Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:
RAI KWA CCM: WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO
Kauli hii iliwahi kutolewa katika hotuba ya Mwalimu Julius K. Nyerere katika Mkutano Mkuu Wa CCM –Dodoma Mwaka 1995. Mwalimu alisema, nanukuu " Watanzania wanataka mabadiliko,wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM."Lengo kuu la hotuba hii ilikuwa ni kuwaasa wana CCM katika mkutano huo ili wachague mgombea ambaye atakidhi matarajio ya wananchi,na sio ya wana CCM. Ni ukweli usiopingika kuwa ile ari ya kutaka mabadiliko miongoni mwa watazania bado ipo na inazidi kukua,siku hadi siku, mwaka hadi mwaka.
Watanzania wengi,hata kama hawasemi kwa umoja wao,lakini huko pembeni, mtanzania mmoja mmoja hafurahishwi na hali ya UFISADI na UFUJAJI wa MALI ya UMMA kama hali inavyozidi kuonekana sasa na haswa kwenye vyombo vya habari. Wengi wetu mmesikia ufujaji wa PESA za UMMA kama kashfa ya ESCROW, EPA, RICHMOND, RADA, nk. Lakini, bado kuna ufisadi mkubwa kwenye halmashauri zetu za miji ambao haupigiwi kelele sana lakini unaumiza wengi kwa kuwa ufisadi huo unazorotesha kasi ya maendeleo na kuifanya serkali iliyoko madarakani kutokuwa na tija. Mipango ya miji ni mizuri,lakini miji haijengwi,barabara zinajengwa kwa kiwango kibovu na kwa ujumla maendeleo ni kidogo lakini gharama ni kubwa kutokana na wizi huu usio na huruma. Mambo haya yanaongeza kasi ya wananchi kutokuwa na imani na serikali yao na chama chake pia. Mwananchi wa kawaida ambaye hana uwezo wa hata kununua dawa ya malaria, hawezi kabisa kuisikiliza taarifa ya kufujwa mabilioni ya shillingi ya umma na bado akazidi kuwa na imani na serikali yake. CCM itafanya jambo jema sana kama italiangalia hili kwa makini na kulitendea kazi. Wakati wote, ni imani yangu kuwa, ni ngumu sana kuirudisha imani iliyopotea kuliko kuilinda iliyopo. Hivyo basi, ni muhimu sana CCM na serikali yake wakibadilika. Na mabadiliko hayaepukiki ili kukidhi matarajio na matumaini ya watanzania.
Katika hili nashauri kuwa: Kwa nafasi ya mgombea wa uraisi, ni vema sana CCM ikamsimamisha mgombea wa uraisi SAFI, asiye na DOA, na mwenye uwezo wa kuunda serikali ADILIFU ambayo itawatumikia wananchi na ambayo haitakumbwa na madudu kama hayo.
Mwalimu Nyerere katika mkutano huo wa CCM –DODOMA (1995) alisema, CCM bado hakijawa chama cha matajiri. Lakini, ni ukweli usiopingika kuwa CCM kinaelekea kuwa Chama Cha Matajiri. Watu wenye uwezo wa kutoa chochote kwa kuwarubuni wajumbe katika chaguzi za ndani ya chama ndio wenye nafasi kubwa ya kuteuliwa na chama kwa ajili ya kugombea. Urubunifu huo hufanywa na wenye fedha hao kwa kujipenyeza katika makundi fulanifulani ya wamama au vijana
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment