imesoma mahala katika tamko la bwana wadogo hawa panaposema 'Hakuna mahala panaposema Waziri Mkuu alilisababishia taifa ----------'
Kwa hiyo wanamtetea waziri Mkuu.
Sikuona kama walisoma popote panapoonyesha kuwa kipindi chote cha sakata hili waziri Mkuu hakuwepo ofisini. Kama mambo yalitendeka yeye akiwepo na yakatendeka bila kujua Haitoshi kumuwajibisha??
--------------------------------------------
On Sun, 12/14/14, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] MAONI NA MTAZAMO WA WANAZUONI VIJANA KUHUSIANA NA MAADHIMIO YA BUNGE KUHUSU RIPOTI YA CAG YA NOV 26-28.2014
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, December 14, 2014, 1:39 PM
JUMUIYA YA
WANAZUONI VIJANA TANZANIA.MAONI NA MTAZAMO WA
JUMUIYA YA WANAZUONI VIJANA TANZANIA KUHUSIANA NA MAADHIMIO
YA BUNGE KUHUSU RIPOTI YA CAG YA NOV 26-28.2014
UTANGULIZI.SISI ni mkusanyiko wa
vijana, ambao ni wahitimu na wanazuoni vijana tuliopata
kusoma shahada ya kwanza katika vyuo vikuu nchini na wengine
wapo vyuoni wakisoma huku pia wengine tukiwa ni miongoni mwa
watanzania wachache walisomeshwa shahada ya pili nje ya nchi
kwenye fani zinazohusiana na masuala mbali mbali ya madini,
nishati ikiwemo mafuta na gesi. Tunafurahi sana
kupata nafasi hiyo ambayo tulidhaminiwa na serikali kupitia
wizara ya nishati na madini, hivyo tunajivunia kuwa ni
miongoni mwa watanzania wachache tuliowezeshwa na kufika
mbali zaidi kielimu na serikali.Tunawajibu mkubwa
wa kuitetea nchi na kuisemea pale tunapoona kuna jambo baya
limefanyika, kwa kuwa uelevu wetu umetokana na kupata elimu
bora iliyotokana na kodi za watanzania wenzetu na hatupo
tayari kuona mambo yakienda mrama.Kama Taifa,
hivi karibuni tumeshuhudia upepo mkali wa kisiasa ukivuma,
wapo tuliouelewa, wapo tuliouamini, wapo tuliousadiki, wapo
tulioutilia mashaka na zaidi ya yote wapo tuliobakia juu juu
na kufuata mkumbo wa mambo.Tukiwa kama wasomi
vijana, tuna wajibu kwa taifa letu kulipigania ili
kuhakikisha kuna usawa kwa kuwa Tanzania ni taifa huru na
linahitaji kuwepo kwa wanasiasa huru na wenye maono ya
kuifikisha nchi pahala salama kwa kuwa uwezo na maadili yao
ni muhimu.Tuna wajibu chanya kabisa, kuhakikisha
nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata misingi imara ya ukweli,
uwazi, uwajibikaji huku ikizingatia msingi mkuu wa haki kwa
kila mtu na watanzania waelewe kuwa kujiudhuru sio ushujaa
au uzalendo. Jiulize wote waliojiudhuru hadi sasa ni
wazalendo wa kweli wa nchi yetu?. Panapotokea
masuala yote ya kitaifa, masuala yanayohusu kuwajibishana,
kutuhumiana, kushughulikiana kama wengine wanavyosema, basi
lazima misingi yote iende sambamba na haki kwa kila
mtuhumiwa.
KUHUSU RIPOTI YA CAGSote tunakumbuka
kwamba hivi karibuni Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) amekabidhi ripoti ya uchunguzi
kuhusiana na sakata la TEGETA ESCROW, sakata ambalo msingi
wake unahusiana na kampuni ya kufua umeme ya
IPTL.Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG
tumeshuhudia namna Taifa lilivyokuwa na hamu kutaka kujua
kilichomo ndani yake.Ripoti iliarifu juu ya
Hadidu za rejea zaidi ya 11 iliyopewa na Waziri Mkuu, Bunge
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.Kwa
nyakati tofauti, na kwa namna tofauti, sisi wenyewe,
tumeshuhudia ripoti hiyo, na tumestahajabishwa na kugeuzwa
geuzwa kwa mapendekezo ya ripoti hiyo kulikofanywa na kamati
ya bunge ya PAC.Katika ripoti ya CAG pamoja na
viambatanisho vyake vyote, tumesoma na kuvirudia na kusoma
na kuvirudia, hakika hakuna sehemu CAG ameshauri, ama
kupendekeza, ama kutafsiri kwamba pesa iliyokuwepo katika
ESCROW AKAUNTI ni mali ya UMMA.Katika ripoti ya
CAG, hakuna sehemu hata moja, wala kurasa hata moja, wala
aya hata moja, iliyosema kwamba Waziri mkuu amelisababishia
hasara Taifa.Katika Ripoti ya CAG, hakuna sehemu
yoyote inayosema kwamba Waziri wa Nishati na Madini
amehusika kwa namna yoyote ile kulihujumu
TaifaKatika Ripoti ya CAG, hakuna sehemu yoyote
inayosema kwamba Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati Na madini
amefanya uzembe, zaidi ya yote, ripoti imemtaja katibu mkuu
huyu kuwa amefanya jitahada kadhaa kuhakikisha serikali
inachukua tahadhari na kama ni kweli muhusika anastahili
kulipwa fedha alizoomba kulipwa ama la.Katika
ripoti ya CAG hakuna sehemu yoyote inayosema kwamba pesa
iliyotolewa kwenye akaunti ya ESCROW ni ama Bil321 au bil
306 kama wanavyouaminisha umma.Ndugu zangu, najua
mtachelewa kutuelewa, na mtashangaa kwa nini tumeamua kusema
haya, lakini ni lazima tubadili sasa mfumo wetu wa siasa za
Tanzania na siasa za kutatua matatizo na changamoto kama
ilivyo sasa.Kwa sasa hivi wanasiasa hasa wabunge,
wamekuwa wakifanya maamuzi kishabiki, kichuki, ki maslahio
binafsi na bila kuzingatia ukweli na misingi ya Utawala
bora.Ndugu zangu, kwenye Ripoti ya CAG kumesema
wazi kwamba, serikali imefanya jitihada stahili kuhakikisha
taratibu zinafuatwa ili kujiondoa kwenye madhara yanayoweza
kutoke baada ya pesa kufuatwa.Ripoti ya CAG
haijamtia hatiani mtu yeyote. Tunashindwa kuelewa misingi ya
kamati ya PAC ya kutaka kuwajibishwa kwa watu bila ya kuwa
na hatia.Vyovyote itakavyokuwa, na vyovyote
itakavyotafsiriwa, sisi tunaamini na tunataka watanzania
waamini kwamba, kuwapoteza watu kama Pro.MUHONGO, kwenye
utumishi wa umma, kwa sababu tu hana mahusiano mazuri na
MADALALI wa rasilimali za nchi hii, ambao historia
imeonyesha maeneo kadhaa walipoiaminiwa na
kuharibu.Kumpoteza Muhongo kwa sababau tu tangu
kuingia kwake ofisini ameziba mianya ya uchotwaji mkubwa wa
pesa za watanzania kupitia sekta ya madini, na sasa mabepari
wameungana na wabunge wenye husda kupambana dhidi ya kweli
na haki anayosimamia Muhongo.Kumpoteza Muhongo
kwa sababu tu yeye na Katibu mkuu wake Eliakim Maswi, hawana
mawasiliano mazuri na Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe (Hii
inatokana na kitendo chao kudhibiti udalali wa
Rasilimali)Kumpoteza Muhongo kwa sababu tu yeye
na katibu mkuu wake hawana mahusiano mazuri na Mbunge
Christopher Ole Sendeka kwa sababu hizo hizo za utetezi wa
RasilimaliKumpoteza Muhongo kwa sababu tu yeye na
Katibu Mkuu wake wamesitisha mkataba wa kutetewa kisheria na
Mbunge Nilmrod Mkono wa Mkono & Co Advocate ambao mpaka
unavunjwa alishalipwa zaidi ya Bilioni
65.Kumpoteza Muhoingo kwa sababu tu amejitahidi
kupambana kukomesha Mgao na sasa wauza Dizeli na Majenereta
wamekosa sehemu ya kuuzia na kuamua kuunganisha nguvu
kupambana nae. Sisi tunasema, wanaweza
kuunganisha nguvu kupambana na Muhongo na Kumshinda, lakini
sio kwenye Hili la ESCROW. Tunawashuri
wakatafute SKENDO nyingine ambayo angalau iwe na chembe za
ukweli ndani yake.Kwenye Hili la ESCROW
tunaamini, wabunge wamekurupuka, wabunge wametumiwa, wabunge
wamehongwa na wao wamekubali kutumika.KAMATI YA
PAC IMETOA WAPI MAPENDEKEZO YAO?.Msingi mkuu wa
mapendekezo ya ripoti ya kamati ya PAC ulipaswa kuwa ni
Ripoti ya CAG, Tumejaribu kuchambua Ripoti ya
CAG na hatujaona wapi PAC wamepata mapendekezo waliyokuja
nayo, hatujaona nab ado tunaamini kamati hii kama
zilivyowahi kutumika kamati nyingine nayo hii pia imetumika
kisiasa kufanikisha matakwa ya kifisadi.MASWALI
KWA PAC1. Tunaitaka kamati hii itueleze, ni
katika ukurasa wa ngapi, aya ya ngapi, nukta ya ngapi
iliyopo kwenye ripoti ya CAG inayosema kwamba ESCROW ni MALI
YA UMMA?.
2. Tunaitaka PAC itueleze, ni katika ukurusa wa
ngaopi, aya ya ngapi, nukta ya ngapi iliyopo kwenye ripoti
ya CAG inayosema kwamba MUHONGO na wenzake wamefanya makosa
hivyo wawajibishwe.
3. Tunaitaka PAC ituonyeshe, ni wapi katika
ripoti ya CAG imesema fedha ambazo IPTL imezichukua kutoka
kwenye ESCROW ni BIL ama 321 au 306 kama
wanavyodai.
4. Tunaitaka PAC itueleze, kama kulikuwa na
mchezo mchafu, na wakauthibitisha, iweje wizara ya fedha
isihusike?, kwanini Gavana wa BOT na timu yake na Waziri wa
fedha na Timu yake nao wasihusike kwenye hilo kwa kuwa fedha
ilikuwa kwao?.
5. Kama kweli kulikuwa na mchezo mchafu, iweje
BRELLA, na wizara inayoisimamia ambayo ni Viwanda na
Biashara na waziri wake na timu nzima wasiwajibishwe nao
kusajili kampuni ambayo wanadai siyo halali?.
6. Kama ni kweli kuna tatizo, iweje TRA wakubali
kupokea kodi ya zaidi ya Bil 30 kutoka kwa mbia wa IPTL
ambao ni VIP iliyotokana na mauzo ya hisa 30% kwa PAP?.
Kwanini TRA isiwajibishwe kwa kupokea fedha haramu na
kuziingiza kwenye mapato ya serikali ilihali ikijua ni fedha
haramu?.
7. Kama PAC walikuwa wanachambua Ripoti ya CAG,
kwanini walimwita tena CAG na kutumia mawazo yake binafsi na
ambayo hajayaweka wazi moja kwa moja, na kwanini hawakuwaita
watuhumiwa waliowabaini?. Uko wapi utawala wa sharia
hapa?.
8. PAC itueleze, tangu lini Bunge limekuwa
walalamikaji, waendesha mashtaka, wasikilizaji kesi, majaji,
na waandika hukumu?.
MAPENDEKEZO NA MSIMAMO WETU.Kwa kuwa
Bunge wao wamepeleka maombi yao haramu kwa Rais, nasisi
tunapeleka mapendekezo yetu kwa Rais na kumsihi afanye
yafuatayo.
1. Kwa kuwa Swala zima la ESCROW limegubikwa na
siasa, maslahi binafsi, chuki, wivu na kukomeshana, hivyo
tunamuomba Rais asitekeleze azimio hata moja mpaka kwanza
umma utakapoelewa ukweli halisi wa mbivu na mbichi na kila
lililo nyuma ya pazia kuhusiana na sakata hili
2. Tunamuomba Rais Aunde chombo huru, ili swala
hili lichunguzwe na kufanyiwa maamuzi huru ikiwemo na Tuhuma
za baadhi ya Wabunge kuhongwa, kununuliwa na kuwa mawakala
wa Benki ya Standard Charterd.
3. Tunamuomba Rais, aviagize vyombo vyake vya
ulinzi na usalama viwachunguze wabunge hawa kwa kukubali
kutumiwa, kuhongwa na kununuliwa ili kutuondolea watetezi
wetu wa Rasilimali.
MWISHONi mwendawazimu pekee ambaye,
ama mtu mwenye wivu, chuki au maslahi binafsi kama ilivyo
kwa baadhi ya wabunge na wajumbe wa PAC ndiye atakayeweza
kudharau kazi nzuri nay a kizalendo inayofanywa na serikali
hasa kupitia wizara ya nishati na madini na waziri
wake.
Sisi ni Watanzania, na hawa ni wabunge wetu,
panapotokea wao kufanya madudu kama walivyofanya hivi sasa
tuna wajibu wa kuwaonyesha, kuwaeleza na kuwakumbusha kwamba
haya ni madudu. Na hivyo tunawakemea, kuwakanyqa, na
kuwaambia wasirudie tena kufanya uzembe mwengine kama ule,
kutumia kodi zetu watanzania kwenda kutumiwa na wazungu,
madalali wa rasilimali na mabepari wachache ambao wanaona
mfumo hauwafurahishi. Tuna ushahidi kwamba wapo wabunge
wamehongwa kusema na kufanya
waliyoyafanya.Tunawaahidi watanzania wote na
watetezi wa Rasilimali, kwamba tutazunguka nchi nzima
kuhamasisha watanzania kusimamia ukweli, kutetea haki,
wajibu na kuhakikisha hakuna mtanzania mtetezi wa Rasilimali
ataonewa na wanasiasa wasaka tonge kama ilivyotaka kutokea
hivi karibuni.
Tunaanzisha sasa hati ya maombi maalum kwa Raais
(Petition Form) itakayosainiwa na mamilioni ya watanzania
wanaoitakia mema nchi yetu kumuomba Rias apuuze maazimio
haya ya mabepari, wahujumu uchumi na wasaka tonge
walioungana na wasaka Urais.
Mungu ibariki TanzaniaMungu wabariki
wazalendo na watetezi wa kweli wa Rasilimali.
Imesomwa naShaibu
SufianiKaimu Mratibu Umoja wa wanazuoni vijana
Tanzania
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment