Monday, 1 December 2014

[wanabidii] Wito wa kushiriki katika Tamasha la 34 la sanaa na utamaduni, Bagamoyo

TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
(TaSUBa)

WITO KWA WASANII NA VIKUNDI KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA 34 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO LITAKALOFANYIKA KUANZIA TAREHE 21 – 27 SEPTEMBA, 2015


Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo inapenda kuwakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa
kwa ujumla kuomba kushiriki kwa kufanya maonyesho kwenye tamasha la 34 la kimataifa la
sanaa na utamaduni Bagamoyo ambalo litafanyika chuoni (TaSUBa – Bagamoyo) kuanzia
tarehe 21 - 27 Septemba 2015.

Tamasha hili limekuwa na malengo mbalimbali kama vile kuendeleza na kudumisha utamaduni
wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa wasanii na vikundi vya Tanzania
na mataifa mengine kupitia warsha na maonyesho mbalimbali.

Kauli mbiu ya tamasha hili ni 'Sanaa na Utamaduni katika Uchaguzi Huru na Amani'.
Tamasha hili hujumuisha aina mbalimbali za sanaa kama vile Ngoma, Maigizo, Muziki,
Sarakasi, Mazingaombwe, Vichekesho n.k pamoja na maonyesho ya sanaa za ufundi
(Exhibitions).

TaSUBa inawakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na
nchi za nje ili kuweza kushiriki katika tamasha hili kongwe la sanaa na utamaduni wa Mtanzania.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia;
Barua pepe: bagamoyofest@gmail.com
Tovuti: www.tasuba.ac.tz
Namba za Simu: +255(0) 754 310 425, +255(0) 655 840 405 na +255(0) 713 297 626

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment