Wednesday, 24 December 2014

Re: [wanabidii] TATHMINI YANGU, HOTUBA YA RAIS KIKWETE - WIZI WA FEDHA ZA TEGETA ESCROW.

domitian. kachero manumba alisema ''jinai haizeeki'' na rais kasema amewaweka kiporo namie nasema ''jinai haina makombo wala haichachi'' kama kuna jinai ipo siku sheria itachukua mkondo wake tu.

On Dec 24, 2014 7:58 PM, "Alec Domitian" <cdomilia@gmail.com> wrote:
Dear All,

Maoni yangu kuhusu hotuba ya Rais:

1. Hakuhoji pesa shs 73 au 75bn zilibebwa vipi kutoka benki ya Stanbick ndani ya dakika chache - kama sio kwenye viroba au sandarusi? Badala yake yake anakejeli waliosema kwamba hizo pesa zilibebwa kwa njia hiyo - hamna namna nyingine? Mkurugenzi wa Stanbick aliyefukuzwa kazi je? Ni kwa nini?

2. Kwa nini alichaguliwa Wakala Benki Kuu (kwa ajili ya Escrow Account) na sio benki nyingine au taasisi ya fedha hata ya binafsi kama hapakuwepo na maslahi ya serikali kwenye pesa hizo?

3. Kwa nini ripoti ya CAG na ya Prof Muhongo ziko tofauti? Wakati zote zinatoka serikalini? Kwa nini Prof Muhongo hakutoa takwimu zake kwa CAG mpaka aende Bungeni kutoa utetezi wa serikali? Serikali ina takwimu tofauti kwa ajili ya CAG na kwa ajili ya utetezi kama imebanwa? Tuamini kipi? Undumila kuwili?

4. Kwa nini Rais hakuongelea kutoswa kwa mwanasheria Ngwilimi wa TANESCO, kitendo ambacho kina madhara makubwa kwa ripoti ya serikali na utetezi wa Prof Muhongo? Tukae kimya?

5. Kwa nini Rais hakuoneshwa kukerwa na mtu anayeamua kugawa pesa takriban bilioni kama kumi (au zaidi) kwa watu binafsi? Madhara yake na kwenye uchumu wa nchi? Kwa nini hakuanzisha Foundation kama zilikuwa pesa halali? Rais anataka kusema hajui kwamba mgao huo ni faida ya ajabu iliyotokana na OVERCHARGE au tozo lisilo la kawaida kwenye umeme tuliolipia sisi Watz? Bila ridhaa yetu?

6.Ingekuwa enzi za Nyerere kila aliyetajwa (CAG, PCCB, PAC, maazimio ya Bunge) angeachia ngazi na kufilisiwa! Halafu tunasema CCM inafuata nyayo zake?

7. Dawa ya ufisadi huu ni Katiba ambayo bado hatujapata (iliyopitishwa ni ya CCM, kura za CCM na wajunbe wa CCM)

Domilia 

2014-12-24 0:21 GMT-08:00 'julius mtatiro' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
TATHMINI YANGU, HOTUBA YA RAIS KIKWETE - WIZI WA FEDHA ZA TEGETA ESCROW.
1. Nilitarajia angezungukazunguka ili kujaribu kuokoa mwizi huyu au yule - Imekuwa hivyo.

2. Kwa kiasi kikubwa maazimio ya bunge ameyakwepa kwepa tu, ilimradi asiyatekeleze kabisa au akitekeleza iwe hivyo nje ya wakati.

3. Rais ameshindwa kuongea kama mkuu wa nchi, kuwaonesha watendaji na washirika waje kuwa anachukia rushwa, haitaki na anaipiga vita. Kila aliyehusika na wizi wa fedha hizi au mgao wake, rais hasemi kwa uwazi kuwa amevunja taratibu za uongozi, anazungukazunguka.

4. Bodi ya TANESCO ilipaswa kufukuzwa kazi, si kuacha ati imalizie muda wake kwa sababu uko ukingoni. Mchezo huu ni kama ule wa EPA, badala ya kuwaadhibu wezi na kuwaondoa madarakani , wanaombwa warudishe fedha tu.

5. Rais anaonekana hajui msingi wa uchunguzi wa ripoti ya CAG na majumuisho ya PAC. Au amepotosha kila kitu kimakusudi, anahitaji uchunguzi mpya kuchunguza nini ambacho vyombo vya serikali na bunge havijachunguza?

6. Inaonesha wazi kuwa, rais hayuko tayari kuona washirika wake walioiba fedha au kunufaika nazo, wakifikishwa mahakamani.

7. Amejaribu kuonesha ati kashfa hii walioshughulikia ni CCM, na kwamba kama wangeamua kuiacha isingefika hapa ilipo. Rais anasahau kuwa kashfa hii iliibuliwa na gazeti ka THE CITZEN na mbunge DAVID KAFULILA (NCCR) na kusimamiwa kidete na wabunge wa upinzani, na kwamba wabunge wa CCM walikuwa mbogo baada ya kuona watanzania wamekasirika.

8. Inaonesha kuna mgawanyiko mkubwa sana serikalini, na mambo mengi ambayo Rais kayasema leo yalikywa hayajaamuliwa vizuri, ni kama washauri wake walimuachia yeye mwenyewe amalizie, maana waliona watajikaanga kujaribu kukwepa maazimio ya bunge ambayo yako wazi na yalifikiwa baada ya uchunguzi mkubwa.

9. Kikwete ataondoka madarakani huku 9|10 ya maazimio ya bunge hayajatekelezwa.

10. Viongozi wa CCM, Kinana na wenzake, watakuwa hawajaridhishwa kabisa na maamuzi ya JK, ukizingatia kwamba wamekuwa wakizunguka nchi kusisitiza kuwa watu wote walionufaika na fedha za ESCROW washitakiwe na wanyang'anywe mali zao. Pia rejea kauli za NKM wa CCM, Mwigulu Nchemba, wakati akiwa bungeni.

J. Mtatiro,
Jtatu, 22 Dec 2014,
Dar Es Salaam.
 
You'll need Skype CreditFree via Skype

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment