Jaaa mmoja alikutana na rafiki yake akaanza kushangaa. Huyu akauliza 'Mbona unashangaa' Jamaa akamwambia nashangaa kukuona maana niliambiwa umekufa. Huyu akasema hapana sikufa. Huyu akasema 'Aliyeniambia namuamini kuliko wewe hawezi kunidanganya'
Katabazi anasema kwa kuwa rais amesema hela zilizoko kwenye acount ya ESCROW si za umma basi sio za umma. Kwa nini? Rais kasema. Huyu mtu ana tatizo gani?
Fedha ziko huko kwa sababu UMMA (kupitia TANESCO) unafikir kuna fedha zake kwa hiyo unasubiri usuruhishi ili (UMMA) upate haki yake. Fedha hizo zimekwapuliwa kabla ya uamuzi kutolewa. Basi kwa kuwa rais kasema wote tunakubaliana naye?
Siku Rais akiamka na kusema moja kwongeza sita ni tisa Katabazi atawashauri wataalamu wa hesabu wabadilishe majibu. Hii kali
--------------------------------------------
On Tue, 12/23/14, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] WALIOMUITA PRO.MUHONGO NI MUHONGO KAMA JINA LAKE AIBU YAO
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, December 23, 2014, 12:08 PM
WALIOMUITA PRO.MUHONGO NI
MUHONGO KAMA JINA LAKE AIBU YAO
Na Happiness Katabazi
WALE wazushi,Visarata Mtaa,Washambenga,wenye nongwa Kama
ndugu wa mume ambao Katika zogo la Escrow,walimu hukumu
Waziri wa Nishati na Madini, Professa Sospiter Muhongo
Kuwa ni Muhongo kama jina lake na kwamba ni
fisadi wa Escrwo Leo hii wameziweka wapi sura zao?
Licha ya Profesa Muhongo kutoa utetezi wake kupitia hotuba
yake ndani Bunge ambapo pamoja na mambo mengine ,msomi Huyo
alisema Fedha za Escrwo siyo za umma watu wakiwemo wanasiasa
uchwara ambao ni wabunge walimpinga na kumuhukumu Kuwa
ni Muongo mkubwa Kama jina lake na kwamba Fedha za a Escrow
ni za umma.
Lakini Jana Baba mwenye nyumba nyumba, Profesa Jakaya
Kikwete katika hotuba yake alikubaliana na Muhongo Kuwa
Fedha zile siyo za umma ni za IPTL na hazijaibwa wala
Kubebwa kwa Magunia Kama Zitto Kabwe wakati akisoma ripoti
ya PAC bungeni alisema Fedha za Escrow zilibebwa kwa Magunia
bila kufuata Taratibu ya Sheria ya Benki Kuu.
Waswahili wanamsemo wao usemao ' Mnafki hafi hadi
ameumbuka'. Hivyo wanafki,Majaji mama DDP ,DCI ,majaji
,Mashushushu wa 'Kichina' ,mabush Lawyer ,wazushi na
mahakimu uchwara ambao mlijipachika majukumu yasiyo ya kwenu
ya kuhukumu Watu na kuwaita wakina Muhongo ni wezi ,wamekula
Rushwa ,wamechota Fedha ya umma ya Escrow hotuba ya
jana imewaumbua.
Naendelea kusisitiza tuache tabia ya kuhukumu au kushabikia
jambo wakati Hatuna vielelezo Vya kutosha Kwani tukae
tukijua uzushi unaumuiza watu wasiyo na hatia Katika baadhi
ya mambo machafu wasiyo yatenda.
Leo hii kila kona watu wamepandikizwa chuki Mbaya sana
ambapo baadhi ya wananchi ambao wao wakisikia jambo hawataki
kilifanya utafiti wanaliamini, wanaamini Muhongo ni fisadi,
kaiba Fedha za Escrow Kumbe ni uzushi tu unafanywa na wahuni
wachache kwa Malengo Yao binafsi.
Narudia tena Kusema naipongeza hotuba ya Jana ya Rais Jakaya
Kikwete Kwani kwa MTu mwenye akili timamu, na aliyekuwa na
kiu ya kutaka kufahamu ukweli kuhusu zogo la Escrow
ametambua ukweli ni upi na Kamati ya PAC inayoongozwa na
Zitto Kabwe kuna baadhi ya mambo iliyopo tosha.
PAC ilipotosha umma Katika ripoti yake ilisema Kiwango Cha
Fedha kilichokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni Sh.Bilioni
306.7. Wakati ukweli ni kwamba kiasi kilichokuwa kwenye
Akaunti ya Escrow ni Bilioni 202.9. PAC ilisema Fedha za
Escrow ni za umma, Rais amewaumbua amesema siyo za umma ni
za IPTL.
Hali iliyosababisha wananchi kuwajengea
Chuki ya wazi wakina Muhongo, Profesa Anna Tibaijuka, Katibu
Mkuu Eliachim Maswi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa
serikali Jaji Fredrick Werema ,CCM na serikali kwa ujumla
Kuwa Si wazalendo kwa taifa na hao PAC na uongo wao Katika
baadhi ya ripoti Yao ambayo imebainika Kuwa na dosari ndiyo
wazalendo wa kweli.
Kwa hotuba ya jana naweza kusema Tibaijuka amepata
hati yenye Mashaka, Muhongo,Maswi wamepata hati safi. Kwa
hiyo Hakuna Ofisa wa serikali aliyetaja hati chafu.
Kamati ya PAC mlipewa Fedha za walipa kodi mkafanyekazi kazi
ya uchunguzi Matokeo yake mmekuja na ripoti ambayo baadhi ya
uchunguzi wake mlikusanya vielelezo Vya uongo ambavyo
viliingiza taifa kwenye zogo. Kama ni Waungwana, Ombeni
radhi kwa watanzania kwa Udhahifu huo ili tuendelee bila
kuitilia Shaka Kamati yenu siku za usoni .
Hakuna rufaa tena Escrow na mjadala wa Escrow hapa duniani
uliotungwa na Rais Kikwete rasmi jana ,
nafasi iliyobaki ya kujadili Escrow labda ni mbinguni
ambako huko hatuna mamlaka nako.
Atakaye pinga hotuba yake kwa sasa atakuwa anapinga na rais
na anaweza kuhesabika ni mtu anayehatarisha usalama wa
nchi maana ki ukweli Rais ndiyo kiongozi juu wa
Tanzania na ameishasema kuwa fedha za Escrow siyo za umma ni
za IPTL.
Mnaolazimisha kuwa fedha za Escrow ni za umma endeleeni
kulazimisha, ila haitawasaidia maana tayari mjadala huo Baba
mwenye nyumba yaani Rais Kikwete aliufunga mjadala huyo kwa
kusema fedha za Escrow siyo za ummma.
Waliomuita Profesa Muhongo ni Muhongo Kama jina lake
kwasababu eti alisema Fedha za Escrow Si za umma, ni
dhahiri shahiri hotuba ya jana imewaumbua. Mabingwa wa
fitna kajipageni upya ili tukianza Mwaka mmoja muibuke na
jungu jingine mAana shughuli kubwa mnayoifahamu ni
kuwazushia wenzenu uongo.
Binafsi naamini ipo siku ushauri wa kisheria uliotolewa na
aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Werema utakuja
kueleweka ,ni suala la muda. Mungu ibariki Tanzania.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg. www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Disemba 23 Mwaka 2014
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment