Sunday, 14 December 2014

Re: [wanabidii] KIKWETE USIWASIKILIZE 'BUSH LAWYER' KATIKA ESCROW - UHARIRI WA MTATIRO

Sawa Bwana Mtatiro,nakubaliana na wewe kwa upande fulani kwa sababu hata wakati naisoma hii article kichwa kiliniuma kwa namna mada zilivyochanganywa bila kufuata logic flow, paragraph hazina uhusiano n.k . Lakini kichwa kilizidi kuuma baada ya kugundua kuwa huyu ni mwandishi by proffesional!.

Mimi ni mtafiti lakini pia ni mwandishi kwa dhana kuwa waandishi wote ni watafiti na watafiti wote ni waandishi.

Upande ambao sikubaliani na wewe ni kuhusu njia hii ya ukosoaji, sina uhakika kama maadili (ethics) ya uandishi na utafiti yanaruhusu njia hii ya ukosoaji.



Omary Iddy,DAGROFORESTRY RESEARCH TANZANIA FORESTY RESEARCH INSTITUTE(TAFORI)P.O BOX 1257,SHINYANGATANZANIA.Tel:+255 28 276 3249MOBILE:+255 713 728 672FAX:+255 28 276 2198EMAIL:eidomari@yahoo.com

--------------------------------------------
On Fri, 12/12/14, 'julius mtatiro' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] KIKWETE USIWASIKILIZE 'BUSH LAWYER' KATIKA ESCROW - UHARIRI WA MTATIRO
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "Leila Sheikh' via Mabadiliko Forum" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "Moderator Mabadiliko" <moderator.mabadiliko@gmail.com>, "mabadilikoforum@googlegroups.com" <mabadilikoforum@googlegroups.com>
Date: Friday, December 12, 2014, 4:27 PM

Wadau,Dada
Happiness,
Mimi sina ugomvi na maudhui ya makala haya ya
mwandishi Happiness Katabazi japokuwa yanajichanganya,
hayaeleweki na hayajapangwa. Ugomvi wangu uko kwenye kiwango
cha uandishi, haiwezekani mwandishi aliyesomea uandishi wa
habari akaandika makala moja ina makosa zaidi ya zaidi 623
ya kisarufi, kimantiki na kimaana (kwa
wakati mmoja) - Nimeweka kiambatanisho cha baadhi ya makosa
niliyothibitisha.
Mbaya
zaidi, dada Happiness anasema anasomea Sheria. Sasa
haiwezekani Mwandishi mzoefu wa Habari akaandika kwa kiwango
hiki cha uandishi halafu tena huyohuyo akawa anasomea sheria
"yeye mwenyewe anajiita mjuvi wa sheria". Sijawahi
kuona uandishi wa habari wa namna hii na ama uanasheria wa
namna hii. Na kama tuna waandishi wa namna hii na wanasheria
wa namna hii, ndiyo maana nchi inaendelea kuibiwa huku hao
hao waandishi na wanasheria wakiendelea bila aibu kwenda
hadharani na kutetea wezi.
Pamoja na tabia ya dada Happiness kunijia juu sana
na kuvurumusha matusi na dharau juu yangu kila nikimkosoa,
leo nimeamua kwenda mbali zaidi, kuonesha udhaifu mkubwa  katika maandishi yake. Kama
atakuja juu tena sasa hivi wacha aje juu lakini moja ya kazi
zangu siku za usoni itakuwa ni kumsaidia kuhariri kila
aandikacho, ili hiyo inayoitwa "taaluma ya uandishi wa
habari" isiendelee kutiwa aibu kuu. Kwa wasiofahamu,
mimi pia ni mtalaamu wa masuala ya lugha katika ngazi ya
cheti, walau ntatoa mchango wangu kwake.  

Julius Mtatiro,Cert in Linguistics(Nairobi), B.A(Hons)- Dar,
M.A(Hons)- Dar, LLB (Candidate) - Dar,

Freelance Translator and Private Consultant in
Administration, Education and Political
Science.

P.O Box 10979, Dar Es Salaam,

Phone; +255787536759,
Email;
juliusmtatiro@yahoo.com.+255717536759CallSend
SMSAdd
to SkypeYou'll
need Skype CreditFree via
Skype


On Friday, December
12, 2014 4:07 PM, 'nngajilo' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:



Dada nilikuwa mpenzi sana wa kusoma
makala zako lakini kwa makala yako hii naona na wewe umepata
mgao.a

Sent from my Huawei
Mobile

'Happiness
Katabazi' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Kwanini ufikiri? Onyesha
paragraph ambayo inayonyesha Mimi natetea maovu.usiseme
kijumlajumla.minimendika kwa kutumia Mifano Mbalimbali na
wewe Msomaji AMBAE umekosoa makala yangu Huna budi Kuonyesha
KWA vielelezo Udhahifu Katika hii makala yangu ili
nikubaliane na wewe

Sent
from my iPad
On Dec 12, 2014, at
11:40 AM, "'nngajilo' via Wanabidii"
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

Makala yako inaonyesha wewe unatetea uovu
uendelee kufanyika katika nchi hii,nafikiri ni kweli pesa
iliibiwa.

Sent from my
Huawei Mobile

'Happiness Katabazi' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

KIKWETE
USIWASIKILIZE  'BUSH LAWYER' KATIKA
ESCROWNa
Happiness Katabazi
IBARA
 ya 37(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 1977 , inasema hivi: ' Mbali na kuzingatia
Masharti yaliyomo katika Katiba  hii, na Sheria za Jamhuri
ya Muungano  Katika Utendaji  wa kazi  na shughuli
 zake, Rais  atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri
 atakaopewa  na Mtu yeyote , isipokuwa  tu pale
anapotakiwa na Katiba   Onyesh  au na Sheria  nyingine
yoyote  kufanya jambo lolote kulingana  na ushauri
 anaopewa  na mtu au mamlaka yoyote.
Na
Ibara ya 4(2) ya Katiba hiyo inasomeka hivi ; " Vyombo
 vyenye mamlaka ya Utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri
ya Muungano NA serikali ya Mapindunzi ya Zanzibar ; vyombo
vyenye  mamlaka  ya kutekeleza  Utoaji haki vitakuwa ni
Mahakama  na Serikali  ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama
ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , na  vyombo  vyenye
mamlaka  ya kutunga Sheria na kusimamia  utekelezaji wa
shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la
Wawakilishi.
Ibara
ya 4(3) ya Katiba hiyo pia inasema; " Kwa ajili ya
utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya
Muungano , na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya
shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa Katika Ibara hii
, kutakuwa na Mambo ya Muungano Kama yalivyoorodheshwa
 Katika Nyongeza ya kwanza  iliyoko mwishoni mwa Katiba
hii, na pia  kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano , ambayo
ni mambo  mengine yote yasiyo mambo ya Muungano.
Ibara
ya 4(4) ya Katiba hiyo inasema ; " Kila Chombo
kilichotajwa Katika Ibara hii kitaundwa na kutekeleza
majukumu yake  kwa kufuata Masharti mengine yaliyomo katika
 Katiba hii".
Nimelazimika
kuanza na nukuu hizo za Ibara ya Katiba ya nchi yetu
kwasababu makala yangu ya Leo itazungumzia kuhusu
utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais na dhana nzima ya
mgawanyo wa madaraka  Katika taifa letu ambayo mambo yote
hayo yameanishwa Katika wazi Katika Ibara hizo za
Katiba.
Leo
nitajadili kuhusu  Wimbo Ulianza kuchuja kwa kasi ya
 Mwendo wa ' Pikipiki ambayo hainaga  rivasi' wa
ESCROW.
Itakumbukwa
Kuwa wiki Tatu zilizopita Wimbo wa Escrow ulshika kasi kila
Pembe ya nchi na kusababisha kuacha majeraha Katika mihimili
yote mitatu ya nchi yaani serikali, Bunge na
Mahakama.
Sakata
hili la Escrow lilikuwa na sura nyingi ambazo kwa jinsi
lilivyochukuliwa liliweza kulichanganya taifa na kujikuta
katika mgongano wa hali ya juu. Katika hali ya kawaida,
Tanzania imeshawahi kupita katika kashfa nyingi kama zile za
Richmond na Buzwagi na hata EPA, hivyo mambo ya kuwepo
ubadhirifu au harufu ya ubadhirifu katika kuta au dari za
serikali si jambo geni kwa nchi yetu japokuwa kutokuwa geni
huko hakuhalalishi vitendo vyenyewe.
Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mambo mengine
inatoa si haki na wajibu wa raia tu bali pia uwajibikaji wa
kisiasa na kiutendaji kwa watu mbalimbali waliopewa dhamana
ya kushughulikia masuala ya taifa kwa niaba ya wananchi. Ni
wazi kuwa katika serikali kuna dhana ya uwajibikaji wa
kiwaziri yaani kwa kiingereza "Ministerial
Responsibility". 
Katika
dhana hii ya uwajibikaji kuna uwajibikaji wa Waziri Mmoja
mmoja (Individual responsibility) na uwajibikaji wa Mawaziri
wote kwa ujumla (collective responsibility).
 Katika
uwajibikaji binafsi, Waziri mwenye dhamana ya jambo Fulani
katika wizara yake anawajibika kwa matendo yake na ya
watumishi wake katika wizara yake hata kama Waziri huyo
hakutenda yeye jambo hilo. 
Hivi
ndivyo ilivyotokea katika sakata la operesheni tokomeza
ambapo tulishuhudia mawaziri wakijiuzulu nyadhifa zao kwa
matendo maovu yaliyofanywa na askari au watumishi waliokuwa
chini ya Wizara zao. Ni hivyo hivyo hata Edward Lowassa
aliwajibika japokuwa hakukuwa na ushahidi wa kuchukua hata
senti moja.
Uwajibikaji
wa kijumla pia ni jambo la kawaida katika nchi nyingi za
jumuiya ya Madola hasa zinazofuata mfumo wa kiingereza
katika kuendesha serikali zake. 
Bunge
lina uwezo wa kumwajibisha Waziri Mkuu kwa mujibu wa Katiba
 ambapo matokeo yake ni kuanguka kwa baraza lote la
mawaziri. 
Vivyo
hivyo Rais anao uwezo wa kuwawajibisha mawaziri wake mmoja
mmoja au kuvunja kabisa baraza la Mawaziri kama alivyofanya
Rais Ally Hassan Mwinyi mwaka 1994. 
Jambo
hili ni la kisheria pia kisiasa. Tofauti na ilivyo kwa
watumishi wa umma ambao mamlaka zao za nidhamu ni kwa mujibu
wa sheria ya utumishi wa Umma ya mwaka 2002, Mawaziri na
wateule wengine wa Rais huweza kuwajibishwa bila kuzingatia
sheria ya utumishi wa umma kwa kuwa watu hawa hushika na
kuendesha nyadhifa zao kwa matakwa ya Rais (at the pleasure
of the President).
Hata
hivyo, ili Rais amwajibishe mteule wake au ili bunge
limwajibishe Waziri Mkuu au kumlamzimisha waziri kujiuzulu
au hata waziri mwenyewe binafsi kutangaza kujiudhuru, lazima
kuwe na sababu za msingi. 
Sababu
hizi lazima ziwe za wazi na zenye mashiko na ushahidi ambapo
mtu yeyote haitaji kuingizwa darasani kutambua kuwa kuna
kosa limefanyika na hivyo mtu Fulani anatakiwa kuwajibika au
kuwajibishwa. 
Moja
ya sababu za kuwajibishwa popote pale inaweza kutokana na
kukosa uadilifu kwa mtendaji husika, wizara yake kukiuka
sheria au taratibu Fulani, au kuvunja haki za binadamu au
kukitokea kashfa kama hii ya escrow, Richmond, epa nk ambazo
zinagusa moja kwa moja wizara husika au mtu
husika.
Sakata
la escrow kama yalivyo masakata mengine yote yaliyowahi
kutokea hapa nchini liligusa hisia za watu wengi hasa
ukichukulia kuwa nchi  bado inakabiliwa na changamoto
nyingi za kifedha na umasikini na escrow ilitokea kipindi
ambacho hata MSD walikuwa wakilalamikia kutokuwa na Fedha
 za kununulia na kusambaza dawa mahospitalini. 
Hivyo
ni wazi kuwa mtu yeyote kusikia bilioni 300 zimetafunwa na
wachache lazima apate jazba. Siwezi kusema moja kwa moja
kuwa suala la Escrow  pengine hakukuwa na ubadhirifu kabisa
au hata kama hakukuwepo ubadhirifu basi hakuna watu kwenye
ofisi zao ambao hawakutenda kwa makini hivyo kuwezesha
baadhi ya taratibu kukiukwa au pesa kutolewa katika
utaratibu usiokubalika kisheria. 
Vyombo
vya uchunguzi vitatueleza zaidi. Waswahili husema, vita ya
panzi faida ya kunguru, na penye ugumu penyeza rupia, na pia
adui mwombee njaa hata kama shujaa.
Sakata
la escrow pamoja nalo limeibua au kuwezesha mambo mengi
sana. Limekuwa kama mtego wa panya ambao waliokuwemo na
wasiokuwemo wote wanaingia na baadhi ya watu wakauchukulia
huu mwanya kutiumiza haja na matakwa yao ya
kisiasa. 
Hili
lilithibitishwa na uchangiaji bungeni na hata ushabiki
uliokuwa ukiendelea nchini. Naweza kusema sakata hili
limekuzwa sana kuliko uhalisia hasa kutokana na wakati ambao
limetokea. 
Sakata
kwa bahati mbaya sana limeibuka au kupangwa kuibuliwa wakati
watu wana nia mbalimbali za kisiasa na tayari makundi
mbalimbali yameanza kujipanga kikambi, na kuwekeana mbinu
chafu za kuharibiana. 
Ugomvi
binafsi, wivu na vita kati ya vyama vya siasa vilitawala
zaidi kuliko sheria, kanuni na taratibu. Hata kama escrow
kweli ingekuwa watu wameiba Fedha  bado ushughulikiaji wa
watu waliohusika nao unatakiwa kufuata Katiba  ya nchi,
sheria na taratibu za nchi na sio matakwa ya watu binafsi na
kiu tu ya kuona Fulani hayupo kwenye cheo chake.
Baadhi
ya watu walijifanya   wao Wanaofahamu zogo la Escrow
kindakindaki kumbe uzushi mtupu kadri ya uwezo wao waliweza
kutumia baadhi ya vyombo vya habari,majukwaa ya kisiasa ,
 bunge kuaminisha umma kupandikiza Chuki kwa wananchi Kuwa
baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhungo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Eliachim Maswi , Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji
Fredrick Werema , Jaji  Mujulizi, Jaji Luhangisa na wengine
Kuwa ni wezi wa Fedha za umma,hawatakii Mema nchi yetu,
majambazi sugu na wajiudhuru nyadhifa zao.
Watu
hawa walifanya hivi bila kujali haki za watuhumiwa kujieleza
na wala kujali ukomo wa kazi wa mhimili mmoja wa dola kwa
mwingine. 
Haki
ya kujieleza ni ya msingi sana kwa binadamu yeyote
anayetuhumiwa hata kama kosa lake ni kubwa au linakera kiasi
gani na ndio maana kila siku inasisitizwa watu kutochukua
sheria mkononi.
 Haki
hii ya kusikilizwa ina historia ndefu na wanasheria
wanaamini kuwa haki hii inatokana na Mungu mwenyewe, kwamba
Mungu hatamuadhibu mtu bila kumsikiliza na ndivyo
alivyofanya kwa Adam na Eva.
Pale
Bustanini Mungu alimwita Adam kwa kumuuliza " Adam Uko
wapi?"  Adam akajibu "nilisikia sauti yako nikaogopa na
kujificha kwa kuwa niko uchi". 
Mungu
akamuuliza nani amekuambia uko uchi? Na kwa nini mmekula
tunda la mti wa katikati niliowakataza? Adam akajibu, sio
mimi ni huyu Mwanamke uliyenipa. 
Kisha
Mungu akamuuliza mwanamke maswali. Baada ya kujitetea, Mungu
akapitisha adhabu ya kuwafukuza bustanini na kumpa Adam
adhabu ya kuilima nchi na kumletea matunda na kwa mwanamke
kuzaa kwa uchungu na hatimaye akaweka fitna kati ya nyoka na
mwanadamu kwa kusema binadamu watamponda nyoka kila
wamwonapo na nyoka atawagonga kisigino wanadamu. 
Kwa
kufanya hivyo inaaminika kuwa Mungu aliwapa wanadamu wa
kwanza nafasi ya kujitetea kabla ya kuwahukumu. Je, sisi ni
nani wa kuhukumu kabla ya kuwapa wengine nafasi ya
kujitetea?
Siku
ile PAC inasoma ripoti yake, kila mtu aliamini kuwa yote
yaliyosemwa na PAC yalikuwa ya ukweli na asilimia kubwa ya
watu walitamani siku ile ile Muhongo, Sethi, Werema, Pinda
wajiuzulu na ikiwezekana kukatwa vichwa vyao. 
Lakini
hali ilibadilika siku ya pili baada ya Muhongo kuanza kutoa
utetezi wake, ambapo aliwabadilisha kabisa kile watanzania
walichokiamini kutoka PAC na baadhi wakaanza kuona hana
makosa na hata vichwa vya magazeti vilithibitisha hili.
Taifa likagawanyika na hata bunge lenyewe. 
Utetezi
wa Profesa Muhongo ulionekana ni wa kisomi wenye vielelezo
na usio wa kubabaisha. Ni kutokana na utetezi huuu
majadiliano ya bunge yalichukua sura tofauti kabisa, na
ndipo  walipojitokeza walioanza kumtetea na wale walioanza
kuishambulia serikali bila kujali mgawanyo wa madaraka
(separation of powers).
Tuliokuwa
  tukifuatilia mjadala huu tangu mapema mwaka huu
ulivyoanza hadi hadi Novemba 29 Mwaka huu  ilipomalizika
Bungeni na  Bunge lilipotoa maazimio yake kuhusu Wimbo huo
wa Escrow kwa kuagiza vyombo vinavyohusika na masuala ya
uchunguzi na Maadili vifanyie kazi maazimio hayo ya Bunge
ambayo maazimio hayo yalitaka     Majina '
yaliyorushwa ' Katika  Wimbo huo wa Escrow uliotungwa
na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila na kuwekwa
'sauti na uzushi ' na Mbunge wa Kigoma Kaskazini
,Zitto Kabwe wachunguzwe.
Mei
18 Mwaka huu, niliandika makala iliyokuwa na kichwa Cha
Habari kisemacho ' KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE'. Na
baadhi ya mambo niliyo yataadharisha Katika makala hiyo
ndiyo yalikuja kujitokeza Katika mjadala wa Escrow Novemba
Mwaka huu.
Nampongeza
  Spika Anne Makinda na Timu yake Kwani  , ameonyesha
ameiva kiutendaji na ana heshimu   dhana nzima ya mgawanyo
wa madaraka hivyo Bunge siyo Chombo peke yake na Chenye
maamuzi ya mwisho Katika kila jambo ndiyo Manaa Makinda mara
kwa Mara alikuwa aliwaambia wabunge wakati kibao Cha Escrow
kikitumbuizwa bungeni Kuwa yeye ni Bush Lawyer  hivyo
anaitaji kujifunza na kuwataka wabunge wengine ambao ni Ma
Bush Lawyer Kama yeye Wakubali kujifunza kuhusu
Sakata.
Kwasababu
 amebaini kuna baadhi ya wabunge wanachangia maoni kuhusu
Wimbo huo lakini hawafahamu Maudhuhi ya Wimbo huo jambo
ambalo ni kweli Kwani kuna baadhi ya wabunge walikuwa
wakitoa maoni Yao ambayo ukipata zama Maoni Yao kwa jicho la
Sheria unaishia kuwaona ni mapunguani wa akili.
Tulishuhudia
baadhi ya wabunge wakisema Profesa Muhongo na wenzake ni
wezi wa Fedha hizo za umma wakati hata CAG Katika ripoti
yake ameshindwa Kusema wazi wazi Fedha za Escrow ni za umma
au laa lakini wabunge wale ghafla wakajigeuza wao ndio CAG,
Mkurugenzi wa Mashitaka  (DPP) na kuanza kuwatungia
mashitaka Profesa Muhongo na wenzake ni wezi wa Fedha za
Escrow ,wameisababishia Tanesco Hasara ya mabilioni na ni
majambazi sugu wakati wataja yote haya hawajatuonyesha
vielelezo Vyovyote kut ushawishi sisi watu ambao akili zetu
zinafikiti sawa sawa tukubaliane nao.
Maana
Ibara ya 59B (2) ya Katiba ya nchi inasema; ' Mkurugezi
wa Mshitaka atakuwa na uwezo  wa kufungua,kuendesha na
kusimamia mashtaka yote nchini.Na at ateuliwa na Rais
.Tuwaulize hawa wabunge, wanasiasa ,wananchi walipora
majukumu ya DPP ya kuwaundia watuhumiwa makosa ,lini Rais
Kikwete aliwateua Kuwa DPP?
Mbali
na wabunge hao kujigeuza DPP kuwatungia Mashitaka viongozi
Hao wa serikali na kidini kuhusu Escrow, pia baadhi ya
wabunge wale waliojigeuza Mahakama, Takukuru,Tume ya Maadili
ya Viongozi wa Umma na Jeshi la Polisi.
Wenye
akili timamu ambao tunafahamu fika nani  yupo nyuma ya
Escrow, tulikuwa tunawaona baadhi ya wabunge ambao
waliojipachika madaraka hayo niliyoyayataja hapo juu Kuwa
uwenda wana matatizo ya akili au uenda fedha wanazodaiwa
kupewa  waliyopewa na watu waliyokuwa wakitaka viongozi hao
waondolewe madarakani bila mamlaka husika kufanya uchunguzi
wao imewapofusha macho hadi wakasahau wao wabunge ni watunga
Sheria ndiyo waliotunga Sheria za kuanzisha Ofisi za
DPP,TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Sheria mbalimbali
zilizoanzisha Taasisi za umma . Aibu sana.
Kifungu
Cha 258(1) Cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya
Mwaka 2002 imetoa Tafsiri ya neno 'wizi'.
Na
ukiifuatilia  ripoti ya PAC na maneno yanayotolewa baadhi
ya wananchi , taarifa ya Benki ya Mkombo,na Hao wanasiasa
uchwara wanaotaka Rais Jakaya Kikwete amtimue kazi Profesa
Muhongo na wenzake ,ni wazi Hakuna ushahidi wowote
unaonyesha hao viongozi wametenda  makosa ya wizi  wa
Fedha za Escrow .
Pia
Hakuna  kosa la  utakatishaji fedha na wala fedha
hazikuchukuliwa katika Benki ya Mkombozi kwa Magunia kama
ilivyodaiwa Kama inavyodaiwa na mambumbumbu wa Sheria
akiwemo Zitto Kabwe ambaye yeye Katika ripoti ya PAC alisema
Fedha za Escow zilipitishwa Katika Benki ya Mkombozi na
waliozichukua waliozichukua kwa Magunia jambo ambalo siyo
kweli kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya
Mkombozi.
Kitendo Cha
Kamati ya PAC siku ile kusoma mapendekezo yake ya awali
ambayo nadiriki Kusema mapendekezo yale ya awali yalikuwa ni
ya jazba Kama siyo ya kutaka kukomoana na kuivuruga
 serikali na ambayo yalikuwa yamevunja dhana nzima ya
mgawanyo wa madaraka na yalikuwa yameegemea  Katika baadhi
ya taarifa za uongo na uzushi sana na uenda pia lilikuwa na
lengo la kuipaka matope Benki ya Mkombozi , waliokuwa
wakiwapatia taarifa za kiuchunguzi uenda ni "
mashushushu wa Kichina yaani mashushushu
Feki".
Kama
hawa ndiyo wa tunga Sheria wetu ambao tuliwashuhudia kupitia
michango Yao bungeni iliyokuwa ikadhihirisha wazi kuingilia
 majukumu ya Taasisi nyingine za umma  wakitaka Muhongo na
wenzake bunge litoe maamuzi ya kuwawajibisha wakati Bunge
halina mamlaka ya kumwajibisha Waziri isipokuwa rais wa
nchi. Tunajifunza nini kutoka kwa baadhi ya wabunge waliotoa
maoni ya aina hiyo?
Tunajifunza
nini kutoka Kwa Kamati ya PAC iliyokuwa ikiongozwa na Zitto
Kabwe ambapo Maazimio ya awali ya Kamati hiyo yalitoa baadhi
ya mapendekezo ambayo binafsi nilisema mapendekezo yale ni
ya kijinga ambayo mwisho wa siku yanaweza kuleta madhara kwa
bunge ,mjumbe mmoja mmoja katika  Kamati ya PAC na kuibua
uasama wa kidini baina ya Zitto na kanisa
Katoliki.
Kwani
Moja ya azimio la awali la Kamati ya Zitto walitaka Benki ya
Mkombozi Itangazwe  ni Benki ya Utakatishaji Fedha
chafu. 
Hii
Kauli ni nzito sana na Ina madhara makubwa Katika Soko la
Ushindani wa Biashara ya mabenki hapa nchi Kwani Benki hiyo
ya Kanisa Katoliki  ,waumini wengine wa Kanisa Hilo na
wananchi wengine wa naitumia na kuamini na kwa mAana hiyo
mdau mkubwa wa Benki ya Mkombozi ni Kanisa Katoliki  wa
Benki ni Kanisa ambalo Kumbe linahusika na Biashara hiyo
chafu ya Utakatishaji Fedha haramu.
Kwa
hiyo Idara ya Usalama wa Taifa, Polisi  zilikuwa zimelala
usingizi wa Pono hadi siku zote hizo zikashindwa kubaini
Kuwa Benki ya Mkombo ni Benki inayotumika kupitisha Fedha
chafu?
PAC
ndiyo wamejifanya wao Ndio wamejifanya TISS, Polisi ambao
ndani ya Miezi mchache tu wamejigeuza makachero waliokubuhu
na wachapakazi ,wakafanya uchunguzi wao wakabaini eti Benki
ya Mkombozi Benki inayotakatisha Fedha chafu.Kituko Cha
Kufunga Mwaka.
Tuiulize
Kamati ya Zitto nayo iliwahi kuhudhuria Mafunzo ya
Ushushushu kule Chuo CPP Moshi ? Maana nijuavyo  Mimi kazi
za upelelezi ni taaluma za watu, watu waliingia darasani
wakafundwa na wakafundika na wametulia kimya wala hawanaga
papa para wala Kutafuta sifa wakati wakifanya kazi
Yao. 
Kamati
ya PAC kwakuwa Nyie siyo wapelelezi Matokeo yake ilienda  
kufanya kazi ya upelelezi ambayo siyo taaluma mliyoisomea
Matokeo yake mmeenda kukusanya vielelezo vingine  vya
kizushi  ambavyo  zilianza kuwaumbua mapema kabisa mfano
taarifa ya Benki ya Mkombozi imewavua nguo  nguo.
Uamuzi
 wa PAC  kukubali kufanyia marekebisho    maazimio ya
awali ya PAC ni wazi ripoti ya PAC bado Ina Mashaka makubwa

Kitendo
Cha Kamati ya Zitto  kuikubali  hoja ya mmoja ya watu
waliotajwa kuchota  Fedha za Escrow ambaye ni  Mwanasheria
mkongwe Andrew Chenge  lililotaka wote waliotajwa katika
Escrow majina yao yafikishwe katika vyombo maalum wafanyie
kazi mapendekezo hayo na siyo Bunge tena Katika dakika za
mwisho ni wazi uenda PAC iligundua mapendekezo yake ya awali
yana mapungufu kisheria na yana puuza dhana nzima ya
mgawanyo wa madaraka (Separation of Power).
Kwa
mtu  mwenye akili timamu na anayefahamu madhara ya azimio
lile,asingethubutu kutoa azimio lile  lililotaka Serikali
itangaze kuwa Benki ya Mkombozi ni Benki ya kutakatisha
fedha chafu mbele ya umma.
Wakati
 PAC haijaonyesha ushahidi wa kuthibitisha hilo Katika
ripoti yake  , Matokeo yake Benki ya Mkombozi imetoa
taarifa yake kwa umma na imekanusha vikali Kuwa Benki yake
haifichi Fedha chafu, watu hawa kuchukua Fedha kwa Magunia
,Fedha zilitoka Benki Kuu Kuja Benki ya Mkombozi kwa mujibu
wa Sheria na Benki Yao na iliwapatia fedha Wahusika
 wahusika kwa utaratibu wa Sheria.
Ndiyo
maana  Wasomi wa fani ya Sheria ambao siyo wanasiasa
wanawadharau sana wanasiasa na wanawaita 'Kunguru'
yaani kazi Yao kubwa ni kubwatabwata tu hata Katika vitu
wasivyo na ushahidi navyo wao wana bwata.
Tujiulize
ni kwanini Kamati ya PAC Imechukua muda mrefu kufanyakazi
yake lakini ndani ya siku saa Chache tu ikakubali kufanyia
marekebisho baadhi ya maazimio yake?
Tujiulize
ni kwanini baadhi ya wabunge wa upinzani Novemba 28 Mwaka
huu, usiku wa Bunge walisusia Kikao wakaondoka lakini Kesho
yake Novemba 29 walivyorejea jioni walikuwa wapole sana na
Kudai eti wametanguliza maslahi ya nchi kwanza na Mbunge wa
Hai( Chadema), Freeman Mbowe akasikika bungeni kwa sauti ya
Upole kabisa akimshauri Waziri Mkuu Mizengo Pinda zaidishe
ukali Kwani amezidi Kuwa mpole mno.
Kama
siyo unafki ni nini.Si ni hawa hawa wapinzani hasa Chama Cha
Chadema walimkalia Kooni Pinda Mwaka Jana, Pinda alipotoa
amri kwa vyombo Vya dola kuwapiga wale wote wasiyotaka kutii
Sheria za nchi?
Tena
wakati Pinda akitoa agizo Hilo, Chadema ndiyo ilikuwa
imeshika kasi kwa kufanya maandamano. Haya Leo hii watu wale
wale waliopinga agizo lile la Pinda Leo hii ndiyo
wanaushawishi Pinda awe mkali?ajabu sana.Nilichokigundua
Katika nchi hii watu wazima ndiyo wanaongoza kwa uongo,
uzushi na tabia mbaya Mbaya.
Kwa
nini Kamati ili kubali kufanyia marekebisho baadhi ya
maazimio yake?Ina maana ilibaini ripoti yake Ina Matundu
mengi  yanayoitaji kuzibwa. Kama ilibaini mapungufu kwanini
sasa tusitilie Shaka pia hiyo ripoti nzima ya PAC uenda Ina
mapungufu mengine zaidi ya hayo waliyokubali kayafanyia
marekebisho dakika za mwisho?
Zitto
ndiyo Mwenyekiti wa PAC ,yeye na Kamati yake wametoa
mapendekezo wakina Profesa Muhongo na wenzake wajiuzulu  na
wachunguzwe.
Lakini
Zitto nayeye kupitia Mvumbuzi wa tuhuma za Ufisadi wa
Zitto,Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde  alitoa
Nyaraka zinazoonyesha Zitto nayeye aliomba Fedha kwa
Singasinga Yule ambaye Katika ripoti ya PAC ya awali Zitto
alitaja Majina ya watu waliopewa Fedha za Singasinga na
Kusema Fedha zile ni chafu na kutaka watu wale wachukuliwe
Hatua ila yeye alivyotuhumiwa kuziomba Fedha zile hakuona ni
Rushwa.
Zitto
Katika historia yake ya Maisha ya siasa amekuwa akipenda
kulazimisha wanasiasa wenzake wanaotuhumiwa kwa tuhuma
mbalimbali wajihuzuru nyadhifa zao eti hiyo ndiyo dhana ya
uwajibikaji.
Lakini
Zitto huyu huyu naye kwa Miaka miwili sasa amekuwa
akituhumiwa na Chama Chake Kuwa ni msaliti wa Chama ,hadi
Chama Chake kilifikia Hatua ya Kumvua nyadhifa zote za
uanachama na hivi sasa Zitto ni Mbunge wa
Mahakama.
Yeye
wakati akikabiliwa tuhuma hizo za Usaliti wa Chama Chake na
sote tunafahamu tuhuma za Usaliti ni tuhuma kubwa sana,
Zitto hakujihudhuru nyadhifa zake  Kama Cheo Cha Ubunge,
Naibu Katibu Mkuu.
 Zitto
alishupaa hadi viongozi wa Chadema walivyomvua madaraka kwa
Kusema huo Umaarufu anaolinga nao amepata kutokana na
Chadema hivyo Zitto siyo maarufu kuliko Chadema jambo ambalo
ni kweli Kwani Umaarufu aliyokuwa nayo Zitto Miaka ile siyo
aliyonayo sasa Kwani HIvi sasa Baadhi ya watu wamekosa Imani
na Zitto kutokana na tuhuma za Usaliti kwa Chama Alichokuwa
alilitumikia cha Chadema.
Kama
Kujihudhuru kwa tuhuma tu na Kujihudhuru kuna mjengea Mtu
heshima, kwanini Zitto asingeanzaga yeye Kujihudhuru ili awe
mfano?Maana na yeye alikumbwa na anaendelea kuandamwa na
kashfa Chungu mbovu zikiwemo za kuhongwa fedha kwaajili ya
kusaliti Chadema?
Hivi
kashfa zilizokuwa zikimwandama Zitto si kashfa nzito kuliko
kile kinachodaiwa kuwa ni kashfa ya Escrow iliyomwandama
Jaji Werema, Profesa Muhongo, Tibaijuka,Maswi?
Watoto
wa mjini tunamuita Mtu msaliti ni  ' Chaja ya Kobe'
.Yaani anatoa Siri za upande mmoja anapeleka upande
mwingine.Maana Chaja ya Kobe Ina Chaji aina zote za Betri za
simu.
Profesa
Muhongo tangu ashike wadhifa wa kuongoza Wizara ya Nishati ,
amekutana na misukosuka mizito ambayo Iliiletea taifa Hasara
kubwa barabara kuaribiwa,baadhi ya wananchi kuumizwa na
nyumba zao kuchomwa Moto baadhi ya wananchi huko Mtwara wapo
magereza na wengine wanakabiliwa na Kesi za jinai kwasababu
walisababisha vurugu kubwa huko Mtwara wakishinikiza Bomba
la Gesi lisijengwe Mtwara Kuja Dar Es Salaam.
Tulishuhudia
Mwenyekiti wa IPP, Reginal Mengi alivyokuwa akikabana Koo na
Muhongo kwa kile kilichodaiwa na Mengi Kuwa Muhongo
anawadharau wafanyabiashara wazawa Kuwa hawana
Fedha.
Tulishuhudia
Katika Bunge la Bajeti la Mwaka huu, jinsi baadhi ya wabunge
walivyokuwa wamempania Profesa Muhongo ili Wawakikishe
Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini isipite.
Lakini
Hila zote hizo zilishindwa Bajeti ikipita, wafanyabiashara
waliokuwa wakidai wana fedha za kutosha ili Wapewe vitalu
Vya gesi walishindwa kwenda kujiorodhesha TPDC na kutimiza
vigezo na bomba la gesi likajengwa Mtwara na Hali ya utulivu
imerejea Mtwara.
Minasema
mnyonge mnyonge ni lakini haki yake mpeni.Kama kuna mazuri
yaliyofanywa na Muhongo chini ya Utawala wake basi Nyie
mabingwa wa fitna  my aseme siyo kila kukicha Kusema Mabaya
ya Muhongo mazuri yake hamuyasemi.
Hivyo
ndiyo maana napongeza uamuzi wa  Bunge chini ya Spika
Makinda kuamua kupeleka maazimio ya bunge kwenye Taasisi za
dola ili zifanyie kazi na wataalamu Kwani hata mwenyekiti wa
PAC yaani Zitto na yeye ni mtuhumiwa.
Ndiyo
maana Nampongeza Spika Makinda na Timu yake kutoka azimio la
kutaka maazimio hayo yapelekwe kwenye mamlaka za dola
zinazohusika na masuala ya uchunguzi zitafanyie kazi
kitaalamu tuhuma hizo maana za Wimbo wa Escrow ambao umeanza
kushuka chati kwa kasi sana.
Maana
Hakuna ubishi PAC haina mamlaka Ya kuchunguza tuhuma za
Uhalifu na kufikisha mtuhumiwa mahakamani ,mamlaka zenye
mamlaka hayo ndiyo zenye jukumu la kufanyia kazi maazimio
hayo ya Bunge.
 Tayari
 Spika Makinda ameishatamka zaidi ya Mara mbili bungeni na
Mara ya mwisho ni Novemba 29 Mwaka huu, akifunga vikao Vya
Bunge Alisema  kuna baadhi ya wabunge wanatumiwa na
wafanyabiashara Kuja kuwasemea Shida zao bungeni na kwamba
siku walikamatwa na polisi NA kufikishwa Mahakamani yeye
hatakuwa Tayari kwenda kuwawekea dhamana na wa akawataka
waache tabia hiyo.
Na
Katika Escrow kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na
mamlaka husika kuwa kuna  mwanasiasa na mfanyabiashara
wenye Nguvu za kiuchumi wamekuwa wakidaiwa kutapanya Fedha
kwa wanasiasa, vyombo Vya Habari na wapambe washikilie Bango
suala la Escrow ili Rais Kikwete aweze kumtaka Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, Profesa Muhongo, Jaji Werema, Maswi na
wengine wajiudhuhuru kwasababu ni wahusika wa ufisadi wa
Escrow.
Minasema
Kama taarifa hizi ni za kweli Hao watu Wawili ndiyo wapo
nyuma ya sekeseke hili lililoacha majeraha Katika Mhimili wa
Mahakama, Bunge na serikali ikabainika hakuna matendo yoyote
ya kijinai,kimaadili yaliyotendwa na watu waliotajwa kwenye
Wimbo wa Escrow, serikali kupitia njia zake inazozijua
iwashughulikie kikamilifu waliopo kwenye sekeseke la Escrow
na wale wabunge ambao Spika Makinda ametuambia wamekuwa
wakipewa Fedha za Wafanyabiashara Kuja kuwasema mambo Yao
bungeni ambayo hayana tija kwa taifa zaidi ya kutaka
kuivuruga nchi kwa kuwapandika wananchi Chuki Mbaya ambayo
mwisho wa siku wananchi wanaanza kumkukia Waziri Mkuu Pinda,
Profesa Muhongo na serikali kwa ujumla Kumbe siyo
kweli.
Tuwaulize
wale wote wanaoshabikia suala la Escrow na wanataka Muhongo
,Pinda Wafukweze kazi Wanaofahamu madhara ya hayo
wanayoyasema?
Kama
wangekuwa wa nafahamu wasingekuwa wanafadhili na kuchochea
taarifa hizo potofu ambazo hata CAG Katika ripoti yake
hajathibitisha Kama Fedha zile ni za umma na kweli zilibwa
na wahusika.
Kumbukeni
Nyie wapayukaji mnaopayuka  bila vielelezo Kuwa Kikwete
awatimue kazi viongozi Hao,  Hao nao wana Mungu anawalinda
na vile vile wanastahili heshima Katika Jamii
inayowazunguka.
Kitendo
Cha kuwaita eti ni wezi wakati  hata hiyo ripoti ya PAC,
CAG haijasema kuna wizi umefanyika Katika Fedha za Escrow
,mnawakosea adabu na Mungu atawadhibu hapa hapa Duniani
licha Tayari Mungu ameishaanza kuwaanika hadharani wale wote
waliokuwa NA ajenda chafu kuhusu Escrow.
Kama
kweli Escrow ni kashfa na Fedha za umma zimeibwa, ni kwanini
kuwepo na taarifa Kuwa kuna mfanyabiashara na mwanasiasa
wanatapanya Fedha kwa baadhi ya wa Bunge na baadhi ya
waandishi wa Habari ili waandike wanavyotaka wao kuhusu
Escrow kushinikiza Pinda, Muhongo ,Werema wajiudhuhuru
nyadhifa zao?
Hivi
Hao waliopo nyuma ya Mpango huu Kama kweli wana uchungu wa
Fedha za Escrow zimeliwa,kwanini sasa wasijitokeze hadharani
kuamasisha wanasiasa,wananchi,vyombo Vya Habari bila
kuvihonga Fedha wakidai Fedha za Escrow?
Kwani
wanatumia Fedha Katika Escrow? Na Nyie Mavuvuzera wa Escrow
Kama kweli ni wazalendo wa taifa Hilo na mnadai Fedha za
Escrow zimeibwa ,kwanini basi hamjitolei kupiga kelele bila
kutumiwa kupokea bahasha? 
Hata
Kama ni kweli wamekula hizo Fedha,wakishajihudhuru nyadhifa
zao Ndio hizo Fedha za Escrow zitarudi?
Haya
hata hizo Fedha zikirudi , Ndio Nyie mavuvuzera wa Escrow
ndiyo mtaitwa mmoja mmoja Mpewe Fedha hizo mkononi mkalipie
Ada watoto wenu mashuleni?
Watanzania
Hasa wanasiasa wanaume acheni tabia ambazo hata sisi watoto
 wa kike siku hizi Tumeacha kuzifanya, yaani ya roho Mbaya
, tabia za Chuki, wivu,uzushi, husuda,kulipizana
visasi,kutaka Kumuendesha Waziri Muhongo jinsi unavyotaka
 eti Kwasaabu alikunyima 'ulaji ' Fulani.
Au
Waziri Mkuu Pinda anataka Kugombea Urais basi unaamua
kumzulia  zengwe ili aonekane hafai ni mchafu, jinsi
unavyotaka  wewe eti kwasababu una Nguvu ya Fedha na mali
.Ni Ujinga wa aina yake na dhambi kwa Mungu Kwani Biblia
inasema ole wake anayeshiriki Katika mashauri ya
uongo.
Eleweni
siyo kila kila kiongozi atakubali kuendeshwa na matajiri
wanavyotaka, kuna baadhi ya viongozi ndani ya serikali
nawafahamu ni waadilifu wa nafanyakazi zao kwa kufuata
Sheria na siyo matakwa ya wafanyabiashara na wanasiasa
uchwara kutekeleza ajenda zao chafu.
Wafadhili
na waasisi wa zengwe la Escrow hivi sasa mnatakiwa Mkae
chini na Kama mnaakili timamu, mjiulize ni kwanini Bunge kwa
kauli Moja lilitoa azimio la Kusema Bunge halina mamlaka ya
kuwawajibisha watuhumiwa.  mwenye mamlaka ni aliyewateua na
Bunge likasema litapelaka mapendekezo kwa mamlaka za
serikali zifanyie kazi.
Nawaombea
 kwa Mungu  watendaji wote waliopo kwenye mamlaka husika
ambazo zinafanyia kazi jambo hilo ,Mungu awaongoze na awape
hekim na busara ili muweze kutenda haki katika kufikia
uamuzi  na anayestahili kupata haki yake na apewe bila
kudhurumiwa.
Historia
inaonyesha ni Bunge hili mwaka 2004 lilizushusha uzushi
mkubwa kuwa aliyekuwa Balozi wa Italia, Profesa Costa Mahalu
amefadha ubadhilifu katika ununuzi wa jengo la Ubalozi wetu
Italia.
Takukuru
wakakurupuka wakamfungulia kesi mahakamani na mwisho wa siku
Aliyekuwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Elvin Mugeta alimwachilia huru Mahalu kwasababu
hakuwa ametenda makosa aliyoshitakiwa nayo na DPP akakata
rufaa Mahakama ya Rufaa na mapema mwaka huu, DPP mwenyewe
akatumia mamlaka yake kuiondoa rufaa ile kwasababu alikuwa
hana haja ya kuendelea na rufaa ile.
Siyo
Siri wakati Kesi ya Mahalu ilipokuwa ikiendelea huku mitaani
tena baadhi ya maofisa wa serikali toka Taasisi za
kichunguzi walikuwa wakisema wazi wazi Kuwa Kesi hiyo
ilikuwa na mkono wa Kikwete na wakati wakisema hayo hawatoi
 ushahidi Kuwa Kikwete alikuwa akimgandamiza
Mahalu.
Ni
tabia Mbaya sana kumzushia Rais tuhuma Kama hizi Kwani
zinaweza kusababisha kupandikiza Chuki baina ya mtuhumiwa na
rais na familia yake.
Tumeshuhudia
Leo hii Mahalu amekuwa msaada mkubwa Katika taifa Hilo hasa
Kipindi kile Cha Bunge Maalum la Katiba, sote ni mashahidi
alivyoweza kutumia taaluma yake ya Sheria na kushirikiana na
wajumbe wenzake kuanzisha Katiba Pendekezwa
imepatikana.
Siku
zote minasemaga Mtu Aliyesoma vizuri Darasani amesoma tu
.Ila nchi hii imezuka tabia ya kudharau wasomi na kumpuuza
kila ushauri au Utendaji unafanywa na wasomi wa ngazi ya juu
Kama Maprofesa, Madaktari.Matokeo yake baadhi ya wasomi Hao
wameamua kukaa pembeni.
Hivi
inaingia akilini tumpoteze Profesa Muhongo,Tibaijuka, Werema
kwa hoja kirahisi rahisi tu ambazo zinatolewa na watu ambao
Tayari nao tunawatilia Mashaka uadilifu wao? Tujipe muda
kwanza Tusubiri uchunguzi wa vyombo Vya dola vitatuleta
majibu gani.
Ni
wabunge hawa hawa walimwandama aliyekuwa Katibu wa Wizara ya
Nishati  na Madini, David Jairo   Kuwa ni kiongozi jeuri,
aliyetoa Rushwa kwa wabunge ili Bajeti ya Wizara yake ipite,
lakini Makinda alikataa akasema Bunge lake halina mamlaka ya
kumwajibisha Jairo hivyo maazio ya Bunge an aagiza yapelekwe
kwenye Taasisi husika zitafanyie uchunguzi.
Kweli
Taasisi zilifanywa uchunguzi wake kitaalamu na mwisho wa
siku sijatoka na ripoti Kuwa Jairo hakutenda makosa
aliyedaiwa Kutenda na wabunge hivyo Jairo.
Wazushi
Hao ambao wanaomzushia  Rais Kikwete wapo kila kona  Kwani
hata Sakata hili la Escow huku mitaani ,walidiriki Kusema
zogo la Escrow limeundwa  kwa makusudi na Kikwete Kwani
Kikwete amekuwa na tabia ya Kuzusha zogo halafu anaenda nje
ya nchi anatuacha tuparulane yeye anafuatilia  zogo Hilo
kupitia mitandao na Televisheni akiwa nje ya nchi huku
akicheka.
Wazushi
Hao walinitaka nikumbuka Enzi za zogo la Oparesheni Tokomeza
Ujangili ,rais Kikwete alilijua zogo Hilo litalipuka baada
ya muda mchache yeye kufika nje ya nchi.
Kwa
hiyo zogo la kashfa ya Oparesheni Tokomeze Ujangili
liliposhika kasi na Desemba Mwaka Jana Bungeni mawaziri
watatu akiwemo Dk.Mathayo David, Balozi Kagasheki na
Dk.Emmanuel Nchimbi na Shamsi Vuai Nahodha  yeye Kikwete
alikuwa nje ya nchi ila alikwenda huko eti kwa Lengo la Kuja
kujiokosha Mbele ya safari Kuwa wakati zogo Hilo lilitokea
yeye halikuwa hajui na alikuwa nje ya nchi.
Watu
wengine wanasema Kikwete hawezi kuwachukulia Hatua wadaiwa
Kwasababu zogo Hilo la Escrow linaiusu familia yake yaani
mkwe wake aliyemuona Mtoto wake wa kwanza na mwanae wa
Kiume,ndiyo taarifa hizo Mbaya zinasambazwa kwenye mitandao
ya kijamii kwa sasa. Ukweli au uongo wa hili wanaujua
wasambazaji na watengenezaji wa SMS hiyo.
Vyovyote
Iwavyo minapenda kutoa raia kwa wananchi wenzangu waache
tabia ya kushabikia na kutoa hukumu Katika  mambo ambayo
hawayajui chimbuko  lake Kwani mwisho wa siku wanaonekana
ni wendawazimu Mbele ya wajuzi wa mambo.
Maana
huku vijiweni mitaani tunawashuhudia wanaume wazima na ndevu
zao wanazungumzia jambo la Escrow  bila woga wanasema
wanataka Fedha zao zilejeshwe na Hao viongozi ni wezi
wafikishwe.
Ukiwahoji
ni kiasi gani Cha Fedha kimeibwa hawajui?Fedha zile zilikuwa
ni mali ya umma au mtu binafsi hawajui? Kilibwa nani na lini
hawajui? Wanafahamu kosa la wizi ili lithibitishwe ni lazima
kuna vitendo gani vimetendwa na mtuhumiwa
hawajui? 
Ushahidi
 wa viongozi Hao wa umma kuiba Fedha hizo wanao wanajibu
hawana ila walisoma taarifa za Escrow kwenye magazeti basi
nao wameamua kuwaita viongozi wale ni wezi eti kwasababu
Gazeti limesema.Ujinga wa aina yake.
Ni
hatari sana kwa taifa Kuwa na watu wa aina hii ambao ni
waropokaji na wasiyotaka kufanyia utafiti kwa kina jambo
Fulani ndiyo watoe Itimisho.
Wao
wanatoa itimisho Kabla hata ya kujua undani wa jambo husika
wanalolitaka ikiwa.  Mnajichumia dhambi bure kwasababu
mnashikiriki Katika mashauri ya uongo.
Niitimishe
kwa kutoa rai yangu kwa Rais Kikwete siku ikifika ya yeye au
Taasisi zake kutolea uamuzi jambo Hilo,watende haki  bila
kutoa watu kafara kwa Kigezo tu cha kujisafisha Chama Cha
CCM kuelekea uchaguzi Mkuu na serikali za Mitaa.
Kwa
utafiti wangu niliofanya zogo la Escrow haliwezi kusababisha
wananchi wakaachaa kuipigia CCM kura za ndiyo Kwani kazi ya
Kujenga Chama iliyofanyiwa na Mzee Mangula, Abdulahman
Kinana, Nape Nnauye na maofisa wengine wa Chama Katika
kutekeleza Ilani ya CCM ni vigezo tosha kwa CCM kupata
ushindi mnono Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Desemba
14 Mwaka huu, na uchaguzi Mkuu Mwaka 2015.
Hata
  wapinzani wanalijua hilo Kwani kuna baadhi ya wabunge wa
upinzani na madiwani wamelishalijua Hilo.
Tulimsikia
Kafulila Bungeni akisema serikali ya CCM itaanguka Kama
Muhongo na wenzake hawatawajibika. 
Watu
wenye akili timamu tulishia kujiuliza hivi  huyu Kafulila
si ni Mbunge  wa Upinzania wa Chama Cha NCCR - Mageuzi
?Hivi serikali ya CCM kweli ikianguka Kama alivyodai Sindio
itakuwa faida kwa wapinzani ?Sasa Kwani Kafulila alijifanya
anaionea huruma serikali ya CCM isianguke ?Kama siyo unafki
ni kitu gani?
Rais
Kikwete Kumbuka hawa hawa baadhi ya viongozi wa upinzani
ndiyo wamekuwa wakienda kwa nchi wafadhili kuzieleza nchi
hizo zitunyime misaada kwasababu Viongozi wa serikali
wamekuwa mafisadi wameshindwa kusimamia Fedha za misaada
zinazotolewa na Mataifa hayo.
Minawauliza
nyie baadhi ya viongozi wa vyama Vya upinzani mkishaenda
kuissma vibaya Tanzania kwa Mataifa ya kigeni mtapata faida
gani Kama siyo Kuwaumiza Watanzaia walalahoi ambayo watakosa
huduma za kijamii Mataifa hayo yakisitisha kutoa
misaada?
Inasemekana
Wazengu Wengi wanatuona sisi Waaafrika ni watu tusiyo na
akili timamu,wezi,tusiyopenda maendeleo?Haya mlivyoenda
kuwaambia Wazungu serikali ya nchi yenu inavuja Fedha za
umma ndiyo WAzungu wamewaona Nyie mnaakili sana,siyo wezi na
wamewapatia   makazi ya kudumu huko huko Ulaya?Mbona
mmerudi hapa hapa Tanzania kuishi Katika nchi ambayo
viongozi wake ni wezi?
Baadhi
 ya wananchi wanaopayuka mitaani na kwenye vyombo Vya
Habari wakinipa fanya wanakusii sana wewe umwajiishe Pinda,
Muhongo na wenzake siku za nyuma watu Hao ndiyo walikuwa
vinara wakusema wewe ni Rais dhaifu, Huna Kauli wala huwezi
kufanya maamuzi magumu, chekibomu, rais wa
kupendakuchekacheka na Huna akili.
Sasa
Kikwete jiulize  imekuwaje ghafla watu Hao wanakuona leo
hii baada ya bunge kutoa maazio yake kuhusu zogo la Escrow
wakuone wewe ni rais mchapakazi , unauwezo wa kutoa maamuzi
na siyo rais dhahifu?
Rais
Kikwete umekuwa ukipenda kuwataka Watanzaia wasiwe na akili
za Mbayuwai na kwamba akili za kuambiwa wachanganye na akili
zao.
 Na
Mimi Leo naitimisha kwa kumwambia Rais Kikwete asiwe Kama
Mbayuwaia,akili za kuambiwa achanganye na zake. Na
Usiwasikilize 'Bush Lawyers' na wazushi Katika
Escrow.
Mungu
Ibariki Tanzania
Chanzo:
Facebook: Happy KatabaziBlogg: www.katabazihappy.blogspot.com0716
774494Disemba
12 Mwaka 2014.

 

























Sent from my iPad



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment