Hao vijana wana mtindio wa akili...riport ya CAG haikuwa ya mwisho katika sakata la escrow...na vijana wasidhani kuwa wapo chuo basi wana akili kuzidi kila mtu.....kazi ya bunge ilikuwa ni kusynthesize report na kupendekeza maamuzi...vyombo vya uchunguzi pia viliagizwa vifanye uchunguzi utaosaidia mamlaka za uteuzi kufanya maamuzi.....hayo matamko ni ya nini? .....wamwache rais afanye kazi yake. Ayayewajibika na awajibike hata kama ni kisiasa....ngupula
'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>Hii yote ni mikakati ya kukiangusha Chama Cha mapinduzi.
>Kama Rais atawasikiliza ambao hawakusikilizwa na wananchi akae akijua kuwa wananchi walilisikiliza Bunge kama wanavyosikiliza na kuangalia mpira wa Manchester.
>Wanajua kilichoongelewa. Hakuna mwananchi atakayewasikiliza vijana wadogo hao ambao kwenye majukwaa ya siasa wala hawataonekana. UKAWA itakapo simama na kuwakumbusha wananchi kilichoongelewa bungeni na kuwa Rais amekipuuza huo utakuwa mwisho wa CCM. Siamini kama rais au wasaidize wake watawasikiliza hawa vijana wa vyuo hata wangekuwa na la kusema. wamechelesa na huenda ni heri wqakanyamaza.
>--------------------------------------------
>On Tue, 12/16/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
>
> Subject: [wanabidii] KUUNGA MKONO KAULI YA JUMUIYA YA WANAZUONI VIJANA TANZANIA
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Tuesday, December 16, 2014, 11:45 AM
>
> UMOJA
> WA
> WANAZUONI WA VYUO VIKUU DODOMA KUUNGA MKONO KAULI YA JUMUIYA
> YA WANAZUONI
> VIJANA TANZANIA ILITOLEWA JANA MJINI DAR ES SALAAM.
>
>
>
> UTANGULIZI.
>
>
>
>
>
> SISI ni mkusanyiko wa wanazuoni wanaosoma vyuo vikuu
> mbalimbali mkoani Dodoma,
> tumejitokeza kuzungumza na nyinyi waandishi wa habari
> kuhusiana na mambo
> mbalimbali yanayofanyika nchini ikiwemo suala zima la
> AKAUNTI YA TEGETA ESCROW.
>
>
>
> Pia, tumejitokeza kuunga mkono kauli ya Jumuiya yetu ya
> vijana wanazuoni juu ya
> tamko lao walilolitoa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
> jana na kupewa nafasi
> kubwa kwenye vyombo hivyo ikiwemo magazeti na radio.
> Tunashukuru sana kwa hilo
> ndugu waandishi.
>
>
>
> AKAUNTI YA ESCROW
>
>
>
> Kabla hatujazungumza tunapenda kuwaasa hasa wanasiasa jambo
> lolote ukiwa hauna
> uhakika nalo, usipende kulizungumzia mbele ya umma kwa kuwa
> mwanasiasa ni mtu
> makini na mwenye uelewa mpana wa mambo.
>
>
>
> Tumekaa kwa muda mrefu tukisoma taarifa mbalimbali kwenye
> magazeti na kwenye
> mitandao kuhusiana na suala la akaunti ya ESCROW ili kujua
> ukweli wa suala
> hilo, ambalo kwa kiasi kikubwa linazidi kupotoshwa.
>
>
>
> Tunafurahi sana kupata nafasi hiyo ya kuzungumza na nyinyi
> waandishi wa habari
> kwa kuwa ni watu muhimu na mtaweza kuhabarisha umma juu ya
> usahihi wa
> taarifa
>
>
>
> kuhusiana na sakata hilo, baada ya kufanya utafiti wa
> kutosha na kuelewa mambo
> mengi.
>
>
>
> Sisi wanazuoni tunawajibu mkubwa wa kuitetea nchi na
> kuisemea pale tunapoona
> kuna jambo baya limefanyika, kwa kuwa uelevu wetu umetokana
> na kupata elimu
> bora iliyotokana na kodi za watanzania wenzetu na hatupo
> tayari kuona mambo
> yakienda mrama.
>
>
>
> Tukiwa kama wasomi vijana, tuna wajibu kwa taifa letu
> kulipigania ili
> kuhakikisha kuna usawa kwa kuwa Tanzania ni taifa huru na
> linahitaji kuwepo kwa
> wanasiasa huru na wenye maono ya kuifikisha nchi pahala
> salama kwa kuwa uwezo
> na maadili yao ni muhimu.
>
>
>
> Pia, tunapaswa kuhakikisha nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata
> misingi imara ya
> ukweli, uwazi, uwajibikaji na kuzingatia uhuru wa haki kwa
> kila mtu na
> watanzania waelewe kuwa kujiuzuru sio ushujaa au uzalendo.
> Jiulize wote
> waliojiuzuru ni wazalendo wa kweli wa nchi yetu?.
>
>
>
> Wabunge wametufedhehesha, wametunyong'onyesha na
> wameonyesha ni jinsi gani
> wameshindwa kuwa wakweli kwenye kusimamia sheria na uhuru wa
> haki wa kila
> mtu(natural justice) kwa kutengeneza tuhuma na kisha kumtaka
> Rais Jakaya Kikwete
> awawajibishe watu hao.
>
>
>
> Sote sie tunakumbuka kwamba hivi karibuni Ofisi ya Mdhibiti
> na Mkaguzi Mkuu wa
> Hesabu za Serikali (CAG) ilitoa taarifa ya uchunguzi wake wa
> akaunti ya TEGETA
> ESCROW kwa serikali na kwa bunge na ripoti hiyo iliweza
> kuvuja kwenye mitandao
> mbalimbali
>
>
>
> Kuvuja
> huko kulitusaidia sie kupata taarifa za ripoti hiyo na
> kuzisoma kwa umakini,
> ueledi na ufanisi mkubwa na kugundua kinachozungumzwa sasa
> ni mchezo wa kisiasa
> unaochezwa na wabunge wakishirikiana na wafanyabiashara
> mbalimbali.
>
>
>
> Ripoti
> iliarifu juu ya hadidu za rejea 11 ilizopewa, pamoja na
> kutaja ofisi mbalimbali
> zilizoanza kuomba kufanyiwa uchunguzi kabla ya Ofisi ya
> Bunge, ikiwemo Ofisi ya
> Waziri Mkuu na Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
> Madini.
>
>
>
> Jitihada
> za ofisi hizo, zilisaidia kupatikana kwa taarifa bora na
> yenye mantiki kwa
> jamii na ndio maana katika uchunguzi wake, CAG hakusema kuwa
> ESCROW ni fedha za
> umma au la, pia alisema kuwa uchunguzi wake haukumtia
> hatiani mtu au kikundi
> chochote cha watu kilichohusika katika sakata hilo. Je
> tujiulize yale
> yanayozungumzwa kwenye mitandao na uamuzi wa kamati ya Bunge
> ya Hesabu za
> Serikali(PAC) imepata wapi?.
>
>
>
> Tunatambua
> kilichofanywa na PAC kugeuza ripoti ya CAG na kuitengeneza
> ripoti yao isiyojaa
> uzalendo wa hali ju ni kumharibia jitihada za Rais Jakaya
> Kikwete kuonekana ni
> kiongozi anayeongoza serikali ya kifisadi wakati sio kweli.
> Rais Kikwete
> amefanya mambo mengi makubwa kwa nchi hii na tutamkumbuka
> kwa ukarimu wake
> aliokuwa nao licha ya kuwepo kwa upuuzi, uzandiki
> unaoendeshwa na watu hasa
> wabunge huku yeye mwenyewe akiwa anacheka na kutoa ushahidi
> wa kila jambo
> kwenye vyombo vya habari.
>
>
>
> Katika
> ripoti ya CAG pamoja na viambatanisho vyake
>
>
>
> vyote,
> tumesoma na kuvirudia na hakuna iliyosema kwamba Waziri mkuu
> amelisababishia
> hasara Taifa au mawaziri wengine nao wameshiriki kuliletea
> hasara taifa huku
> wabunge wenyewe wakiwa wanafanya shughuli za kitaifa
> kishabiki, kichuki,
> kimaslahi binafsi bila kuzingatia ukweli na misingi ya
> Utawala bora.
>
>
>
> Ndugu
> zangu, kwenye Ripoti ya CAG kumesema wazi kwamba, serikali
> imefanya jitihada
> stahili kuhakikisha taratibu zinafuatwa ili kujiondoa kwenye
> madhara yanayoweza
> kutoke baada ya pesa kufuatwa.
>
> Ripoti
> ya CAG haijamtia hatiani mtu yeyote je kinachozungumzwa na
> PAC ni sahihi? Au
> mapendekezo yao kwa Rais yamezingatia utawala bora?.
>
>
>
> Haya
> ni maswali ambayo PAC inapaswa kuyajibu ili umma wa
> watanzania na sisi wasomi
> tuelewe kuliko kukaa juu juu na kuimba wimbo wa Waziri wa
> Nishati na Madini,
> Profesa Sospeter Muhongo ajiuzuru, au Katibu wake, Eliakim
> Maswi ajiuzuru au
> hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema naye
> ajiuzuru. Je
> kujiuzuru kwao ndio suluhisho la matatizo au ndio
> uzalendo?.
>
>
>
> Tunashindwa
> kuelewa misingi ya kamati ya PAC ya kutaka kuwajibishwa kwa
> watu hao bila ya
> kuwa na hatia yeyote ikiwa taasisi ya ukaguzi inasema hakuna
> kosa
> lililofanyika, Je PAC wamepata wapi makosa?.
>
>
>
> MAPENDEKEZO
> NA MSIMAMO WETU.
>
>
>
>
>
> Kwa
> kuwa Bunge wao wamepeleka maombi yao haramu kwa Rais, nasisi
> tunapeleka
> mapendekezo yetu kwa Rais na kumsihi afanye
> yafuatayo
>
>
>
> 1. Kwa
> kuwa Swala zima la ESCROW limegubikwa na siasa, maslahi
> binafsi, chuki, wivu na
> kukomeshana, hivyo tunamuomba Rais asitekeleze azimio hata
> moja mpaka kwanza
> umma utakapoelezwa ukweli halisi wa mbivu na mbichi na kila
> lililo nyuma ya
> pazia kuhusiana na sakata hili
>
> 2.
> Tunamuomba Rais aunde chombo huru, ili swala hili
> lichunguzwe na kufanyiwa
> maamuzi huru pamoja na kuviagiza vyombo vyake vya ulinzi na
> usalama
> viwachunguze wabunge hawa kwa kukubali kutumiwa, kuhongwa na
> kununuliwa ili
> kutuondolea watetezi wetu wa Rasilimali.
>
>
>
> Mungu
> ibariki Tanzania.
>
> Imesomwa
> na
>
> Josephat
> Joachim
>
> 0768-911840
>
> ………………………………………………………
>
> Katibu
> Mtendaji wa Umoja wa wanazuoni wa Vyuo Vikuu
> Dodoma.
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment