Ndugu zangu,
Wasadikika hawaishiwi maajabu. Katika dunia hii kawaida ni hewa kuzaa hewa. Lakini, kwenye Nchi ya Kusadikika hewa inaweza kuzaa kitu, na Wasadikika wakaamini wanachoambiwa na wenzao akina Sadiki, kuwa hewa imezaa kitu. Wasadikika hufikia hata kushangilia habari hiyo ya ajabu.
Maana, kwenye Sakata la Richmond, Wasadikika, kupitia Bunge lao la Kusadikika, waliunda Kamati Teule yenye hata magwiji wa sheria ndani yake akiwamo Msomi kwa jina la MwenyeKiwembwe.
Mwanasheria MwenyeKiwembe na wenzake wakasafiri mpaka Marekani, kwenye nchi ya watu weledi na wenye nguvu sana duniani. Na ajabu ni kuwa, Kamati Teule ya akina MwenyeKiwembe na wenzake huko Marekani hawakuikuta ofisi ya Richmond wala watendaji wake mitaani,
Mpaka leo, Wasadikika wanajiuliza, hivi inakuwaje Dowans , kutoka huko huko Marekani, waje kwenye Nchi ya Kusadika na kurithi mali za kampuni hewa ya Richmond, halafu Dowans hao hao wapate mrithi mwingine kutoka huko huko Marekani kwa jina la Symbion?
Naam, kwenye Nchi ya Kusadikika Hewa inaweza Kuzaa Kitu...!
Maggid,
Iringa, Mkoa kwenye Nchi ya Kusadikika.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment