Sunday, 14 December 2014

Re: [wanabidii] Re: Yanayojiri ktk Uchaguzi Serikali Mitaa - Dec 14, 2014

 Kituo cha sharif shamba,ilala uchaguzi umehairishwa hadi tarehe 21.12.2014 kwa sababu form za wagombea viti maalum hazikufika pia mjina la mgombea ujumbe kamati mchanganyiko limekosewa.




2014-12-14 11:45 GMT+03:00 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>:
Wananchi wa kawe walalamika utaratibu wa majina yao kutosomeka vizuri copy za makaratasi zaloa na mvua na kupigwa na jua la njaa majina kutosomeka. Wengi wakatishwa tamaa.


On Sunday, December 14, 2014 11:39:13 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Unaweza kusema CCM inalazimisha mapenzi kwa wananchi. Wananchi wameichoka. Wananchi hawaipendi CCM. Leo nimefika katika kituo changu nilichojiandikishia kupiga kura hapa jijini Mbeya, nikiwa na hamu kabisa ya kutumia haki ya msingi kumchagua kiongozi nimtakaye. Mbali na mimi niliwakuta pia wananchi wengine waliokuwa kituoni kwa lengo hilo hilo. Cha ajabu na cha kusikitisha tunaambiwa hakuna kupiga kura, kisa mgombea wa CCM amepita bila kupingwa. Kwamba mgombea wa UKAWA alienguliwa katika hatua za mwishoni kwa kutokutimiza taratibu za wagombea. Wananchi tukasema basi tumpigie kura huyo huyo wa CCM kuonesha kama tunamtaka yeye au la, wasimamizi wakasema kanuni haziruhusu kufanya hivyo! Tunajua hizo ni hila za CCM kuengua wagombea wa vyama vinavyounda ukawa kiujanja ujanja lakini naomba niwaambie kuwa kufanya hivyo ni sawa na kulazimisha mapenzi kwa wananchi! Kufanya hivyo ni sawa na mwanaume kulazimisha mapenzi kwa mwanamke ilihali hakutaki au kinyume chake! Naomba CCM wajue kuwa wakati wa kuongoza watapata shida kwani watakuwa wanaongoza wananchi wasiowapenda!

On Sunday, December 14, 2014 11:26:54 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, S. Liwowa ametangaza ushindi kwa CCM katika vitongoji vyote vya Wilaya hiyo baada ya vyama vya Upinzani kushindwa kusimamisha wagombea.

On Sunday, December 14, 2014 11:20:25 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
huku kwetu morogoro hali bado shwari hasa Kata ya kihonda magorofani.

On Sunday, December 14, 2014 11:14:37 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Songea mjini katika mtaa wa CCM kata ya mjini hali ni nzuri wasimamizi wa uchaguzi wamefika mapema vituoni, na majina ya wagombea yote yamebandikwa vizuri na yanasomeka
na ulinzi umeimarishwa

On Sunday, December 14, 2014 11:09:59 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Uchaguzi mtaa wa mtambani - vingunguti dsm umehairishwa kisa ukosekanaji wa vitendea kazi. Baadhi ya raia waliokuwa wakipinga hatua hiyo, tayari wamewekwa nguvuni.

On Sunday, December 14, 2014 11:08:32 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Hapa kibangu-ubungo mambo swafi 

On Sunday, December 14, 2014 11:07:35 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Huku kwetu kinyerezi visanduku vya kupigia kura havijaletwa mpaka sasa

On Sunday, December 14, 2014 11:05:55 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:

 



On Sunday, December 14, 2014 11:04:04 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Kiusa Sokoni mambo ni shwari zoezi linakwenda salama, ulinzi umeimarishwa eneo hili la soko lina wananchi waliojitokeza kwa wingi hivyo foleni ni kubwa

On Sunday, December 14, 2014 11:01:32 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Nipo kituo cha kawe wilaya ya kinondoni hali ilikuwa si shwari asubuhi baada ya watu kuambia wapige kula bila kuwepo kwa wino wa kupaka kidoli wananchi walichachamaa ila kwa sasa zoezi lipo salama kabisa

On Sunday, December 14, 2014 11:00:03 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Baadhi ya wapiga kura wa Kigoma Ujiji kata ya Rusimbi mtaa wa Kawawa kituo cha ofisi ya serikali za mtaa kawawa wamemshambulia kwa ngumi bwana Omari kutoka mtaa wa kaburini kwa kosa la kujaribu kupiga kura kituo na mtaa Rusimbi ambao sio mtaa wake.Anaendelea kuripoti kuwa hakuna ulinzi wowote katika eneo la tukio hadi sasa ingawa hali imeanza kutulia

 



On Sunday, December 14, 2014 10:57:56 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
mkuu ni hapa wilaya ya kilosa kijiji cha ruaha hali si shwari hapaa vuguvugu la vurugu linanukia mana wananchi wamekuwa wakali

On Sunday, December 14, 2014 10:55:21 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Hiki ni kituo cha kupigia kura kilichopo Majengo A kata ya Majengo Sumbawanga.Kilifunguliwa saa mbili lakini mpaka sasa vifaa havijafika



On Sunday, December 14, 2014 10:53:49 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Mpaka wakati huu kata ya vingunguti kula hazijaanza kupigwa sababu karatasi za kupigia kura hazijafika. Hapa kuna mchezo mchafu.

On Sunday, December 14, 2014 10:45:21 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Kata ya Kinyerezi eti imepokea karatasi na makabrasha ya kura za Kata ya Gerezani .Na Gerezani nadhani watakuwa wamepokea za Kinyerezi au Kata gani ila kwa kifupi kuna tatizo kubwa hadi muda huu niko kituoni hakuna kinacho endelea .

On Sunday, December 14, 2014 10:41:27 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Kituo cha Sumbawanga mjini bus stand kilichopo ndani ya Kituo cha Polisi kimefunguliwa ila mpaka sasa Karatasi za kupiga kura hazijafika

On Sunday, December 14, 2014 10:40:16 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Sumbawanga mjini kuwa kituo cha Anglikana A hakijafunguliwa , mabox yapo nje, wasimamizi hawajafika makaratasi pia na mkurugenzi kazima simu yake

On Sunday, December 14, 2014 10:38:51 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Kata ya Iwambi Mtaa wa Ilumbila ambapo kuna kutoelewana baada ya wagombea wa Chadema Kuenguliwa .



On Sunday, December 14, 2014 10:37:09 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Kutoka kwa Mkuu wa wangalizi wetu Lucy aliyeko Songea Mjini, anatuambia kuwa kata ya misufini hadi sasa kura hazijaanza kupigwa kwa sababu fomu za kupiga kura nafasi ya uenyekiti wa mtaa zimechanganywa, kwani kwenye nembo ya CCM jina lililoandikwa ni la mgombea wa CHADEMA kama inavyoonyesha kwenye picha



On Sunday, December 14, 2014 10:25:20 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Kwa hapa ifakara zoezi limeanza SAA 2 kamili vituo vyote vifaa vimewasili kwa wakati. Amani imetawala, hakuna malalamiko. Kura zinapigwa kwa utulivu mkubwa

On Sunday, December 14, 2014 10:18:57 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Uchaguzi wa kijiji cha Kagunga, Kigoma Kaskazini umefutwa hadi siku nyingine baada ya mtendaji wa kata kusema ACT imefutwa katika uchaguzi huo. Hata hivyo msimamizi mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza.

Wagombea wa vijiji 2 wa chama cha ACT walitumia anuani ya Shule kama anuani yao. Mtendaji kawaeungua. Wananchi wamemgoma. Uchaguzi umeahirishwa.

Kijiji cha Kagunga na Zashe kata ya Kagunga Jimbo la Kigoma Kaskazini

On Sunday, December 14, 2014 10:17:06 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
- Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana

On Sunday, December 14, 2014 10:09:15 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Mtaa wa faru kata ya vingunguti mpaka sasa uchaguzi bado karatasi za kupigia kura hazijafika eneo la kupigia kula, vifaa vya uchaguzi vimefika saa moja na nusu eneo la tukio

On Sunday, December 14, 2014 10:07:42 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Uchaguzi huu umekua na baadhi ya Changamoto. Kinondoni wino umekosekana. Mtu anapiga kura na kuondoka hivo kuna uwezekano watu kupiga kura mara mbili. Msimamizi wa Uchaguzi amewapa kazi mawakala kuhakikisha mtu harudii. Je wakala kazi yake ni kuhakikisha mtu harudii kupiga kura au kuhakikisha kura haziibiwi?

Changamoto namba mbili ni majina. Majina yamefifia, huwezi kuliona jina kirahisi. Hii imekua changamoto kwani watu wakikosa majina wanaondoka.

On Sunday, December 14, 2014 10:06:40 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Nipo kituocha kimandolu shuleni. Turn up ni kubwa sijapata ona. Kama usipofanyika utaratibu mwingine, kuna hatari ya watu kutopiga kura leo. Sina uhakika kama hawa watu wote wanawezapoga kura ndani ya muda uliopangwa.

On Sunday, December 14, 2014 9:58:21 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Huku kwetu Kinyerezi kituo cha Midway secondary school vifaa vya kupiga kura mpaka naondoka kituoni mida ya saa tatu asubuhi vifaa vya kupigia kura vilikuwa havijafika kabisa. Tatizo ni kwamba vifaa vilivyopokelewa ni vya Gerezani badala ya Kinyerezi!

On Sunday, December 14, 2014 9:52:32 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Majengo, Msua, Katuma, Katandala, Tunesco, Kisiwani, nk ni kata za Sumbawanga mjini hadi sasa ni saa 10:00 am hakuna kinachoendelea

On Sunday, December 14, 2014 9:49:54 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Nipo jimboni kwetu Buchosa. Ni saa 3 asubuhi. Vituo vyote vya kupiga kura vimefunguliwa, lakini hakuna karatasi za kupigia kura. Kuna taatifa kuwa vituo vyote jimboni havijaanza kupiga kura. Watu wapo vituoni wanasubiri.

On Sunday, December 14, 2014 9:48:09 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
mi nipo hukui mkuranga, mpaka sasa ofisi haijafunguliwa, na tumeambiwa kuwa form za wajumbe hazijafika, tupo hapa, tunasubiria, nimempigia simu mke wangu, aniletee chupa ya chai hapa hapa, ninywe chai, ili nipate nguvu ya kupiga kura, sitaki kurudi nyumbani.

On Sunday, December 14, 2014 9:47:30 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
kata ya Zagayu wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu uchaguzi bado haujaanza hadi muda huu kwa sababu karatasi za kupigia kura hazijafika yapo masanduku ya kura tu.

On Sunday, December 14, 2014 9:32:40 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
mpaka mda huu, hapa kahama, shinyanga mtaa wa Nyahanga shuleni watu bado hawajaanza kupiga kura. Watu wamejitokeza kwa wingi sana hasa vijana, waeendesha pikipiki wapo wakisubili kupiga kura ni jambo la faraja kuona nao vijana sasa wamehamasika kupiga kura. 

On Sunday, December 14, 2014 9:32:14 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Sumbawanga mjini- kata majengo, msua, katandala, katuma, kisiwani vituo bado vimefungwa na sasa no saa 9:17 a.m

On Sunday, December 14, 2014 9:31:45 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Ni saa tatu na dkk kibao upigaji kura hado haujaanza hapa Kakola mkoani Shinyanga.

On Sunday, December 14, 2014 9:31:07 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Nipo hapa sinza block C mugabe shule, nilijiandikisha namba 65 na jina serikali ya mtaa
Kwenye list lipo mpaka sasa cha ajabu kituoni halipo naona jina tofauti 

On Sunday, December 14, 2014 9:29:40 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Kigamboni mtaa wa Ferry uchaguzi umeingia dosari baada ya mjumbe mmoja wa UKAWA kupitia CUF jina lake kuonekana kwenye karatasi ya kupigia kura wakati alikuwa amekwisha jitoa

On Sunday, December 14, 2014 9:28:44 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Uchaguzi serikali za mitaa tabora kizungmkuti

mpaka sasa ni sa 2:33 hakuna kituo hata kimoja kimeshafunguliwa. Tumefika kituoni zaidi ya mara 3 hakuna majina, wasimamizi bali mawakala ndo wamefika. tumejaribu kupiga simu vituo kadhaa bado hari iko hivyo tu.

On Sunday, December 14, 2014 9:27:23 AM UTC+3, Juma Mzuri wrote:
Uchaguzi Manispaa ya Sumbawanga Kizungumkuti! Hadi sasa hakuna kituo kilichofunguliwa wapiga kura wapo kibao katika vituo.

On Sunday, December 14, 2014 6:52:48 AM UTC+3, Abdalah Hamis wrote:
Yanayojiri ktk Uchaguzi Serikali Mitaa - Dec 14, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment