Tuesday, 16 December 2014

Re: [wanabidii] KAMANI AFUNGUA SEMINA KUHUSU MAKABILA YA ASILI

Tukubali tukatae makabila yanayoitwa ya asili -yamebadilika.Kutaka yaishi kizamani ni kutaka wasiendelee wabaki nyuma.Tufahamu climate change na mwingiliano wa makabila na wageni kumeongeza maradhi pia. Baadhi ya miti imekauka na ukungu hakuna matunda pia mimea ya kutambaa na shrubs zilizokua na matunda. Wanyamapori wamepungfua na wengine kutokana na mabadiliko ya tabia nchi vidudu vilivyolala vya maradhi vimeibuka wanaweza kuambukiza na kuwaua wakiwala. kuoana au kuoza wasichana umri mdogo kumepitwa na wakati. Kuwa na mifugo mamilioni kama wealth status ardhi haitoshelezi inakuwa kame maana matajiri hao nao wameongezeka.

Kubadilika kimila hawazingatii sheria za kukaribisha wageni za kimila na za nchi. Viongozi wa mila wanaingiza wageni wenye mifugo au wawindaji kinyemela. Tukumbuke wasomali 1980s-mid 1990s walivyotesa Serengeti-Loliondo wakikaa maboma ya wenyeji. Tembelea kwa Hazabe-wapo waliooa wazungu wapo ulaya hawakurudi kuleta maendeleo kwao na wapo waliowaoa wahadzabe wa makabila mengine na kubadilisha mazingira ya nyumba na uchumi wa familia hizo. Tembelea Mererani, Naitolia,  Namerok, Landanai, Engerosambu, Soitsambu, Loiborsirret uone mijengo. Pia ndani ya NCAA na lake Eyasi. Hukosi kuona mabadiliko ya mijengo, kilimo cha plogh na trekta. Msitake kutuambia watu ni static. wanavuna madini Mererani, Loiborsirret na kuporomosha mijengo. anakagua mifugo kwa pikipiki, mama hachotei maji punda bali landrover imejazwa madumu dreva anajaza au boza linavutwa kwa trekta. tajiri ana ngome 10 elfu, mbuzi elfu 5 na kondoo (wanauzwa sana) mjengo wa kisasa, trekta, boza la maji, Musso gari ya fahari, vivalo vya kimasai lakini material sio cotton, simu za malaki na bangili sio shaba bali dhahabu, ana bar, kilimo shamba hekta 20+ analima mahindi na maharage anapeleka maharage kenya, ana punda 10, lodging, taxi etc wake 10 watoto 60 wajukuu 300. Ardhi haiongezeki. wanapohamahama wanaongeza mifugo. Unapoongea kabila za asili msiangalie mavazi yao tu-fanyeni analysis ya uchumi wao na impact on the environment katika semi arid area na kilimo ambako huko hakifai kinamaliza malisho ya mifugo yao na wanyama pori. waliruhusiwa kuishi nao kwa vile hawalimi ila sasa wanalima na kuwa na shughuli nyingi za uchumi. hata NCAA inaathirika na mabadiliko yao haya ambayo ni maendeleo usitegemee wabaki kama miaka 100 iliyopita.

Muhimu basi kusaidia wala matunda hadza, Sandawe etc wawe na huduma nzuri ya maji, shule, zahanati; kuwe na land use planning na certification ya individual na group titles na kulinda ardhi yao wafugaji wahamaji wasiwaingilie na kuchukua maeneo yao pia watu wengine. kuwaanzishia wildlife ranches-wafuge wanyama katika ranch ili wale chama waliyozoea kula, wasaidiwe wafuge nyuki waumao na wasiouma kwa mizinga ya kisasa wale na kuuza asali na wasaidiwe kupata soko la natural honey.

Wasitegemee kuhamahama wawinde wanyama pori wanaolindwa au kutegemewa kiutalii. Wanyama huhama na hupungua ktk misimu mingine. Pia wapande traditional trees wanazotegemea kwa matunda. Wapande katika vijiji na nje ya nyumba zao, katika plantations wakichanganya na misitu iliyobakia. Traditional plants za vegetables and fruit trees hupandwa pia. Zipo NGOs zenye uzoefu huu pia taasisi za research kama Sokoine University.

Haki ya kila mtanzania ni kuishi ktk ardhi yake awe na hati miliki na aitumie sustainably. Kwa sasa inaonekana wafugaji wahamaji ndio wanahaki zaidi kuzagaa na mifugo kulishia mashamba ya awtu kuwapiga na kuwaua kuwatia vilema na umasikini. Wengine kwao wanalima lakini hawalishii mifugo mashamba yao ila wakifika kwa wenzao kilometa  1000 km wanalishia mashamba na kuwapiga. nao sasa wameamua kugeuza kibao kuwaulia mifugo, kuwachomea nyumba na mapigano-tutafika. traditional life inayotetewa hapa sio hii inayozagaa sana na sio kuwaacha wakae baadhi ya wala matunda katika vibanda vya nyasi wazungu waje kufanya utafiti, kupiga picha za utalii na kutengeneza film. Unaweza kuishi kimila kimaisha, kuvaa kimila lakini umesoma, unaelimu, unafuga na kulima sustainably; unafuga nyuki kula na kuuza asali. Tutenganishe traditionalism na impoverishment without education na kulinda utamaduni ukiwa na maendeleo pia. Tusikubali kuendeshwa na wazungu kwa masuala yao ya ubinafsi wao. Wao mbona kwao wamefanyawatu awwe na maendeleo na traditional medicine zinazalishwa viwandani na kupimwa na nyingine ndio hizo makampuni nyanatajirika na Forever na GNLD na ni big industries za kuuza traditional/natural products wapandazo ktk plantation economy.*:-h wave

On Tuesday, 16 December 2014, 13:05, zainul mzige <zainul.mzige21@gmail.com> wrote:

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani   akifungua  semina ya siku mbili ya kimataifa inayozungumzia makabila ya asili, haki zao na namna ya kuboresha maisha na mifumo ya chakula . Semina hiyo inayofanyika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam inajiandaa kwa kongamano la dunia nzima kuhusiana na jamii za asili ambalo litafanyika Roma Italia, Februari 2015.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).

Mwakilishi Shirika la Kimataifa la maendeleo ya Kilimo, IFAD, Bw.Francisco Pichon akisisitiza jambo wakati wa kongamano hilo.

Washiriki wa semina hiyo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa kuhusu haki za makabila ya asili na namna ya kuboresha maisha yao na mifumo ya chakula .

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani  (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa kongamano hilo.

KAWAIDA

001
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani   akifungua  semina ya siku mbili ya kimataifa inayozungumzia makabila ya asili, haki zao na namna ya kuboresha maisha na mifumo ya chakula . Semina hiyo inayofanyika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam inajiandaa kwa kongamano la dunia nzima kuhusiana na jamii za asili ambalo litafanyika Roma Italia, Februari 2015.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
002
Mwakilishi Shirika la Kimataifa la maendeleo ya Kilimo, IFAD, Bw.Francisco Pichon akisisitiza jambo wakati wa kongamano hilo.
003
Washiriki wa semina hiyo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa kuhusu haki za makabila ya asili na namna ya kuboresha maisha yao na mifumo ya chakula .
004
005
006
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani  (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa kongamano hilo.

Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
+255714940992.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment