Monday, 29 December 2014

Re: [wanabidii] Re: RAI KWA CCM: WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO

CCM haiwezi tena kuleta mabadiliko. Imeshakuwa hijacked na wezi na mafisadi hakuna kurudi nyuma.
em

2014-12-29 5:01 GMT-05:00 Godfrey Ngupula <godfreyngupula@gmail.com>:

RAI KWA CCM: WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO
Kauli hii iliwahi kutolewa katika hotuba ya Mwalimu  Julius K. Nyerere katika  Mkutano Mkuu Wa CCM –Dodoma Mwaka 1995. Mwalimu alisema, nanukuu " Watanzania wanataka mabadiliko,wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM."

Lengo kuu la hotuba hii ilikuwa ni kuwaasa wana CCM  katika mkutano huo ili wachague mgombea ambaye atakidhi matarajio ya wananchi,na sio ya wana CCM. Ni ukweli usiopingika kuwa ile ari ya kutaka mabadiliko miongoni mwa watazania bado ipo na inazidi kukua,siku hadi siku,  mwaka hadi mwaka.

 

Watanzania wengi,hata kama hawasemi kwa umoja wao,lakini huko pembeni,  mtanzania mmoja mmoja hafurahishwi na hali ya UFISADI na UFUJAJI wa MALI  ya UMMA kama hali inavyozidi kuonekana sasa na haswa kwenye vyombo vya habari. Wengi wetu mmesikia ufujaji wa PESA za UMMA kama kashfa ya ESCROW, EPA, RICHMOND, RADA, nk. Lakini, bado kuna ufisadi mkubwa kwenye halmashauri zetu za miji ambao haupigiwi kelele sana lakini unaumiza wengi kwa kuwa ufisadi huo unazorotesha kasi ya maendeleo na kuifanya serkali iliyoko madarakani kutokuwa na tija. Mipango ya miji ni mizuri,lakini miji haijengwi,barabara zinajengwa kwa kiwango kibovu na kwa ujumla maendeleo ni kidogo lakini gharama ni kubwa  kutokana na wizi huu usio na huruma. Mambo haya yanaongeza kasi ya wananchi kutokuwa na imani na serikali yao na chama chake pia. Mwananchi wa kawaida ambaye hana uwezo wa hata kununua dawa ya malaria, hawezi kabisa kuisikiliza taarifa ya kufujwa mabilioni ya  shillingi ya umma na bado akazidi kuwa na imani na serikali yake. CCM itafanya jambo jema sana kama italiangalia hili kwa makini na kulitendea kazi. Wakati wote, ni imani yangu kuwa, ni ngumu sana kuirudisha imani iliyopotea kuliko kuilinda iliyopo. Hivyo basi, ni muhimu sana CCM na serikali yake wakibadilika. Na mabadiliko hayaepukiki ili kukidhi matarajio na matumaini ya watanzania.

 

Katika hili nashauri kuwa: Kwa nafasi ya mgombea wa uraisi, ni vema sana CCM ikamsimamisha mgombea wa uraisi SAFI, asiye na DOA, na mwenye uwezo wa kuunda serikali ADILIFU ambayo itawatumikia wananchi na ambayo haitakumbwa na madudu kama hayo.

 

Mwalimu Nyerere katika  mkutano huo wa CCM –DODOMA (1995) alisema, CCM bado hakijawa chama cha matajiri.  Lakini, ni ukweli usiopingika kuwa CCM kinaelekea kuwa Chama Cha Matajiri. Watu wenye uwezo wa kutoa chochote kwa kuwarubuni wajumbe katika chaguzi za ndani ya chama ndio wenye nafasi kubwa ya kuteuliwa na chama kwa ajili ya kugombea. Urubunifu huo hufanywa na wenye fedha hao kwa kujipenyeza katika  makundi fulanifulani ya wamama au vijana  na kutoa misaada mbalimbali kwa kujifanya ni watu  wenye nia njema,  lakini  muda si mrefu watu hao hutangaza kugombea. Hii ni rushwa ya kabla ya uchaguzi, na rushwa hupofusha macho. Lakini,muda si punde, watu wa jinsi hiyo wakishachaguliwa,hudhihirisha makucha yao kwa kutokomea kusikojulikana mpaka kipindi kingine cha uchaguzi ambapo hurudi tena kwa kasi na mafungu makubwa ya fedha, tayari kwa urubunifu mwingine.

 

Mwaka 2015 tunaingia katika uchaguzi wa raisi, wabunge na madiwani. CCM isipokuwa makini, mgombea atayesimamishwa na chama atakuwa ni yule mwenye uwezo wa kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu na kurubuni baadhi ya wajumbe wa NEC taifa ili achaguliwe.

 

Ni ukweli usiopingika kuwa, UZALENDO, UADILIFU na UWAJIBIKAJI ni kama havipo katika serikali yetu. Kilio hicho cha wananchi kinaonekana waziwazi mitaani, katika makundi ya vijana na haswa katika maoni ya tume ya WARIOBA iliyounda rasimu ya kwanza ya mabadiliko ya katiba. Kwa serikali yeyote inayotaka kuendelea kushika dola, UZALENDO, UADILIFU na UWAJIBIKAJI ni lazima  vizingatiwe,  la sivyo tutarajie anguko kubwa wakati wowote ujao.

 

Katika hili nashauri;

Kwa nafasi ya uraisi, CCM kama chama kiangalie ni mgombea gani anabeba matumaini ya wengi, haswa kwa kuleta mabadiliko ya kiutendaji kwa kuzingatia usawa,uzalendo na uwajibikaji. Raisi ajae ni lazima awe na uwezo wa kukemea mabaya na kusifia mema. Ni lazima awajibishe mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi huku tajiri na masikini wote wakilipa kodi. Tajiri akiwa tajiri kwa haki yake na masikini akiendelea kuwa masikini kwa haki yake. Na pia,  ni lazima kwa nguvu zake zote ahakikishe kodi inayokusanywa inatumika vizuri kwa manufaa ya umma.

Mataifa yote makubwa wanapochagua raisi huangalia taifa linapitia katika kipindi gani na wanahitaji nini. Hilo tunaweza kujifunza kutoka  kwa wenzetu wa Marekani. Taifa letu linahitaji Uwajibikaji,uzalendo na uadilifu wa viongozi. Ni lazima raisi ajae awe yeye kwanza ana sifa hizo na kisha awe na uwezo wa kuwajibisha mfumo mzima uende kama yeye alivyo kwa manufaa ya umma.

 

Kwa nafasi ya ubunge: nashauri uwepo uwakilishi sahihi wa wananchi na sio uwezo wa kuhonga na kurubuni. Ikumbukwe kuwa, wananchi wanataka wawakilishi wao kwa maslahi yao. Hivyo, basi mwakilishi ni vizuri sana akitokana na wananchi wenyewe na awe amekerwa na shida zao na umasikini wao. Hivyo basi ni muhimu sana chama kikajiridhisha kwa hakika kabisa nini kimekuwa kigezo cha wananchi kumchagua nani kwa uwakilishi huo. Na kigezo muhimu ni lazima kiwe ni sera,mawazo, na uwezo wa mwakilishi huyo na sio kingine.

 

NOTE: Nashauri pia chama kiwe makini sana na upandikizaji mkubwa wa maafisa usalama wa taifa katika nafasi mbali mbali za ubunge. Kwa uelewa wangu mtu yeyote aliyeajiliwa na idara  ya usalama wa taifa ameapa kuilinda serikali wakati wote wa uhai wa mtu huyo. Mbunge anaapa kuisimamia serikali wakati wote hata iweje ili itimize majukumu yake. Usalama wa taifa kusimama kama mbunge ni kuwahadaa wananchi, kwani kuna mkanyiko wa kimaslahi. Hatimaye yake ni kuwa na bunge butu lisilotimiza wajibu wake vizuri. Serikali inazo njia nyingi za kupenyeza watu wake kwa maslahi yake katika vyombo vyake,nashauri ivitumie hivyo.

 

MWISHO: Nawashauri wana CCM vijana. Kwa muda mrefu tumetumiwa kama njia katika kutimiza malengo ya baadhi ya wagombea fulani wa uraisi au ngazi nyinginezo,  lakini kwa sasa tuseme HAPANA. Sisi kama vijana, bila kujali mapenzi yetu binafsi ni muhimu  tukiangalia ni nini matarajio ya watanzania walio wengi kwa sasa,na nini matatizo au changamoto taifa letu linapitia na ni nani anaweza kuwa suluhisho lake?. Mwisho wa siku basi tusimame na mgombea ambaye atakidhi matarajio hayo. Ni kweli wazee wetu wametulea mpaka hapa tulipo,lakini tukumbuke kuwa wao watapita na kutuachia chama mikononi mwetu. Ni vema tukiachiwa chama kilicho hai na si chama kinachokufa, na hivyo tukibaki kuwa wapinzani wa serikali iliyoko madarakani tukibeba shutuma tusizohusika nazo kabisa. Kijana, hebu tumia akili yako na kataa kutumiwa kwa maslahi ya watu binafsi ambao wanataafuta kuwa viongozi kwa heshima tu na si kutumikia wananchi kwa moyo na uadilifu. 

 

Godfrey W. Ngupula

ngupula@yahoo.co.uk/ godfreyngupula@gmail.com

0762835412/0715835412

 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment