, hili la TANESCO sio tukio la kipekee;
> Kitendo hiki cha halali na kwa mujibu wa Kanuni kilichofanywa na Kamati
> yangu  kimetafsiriwa kwa makusudi na baadhi ya watu kwamba ni ishara ya kuwa
> sisi au zaidi kwamba mimi nina maslahi binafsi na TANESCO na hususan
> Mkurugenzi wake Injinia Mhando, ndio maana tumetaka maelezo ya Bodi. Ukweli
> kwamba Kamati ya POAC tumewaita pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu
> (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa jambo hilo hilo
> umefichwa kwa makusudi!
> Baada ya  tukio hilo, nikiwa hapa Dodoma, mwandishi wa habari wa gazeti moja
> alinifuata akiniambia kuwa wamekutana na Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu
> wake, Nd. Eliachim Maswi hapa hapa Bungeni na wamewaambia kuwa mimi nimepewa
> rushwa. Hakutaja nimepewa rushwa na nani, kiasi gani na wala kwa lengo
> gani!
> Nimejaribu kumtafuta kwa simu Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake ili
> wanipe ufafanuzi juu ya mimi na Kamati ya POAC kuhusishwa na tuhuma hizi
> bila mafanikio, hali ambayo inaniondolea mashaka juu ya ushiriki wao katika
> kueneza au kuthibitisha uvumi huo. Najaribu sana kujizuia kutokuwa na
> mashaka na ushiriki wao huo ikizingatiwa uzito na taswira ya nafasi zao
> katika jamii, lakini wameshindwa kunidhihirishia tofauti.
> Sasa naomba kutoa ufafanuzi rasmi kuhusu mlolongo wa matukio hayo tajwa
> ambayo yanatumiwa na baadhi ya wanasiasa kuonesha kwamba eti nimehusika na
> vitendo vya rushwa.
>
> Binafsi sijawahi kuwa na mawasiliano ya aina yeyote na uongozi wa TANESCO
> kushawishiwa juu ya hatua ambazo POAC ndio imezichukua za kutaka
> kujiridhisha juu ya utaratibu uliotumika. Ieleweke wazi kabisa kuwa, hakuna
> wakati wowote, popote ambapo mimi binafsi au Kamati yetu imekataa Mkurugenzi
> Mkuu wa TANESCO kuchunguzwa kwa tuhuma zozote. Ambacho tumesisitiza wakati
> wote ni ufuatwaji wa taratibu, kanuni na sheria, hili nitalisimamia iwe
> masika au kiangazi;
>
> Ni kwa sababu hiyo, na kwa kujiamini kabisa nimeunga mkono suala la tuhuma
> za rushwa zinazotajwa zichunguzwe na Kamati ya Haki, Maadili na  Madaraka
> ya  Bunge kwa kina;
>
> Nimekwenda mbali zaidi kukiomba chama changu CHADEMA kifanye pia uchunguzi
> na tathmini yake kwa kina kujiridhisha na tuhuma hizo;
>
> Natumia fursa hii pia kuomba vyombo vya Dola vichunguze tuhuma hizo kwa
> nafasi yake ili kuweza kupata ukweli;
>
> Ninaahidi kushiriki kikamilifu iwapo nitatakiwa katika uchunguzi wowote
> utakaofanywa na niko tayari kuwajibika iwapo nitakutwa na hatia yeyote.
> Napenda niwatoe hofu wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini walionituma kuja
> kuwawakilisha hapa Bungeni na Watanzania wote kwa ujumla kwamba:-
>
> Mimi Zitto Zuberi Kabwe sina bei, sijawahi kuwa nayo na sitarajii kuwa nayo
> huko mbeleni. Daima nimesimamia kidete maadili ya uongozi bora katika maisha
> yangu yote ya siasa, na nawaahidi sitarudi nyuma katika mapambano dhidi ya
> rushwa katika nchi hii pamoja na mikakati ya aina hii ya kunidhoofisha na
> kunivunja moyo;
>
> Nafarijika na salam mbali mbali zinazotolewa kunifariji na kusisitiza kuwa
> nisilegeze kamba katika mapambano haya, nimepokea ujumbe mwingi kwa simu,
> sms, tweeter na hata facebook na niko pamoja nanyi Watanzania wenzangu kamwe
> sitarudi nyuma hadi kieleweke. Naamini katika nchi yetu tunazo rasilimali za
> kutosha mahitaji/haja ya kila mmoja wetu lakini si 'tamaa/ulafi' wa baadhi
> ya watanzania wenzetu;
>
> Napenda kuweka rekodi sawa kwa Watanzania kwamba nimekuwa Mbunge hiki ni
> kipindi cha pili, Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya
> Umma (POAC) huu ni takriban mwaka wa saba sasa, Kamati yangu inasimamia
> mashirika 259 ya Umma na si TANESCO peke yake. Mchango wa Kamati hii katika
> Bunge na kwa ustawi wa Mashirika ya Umma ni bayana na haujawahi kutiliwa
> shaka. Kamati yetu imeokoa upotevu mkubwa wa mali za umma na kuokoa fedha za
> umma kutokana na umakini wake. Tumefanya hivyo CHC hivi karibuni, Kiwira na
> kwenye mashirika mengine mengi. Kote huko uadilifu na uzalendo wa Kamati hii
> haujawahi kuhojiwa. Inatuwia vigumu kuona kuwa tunahojiwa katika suala hili
> la TANESCO. Hapa pana kitendawili.
>
> Zipo hoja pandikizi za kutaka Kamati ya POAC ivunjwe na haswa zikinilenga
> mimi binafsi. Nafahamu kiu ya wasioitakia mema nchi yetu kuiona POAC
> ikivunjwa au sura zikibadilishwa kwa kuwa Kamati hii imekuwa mwiba kwa
> mikakati yao ya kifisadi. Kwa maoni yangu, Kamati ya POAC isihusishwe na
> tuhuma hizi kwa vyovyote vile. Niko tayari nihukumiwe mimi kama mimi na sio
> kuhusisha wajumbe wengine ambao hawatajwi mahala popote katika tuhuma hizi
> mbaya sana katika historia ya Bunge letu. Nitakuwa tayari kunusuru Kamati ya
> POAC na maslahi ya taifa letu kwa kujiuzulu Uenyekiti iwapo itathibitika
> pasipo shaka kuwa nimehongwa. Kamati ya POAC ni muhimu zaidi kuliko mimi.
>
> Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana
> Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui
> kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
>
> Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo
> mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa.
>
> Ni lazima tufike mahali kama viongozi kwamba utaratibu unapokiukwa na yeyote
> yule, au uongo unapotolewa hadharani tuseme bila kuogopa. Hili ndio jukumu
> letu kama wabunge na viongozi. Kusimamia ufuatiliaji wa utaratibu ni jukumu
> letu kama Kamati ya POAC na ndio sababu ya msingi ya kuanzishwa kwa mamlaka
> kama CAG na PPRA. Haiwezekani, tuwe na set ya kanuni kwa kundi fulani na
> nyingine kwa makundi mengine, au kuhukumu ufuataji wa taratibu kwa kuangalia
> sura ya mtu usoni
> Mwisho
> Kumejengeka tabia hivi sasa ya kuwamaliza wanasiasa wenye kudai uwajibikaji
> na uzalendo. Kumeanzishwa kiwanda kwenye medani ya siasa cha kuzalisha
> majungu na fitna zenye lengo la kuwachonganisha wanasiasa wa aina hiyo na
> wananchi kwa kutumia vyombo vya habari na nguvu ya fedha. Naamini mbinu hizi
> chafu, kama nyingine nyingi zilizojaribiwa kwangu huko nyuma nazo
> zitashindwa.
> Naamini katika kweli na kweli daima huniweka huru. Naamini kuwa mwale mdogo
> wa mwanga wa mshumaa hufukuza kiza. Kwa imani hiyo, sitasalimu amri mbele ya
> dhamira zao ovu hata nitakapobaki peke yangu katika mapambano hayo ya
> kulinda na kutetea rasilimali za taifa zinufaishe watanzania wote.
> Daima nitaongozwa na busara ya Hayati Shabaan Robert isemayo, 'Msema kweli
> huchukiwa na marafiki zake, nitakapofikwa na ajali hiyo, sitaona wivu juu ya
> wale wawezao kudumu na marafiki zao siku zote, siwezi kuikana kweli kwa
> kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale
> uwongo utakapojitenga".
> Ahsanteni sana.
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone
>  posting
>  to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of
> his or her postings, and hence statements and facts must be presented
> responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and
>  Guidelines.
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>                         
>
>
>
>
> --
>
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
>                         
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
        +255 - 753 - 555556
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment