Monday, 29 December 2014

Re: [wanabidii] Re:Kujiuzuru baada ya kutenda uhalifu ni style ya zamani,sio sasa

manaibu waziri hawaingii katika baraza la mawaziri sasa yeye aliingiaje?

On Dec 29, 2014 5:07 PM, "'leonard magwayega' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
MWIGULU NDUGU YANGU NAKUKUMBUKA KUWA ULIKUWA KIONGOZI MAKINI SANA KWENYE UONGOZI WA RAIS JULIUS RUGEMARILA DARUSO PALE UDSM MLIMANI. JUHUDI ZAKO NAZIKUBALI ILA NINA WASIWSI KAMA HICHO UNACHOKITAKA KITAFANYIKA MAANA SINGASINGA NA CHENGE WAMEIWEKA MFUKONI MWAO SERIKALI YOTE YA BOSI WAKO ALIYEKUTEUWA KATIKA NAFASI HIYO, JE KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYO UTAWEZA KUFIKIA TARGET YAKO? LABDA! JITAHIDI, SISI YETU MACHO ILA TUNAKUUNGA MKONO KWA JUHUDI ZAKO MAKINI.
ADVOCATE BOB LEO.

On Saturday, November 22, 2014 6:42 PM, 'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

BREAKING NEWZZ KUTOKA DODOMA,MWIGULU
AAMUA KUPIGANIA HAKI YA MASIKINI NA
WANYONGE KWENYE SAKATA LA IPTL/ESCROW.
AAMUA KUTANGAZA MISAMO WAKE WAZI WAZI
MBELE YA MAWAZIRI WOTE,SOMA HAPA CHINI.
Dondoo Kutoka Kikao cha Ndani ya Baraza la
Mawaziri kilichofanyika jana Dodoma kilichofanyika
Ofisi za TAMISEMI.
Kikao rasmi cha kujadili sakata la IPTL/ESCROW
namna wahusika watakavyowajibishwa au
kuokolewa.
1.Misimamo ya Mawaziri tofauti tofauti.
Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu waziri wa
Fedha anatajwa kuwa Waziri wa kwanza kuonesha
msimamo wake wazi wazi kuwa Sakata la IPTL/
ESCROW ni hujuma dhidi ya Uchumi wa
Nchi.acharuka,AAGIZA MALI ZOTE NA PESA
ZOTE ZILIZOLIWA, ZILIZOTAWANYWA
ZIKAMATWE.Naibu huyu ambaye mara kadhaa
amekuwa akitajwa na vyombo vya habari kwa
juhudi zake za kuokoa matumizi mabaya ya fedha
na hata Watanzania wengine kuamua kumbatiza
jina la Sokoine wa pili ikiwa ni kufuata nyayo za
aliyewahi kuwa Kiongozi Makini Nchini hayati
Moringe Sokoine.
Mwigulu ndani ya kikao hicho cha siri anatajwa
kuendeleza ujasiri wake kuhusu mambo yenye
masilahi ya Taifa. Wakati watu na tetesi
mbalimbali zilikuwa zinaongelea kujiuzulu, Mwigulu
amejitokeza kwenyw kikao hicho na kusema CAG
ameshamaliza utata, sasa mali zote, fedha zote
za IPTL zikamatwe na wahusika wote
wakamatwe.
Nanukuu kama nilivyosikia"Tumezoea kusema eti
tumewajibisha watu kwa wao kujiuzuru, "Kujiuzuru
ni kupewa Likizo ya kwenda kula fedha ulizo
ziiba"anasema Mwigulu, Hili ni jambo la mazoea,
sasa, CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya
umma, sasa zikamatwe zote, na wahusika wote
wakamatwe"
Mwigulu alienda mbali zaidi na kusema hata
ambao walishastaafu na wamehusika kulihujumu
taifa wakamatwe na akaunt zao zikamatwe,
zifilisiwe zirudishwe kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Naibu huyo anayeshughulikia
mambo ya sera, Mwigulu ameagiza mtumishi wa
TRA aliyepewa 1.6bilion afukuzwe kazi, akamatwe,
na akaunti ifilisiwe fedha irudi serikalini. Pia
mitambo ya IPTL ikamatwe irudishwe serikalini.
Utamaduni wa watu kujiuzulu na kuhesebu kuwa ni
adhabu ni jambo la zamani, sasa ili kukomesha
wizi, uzembe na ufisadi sasa tuwakamate
wahusika wote, tuwafilisi na tuwaweke ndani na
tuwafunge.
Habari za uhakika kutoka kikao cha baraza la
Mawaziri zinasema, jana Mwigulu Nchemba
aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri
mkuu nakusema kujiuzuru sio adhabu stahiki kwa
wizi Mkubwa kama huu wa Mali ya Umma,Hisia
hizo zikiwa zimegubikwa na maisha yake halisi ya
umasikini aliyokulia na huku akihusisha Wizi wa
fedha na hujuma dhidi ya Watanzania
Masikini.Mbunge huyo wa iramba anasisitiza kwa
kusema " Tazama wanafunzi, watoto wa masikini
zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa
hospitalini hakuna masikini wanakufa, watu wasio
na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya
maabara, walimu wanadai, wazabuni wanauziwa
nyumba zao na mabenki huku wakiidai serikali kwa
huduma walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya
kujiuzuru? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha
walizo waibia masikini? Hapana, "Enough is
enough" ndg Waziri mkuu tuwakamate, tuwafilisi,
tuwafunge. Pesa na mali virudi serikalini."
Kwa yule mtumishi wa TRA aliyekula fedha za
IPTL zaidi ya 1.6 B,Mwigulu akatoa agizo kuwa
"Nimemwagiza kamishna wa kodi amfukuze kazi
yule wa TRA iliyoko chini ya wizara yangu, na
afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe, na
wahusika wakamatwe. Hatuwezi kuendeleza
mazoea ya kufunga masikini na kuwapa likizo wezi
wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko
kwenye siasa wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi
serikalini."
Taarifa za uchunguzi zunasema tayari TRA
imechukua hatua."
Naibu Waziri KILIMO Mh.Godfrey Zambi
wanusurika Kukunjana na Werema(Mwanasheria
Mkuu wa Serikali).
Wakati kikao kikiwa kimepanda joto la
juu,Mawaziri wakifikia makubaliano kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na madini Maswi na
Mawaziri waliohusika ni lazima waachie
ngazi,Ndipo Werema alipotaka kumkunja Mh.Zambi
baada ya kutoleana maneno machafu dhidi ya mali
ya uma.
Madai yanakwenda mbali kuwa,Zambi alikuwa
anapigia kelele kuwa inawezekanaje Mwanasheria
mkuu kubariki wizi wa Fedha za Umma?.Ni wapi
watu wa msoma wakasifika kwa wizi wa mali za
Umma?.Chokochoko hizo ndio zilipelekea Ugomvi
kati ya Zambi na Werema.
Mbali na Mawaziri hao,Mh.Tibaijuka amekuwa
Mwizi wakwanza wa IPTL kukubali kuwajibika
katika sakata hili mbele ya kikao cha baraza la
Mawaziri.
Ni wakati Muafaka sasa kwa Watanzania wote
kuunga kupaza sauti kama akina Zitto
walivyofanya,Kuunga mkono zaidi Machozi ya
akina Mwigulu waliojitolea kutetea Masikini wakati
huo huo wanahujumiwa na Mawaziri wenzao ndani
ya Chama tawala,Mwigulu ameanua kujilipua
Mzima mzima bila kujali yeye ni nani ndani ya
Chama kwa Malengo kuwa CCM haipo tayari
kukumbati waovu na wezi.
UPDATEs zitawajia Kesho baada ya kikao cha leo
Usiku kingine.
       
                      👆
Nimecopy jinsi ilivyo

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment