Monday, 29 December 2014

[wanabidii] TATHMNI YANGU BINAFSI KUHUSU SIKU YA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI.

TATHMNI YANGU BINAFSI KUHUSU SIKU YA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI.
Kuanzishwa kwa kundi hili kumechangiwa pamoja na mambo mengine kuguswa kwa waanzilishi wake na matukio ya kutisha ya ajali yaliyowahi kutokea katika nchi hii tena kwa kuongozana. Ajali nyingi zinapotokea watu wengi wamekuwa wakijiuliza hivi chanzo ni nini? au nini kifanyike? lakini wengine wamekuwa wakinyoosha vidole tu kwa askari wa usalama barabarani kwamba wamekuwa wanazembea katika kazi yao. Sisi wenyewe kama wananchi hatujawa mstari wa mbele katika kuhakikisha ajali zinakwisha nchini au kupungua kwa kasi kubwa. Na ndio maana sio ajabu kuona watu wakimshabikia dereva anayeendesha kwa kasi mbaya au mwendo hatarishi barabarani. Watu humshangilia dereva anayefika mwisho wa safari mapema sana kabla ya muda. Abiria mara nyingine huungana na dereva au kondakta kuwashambulia kwa maneno askari waliolisimamisha basi kwa lengo la kuonya au kukagua jambo fulani kwa madai kuwa wanacheleweshwa, lakini abiria hawa hawa ikitokea ajali huwa wa kwanza kusema dereva akienda mwendo kasi. Binafsi naamini kuwa ajali katika nchi hii zitapungua sana iwapo abiria watajengewa uwezo kuweza kudhibiti vitendo vya madereva wao, zitabaki zile ajali ambazo tu zinatokana na mechanical fault ya gari au ubovu wa njia au hali ya barabara mathalani utekelezi nk
Juhudi za kundi hili zilipoanza watu wengi walibeza au wengine walitusalimu kwa maneno ya kejeli, wengine kutupachika majina ya usalama barabarani, au hata kuitwa Kamanda Mohammed Mpinga ilhali tu kuoinesha kwamba ukiwa mstari wa mbele kuhamasisha usalama barabarani ati unaingilia kazi ya kamanda Mpinga au jeshi la polisi kwa ujumla. Mtazamo huu ni hasi kwani inapotokezea ajali hafi wala kuumia askari au kamanda Mpinga au Johansen Kahatano wanaokufa ni ndugu zetu, watoto wetu, shangazi mjomba, dada, kaka na sisi wenyewe. Je, ikiwa kila mtumiaji wa njia atafanya juhudi kuhakikisha njia zinakuwa salama kwa yeye mwenyewe kubadili tabia kisha kubadili tabia za wenzake je, rate ya ajali itakuwa hii iliyopo sasa? Kwa kweli jukumu hili si la polisi ni la sisi wote kama watumiaji. Concept ya road safety ambassadors hapa nchini ndio inaonekana mpya lakini ipo katika nchi nyingi tu ambapo wananchi wanajitolea kuhakikisha usalama barabarani.
Kundi hili inabidi lijipambanue na kujionesha miongoni mwa jamii kama consumer group ambazo kama zilivyo CCC za EWURA, SUMATRA nk hili pia liwe CCC ya masuala ya barabarani. Kundi linapaswa kuinfluence policy and legislative changes at the same time behavioral changes and community sensitization and awareness to road safety issues.
Tumefanikiwa sana, tangu pale tulipoanza na Asina A Omari Fredrick MbomaJuma KibachaJohn SekaEmmanuel Kihaule na Possi Abdallahna mimi mwenyewe hadi kufikia wanachama 700 sasa. Tunadhani idadi hii iongezeke zaidi na community outreach campaign iwe kubwa zaidi.
Kila mwana kundi hili ajue anao wajibu wa walau mara moja au mbili kwa wiki kuingia humu na kupost kitu au kuchangia mjadala wowote unaoendelea humu. The group must remain active and not dormant.
Ni jukumu letu kuongeza members, picha, matukio na kusuggest offline activities, lakini lililokubwa ni kujitolea. Tuchukue mifano toka penginepo ili kusaidia kubioresha utendaji wa jeshi la polisi. Tuwafichua madereva wenzetu waovu, tuwafichue polisi waovu, na tujikosoe sisiw wenyewe. Tujielimishe na tuelimishane na mwisho tuwe proud of our group.
Kundi hili litoke hapa na kufika hatua ya kutambulika na mamlaka za nchi kiasi tuweze kushiriki mikutano na forum nyingi zaidi. Taaluma ya kila mmoja wetu hapa ilete positive changes to road safety issues.
Tusikatishwe tamaa na yeyote atayeonesha kutubeza. Tushikamane na daima tusonge mbele.Asanteni sana

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment