Nakubaliana na Hitimisho la makala hii, pengine ukilinganisha vijana wote walio katika umri katik ya 30-40 katika medani za siasa ya Tanzania, Mhe. Zitto ana profile/background ya kipekee. Binafsi napenda namna anavyoutumia utafiti katika hoja zake.
Omary Iddy,DAGROFORESTRY RESEARCH TANZANIA FORESTY RESEARCH INSTITUTE(TAFORI)P.O BOX 1257,SHINYANGATANZANIA.Tel:+255 28 276 3249MOBILE:+255 713 728 672FAX:+255 28 276 2198EMAIL:eidomari@yahoo.com
--------------------------------------------
On Tue, 12/9/14, 'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Zitto Kabwe: Mhanga wa mafanikio yake
To: "Abdalah Hamis" <hamisznz@gmail.com>, wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, December 9, 2014, 1:35 PM
Nakubaliana na sifa zote za
Zitto...lkn UAMINIFU ni shaka sana kwa rafiki yangu huyu
haswa unapozungumzia nafasi ya Rais. na hiyo ndio sifa mama
pia.
Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
ZITTO
Zuberi Kabwe ni mwanasiasa mdogo kiumri lakini mwenye
mafanikio na changamoto nyingi kiuongozi na kisiasa kuliko
umri wake. Katika makala haya tunajadili wasifu wa
mwanasiasa huyu katika maeneo mbalimbali yanayohusu sifa
muhimu za Rais ajaye.
Zitto
alizaliwa tarehe 24 Septemba 1976 katika Kijiji cha
Mwandiga, Wilaya ya Kigoma. Alisoma katika Shule ya Msingi
Kigoma kutoka mwaka 1984 hadi mwaka 1990. Alisoma katika
Shule ya Sekondari Kigoma (1991-1994) na kumalizia katika
Shule ya Sekondari Kibohehe (Moshi) kati ya mwaka 1994 na
1995, akiwa amepata daraja la kwanza (Division
1:8).
Alisoma
katika Shule ya Juu ya Sekondari Galanos (Tanga) mwaka 1996
na kumalizia katika Shule ya Sekondari Tosamaganga (Iringa)
mwaka 1998, akiwa amepata daraja la pili huku akiibuka
mwanafunzi bora katika somo la uchumi katika Mkoa wa
Iringa.
Zitto
ana shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
aliyoisomea kati ya mwaka 1999 na 2003, akiwa amepata alama
3.5 (second upper class). Zitto ana Diploma ya Juu katika
Masoko ya Kimataifa kutoka Chuo cha Inwent-IHK kilichopo
mjini Bonn nchini Ujerumani aliyehitimu mwaka 2004, na ana
shahada ya umahiri katika sheria na biashara kutoka Chuo cha
Sheria cha Bucerius nchini Ujerumani aliyohitimu mwaka
2010.
Mambo
mawili yanajitokeza kuhusu elimu ya Zitto
Mosi,
amesoma vizuri; hii ni sifa muhimu kwa kiongozi wa kisiasa
katika nyakati za sasa kwa sababu elimu ni msingi wa fikra
na falsafa unaohitajika kwa kiongozi kuweza kutoa dira na
ushawishi.
Aidha,
tafiti nyingi zinaonyesha kwamba elimu ni sifa ya kwanza ya
kiongozi miongoni mwa wapiga kura walio wengi nchini
Tanzania.
Pili,
ukichunguza miaka aliyosoma Zitto utaona kwamba amesoma
miaka mingi zaidi kwa elimu ya sekondari na Chuo Kikuu
kuliko ilivyo kawaida.
Hii
ni kwa sababu alipokuwa akisoma Shule ya Sekondari Kigoma
alifukuzwa shule kwa kudaiwa kuwa alianzisha, kuendesha na
kufanikisha mgomo yeye akiwa Kiranja Mkuu. Ndipo akalazimika
kuhamia Shule ya Sekondari Kibohehe mkoani
Kilimanjaro.
Aidha
alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Zitto alilazimika
kurudia mwaka baada ya kusimamishwa masomo kutokana na
kuhusishwa na mgomo wa kupinga sera ya uchangiaji wa gharama
za elimu ya juu.
Alikuwa
ametuhumiwa kuwa alikuwa miongoni mwa viongozi waliochochea
mgomo huo yeye akiwa Mwenyekiti wa wanafunzi waliokuwa
wanakaa Hosteli ya Kijitonyama.
Hii
maana yake ni kwamba 'ukorofi' wa Zitto tunaouona leo
ulianza siku nyingi.
Zitto
amefanya kazi katika maeneo kadhaa kabla ya kuwa mbunge.
Alipata kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Wanafunzi
nchini (TSNP) kati ya mwaka 2001 na 2003.
Na
kabla hajagombea ubunge na kushinda, Zitto alipata kuajiriwa
na Shirika la Ujerumani (FES) kama Meneja wa Miradi kati ya
mwaka 2004 na 2005.
Kiuongozi,
Zitto alikuwa Kiranja Mkuu wakati akisoma Shule ya Sekondari
Kigoma na baadaye kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) kati ya mwaka 2001 na
2003.
Ndani
ya CHADEMA, Zitto alishika nafasi kadhaa za uongozi kabla
'hajakorofishana' na viongozi wenzake. Kwanza, alikuwa
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje mwaka 2004 na wakati huo huo
akiwa pia Mkurugenzi wa Uchaguzi na kampeni wa chama
hicho.
Mara
baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2005, Zitto
alichaguliwa kuwa Katibu wa wabunge wa CHADEMA. Mwaka 2007
alichaguliwa na Baraza Kuu la CHADEMA kuwa Naibu Katibu Mkuu
Bara, nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka jana baada ya
kuondolewa na Kamati Kuu ya chama hicho.
Ndani
ya Bunge, Zitto alipata kuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Kamati
ya Mashirika ya Umma (POAC) na baadaye kuwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Ni katika
kipindi cha uenyekiti wa Zitto, ndipo ambapo kamati hizi
zilijulikana sana kwa jamii.
Kihaiba,
Zitto ana sifa mbili muhimu ambazo ni taswira chanya ya
uongozi lakini wakati huo huo ikiwa ni taswira tata ya
kiuongozi katika mazingira ya kitanzania.
Sifa
ya kwanza ni tamaa na ujasiri wa kupenda kufanya makubwa
ambayo hugeuka kuwa kero kwa baadhi ya viongozi wenzake
anaofanya nao kazi.
Kwa
mfano, akiwa anamaliza muda wake kama Katibu Mkuu wa DARUSO
'alilazimisha' hesabu za taasisi hiyo zikaguliwe na
wakaguzi wa hesabu (auditors) kabla hawajakabidhi ripoti kwa
uongozi mpya.
Hii
haikuwa kawaida ya DARUSO na baadhi ya viongozi wenzake
hawakulipenda jambo hili na wakamnunia.
Zitto
amekuwa kinara wa kuibua 'madudu' mengi serikalini
kuanzia kashfa ya Buzwagi, mabilioni ya Uswisi na sasa
sakata la kashfa ya akaunti ya Escrow.
Pengine,
taswira ya Zitto kuhusu tamaa na ujasiri wa kupenda kufanya
mambo makubwa ni kitendo cha kamati anayoiongoza ya PAC
kuwasweka ndani viongozi wa juu wa TPDC kwa kushindwa
kutekeleza amri ya kamati hiyo.
Bila
kuingia ndani ya sakata hili, ni wazi kwamba hili ni jambo
ambalo lilikuwa halijawahi kutokea huko nyuma na linaweza
likawa limefungua ukurasa mpya katika mahusiano kati ya
Kamati za Bunge na uongozi wa taasisi za umma.
Sifa
ya pili kihaiba kuhusu Zitto ni uvumilivu. Katika maisha
yake ya kisiasa, Zitto amekumbana na misukosuko mingi hasa
kuhusu kashfa mbalimbali zinazomlenga.
Tangu
azozane na viongozi wenzake ndani ya CHADEMA kufuatia uamuzi
wake wa kugombea uenyekiti mwaka 2009, Zitto amekuwa
akirushiwa kashfa mbalimbali zenye lengo la kuchafua taswira
yake kisiasa katika jamii.
Pamoja
na kwamba hakuna hata kashfa moja ambayo imepata
kuthibitishwa kimantiki na kisheria, kashfa hizo
zimefanikiwa kutikisa taswira yake kiuadilifu.
Kifamilia,
Zitto Kabwe hajaoa lakini ana mtoto mmoja wa kiume maarufu
kwa jina la Chachage.
Hili
ni jina alilompa mtoto wake kutokana na mapenzi makubwa
aliyokuwa nayo kwa mhadhiri maarufu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, marehemu Profesa Chachage Seithy Chachage.
Kikazi,
Zitto ana sifa tatu zinazomtenga kwa mbali na wanasiasa
wengi hapa Tanzania. Mosi, Zitto anaamini kikamilifu katika
itikadi, falsafa na sera kama msingi wa uongozi wa
kisiasa.
Katika
kipindi ambacho ujamaa umepoteza mashiko katika Bara la
Afrika, yeye anajipambanua waziwazi kwamba ni mjamaa
akiamini katika falsafa ya Unyerere.
Zitto
anaamini kwamba kijiji ndiyo kitovu cha maendeleo ya
Mtanzania na ni muhimu kuwekeza katika kilimo. Ndiyo
mwanasiasa pekee nchini na pengine katika bara la Afrika
aliyeweza kuisimamia kwa vitendo dhana ya hifadhi ya jamii
kwa mwananchi wa kawaida hadi katika ngazi ya
kijiji.
Ni
kwa sababu hii, amekuwa mwanasiasa wa kwanza barani Afrika
kushinda tuzo ya hifadhi ya jamii. Zitto pia anaamini katika
demokrasia rasilimali kama msingi wa kuwapa wananchi fursa
ya kumiliki na kufaidika na rasilimali za taifa.
Pili,
Zitto anajipambanua kifikra. Hili linajitokeza katika ukweli
kwamba Zitto ni miongoni mwa wananasiasa wachache hapa
nchini wanaosoma sana. Mimi na yeye kila mwisho wa mwaka
huwa tunapeana hesabu kuhusu idadi ya vitabu ambavyo kila
moja wetu amevisoma kwa mwaka huo.
Aidha,
Zitto ni mwandishi mzuri akiwa ni miongoni mwa wanasiasa
wachache kabisa hapa nchini wenye uwezo na utayari wa
kuandika makala. Kwa sababu hii sio kazi ngumu kujua
anachofikiri na kukiamini Zitto kwani fikra zake zipo wazi
kupitia maandishi yake.
Sifa
ya tatu kikazi inayomtenga na wanasiasa wenzake wa upinzani
hapa nchini ni mtandao mpana alionao ndani na nje ya
nchi.
Kwa
hapa nchini, Zitto ni mwanasiasa pekee wa upinzani
aliyeonyesha uwezo wa kufanya kazi na kushirikiana na
wanasiasa wa vyama vingine bila kujali tofauti zao za
kisiasa.
Zitto
ana uhusiano mzuri na viongozi mbalimbali nchini, wakiwemo
viongozi wastaafu wanaoheshimika nchini.
Zitto
ana mahusiano mema ya kikazi na viongozi wa vyombo vya dola
ndani ya Jeshi la Wananchi, Polisi na Usalama. Hii ni sifa
muhimu kwa kiongozi anayejiandaa kuwa mkuu wa nchi na
dola.
Aidha,
Zitto ana mahusiano mema ya kikazi na viongozi mbalimbali
katika bara la Afrika, Amerika, Ulaya na Asia, pamoja na
taasisi za kimataifa.
Hii
nayo ni sifa muhimu kwa kiongozi anayejiandaa kushika
uongozi wa juu wa nchi kwa sababu mafanikio ya kiongozi wa
juu hutokana kwa kiasi kikubwa na mahusiano yake na Jumuiya
ya Kimataifa.
Mafanikio
ya Zitto Kabwe ndiyo pia udhaifu wake, hasa katika mazingira
ya siasa za Tanzania. Kikazi, Zitto anaponzwa na tabia yake
ya kutokuendana na utamaduni wa kimaisha na kisiasa wa
Tanzania.
Kwa
mfano, katika jamii yetu watu wanaofanya kazi kwa bidii sana
hutazamwa kwa jicho lisilo chanya sana. Tangu tukiwa
shuleni, mwanafunzi anayesoma sana hupachikwa majina ya
ajabu ajabu kama vile 'mnoko', ametumwa na kijiji,
'msongo', n.k.
Tukiwa
kazini, watu wanaofanya kazi sana kwa kuzingatia taratibu si
miongoni mwa watu wanaopendwa.
Watu
wa namna hii huonekana kama wanajipendekeza na 'kujifanya
wajuaji' na hivyo hupachikwa majina mbalimbali na hata
kupakaziwa.
Utamaduni
huu pia upo katika siasa na kwa kiasi umemponza sana Zitto
kwani anaonekana kama ni mwanasiasa mwenye kimbelembele kwa
tabia yake ya 'kung'ang'ania' hoja mbalimbali zenye
maslahi mapana kwa jamii na nchi.
Pili,
ukaribu wa Zitto na viongozi wa serikali umefifisha taswira
yake kisiasa kama mpinzani.
Tangu
mfumo wa vyama vingi uanze katika nchi yetu viongozi wa
upinzani wamejitahidi kujenga taswira kwamba wapinzani ni
wakombozi na CCM ni wakoloni weusi.
Kwa
hiyo siasa za upinzani ni siasa za harakati mithili ya
wapigania uhuru enzi za ukoloni.
Kwa
sababu ya taswira hii, kiongozi yeyote wa upinzani anayekuwa
karibu na viongozi wa CCM na serikali kwa uwazi huonekana
kwamba ni msaliti wa harakati za ukombozi.
Kwa
utamaduni wetu wa kisiasa upinzani si ushindani wa hoja kati
ya chama cha upinzani dhidi ya CCM, bali ni harakati za
kumtoa 'mkoloni' mweusi kwa kile kinachoelezwa kwamba ni
ukombozi wa pili.
Eneo
la tatu la udhaifu wa Zitto katika maziingira ya siasa za
upinzani Tanzania lipo katika aina ya siasa
anazofanya.
Wakati
yeye huamini kwamba kazi ya upinzani ni kujenga hoja
mbadala, viongozi wenzake wa upinzani wanaamini kwamba kazi
ya msingi ya upinzani ni kushambulia haiba na matendo ya
viongozi wa chama tawala.
Kwa
sababu ya tofauti hizi za kimtazamo, Zitto amejikuta yupo
mbali kabisa na viongozi wenzake wa upinzani na hivyo
kujikuta kama mtoto yatima akilelewa na walezi wasio
mpenda.
Nilipomuuliza
yeye anaamini ni kwa nini aligombana na viongozi wenzake
ndani ya CHADEMA, Zitto alikuwa wazi kabisa kwamba ilikuwa
ni mapema mno kwa yeye kugombea uenyekiti wa CHADEMA mwaka
2009.
Kwamba
tangu agombee uenyekiti mwaka 2009, wenzake walimuona ni
msaliti na mahusiano yao hayajawahi kurudi katika hali ya
kawaida.
Ni
wazi kuwa Zitto ameshindwa kuenea katika utamaduni wetu wa
kisiasa, ambao hauruhusu ushindani wa kisiasa hasa ndani ya
vyama vya upinzani.
Kiongozi
wa upinzani huongoza hadi pale atakapochoka au kuchokwa sana
na hata pengine atakapoitwa na mola.
Kwa
hiyo Zitto alikuwa 'mjinga' kwa kuamini kwamba angeweza
kupata uenyekiti wa CHADEMA kwa kujaza fomu na hatimaye
kupigiwa kura.
Nami
lazima nikiri kwamba nilikuwa 'mjinga' kwa kumshawishi
na hatimaye kumtia moyo kugombea nikiamini kwamba ushindani
wa kisiasa ndani na baina ya vyama ndiyo msingi na kiashiria
cha kukua kwa demokrasia katika nchi.
Pengine
udhaifu mkubwa wa Zitto kama kiongozi upo katika maeneo
makubwa mawili.
Kwanza,
ni kushindwa kupima maana na matokeo mapana ya kauli zake
kabla hajazitoa. Mara kadhaa Zitto amekuwa akitoa kauli
ambazo huacha ukakasi mkubwa katika jamii.
Kwa
mfano, akiwa katika kampeni za ubunge mwaka 2010 alitangaza
kwamba katika awamu ijayo angerudi kugombea urais na siyo
ubunge tena.
Zitto
alitoa tangazo hili huku akijua kwamba chama chake kilikuwa
na mgombea urais na kwamba kauli kama ile ingeweza kupunguza
imani ya wapiga kura kwa mgombea wa chama chake kwa
kuonyesha kwamba asingeshinda na pengine alikuwa
hafai.
Pili,
baadhi ya kauli za Zitto huonyesha kwamba ni kiongozi
anayechokozeka kirahisi.
Kwa
mfano, alipomwagiwa 'upupu' na Tundu Lissu mapema mwaka
huu kwamba alikuwa amehongwa magari na Nimrod Mkono, Zitto
alitoa kauli ya haraka tata kwamba, yeye asingekufa kama
alivyokufa Chacha Wangwe ("Chacha died, I
won't").
Hii
ni kauli tata kwa sababu inatoa taswira kwamba pengine
Chacha Wangwe hakufa kwa ajali kama inavyojulikana bali
aliuawa na watu ndani ya chama chake.
Pili,
kwamba yeye asingekufa kama Wangwe inaweza kutoa taswira
kwamba Zitto ana nguvu za ziada za kumkinga na
kifo.
Eneo
la pili la udhaifu wa Zitto lipo katika mahusiano ya
kimapenzi yasiyoeleweka kwa mtu mwenye dhamana ya uongozi.
Zitto amekuwa akihusishwa na wasichana kadhaa maarufu hapa
nchini ambao maadili yao kindoa yanatia shaka katika
mazingira ya Kitanzania.
Inapokuja
katika mahusiano ya kimapenzi, Zitto hujisahau kabisa kwamba
yeye ni kiongozi mkubwa katika jamii pamoja na kwamba ana
haki zake kama binadamu.
Pengine
hili ndilo eneo ambalo Zitto ameshindwa kujitofautisha na
wanasiasa wenzake hapa nchini, ambao wengi wao nao uadilifu
wao katika eneo hili ni wa mashaka.
Hitimisho
Zitto
Kabwe ni kiongozi aliyejipambanua kiitikadi, kifalsafa,
kisera na kimsimamo. Husimamia anachokiamini bila kujali
wengine wanaamini nini na watamwonaje.
Ni
miongoni mwa viongozi wachache kabisa hapa nchini
wanaoheshimu kazi za kitafiti na kitaalamu.
Ni
kiongozi mwenye bidii, umakini na weledi katika kazi. Katika
umri wake wa miaka 38, Zitto Kabwe amefanya mambo makubwa
kisiasa na kijamii.
Hoja
zake kuhusu mikataba ya madini zilifanikisha kubadilishwa
kwa sheria ya madini na kwa mara ya kwanza kuifanya nchi
yetu ianze kuambulia angalau mapato kidogo katika sekta
hii.
Pamoja
na sifa alizonazo za kuweza kuwa kiongozi mkuu wa nchi,
Zitto Kabwe hatagombea mwakani kwa sababu za kikatiba.
Pengine hii ni fursa kwa Zitto kuendelea kujipanga zaidi na
kurekebisha baadhi ya maeneo yanayotia doa taswira yake
kiuongozi.
Hata
hivyo, mafanikio ya Zitto kisiasa huko mbele yatategemea
zaidi na aina ya taasisi ya kisiasa atakayofanya nayo
kazi.
Kama
Zitto ataendelea kufanya siasa ndani ya chama chake cha sasa
na viongozi hawa waliopo, hakuna shaka kwamba taswira ya
usaliti itaendelea kushamiri kwa sababu siasa zake
haziendani na utamaduni wa kisiasa wa viongozi wa sasa wa
chama hicho.
Kwa
sababu hii, Zitto Zuberi Kabwe anahitaji kuchukua hatua
nyingine moja kubwa ya kijasiri katika maisha yake ya
kisiasa, ambayo ni kujiunga na chama ambacho ana nafasi na
fursa ya kujenga utamaduni mpya wa kisiasa hapa
nchini.
Makala
hii imeandikwa na Dk Kitila Mkumbo via Raia
Mwema: Zitto
Zuberi Kabwe: Mgombea ambaye hatagombea, mhanga wa mafanikio
yake
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment