Monday, 1 December 2014

[wanabidii] TIDO MHANDO AAJIRIWA AZAM MEDIA.

Kampuni ya Azam Media Limited, leo
imetangaza kuwa Tido Mhando ameteuliwa
kuwa kaimu-Mkurugenzi mtendaji, Uhai
Production Ltd.(UPL).
Tido, anaungana na Rhys Torrington ambaye ni
Mkuregenzi Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd
na mtangazaji huyo maarufu wa mpira zamani
nchini, Mhando ataanza majukumu yake mara
moja, ikiwa jukumu lake kubwa ni utengenezaji
na uboreshaji wa vipindi vya kitanzania katika
televisheni na redioni.
Mhando mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 40
kwenye tasnia ya utangazaji na Uandishi wa
Habari, ni mtu anayejulikana na kuheshimika
katika tasnia hiyo ukanda wa Afrika Mashariki
na Ulimwenguni kote.
Tido Mhando sasa wa Azam TV
Alianza kazi kama DJ Radio Tanzania na
mnamo mwaka 1985 alijiunga na BBC idha ya
Kiswahili Nairobi kama mwandishi wa habari.
Ukuwaji wake ndani ya shirika ulimpelekea
kuhamishiwa jijini London mwaka 1991 ambapo
aliteuliwa kuwa Mwafrika wa kwanza kuongoza
idara ya Idhaa ya Kiswahili BBC. Baada ya
kurejea Tanzania, Mhando ameshika nyadhifa
mbali mbali za juu zikiwemo Mkurugenzi Mkuu
wa TBC na hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa
Mwananchi Communication Ltd.
Akizungumzia uteuzi wake, Mhando amesema;
"Ninayo furaha kubwa kujiunga na Azam
Media, pia na changamoto kubwa zilizopo
mbele yetu kuifanya kuwa kampuni pekee ya
Televisioni na Redio yenye ubora katika kutoa
burudani hapa nchini (Tanzania) pia na ukanda
wote wa Afrika,".
Mhando ofisi zake zitakuwepo katika jengo la
kisasa la Uhai Production Tabata, Dar es
salaam. UPL inajulikana kwa ubora wake katika
kurusha matangazo yake moja kwa moja kama
vile, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
pamoja na vipindi vingine maarufu kama Kwetu
House na Morning Trumpet.
Pia katika wiki zijazo UPL itazindua studio zake
mpya zenye kiwango cha kimataifa ambazo
zitamuwezesha Mhando kuwa na uwezo
mkubwa wa kutengeneza vipindi mbali mbali
vyenye viwango vya kimataifa akishirikiana na
watengenezaji wazawa
Akizungumzia uteuzi huo, Muingereza
Torrington amesema: "Tunayo faraja kubwa
kwa Tido kujiunga nasi wakati tunakaribia
kutimiza mwaka wetu wa kwanza tokea tuanze
kutoa huduma, inanipa furaha kwamba Azam
TV imekuwa kwa kasi na kuwa wasambazaji
wakuu na watoa huduma bora satellite Pay Tv
Tanzania,".
"Kwa uzoefu wake nategemea Tido
atachukuwa jukumu la kutupeleka katika hatua
nyingine ya mafanikio kibiashara kwa
kutengeneza vipindi na burudani mbali mbali
kwajili ya wateja wetu Tanzania na kuvuka
mipaka yetu. Na mtakia kilala kheri katika
majukumu yake mapya," amesema.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment