Thursday, 18 December 2014

Re: [wanabidii] RAIS AMTEUA DKT JAMES P MATARAGIO KUWA MKURUGENZI MTENDAJI TPDC

Tuombe Mungu, na yeye mteuliwa amtangulize Mungu mbele, kwa maana sekta hii ni nyeti na ina siasa; na kwa mazingira ya Tanzania ambapo, wakati mwingine, siasa inaonekana kutawala utaalamu na fani, inambidi awe makini kweli. 'Modus operandi' kwa nchi kama Marekani zinaheshika sana kuliko hapa kwetu...kuwa makini ndugu, ili wasifu wako usijepata doa!

Mfano mzuri ni kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, hata kama alivyosema kwenye utetezi wake wa jana kuwa ni kweli, basi, hana ujanja, wasifu wake aliopata nchini na kwenye nyanja ya Kimataifa haupo kama ulivyokuwa mwanza kabla ya sakata la Tegeta Escrow, la hasha, umeshatiwa doa. Na kama kiongozi wa umma, hustahili hata kutuhumiwa, maana kitendo cha kutuhumiwa tu, mwenendo wako una walakini! Hivyo sio msafi, ana doa!

'Now, you know what I mean, be careful brother, and do everything for the people of this land, and God will defend your course!'

Congrants and welcome home!

2014-12-18 18:13 GMT+03:00 fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>:

RAIS AMTEUA MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI (TPDC)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.

Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-

ELIMU:-
Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri  Rolla, Missouri, Marekani (2005)
MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994

UZOEFU WA KAZI:-
Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.

Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.

Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.

Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Desemba, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
-----------------------
Fratern Kilasara
,

P. O. Box - (Home): 62810; or (Office): 65300
Dar es Salaam - Tanzania.
Mobile (Personal): +255 (0)715 40 41 53 or +255 (0)754 40 41 53
Emails: kilasara.fratern@gmail.com or kilasara.fratern@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment