Wednesday 18 December 2013

[wanabidii] TAARIFA YA AWALI KUHUSIANA NA TUKIO LILILOTOKEA MALINYI MKOANI MOROGORO.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Mnamo tarehe 18/12/2013 majira ya saa tatu asubuhi katika kata ya Malinyi, tarafa ya Malinyi, wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, kundi la watu kutoka maeneo mbalimbali kijijini hapo walivamia  kituo cha Polisi Malinyi kwa lengo la kutaka kuwatoa kwa nguvu watuhumiwa 4 waliokuwa wamekamatwa kwa tuhuma za mauaji.

Katika jitihada za kuhami kituo, askari polisi walitoa tahadhali mbalimbali za kuwataka wananchi hao watawanyike ikiwemo  kupiga mabomu ya machozi, lakini wananchi hao waliendelea kukaidi amri hiyo. Katika purukushani hizo za askari kutetea kituo na wavamizi kuendelea kuharibu mali za kituo ikiwemo kukichoma moto, wananchi 3 walipoteza maisha na wengine 3 walijeruhiwa.

Kufuatia tukio hilo,  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, ametuma timu maalumu ikiongozwa na Kamishina wa  Operesheni  na Mafunzo (CP) Paul Chagonja kutoka Makao Makuu ya Polisi  kwenda  kuongeza nguvu katika Operesheni ya kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo, ili wafikishwe katika mkondo wa sheria haraka.

Jeshi la Polisi linalaani vikali tukio hilo  linaloashiria  vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani, tukio ambalo limesababisha vifo na majeruhi pamoja na kujenga hofu miongoni mwa jamii.

Aidha, IGP Mwema ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro hususani wilaya ya Ulanga kata ya Malinyi, kuwa watulivu na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wakati uchunguzi ukiendelea, mtu yeyote mwenye taarifa  za wahalifu hao anaombwa kutoa taarifa kwenye namba ya simu ifuatayo 0754 78 55 57 au katika kituo chochote cha Polisi, ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP 
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment