Monday 30 December 2013

Re: [wanabidii] Rasimu ya Pili ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania



RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO

WA TANZANIA

________


YALIYOMO

______

Ibara Kichwa cha Habari


UTANGULIZI


SURA YA KWANZA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


SEHEMU YA KWANZA
JINA, MIPAKA, ALAMA, LUGHA NA TUNU ZA TAIFA

1. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 3. Alama na Sikukuu za Taifa.
4. Lugha ya Taifa na lugha za alama. 5. Tunu za Taifa.

SEHEMU YA PILI
MAMLAKA YA WANANCHI, UTII NA HIFADHI YA KATIBA

6. Mamlaka ya wananchi. 7. Watu na Serikali.
8. Ukuu na utii wa Katiba.
9. Hifadhi ya utawala wa Katiba.

SURA YA PILI

MALENGO MUHIMU, MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI NA SERA ZA KITAIFA

10. Malengo Makuu.
11. Utekelezaji wa Malengo ya Taifa. 12. Sera ya Mambo ya Nje.

SURA YA TATU
MAADILI NA MIIKO YA UONGOZI NA UTUMISHI WA UMMA

SEHEMU YA KWANZA
MAADILI YA UONGOZI NA UTUMISHI WA UMMA

13. Dhamana ya Uongozi wa Umma. 14. Kanuni za Uongozi wa Umma.
15. Zawadi katika Utumishi wa Umma.


i
 


16. Akaunti nje ya nchi na mikopo.
17. Wajibu wa kutangaza mali na madeni. 18. Mgongano wa maslahi.
19. Matumizi ya mali ya umma.
20. Utekelezaji wa masharti ya maadili.

SEHEMU YA PILI MIIKO YA UONGOZI WA UMMA

21. Utii wa Miiko ya Uongozi wa Umma. 22. Marufuku baadhi ya vitendo.

SURA YA NNE
HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI

SEHEMU YA KWANZA HAKI ZA BINADAMU

23. Uhuru, utu na usawa wa binadamu. 24. Haki ya kuwa hai.
25. Marufuku kuhusu ubaguzi. 26. Haki ya kutokuwa mtumwa. 27. Uhuru wa mtu binafsi.
28. Haki ya faragha na usalama wa mtu. 29. Uhuru wa mtu kwenda anakotaka. 30. Uhuru wa maoni.
31. Uhuru wa habari na vyombo vya habari. 32. Uhuru wa imani ya dini.
33. Uhuru wa mtu kujumuika na kushirikiana na wengine. 34. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.
35. Haki ya kufanya kazi.
36. Haki za wafanyakazi na waajiri. 37. Haki ya kumiliki mali.
38. Haki ya uraia.
39. Haki ya mtuhumiwa na mfungwa. 40. Haki ya watu walio chini ya ulinzi.
41. Uhuru na haki ya mazingira safi na salama. 42. Haki ya elimu na kujifunza.
43. Haki ya mtoto.
44. Haki na wajibu wa vijana.
45. Haki za watu wenye ulemavu.
46. Haki za makundi madogo katika jamii. 47. Haki za wanawake.
48. Haki za wazee.











ii
 


SEHEMU YA PILI
WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI NA MIPAKA YA HAKI ZA BINADAMU


(a) Wajibu wa Raia kwa Taifa 49. Wajibu wa raia.
50. Wajibu wa kushiriki kazi. 51. Ulinzi wa mali ya umma. 52. Haki na wajibu muhimu.


(b) Wajibu wa Mamlaka za Nchi


53. Hifadhi ya haki za binadamu.
54. Usimamizi wa haki za binadamu.


(c) Mipaka ya Haki za Binadamu


55. Mipaka ya haki za binadamu.


SURA YA TANO
URAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO


56. Uraia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 57. Uraia wa kuzaliwa.
58. Uraia wa kuandikishwa.
59. Hadhi ya watu wenye asili au nasaba ya Tanzania.


SURA YA SITA MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO


60. Muundo wa Muungano.
61. Vyombo vya utendaji vya Jamhuri ya Muungano. 62. Mamlaka ya Serikali ya Muungano.
63. Mambo ya Muungano. 64. Nchi Washirika.
65. Mamlaka ya Nchi Washirika.
66. Mahusiano kati ya Nchi Washirika. 67. Mawaziri Wakaazi.
68. Mamlaka ya wananchi.
69. Wajibu wa kulinda Muungano.


SURA YA SABA
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO


SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI, RAIS, MAKAMU WA RAIS NA BARAZA LA MAWAZIRI


(a) Serikali


70. Serikali ya Jamhuri ya Muungano.



iii
 


(b) Rais


71. Rais wa Jamhuri ya Muungano. 72. Madaraka na majukumu ya Rais. 73. Utekelezaji wa madaraka ya Rais. 74. Rais kuzingatia ushauri.
75. Rais kushindwa kumudu majukumu yake.
76. Utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais kabla ya kumaliza muda wake. 77. Utekelezaji wa majukumu ya Rais akiwa hayupo.


(c) Uchaguzi wa Rais 78. Uchaguzi wa Rais.
79. Sifa za Rais.
80. Utaratibu wa Uchaguzi wa Rais.
81. Malalamiko kuhusu uhalali wa Uchaguzi wa Rais. 82. Kiapo cha Rais na muda wa kushika madaraka. 83. Haki ya kuchaguliwa tena.


(d) Masharti Mahsusi kuhusu Mamlaka ya Rais


84. Madaraka ya kutangaza vita.
85. Madaraka ya Rais kutangaza hali ya hatari. 86. Mamlaka ya Rais kutoa msamaha.
87. Kinga ya mashtaka dhidi ya Rais. 88. Bunge kumshtaki Rais.
89. Maslahi ya Rais.


(e) Makamu wa Rais


90. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. 91. Upatikanaji wa Makamu wa Rais.
92. Sifa za Makamu wa Rais. 93. Kiapo cha Makamu wa Rais.
94. Wakati wa Makamu wa Rais kushika madaraka. 95. Bunge kumshtaki Makamu wa Rais.
96. Upatikanaji wa Makamu wa Rais wakati nafasi hiyo inapokuwa wazi.


SEHEMU YA PILI
BARAZA LA MAWAZIRI LA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO


(a) Baraza la Mawaziri


97. Kuundwa kwa Baraza la Mawaziri.
98. Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri. 99. Waziri Mwandamizi.
100.Kazi na mamlaka ya Waziri Mwandamizi. 101.Sifa za Mawaziri na Naibu Mawaziri.
102.Kiapo, muda na masharti ya kazi ya Waziri na Naibu Waziri. 103.Utekelezaji wa shughuli za Serikali Bungeni.



iv
 


(b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali


104. Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


(c) Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu

105. Katibu Mkuu Kiongozi.
106. Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.


(d) Utekelezaji wa Shughuli za Baraza la Mawaziri


107. Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu. 108. Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.

SURA YA NANE UHUSIANO NA URATIBU WA SERIKALI


109. Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali. 110. Malengo ya Tume.
111. Majukumu ya Tume. 112. Sekretarieti ya Tume.


SURA YA TISA
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO


SEHEMU YA KWANZA
KUUNDWA NA MADARAKA YA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO


113. Kuundwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano. 114. Muda wa Bunge.
115. Madaraka ya Bunge.
116. Mipaka ya Bunge katika kutumia madaraka yake. 117. Madaraka ya Bunge kutunga sheria.
118. Utaratibu wa kubadilisha Katiba.
119. Utaratibu wa kubadilisha masharti mahsusi. 120. Utaratibu wa kutunga sheria.
121. Utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha. 122. Madaraka ya Mkuu wa Nchi kuhusu Muswada wa Sheria. 123. Kupitishwa kwa hoja za Serikali.


SEHEMU YA PILI WABUNGE


(a) Uchaguzi wa Wabunge


124. Uchaguzi wa Wabunge.
125. Sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge. 126. Utaratibu wa uchaguzi wa Wabunge. 127. Kiapo na masharti ya kazi ya Ubunge. 128. Kupoteza sifa za Ubunge.


v
 


129. Haki ya wapiga kura kumwajibisha Mbunge. 130. Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge.
131. Tamko rasmi la Wabunge kuhusu Maadili ya Uongozi.


SEHEMU YA TATU UONGOZI WA BUNGE


(a) Spika na Naibu Spika


132. Spika na mamlaka ya Spika. 133. Ukomo wa mamlaka ya Spika. 134. Naibu Spika.
135. Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika.
136. Utaratibu wa uchaguzi na kiapo cha Spika na Naibu Spika.


(b) Ofisi ya Bunge


137. Katibu wa Bunge. 138. Sekretarieti ya Bunge.


SEHEMU YA NNE UTARATIBU WA SHUGHULI ZA BUNGE


139. Kanuni za Kudumu za Bunge. 140. Rais kulihutubia Bunge.
141. Mikutano ya Bunge.
142. Uongozi na vikao vya Bunge. 143. Akidi ya vikao vya Bunge. 144. Kamati za Bunge.


SEHEMU YA TANO MADARAKA NA HAKI ZA BUNGE

145. Uhuru wa majadiliano Bungeni. 146. Mipaka ya majadiliano Bungeni.


SEHEMU YA SITA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE


(a) Tume ya Utumishi wa Bunge


147. Tume ya Utumishi wa Bunge.
148. Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Bunge.


(b) Mfuko wa Bunge


149. Mfuko wa Bunge.





vi
 


SURA YA KUMI MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO


SEHEMU YA KWANZA
MISINGI YA UTOAJI HAKI NA UHURU WA MAHAKAMA

150. Kuanzishwa kwa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano. 151. Misingi ya utoaji haki.
152. Uhuru wa Mahakama.


SEHEMU YA PILI MUUNDO WA MAHAKAMA

(a) Mahakama za Jamhuri ya Muungano


153. Muundo wa Mahakama.

(b) Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano

154. Mahakama ya Juu.
155. Akidi ya vikao vya Mahakama ya Juu. 156. Mamlaka ya Mahakama ya Juu.
157. Madaraka ya Majaji wa Mahakama ya Juu.

(c) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu

158. Uteuzi wa Jaji Mkuu.
159. Uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu.
160. Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu. 161. Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Juu.
162. Muda wa kuwa madarakani kwa Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Majaji wa Mahakama ya Juu.
163. Utaratibu wa kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu.
164. Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji wa Mahakama ya Juu.

(d) Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano

165. Mahakama ya Rufani.
166. Akidi ya vikao vya Mahakama ya Rufani. 167. Mamlaka ya Mahakama ya Rufani.
168. Madaraka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.


(e)Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani


169. Uteuzi wa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani.
170. Uteuzi wa Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani. 171. Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
172. Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Rufani.
173. Muda wa kuwa madarakani kwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Majaji wa Mahakama ya Rufani.
174. Utaratibu wa kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani. 175. Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.


vii
 



(f)Usimamizi wa Shughuli za Mahakama


176. Msajili Mkuu wa Mahakama.
177. Majukumu ya Msajili Mkuu wa Mahakama. 178. Mtendaji Mkuu wa Mahakama.
179. Majukumu ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama.

SEHEMU YA TATU
TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA NA MFUKO WA MAHAKAMA

(a) Tume ya Utumishi wa Mahakama


180. Tume ya Utumishi wa Mahakama.
181. Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama. 182. Uanachama katika vyama vya siasa.


(b) Mfuko wa Mahakama


183. Mfuko wa Mahakama.


SURA YA KUMI NA MOJA
UTUMISHI WA UMMA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO


184. Misingi mikuu ya Utumishi wa Umma.
185. Ajira na uteuzi wa viongozi wa taasisi katika Serikali. 186. Tume ya Utumishi wa Umma.
187. Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.
188. Mamlaka na majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma.


SURA YA KUMI NA MBILI UCHAGUZI KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI
NA VYAMA VYA SIASA

SEHEMU YA KWANZA UWAKILISHI WA WANANCHI

189. Ushiriki katika uchaguzi na kura ya maoni.

SEHEMU YA PILI TUME HURU YA UCHAGUZI

(a) Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi

190. Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi. 191. Kamati ya Uteuzi.
192. Ukomo wa kushika nafasi ya madaraka ya Ujumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
193. Wajibu wa Tume Huru ya Uchaguzi. 194. Malalamiko kuhusu uchaguzi.




viii
 


(b) Mkurugenzi wa Uchaguzi

195. Uteuzi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi. 196. Majukumu ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.

SEHEMU YA TATU
USAJILI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA SIASA

(a) Vyama vya Siasa 197. Usajili wa vyama vya siasa.

(b) Msajili wa Vyama vya Siasa

198. Uteuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa. 199. Wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa.


SURA YA KUMI NA TATU TAASISI ZA UWAJIBIKAJI

SEHEMU YA KWANZA
TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI

200. Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji. 201. Uteuzi na sifa za Wajumbe.
202. Kamati Maalum ya Uteuzi. 203. Majukumu ya jumla ya Tume.
204. Muda wa kukaa madarakani kwa Mjumbe wa Tume. 205. Kuondolewa madarakani kwa Mjumbe wa Tume. 206. Uhuru wa Tume.
207. Uwezeshaji wa nyenzo na rasilimali.


SEHEMU YA PILI TUME YA HAKI ZA BINADAMU

208. Tume ya Haki za Binadamu. 209. Kamati ya Uteuzi.
210. Kazi na majukumu ya Tume.
211. Muda wa kukaa madarakani kwa Kamishna wa Tume. 212. Kuondolewa madarakani kwa Kamishna wa Tume. 213. Uhuru wa Tume.
214. Uwezeshaji wa nyenzo na rasilimali.

SEHEMU YA TATU
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

215. Uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. 216. Sifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
217. Kazi na majukumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
218. Muda wa kukaa madarakani kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
219. Kuondolewa madarakani kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
220. Uwezeshaji wa nyenzo na rasilimali.


ix
 



SURA YA KUMI NA NNE

MASHARTI KUHUSU FEDHA ZA JAMHURI YA MUUNGANO

(a) Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano

221. Mfuko Mkuu wa Hazina.
222. Masharti ya kutoa fedha za matumizi katika Mfuko Mkuu wa Hazina.
223. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina.
224. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali kuanza kutumika.
225. Mfuko wa matumizi ya dharura.
226. Mishahara ya baadhi ya watumishi kudhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina.

(b) Deni la Taifa na Mikopo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano

227. Deni la Taifa.
228. Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kukopa. 229. Mamlaka ya Serikali za Nchi Washirika kukopa.
230. Masharti ya kutoza kodi.

(c) Vyanzo vya Mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Ununuzi wa Umma

231. Vyanzo vya mapato vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano. 232. Ununuzi wa umma.


(d) Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano


233. Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano. 234. Benki za Serikali za Nchi Washirika.


SURA YA KUMI NA TANO
ULINZI NA USALAMA WA JAMHURI YA MUUNGANO


(a) Ulinzi na Usalama wa Taifa

235. Usalama wa Taifa.
236. Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Taifa.
237. Kuanzishwa kwa Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa. 238. Majukumu ya Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.


(b) Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania


239. Kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. 240. Uteuzi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.
241. Madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu.
242. Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.





x
 


(c) Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano


243. Kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi.
244. Misingi ya utendaji wa Jeshi la Polisi. 245. Uteuzi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi.
246. Majukumu na uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi. 247. Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi.

(d) Idara ya Usalama ya Jamhuri ya Muungano

248. Kuanzishwa kwa Idara ya Usalama wa Taifa.
249. Uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa. 250. Usalama katika Nchi Washirika.

SURA YA KUMI NA SITA MENGINEYO

251. Utaratibu wa kujiuzulu katika utumishi wa umma. 252. Masharti kuhusu kukabidhi madaraka.
253. Baadhi ya watumishi wa umma kutoshika nafasi za kisiasa. 254. Ufafanuzi.
255. Jina la Katiba na kuanza kutumika.
256. Kufutwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Sura ya 2.


SURA YA KUMI NA SABA MASHARTI YATOKANAYO NA MASHARTI YA MPITO

SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YATOKANAYO

257. Matumizi ya baadhi ya masharti ya Katiba.

SEHEMU YA PILI
MASHARTI YA KIKATIBA NA SHERIA ZA NCHI

258. Kuendelea kutumika masharti ya Katiba. 259. Kuendelea kutumika sheria za nchi.


SEHEMU YA TATU UTUMISHI WA UMMA
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano


260. Kuendelea kuwepo kwa Rais madarakani.
261. Kuendelea kuwepo kwa Makamu wa Rais madarakani.
262. Kuendelea kwa Waziri Mkuu, Mawaziri na Naibu Mawaziri.


(b) Watumishi wa Umma


263. Kuendelea kwa utumishi wa umma.




xi
 


SEHEMU YA NNE BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO


264. Kuendelea kwa Ubunge na Uongozi wa Bunge. 265. Kuvunjwa kwa Bunge.

SEHEMU YA TANO MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO


266. Kuendelea kwa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu. 267. Kuendelea kwa mashauri yaliyopo mahakamani.

SEHEMU YA SITA MASHARTI YA MPITO

268. Muda wa Mpito.
269. Utekelezaji wa masharti ya Katiba Mpya. 270. Kamati ya kusimamia Muda wa Mpito.
271. Kufutwa kwa Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito. ______


NYONGEZA

_______
































xii
 


UTANGULIZI


KWA KUWA, sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu, uhuru, haki, usawa, udugu, amani, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu;


NA KWA KUWA, tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye mfumo wa demokrasia na utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi, na Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa na kwamba wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu;


NA KWA KUWA, tunatambua umuhimu wa kutunza mali ya Mamlaka za Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu, ubadhirifu na kuhimiza matumizi bora na endelevu ya rasilimali na maliasili zetu pamoja na kulinda na kuhifadhi mazingira yetu kwa mustakabali wa maisha ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;


NA KWA KUWA, tunatambua umuhimu na faida za kujenga, kukuza na kuendeleza amani, umoja, urafiki na ushirikiano miongoni mwa Watanzania, mataifa mbalimbali ya Afrika na dunia kwa ujumla;


NA KWA KUWA, azma ya kujenga Umoja wa Bara la Afrika inadhihirishwa na Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;


NA KWA KUENDELEZA DHAMIRA YETU HIYO, ni muhimu:
(a) kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano wa nchi za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
(b) kujenga Taifa huru na linalojitegemea;
(c) kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria;
(d) kukuza na kuendeleza maadili, uwajibikaji na uwazi;
(e) kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kimazingira na kulinda urithi kwa ujumla;
(f) kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya watu; (g) kujenga na kuendeleza utii wa mamlaka ya Katiba; na
(h) kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa Taifa miongoni mwa Watanzania;


NA KWA KUZINGATIA, urithi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa letu wa kujenga nchi yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila, dini, rangi, jinsi au ubaguzi wa aina nyingine yoyote;


NA KWA KUZINGATIA, uzoefu wa zaidi ya Miaka Hamsini ya Uhuru wa Tanganyika, Miaka Hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar na Miaka Hamsini ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na umuhimu wa ushiriki mpana na bayana wa wananchi katika utungaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;








1
 


HIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA imetungwa na SISI WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kupitia KURA YA MAONI kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria, kujitegemea na isiyofungamana na dini.




















































2
 


SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


SEHEMU YA KWANZA
JINA, MIPAKA, ALAMA, LUGHA NA TUNU ZA TAIFA


 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.














Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Alama na Sikukuu za Taifa.















Lugha ya Taifa na lugha za alama.
 
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi na Shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ambazo kabla ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964, zilikuwa nchi huru.
(2) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na lisilofungamana na dini.
(3) Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika ibara ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa Makubaliano hayo.

2. Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanganyika likijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari.

3.-(1) Alama za Taifa zitakuwa ni: (a) Bendera ya Taifa;
(b) Wimbo wa Taifa; na (c) Nembo ya Taifa,
kama zitakavyoainishwa katika sheria za nchi. (2) Sikukuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a) Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9 Disemba;
(b) Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12 Januari;
(c) Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili; na
(d) Sikukuu nyingine zitakazoainishwa na sheria za nchi. (3) Kila Sikukuu ya Kitaifa itakuwa ni siku ya mapumziko.

4.-(1) Lugha ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano ni Kiswahili na itatumika katika mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), lugha ya Kiingereza au lugha nyingine yoyote inaweza kutumika kuwa lugha rasmi ya mawasiliano ya kiserikali pale itakapohitajika.
(3) Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa mawasiliano mbadala zikiwemo lugha za alama, maandishi yaliyokuzwa na nukta nundu kwenye sehemu muhimu za umma na katika vyombo vya habari vinavyotangaza habari zake kitaifa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum.
 




- 3 -
 


Tunu za Taifa. 5. Jamhuri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa zifuatazo:
(a) utu;
(b) uzalendo; (c) uadilifu; (d) umoja; (e) uwazi;
(f) uwajibikaji; na (g) lugha ya Taifa.

SEHEMU YA PILI
MAMLAKA YA WANANCHI, UTII NA HIFADHI YA KATIBA

 

Mamlaka ya wananchi.












Watu na Serikali.
 
6. Jamhuri ya Muungano ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia inayozingatia haki ya kijamii, na kwa hiyo:
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi ambao kwa umoja na ujumla wao wanaimiliki na kuipatia Katiba hii uhalali;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi; na
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

7.-(1) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake, katika uendeshaji na utekelezaji wa shughuli zake, utazingatia azma ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo (1), mamlaka ya nchi na vyombo vyake vinawajibika kuelekeza sera, sheria na shughuli zake zote kwa lengo la kuhakikisha kwamba:
(a) utu, heshima na haki nyingine za binadamu zinalindwa, zinathaminiwa, zinahifadhiwa na kudumishwa kwa kuzingatia mila na desturi za Watanzania na mikataba mbalimbali iliyoridhiwa na Jamhuri ya Muungano;
(b) sheria za nchi zinasimamiwa na kutekelezwa;
(c) shughuli zinazofanywa zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na kutumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
(d) ardhi ikiwa rasilimali kuu na msingi wa Taifa inalindwa, inatunzwa na kutumiwa na wananchi wa Tanzania kwa manufaa, maslahi na ustawi wa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;
(e) maendeleo ya uchumi wa Taifa yanapangwa na kukuzwa kwa ulinganifu na kwa pamoja na kwa namna ambayo inawanufaisha wananchi wote;
(f) kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu kipato chake;
 

- 4 -
 


(g) kunakuwepo fursa na haki zilizo sawa kwa wananchi wote, wanawake na wanaume, bila ya kujali rangi, kabila, nasaba, itikadi, dini au hali ya mtu;
(h) aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
(i) utajiri wa rasilimali na maliasili za Taifa unaelekezwa katika kuleta maendeleo, kuondoa umaskini, ujinga na maradhi; na
(j) nchi inaongozwa kwa kufuata misingi ya demokrasia, utawala wa sheria na kujitegemea.


 

Ukuu na utii wa Katiba.


















Hifadhi ya Utawala wa Katiba.










Malengo Makuu.
 
8.-(1) Katiba hii ni sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), endapo masharti ya sheria yoyote yatatofautiana na masharti ya Katiba hii, masharti ya sheria hiyo yatakuwa batili na yatatenguka kwa kiwango kile kinachotofautiana na masharti ya Katiba hii.
(3) Mtu yeyote, chombo, taasisi, jumuiya na wakala wowote wa mamlaka ya nchi na mamlaka binafsi zinao wajibu wa kuzingatia masharti ya Katiba hii na sheria za nchi na kuzitii.
(4) Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo cha dola, ofisa wa Serikali au mtu binafsi ni sharti ufuate na kuendana na masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba sheria, mila, desturi au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na masharti ya Katiba hii utakuwa batili.
(5) Serikali itaweka utaratibu wa kuwawezesha wananchi kuifahamu, kuilinda na kuitii Katiba.


9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.

(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya ibara ndogo ya (1) ni batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria za nchi.

SURA YA PILI

MALENGO MUHIMU, MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI NA SERA ZA KITAIFA

10.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha haki, udugu, amani, umoja na utengamano wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora, maendeleo endelevu na kujitegemea.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu, ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kimazingira.
(3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya:
(a) kisiasa, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili -
 



- 5 -
 


(i) kuhakikisha kuwa inazuia, inapinga na kuondoa dhuluma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji, rushwa, uonevu na upendeleo miongoni mwa wananchi kwa misingi ya itikadi, asili ya mtu, sehemu anayotoka, nasaba, kabila, jinsi, dini au imani yake;
(ii) kuhakikisha uwepo wa amani na kujenga utamaduni wa kuenzi, kuheshimu na kudumisha amani, umoja na utengamano, ushirikiano na uvumilivu wa kisiasa kwa madhumuni ya kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi;

(iii) kuhakikisha uwepo wa ulinzi, usalama na ustawi wa watu na mali zao, na kuepuka kufanya jambo lolote litakalohatarisha au kwenda kinyume na lengo hilo;
(b) kijamii, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili -
(i) kuhakikisha kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata mila, desturi na Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu na mikataba mingine ya kimataifa iliyoridhiwa na Tanzania;

(ii) kuhakikisha kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi na fursa zilizo sawa kwa raia wote, bila ya kujali itikadi, jinsi, rangi, kabila, dini, nasaba, hali ya mtu au mahali alipo;
(iii) kujenga utamaduni wa kuwepo ushirikiano, maelewano na maridhiano, uvumilivu na kuheshimu mila, desturi na imani ya dini ya kila mtu;
(iv) kuhakikisha kuwa msaada na hifadhi ya jamii inatolewa kwa watu wasiojiweza, wazee, wagonjwa, watoto na watu wenye ulemavu;
(v) kuwezesha upatikanaji na utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za uwakili;
(vi)kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake;
(c) kiuchumi, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili -
(i) kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini;
(ii) kuhakikisha kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
(iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima, wafugaji na wavuvi;
(iv) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji;

- 6 -
 


(v) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao;
(vi) kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;
(vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao na pembejeo;
(viii)kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani, upatikanaji wa pembejeo za kilimo, maeneo ya ufugaji na vifaa vya uvuvi;
(ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na nafasi za wazi kwa watu wote na kuanzisha shughuli za kiuchumi na kukuza mazingira yaliyo bora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi;
(x) kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halali inayompatia kipato;
(xi) kuhamasisha uwekezaji wa pamoja baina ya raia na wasio raia katika miundombinu ya uchumi, uvunaji wa rasilimali na maliasili za Taifa;
(xii) kuweka utaratibu wa usimamizi wa kiuchumi na uandaaji wa mipango, kuwezesha malengo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kutekelezwa;
(xiii)kuwezesha na kuendeleza matumizi ya sayansi na teknolojia na kukuza ubunifu katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya Taifa kwa jumla;
(d) kiutamaduni, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili -
(i) kulinda na kuhifadhi urithi wa asili, malikale na sehemu zenye umuhimu wa kihistoria au kidini ili kuepuka uharibifu, udhalilishaji, wizi au utoroshaji nje ya nchi;
(ii) kulinda, kuhifadhi na kuendeleza tamaduni za watu wa jamii mbalimbali ambazo zinaendeleza na kukuza utu na hadhi yao kwa namna ambayo haikinzani na Malengo Muhimu, Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali na Sera za Kitaifa;
(iii) kutambua, kulinda na kuendeleza lugha ya Kiswahili; na
(e) kimazingira, Serikali itachukua hatua zinazofaa ili -
(i) kuhakikisha kuwa ni haki na wajibu wa kila mtu kulinda na kudumisha mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;
(ii) kuhakikisha kuwa taasisi za umma na asasi za kiraia zinawajibika kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa matakwa ya kisheria katika kulinda na kuhifadhi mazingira;



- 7 -
 


(iii) kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania ndiyo wenye haki ya kumiliki rasilimali za kijenetiki za Tanzania kwa manufaa ya Taifa.

 
Utekelezaji wa Malengo ya Taifa.









Sera ya Mambo ya Nje.
 
11.-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera kwa madhumuni ya kujenga jamii iliyo bora, huru na makini.
(2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa katika Katiba hii.


12.-(1) Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano inalenga na kuzingatia maslahi ya Taifa na mamlaka kamili ya nchi na kwamba sera hiyo inatekelezwa kwa uwazi ili -
(a) kukuza ujirani mwema, ushirikiano wa kikanda na wa kimataifa;
(b) kukuza maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi wenye tija kwa Taifa na raia wake;
(c) kuunga mkono na kuendeleza jitihada za kuimarisha Umoja wa Afrika, sera ya kutofungamana na upande wowote na ushirikiano na nchi zinazostawi duniani;
(d) kuheshimu sheria za kimataifa;
(e) kuzingatia mikataba ya kimataifa na ya kikanda yenye maslahi kwa Jamhuri ya Muungano na kutatua migogoro ya kimataifa kwa njia ya majadiliano, usuluhishi, maridhiano au mahakama;
(f) kukuza uzingatiaji wa haki za binadamu na uhuru wa watu;
(g) kupambana na makosa ya kimataifa ya jinai; na (h) kuheshimu uhuru wa mataifa mengine.
(2) Bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine, itakayoelekeza na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje.
 

SURA YA TATU
MAADILI NA MIIKO YA UONGOZI NA UTUMISHI WA UMMA

SEHEMU YA KWANZA
MAADILI YA UONGOZI NA WATUMISHI WA UMMA

 
Dhamana ya Uongozi wa Umma.
 
13.-(1) Madaraka anayopewa kiongozi wa umma:
(a) ni dhamana na atatumia madaraka hayo na kutekeleza wajibu wake kwa:
(i) kuzingatia masharti ya Katiba hii; (ii) kuheshimu wananchi;
(iii) kukuza hadhi ya Taifa na kulinda heshima ya ofisi anayoitumikia; na
(iv) kukuza imani na heshima ya ofisi kwa wananchi; (b) yanatoa wajibu kwa kiongozi kuwatumikia wananchi.
 

- 8 -
 


(2) Dhamana ya uongozi na heshima kwa kiongozi wa umma itazingatia mambo yafuatayo:
(a) uteuzi kwa misingi ya mwenendo wa mtu, uwezo, sifa au uchaguzi uliyo huru na wa haki;
(b) uwezo pasipo upendeleo katika kufanya uamuzi na kuhakikisha kwamba uamuzi haufuati udugu, ukabila, udini, upendeleo, rushwa au ubaguzi wa aina yoyote;
(c) utoaji wa huduma pasipo upendeleo na kwa kufuata maslahi ya umma kwa kuonyesha -
(i) uwazi, ukweli na uaminifu katika utekelezaji wa kazi za umma;
(ii) wajibu wa kutangaza maslahi binafsi ili kuepuka mgongano wa maslahi;
(d) uwajibikaji kwa umma katika kufanya uamuzi na katika utendaji; na
(e) uadilifu, nidhamu na kujituma katika kutoa huduma kwa umma.

 
Kanuni za Uongozi wa Umma.
















Zawadi katika Utumishi
wa Umma.
 
14.-(1) Kiongozi wa umma, akiwa katika kazi za ofisi au kazi binafsi au wakati amejumuika na watu wengine, atahakikisha kwamba mwenendo wake:
(a) hauruhusu kutokea mgongano wa maslahi kati ya maslahi binafsi na maslahi ya utumishi wa umma;
(b) hauhatarishi maslahi ya umma kwa ajili ya maslahi binafsi; au
(c) haushushi hadhi ya ofisi anayofanyia kazi.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kusimamia utekelezaji wa masharti yanayohusu kanuni za uongozi wa umma.
(3) Wadhifa wa "Kiongozi wa umma" kama ulivyotumika katika Sehemu hii utajumuisha viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa kama watakavyoainishwa kwenye sheria za nchi.

15.-(1) Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara au kiongozi wa taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:
(a) aina ya zawadi;
(b) thamani ya zawadi;
(c) sababu ya kupewa zawadi; na
(d) mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.
(2) Neno "zawadi" kama lilivyotumika katika Ibara hii linajumuisha kitu chochote chenye thamani atakachopewa Kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuli za umma.
(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.
 




- 9 -
 


 
Akaunti nje ya nchi na mikopo.







Wajibu wa kutangaza mali na madeni.






















Mgongano wa maslahi.
 
16. Kiongozi wa umma -
(a) hatafungua au kumiliki akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna ambayo sheria za nchi zinaruhusu; na
(b) hataomba au kupokea mkopo au faida yoyote kwa namna au mazingira ambayo yanashusha hadhi au heshima ya utumishi wa umma.


17.-(1) Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi, mali na thamani yake na madeni yake katika Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha taarifa ya mali na madeni:
(a) yake binafsi;
(b) ya mwenza wake wa ndoa; na
(c) ya watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane,
mara moja kila mwaka kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.
(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine:
(a) ngazi au orodha ya viongozi wa umma wanaopaswa kutangaza mali na madeni yao; na
(b) utaratibu wa kuwasilisha taarifa ya mali na madeni kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kwa mujibu wa Katiba hii.


18.-(1) Kiongozi wa umma hatashiriki katika kufanya uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana maslahi nayo yeye binafsi, mwenza wake, mtoto wake, jamaa yake, rafiki au mtu yeyote wa karibu.
(2) Kiongozi wa umma hatazungumzia kitu chochote katika Baraza la Mawaziri, Bunge, Kamati au chombo kingine chochote rasmi ambacho ana maslahi nacho ya moja kwa moja au vinginevyo, isipokuwa tu kama atatoa taarifa ya mgongano huo wa maslahi katika chombo hicho.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi wa umma kushiriki katika uamuzi unaohusu kuongeza au kuboresha maslahi kwa namna yoyote ile yanayohusu wadhifa alionao, na endapo atashiriki, basi masharti hayo mapya yataanza kutumika kwa kiongozi wa umma atakayekuja baada ya kiongozi husika kuondoka au kumaliza muda wa kukaa katika nafasi ya madaraka iliyompatia fursa ya kushiriki katika kuamua maslahi husika.
(4) Masharti ya ibara ndogo ya (3), hayatamhusu kiongozi wa umma ambaye kutokana na asili ya nafasi ya madaraka au aina ya kazi zake anapaswa kushiriki katika upangaji wa mishahara au maslahi mengine ya watumishi wa umma.
 



- 10 -
 


(5) Kiongozi wa umma hataruhusiwa kushika nafasi za madaraka zaidi ya moja au kutumikia Mihimili ya Dola zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.


 

Matumizi ya mali ya umma.




Utekelezaji wa masharti ya maadili.
 
19. Kiongozi wa umma hataruhusiwa kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali yoyote ya umma, zikiwemo zilizokodishwa kwa Serikali, kwa madhumuni ya kujipatia yeye binafsi au kumpatia mtu mwingine manufaa yoyote.


20.-(1) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine:
(a) utaratibu wa utwaaji wa mali za viongozi wa umma zilizopatikana kwa kukiuka sheria;
(b) utaratibu wa kumwajibisha Kiongozi wa umma aliyekiuka maadili na Miiko ya Uongozi; na
(c) uanzishaji wa mitaala inayohusu Katiba, maadili na uraia, shuleni na vyuoni.
(2) Masharti yaliyoainishwa katika Sehemu hii ya Sura ya Tatu yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa marekebisho stahiki.
 


SEHEMU YA PILI MIIKO YA UONGOZI WA UMMA


 

Utii wa Miiko ya Uongozi wa Umma.
 
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, kiongozi wa Umma atapaswa kuheshimu na kutii maadili ya viongozi wa umma, ikiwemo Miiko ya Uongozi.
(2) Miiko ya Uongozi inayorejewa katika ibara ndogo ya (1), itakuwa kama ifuatavyo:
(a) Kiongozi wa umma hatopaswa -
(i) kuvunja au kukiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;
(ii) kutoa au kupokea rushwa; (iii)kujilimbikizia mali kinyume cha sheria;
(iv) kusema uongo au kutoa taarifa zisizo za ukweli; (v) kutoa siri za Serikali kinyume cha sheria;
(vi) kutumia wadhifa, nafasi au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu, jamaa au marafiki zake au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu;
(vii)kufanya vitendo vya uzembe, uvivu, ubaguzi, kiburi, dharau au unyanyasaji wa kijinsia.
(b) Kiongozi wa umma atapaswa kuheshimu na kuendeleza -
(i) dhana ya uwajibikaji wa pamoja kwa viongozi wanaohusika; na
(ii) maadili na Miiko ya Uongozi wa Umma, ikijumuisha: (aa) kuwa na tabia na mienendo inayokubalika katika
jamii;
(bb) kuheshimu, kutunza na kulinda mali za umma; na
 



- 11 -
 


(cc) kutambua, kuheshimu na kuzingatia Kanuni za Maadili na Mienendo ya Watumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu za Watumishi wa Umma, nyaraka za umma na miongozo mbalimbali ya Serikali kuhusu viongozi na watumishi wa umma.
(iii)kutenganisha biashara na shughuli binafsi na masuala yanayohusiana na uongozi.
(3) Kiongozi wa umma ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya:
(a) kimaadili;
(b) udhalilishaji wa mtu au wa kijinsia; au (c) wizi au ubadhirifu wa mali za umma,
atasimamishwa kazi hadi suala lake litakapoamuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi au taratibu nyingine zinazowahusu viongozi wa umma.


 

Marufuku baadhi ya vitendo.
 
22.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote ya kudumu yenye malipo ya mshahara.
(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kugombea, kuchaguliwa au kuteuliwa kushika nafasi ya madaraka katika chama cha siasa au nafasi ya madaraka ya kisiasa ya aina yoyote chini ya Katiba hii.
(3) Endapo mtumishi wa umma ataamua kugombea, kuchaguliwa au kuteuliwa kushika-
(a) nafasi ya madaraka ya kisiasa ya aina yoyote chini ya Katiba hii; au
(b) uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa,
mtumishi huyo atachukuliwa kuwa utumishi wake umekoma tangu siku ya kuteuliwa kuwa mgombea, kuchaguliwa au kuteuliwa kushika nafasi ya madaraka ya kisiasa au uongozi katika chama cha siasa.
 

SURA YA NNE
HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI

 



Uhuru, utu na usawa wa binadamu.
 
SEHEMU YA KWANZA HAKI ZA BINADAMU

23.-(1) Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa.
(2) Kila mtu anayo haki ya kuheshimiwa, kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
 

 

Haki ya kuishi.


Marufuku kuhusu ubaguzi.
 
24. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka katika Serikali na jamii kwa mujibu wa sheria za nchi.

25.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki ya kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
(2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu, mamlaka ya nchi au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika kutekeleza kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.
 



- 12 -
 


(3) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(4) Haki ya raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya mamlaka ya nchi vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
(5) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, neno "kubagua" maana yake ni kutimiza utashi, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, mahali walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsi, ulemavu au hali yao katika jamii kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima.
(6) Neno "kubagua" lilivyotumiwa katika ibara ndogo ya (2), halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia mamlaka ya nchi kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo mahsusi katika jamii.
(7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi kwamba -
(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu na pia atakuwa na haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na uamuzi wa mahakama au mamlaka nyingine inayohusika;
(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa hilo isipokuwa tu kama itathibitika mahakamani kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;
(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho hakikuwa ni kosa chini ya sheria;
(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendeka;
(e) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu, heshima ya mtu na faragha itahifadhiwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi wa tuhuma na uendeshaji wa mashtaka ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya nchi au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na
(f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kufanyiwa ukatili au kupewa adhabu zinazotweza au kudhalilisha.


 

Haki ya kutokuwa mtumwa.
 
26.-(1) Kila mtu ana haki ya kutotendewa au kutotumikishwa kama mtumwa, kutofanyishwa kazi za kulazimishwa au kutweza, na kwa msingi huo, ni marufuku kwa mtu:
 



- 13 -
 


(a) kufanywa au kutendewa kama mtumwa;
(b) kulazimishwa kufanya kazi bila hiyari yake; au
(c) kusafirishwa kwa nia ya kufanyiwa biashara au faida ya mtu mwingine.
(2) Biashara haramu ya kusafirisha na kuuza binadamu ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano.

 

Uhuru wa mtu binafsi.











Haki ya faragha na usalama wa mtu.







Uhuru wa mtu kwenda anakotaka.
 
27.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi akiwa mtu huru.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu katika -
(a) hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria; au
(b) kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.


28.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na nyumbani kwake, kutoteswa au kudhalilishwa, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake binafsi.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama wa nafsi yake, mali na maskani yake, yanaweza kuingiliwa bila ya kuathiri masharti ya Ibara hii.


29.-(1) Kila raia anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa, kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.
(2) Kitendo chochote halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya -
(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda anakotaka na kumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au
(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda anakotaka ili -
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;
(ii) kumlazimisha kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na sheria nyingine kuutimiza; au
(iii) kulinda maslahi ya umma kwa jumla au kuhifadhi maslahi mahsusi au maslahi ya sehemu fulani ya umma,
hakitahesabiwa au sheria hiyo haitahesabiwa kuwa ni kinyume cha masharti ya Ibara hii.
 


 

Uhuru wa maoni.
 
30.-(1) Kila mtu:
(a) ana haki na uhuru wa -
(i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;
(ii) kufanya mawasiliano na kutoingiliwa katika mawasiliano yake;
 


- 14 -
 


(iii) kufanya ugunduzi, ubunifu na utafiti wa sanaa, sayansi na mapokeo ya asili;
(b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:
(i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi;
(ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na
(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.
(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (1), utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na -
(a) vita au machafuko ya kisiasa; au
(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, jinsi, itikadi, dini au masuala yoyote yanayoweza kuleta madhara kwa Taifa.


 

Uhuru wa habari na vyombo vya habari.





















Uhuru wa imani ya dini.
 
31.-(1) Kila mtu ana haki na uhuru wa -
(a) kutafuta, kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa; na (b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji
wa habari bila kujali mipaka ya nchi.

(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vitakuwa na -
(a) haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazozipata;
(b) wajibu wa:
(i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na
(ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya wananchi dhidi ya habari na taarifa wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza.
(3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao.
(4) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya kulinda: (a) haki na uhuru wa vyombo vya habari; na
(b) habari na taarifa kwa madhumuni ya usalama wa Taifa, amani, maadili ya umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine.


32.-(1) Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi.
(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Serikali.
(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za nchi.
 


- 15 -
 


(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa kutangaza dini kwa namna ambayo italeta uvunjifu wa amani, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini hiyo.
(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongoni mwa wananchi.
(7) Neno "dini" kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.


 

Uhuru wa mtu kujumuika na kushirikiana na wengine.



Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.






Haki ya kufanya kazi.



Haki za wafanyakazi na waajiri.
 
33. Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.


34.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano ana haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi kwa hiari yake, ama moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Kila raia ana haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa.


35.-(1) Kila mtu ana haki ya kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe.
(2) Kila mtu ana haki na fursa sawa kushika nafasi yoyote ya kazi, uongozi au shughuli yoyote iliyo chini ya mamlaka ya nchi.


36.-(1) Kila mfanyakazi ana haki zifuatazo: (a) kufanya kazi bila ubaguzi wa aina yoyote;
(b) kupata ujira na malipo halali kulingana na kiasi na sifa za kazi anayofanya;
(c) kuunda au kujiunga na chama cha wafanyakazi mahali pa kazi; na
(d) kushiriki katika shughuli za chama cha wafanyakazi.
(2) Kila chama cha waajiri na wafanyakazi kitakuwa na haki ya: (a) kuamua kuhusu uongozi, programu na shughuli zake; na (b) kuanzisha, kujiunga na kusimamia shirikisho lao.
(3) Kila chama cha wafanyakazi kitakuwa na haki ya kufanya majadiliano ya pamoja na mwajiri na kuingia mikataba ya hali bora ya kazi.
(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu haki za wafanyakazi na utaratibu utakaowezesha wafanyakazi kutumia haki zao.
 





- 16 -
 


 
Haki ya kumiliki mali.










Haki ya uraia.
 
37.-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria za nchi.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchukuliwa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengine bila ya malipo yanayolingana na thamani halisi ya mali hiyo na yatakayotolewa mapema.
(3) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia halali.


38. Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika, nyaraka za kumwezesha kusafiri.
 


 
Haki ya mtuhumiwa na mfungwa.
 
39.-(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:
(a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu au lugha ya alama -(i) sababu ya kukamatwa;
(ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na (iii) matokeo ya kutoa maelezo;
(b)kutoa maelezo;
(c) kuwasiliana na wakili au mtu mwingine ambaye msaada wake ni muhimu kwa mtuhumiwa;
(d) kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi yake; na
(e) kupelekwa mahakamani mapema iwezekanavyo.
(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha: (a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka yanayomkabili na
kumbukumbu ya mwenendo wa mashtaka;
(b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya mwenendo wa mashtaka na hukumu baada ya shauri kukamilika mahakamani; na
(c) mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamani ili kuthibitisha uwepo wake.
 


 
Haki ya watu waliyo chini ya ulinzi.
 
40.-(1) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki zote za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.
(2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.
(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake, isipokuwa kwa mujibu wa sheria za nchi na mikataba ya kimataifa na wajibu wa nchi katika uhusiano wa kimataifa.
 




- 17 -
 


 

Uhuru na haki ya mazingira safi na salama.
 
41.-(1) Kila mtu anayeishi katika Jamhuri ya Muungano ana haki ya kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya.
(2) Haki ya kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya inahusisha haki kwa kila mtu kutumia maeneo ya umma au sehemu mbalimbali za mazingira yaliyotengwa kwa madhumuni ya burudani, elimu, afya, ibada, utamaduni na shughuli za kiuchumi.
(3) Mtu yeyote anayeishi Tanzania anao wajibu wa kutunza na kuendeleza mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka za nchi kuhusu shughuli au jambo lolote ambalo ni la hatari au lina uwezekano mkubwa wa kuharibu au kuathiri mazingira.
 


 

Haki ya elimu na kujifunza.
 
42.-(1) Kila mtu ana haki ya:
(a) kupata fursa ya kupata elimu bora bila ya vikwazo;

(b) kupata elimu bora ya msingi bila ya malipo na
 

inayomtayarisha kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea na elimu ya ngazi inayofuatia au kuweka msingi wa kuanza kujitegemea;
(c) kupata elimu bora inayotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu; na
(d) kupata fursa sawa ya kupata elimu ya juu ilimradi ana sifa stahiki kupata elimu hiyo,
bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), kila mtu ana haki ya kuchagua taaluma na ajira anayoitaka kwa mujibu wa elimu yake na ujuzi alionao.


Haki ya 43.-(1) Kila mtoto ana haki ya -mtoto. (a) kupewa jina na uraia;
(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu, ukatili na udhalilishaji;
(c) kucheza na kupata elimu bora;
(d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika ukinzani na sheria;
(e) kupata lishe bora, huduma ya afya, makaazi na mazingira yanayomjenga kimaadili;
(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na (g) kupata malezi na ulinzi kutoka kwa wazazi, walezi au
mamlaka za nchi,
bila ya ubaguzi wa rangi, utaifa, lugha, mtazamo wa kisiasa, jamii anayotokea, kipato, uzazi, kabila, dini, jinsi au aina nyingine za hadhi.
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto.
(3) Itakuwa ni wajibu wa kila mzazi, mlezi, jamii na mamlaka za nchi kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa katika maadili stahiki kwa umri wao.




- 18 -
 


 
Haki na wajibu wa vijana.






Haki za watu wenye ulemavu.
















Haki za makundi madogo katika jamii.
















Haki za wanawake.
 
44. Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Nchi Washirika na jamii zitahakikisha kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

45.-(1) Mtu mwenye ulemavu anastahiki:
(a) kuheshimiwa, kutambuliwa na kutendewa kwa namna ambayo haishushi utu wake;
(b) kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika shughuli za kijamii;
(c) kuwekewa miundombinu na mazingira yatakayowezesha kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri na kupata habari;
(d) kutumia lugha za alama, maandishi ya nukta nundu, maandishi yaliyokuzwa au njia nyingine zinazofaa;
(e) kusoma, kujifunza na kuchanganyika na watu wengine; na (f) kupata ajira na kugombea nafasi za uongozi katika nyadhifa
mbalimbali kwa usawa.
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha watu wenye ulemavu kushiriki katika nafasi za uwakilishi.

46.-(1) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha makundi madogo katika jamii:
(a) kushiriki katika uongozi wa mamlaka za nchi;
(b) kupewa fursa maalum za elimu na fursa za kujiendeleza kiuchumi na fursa za ajira; na
(c) kutengewa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi makundi hayo huitumia kama eneo la kuishi na kupata riziki ya chakula.
(2) Serikali na mamlaka za nchi zitachukua hatua za makusudi za kukuza na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kuweka miundombinu ya makazi, elimu na afya kwa ajili ya kizazi cha sasa na vijavyo vya jamii ya watu walio katika makundi madogo.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii, "makundi madogo" maana yake ni jamii za watu wanaoishi kwa kutegemea uoto wa asili na mazingira yanayowazunguka kwa ajili ya chakula, malazi na mahitaji mengine ya maisha.

47.-(1) Kila mwanamke ana haki ya: (a) kuheshimiwa utu wake;
(b) kuwa salama dhidi ya unyonyaji na ukatili;
(c) kushiriki bila ya ubaguzi katika uchaguzi na ngazi zote za maamuzi;
(d) kupata fursa na ujira sawa na mwanaume katika kazi zenye sifa zinazofanana;
(e) kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu na mila zenye madhara; (f) kulindwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale
anapojifungua; na
(g) kupata huduma bora ya afya.
 

- 19 -
 


 






Haki za wazee.
 
(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, heshima, usalama na fursa za wanawake wakiwemo wajane.

48. Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu utakaowezesha wazee kupata fursa ya:
(a) kushiriki katika shughuli za kijamii; (b) kuendeleza maisha yao;
(c) kutambuliwa utu wao na kuheshimiwa pasipo kudharauliwa; na
(d) kupata mahitaji ya msingi kutoka kwenye familia zao, jamii na mamlaka ya nchi.
 


SEHEMU YA PILI
WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI NA MIPAKA YA HAKI ZA BINADAMU

(a) Wajibu wa Raia kwa Taifa


 

Wajibu wa raia.













Wajibu wa kushiriki kazi.
 
49.-(1) Kila raia ana wajibu wa:

(a) kulinda na kutetea Katiba na sheria za nchi;
(b) kulinda na kuheshimu Tunu za Taifa na vitu muhimu vya utambulisho na urithi wa Taifa;
(c) kulipa kodi;
(d) kuheshimu haki, uhuru na maslahi ya watu wengine; (e) kuilinda Tanzania na kushiriki katika ulinzi wa Taifa;
(f) kulinda na kuheshimu utamaduni na maadili ya Taifa; na (g) kulinda na kutunza mazingira.
(2) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuwawezesha raia kutekeleza masharti ya Ibara hii.


50.-(1) Kila raia ana wajibu wa:
(a) kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi halali ya uzalishaji mali; na
(b) kuwa na nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikia malengo ya uzalishaji mali yake binafsi na malengo ya pamoja yanayotakiwa au yaliyowekwa na sheria.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), kazi yoyote ya shuruti ni marufuku katika Jamhuri ya Muungano.
(3) Kwa madhumuni ya Katiba hii, kazi yoyote haitahesabiwa kuwa ni kazi ya shuruti au kazi ya kikatili au ya kutweza endapo kazi hiyo, kwa mujibu wa sheria za nchi ni -
(a) kazi ambayo haina budi ifanywe kutokana na hukumu au amri ya mahakama;
(c) kazi ambayo haina budi kufanywa na askari wa jeshi lolote katika kutekeleza majukumu yao;
(d) kazi ambayo haina budi kufanywa kutokana na kuwapo hali ya hatari, baa au janga lolote linalotishia uhai na ustawi wa jamii; na
 


- 20 -
 


(e) kazi au huduma yoyote ambayo ni sehemu ya -
(i) majukumu ya kawaida ya kuhakikisha ustawi wa jamii;
(ii) ujenzi wa Taifa wa lazima kwa mujibu wa sheria za nchi; au
(iii) jitihada za Taifa za kutumia uwezo wa kila mtu kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha ustawi wa jamii na uchumi wa Taifa na kuhakikisha maendeleo na tija ya kitaifa.


 

Ulinzi wa mali ya umma.









Haki na wajibu muhimu.
 
51.-(1) Kila raia anao wajibu wa kulinda maliasili ya Taifa, mali ya mamlaka ya nchi na mali yoyote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha rasilimali za nchi na maliasili za Taifa.
(3) Kila mtu anao wajibu wa kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na mali inayomilikiwa kwa pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa makini kwa kuzingatia mipango endelevu na haki ya vizazi vijavyo.


52.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilivyofafanuliwa katika Katiba hii.
(2) Kila raia katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.
(3) Mtu yeyote katika Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki, hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi wake.
(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo maalum kwa mtu yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi.
(5) Ili watu wote wafaidi haki na uhuru uliotajwa katika Katiba hii, kila mtu anao wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
 


(b) Wajibu wa Mamlaka za Nchi

 

Hifadhi ya haki za binadamu.
 
53.-(1) Serikali na mamlaka zote za nchi zinao wajibu wa kuzingatia na kuhifadhi haki za binadamu ikiwa ni msingi wa uhuru kama ilivyoainishwa katika Katiba hii.
(2) Haki na uhuru wa kila mtu kama zilivyoainishwa katika Katiba hii zitaheshimiwa, kuhifadhiwa na kudumishwa na mamlaka za nchi, mamlaka binafsi na kila mwananchi.
(3) Haki na uhuru ambao umeainishwa katika mikataba ya kikanda na ya kimataifa kuhusu haki za binadamu ambazo Jamhuri ya Muungano imeridhia, isipokuwa masharti ambayo Jamhuri ya Muungano imeeleza wazi kutojifunga nayo, zitakuwa Sehemu ya Haki za Binadamu zilizoainishwa katika Sura hii.
 


- 21 -
 



 

Usimamizi wa haki za binadamu.
 
54.-(1) Katika kutafsiri masharti ya Sura hii ya Haki za Binadamu, Mahakama au chombo kingine chochote cha kufanya uamuzi kitazingatia mambo yafuatayo:
(a) haki ya usawa, utu na uhuru wa mtu binafsi; (b) sheria za kimataifa na haki za binadamu; na (c) haki za jamii na maslahi ya jamii kwa ujumla.
(2) Mtu anayeamini kuwa masharti yaliyomo katika Sura hii yamekiukwa au yanaelekea kukiukwa na mamlaka, chombo cha uamuzi, sheria au sera yoyote dhidi yake, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu kwa hati maalumu ya maombi kwa mujibu wa sheria za nchi ili kupata nafuu inayohitajika.
(3) Mahakama inaweza, kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1) kutoa maelekezo itakayoona yanafaa, kuweka zuio, katazo au kuamuru jambo lifanyike ambalo lilikuwa limenyimwa.
(4) Shauri katika Mahakama ya kudai haki za kikatiba kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii yanaweza kufunguliwa na:
(a) mtu anayejiwakilisha mwenyewe au taasisi inayowawakilisha wanachama wake;
(b) mtu anayemwakilisha mtu ambaye hawezi kujiwakilisha mwenyewe kwa mujibu wa sheria za nchi; au
(c) mtu anayewakilisha kundi la watu wenye malengo yanayofanana au jamii ya watu fulani wenye kuvunjiwa haki husika.
 


(c) Mipaka ya Haki za Binadamu


 

Mipaka ya haki za binadamu.
 
55.-(1) Haki zote zilizoainishwa katika Sura hii ya Katiba endapo zitahitajika kuwekewa mipaka ni lazima mipaka hiyo kutumika kwa uwazi na kidemokrasia kwa kuzingatia utu, usawa, uhuru na vigezo muhimu, ikijumuisha:
(a) aina ya haki;
(b) umuhimu na sababu za kuweka mipaka; (c) asili na ukubwa wa mpaka husika;
(d) uhusiano baina ya mpaka husika na sababu yake;
(e) njia nyepesi ya kufikia madhumuni ya matumizi ya mpaka husika; na
(f) umuhimu wa kulinda usalama wa nchi.
(2) Bunge litatunga sheria, ambayo pamoja na mambo mengine, itasimamia matumizi na utekelezaji wa masharti ya Ibara hii.
 


SURA YA TANO
URAIA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO


 

Uraia wa Jamhuri ya Muungano.
 
56.-(1) Mtu ambaye, kabla ya Katiba hii kuanza kutumika, ni raia wa Jamhuri ya Muungano ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Uraia wa Jamhuri ya Muungano ni wa aina mbili na utapatikana kwa njia ya kuzaliwa au kujiandikisha.
 



- 22 -
 


 

Uraia wa kuzaliwa.






















Uraia wa kuandiki-shwa.

























Hadhi ya watu wenye asili au nasaba ya Tanzania.
 
57.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanganyika au Zanzibar atakuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa kuzaliwa, mama au baba yake ni, au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa mama au baba yake ni raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kama kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano katika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani, atachukuliwa kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
(5) Endapo uraia wa wazazi wa mtoto aliyepewa uraia chini ya masharti ya ibara ndogo ya (4) utabainika kuwa si uraia wa Jamhuri ya Muungano, uraia wa mtoto huyo utasita.


58.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkaazi wa Jamhuri ya Muungano na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria za nchi anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muungano na ambaye -
(a) amedumu katika ndoa hiyo kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo; na
(b) ametimiza masharti yaliyoainishwa katika sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1),
anaweza kuomba uraia wa kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Endapo ndoa iliyotajwa katika ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake wa Tanzania, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika ibara ndogo ya (2), atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake si raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuandikishwa.
(6) Bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine, kusimamia masuala yanayohusu uraia wa Jamhuri ya Muungano.


59. Bila ya kuathiri masharti yaliyomo kwenye Sura hii, mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi kama itakavyoainishwa
katika sheria za nchi.
 


- 23 -
 



SURA YA SITA
MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO


 

Muundo wa Muungano.















Vyombo vya utendaji vya Jamhuri ya Muungano.




Mamlaka ya Serikali ya Muungano.











Mambo ya Muungano.





Nchi Washirika.
 
60.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na (c) Serikali ya Tanganyika.
(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano; (b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na (c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yataainishwa katika Katiba za Nchi Washirika.


61.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa ndiyo chombo chenye mamlaka ya utendaji, Bunge litakuwa na mamlaka ya kutunga sheria kwa mambo ya Muungano na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama itakuwa ni chombo cha utoaji haki.
(2) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti ya Katiba hii.


62.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji kwa mambo yote yaliyoorodheshwa kuwa Mambo ya Muungano, na wakati inapotekeleza majukumu yake, itazingatia mamlaka yake iliyopewa chini ya Katiba hii.
(2) Utekelezaji wa majukumu ya Serikali utafanywa kwa namna na kwa misingi iliyowekwa na Katiba hii au sheria za nchi.
(3) Bila ya kuathiri au kukiuka masharti ya Ibara hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kwa makubaliano na masharti maalum baina yake na Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanganyika, inaweza kutekeleza jambo lolote lililo chini ya mamlaka ya Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanganyika kwa mujibu wa masharti ya makubaliano hayo.


63. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika Ibara ya 61, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka juu ya mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Katiba hii.


64.-(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Nchi Washirika ni Tanganyika na Zanzibar.
(2) Serikali ya Tanganyika itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanganyika.
(3) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar.
(4) Nchi Washirika zitatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
 


- 24 -
 


(5) Nchi Washirika zitakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na zitatekeleza majukumu yao kwa mambo yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Nchi Washirika kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Nchi Washirika.


 

Mamlaka ya Nchi Washirika.





















Mahusiano kati ya Nchi Washirika.













Mawaziri Wakaazi.
 
65.-(1) Kila Nchi Mshirika wa Muungano itakuwa na mamlaka na haki zote juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa mamlaka hayo, kila Nchi Mshirika wa Muungano itazingatia misingi ya ushirikiano na mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawa kwa ajili ya ustawi ulio bora kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano.
(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Nchi Mshirika wa Muungano itakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Nchi Mshirika wa Muungano.
(3) Nchi Mshirika wa Muungano inaweza, wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya ibara ndogo ya (2), kuomba mashirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kimataifa au kikanda, na Serikali ya Jamhuri Muungano inaweza kutoa ushirikiano kwa Nchi Mshirika wa Muungano kwa namna itakavyohitajika.
(4) Bunge litatunga sheria itakayoainisha, pamoja na mambo mengine, utaratibu wa namna ya utekelezaji bora wa masharti ya Ibara hii.


66.-(1) Kila Nchi Mshirika inaweza, katika kutekeleza majukumu yake katika maeneo mbalimbali, kutekeleza majukumu hayo kwa misingi ya kushirikiana na kushauriana na Nchi Mshirika nyingine au baina ya Nchi Mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kukuza na kulinda maslahi ya Taifa na maendeleo ya wananchi.
(2) Nchi Washirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano zinaweza kushauriana na kushirikiana katika mambo ya uongozi, utawala, vyombo vya uwakilishi na mahakama.
(3) Utendaji wa Serikali za Nchi Washirika au wa chombo chochote kati ya vyombo vya serikali hizo na uendeshaji wa shughuli, utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano, nia, umuhimu na azma ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.


67.-(1) Kila Nchi Mshirika itateua Waziri Mkaazi atakayeratibu na kusimamia mahusiano baina ya Serikali za Nchi Washirika na kati ya Serikali ya Nchi Mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Mawaziri Wakaazi watakuwa na ofisi zao na watafanya kazi wakiwa Makao Makuu ya Serikali ya Muungano.
(3) Pamoja na majukumu mengine watakayopangiwa na Serikali za Nchi Washirika, Mawaziri Wakaazi watakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu ushirikiano au mahusiano ya kimataifa; na
 



- 25 -
 


(b) kuwa kiungo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika na baina ya Serikali za Nchi Washirika.


 

Mamlaka ya wananchi.










Wajibu wa kulinda Muungano.
 
68.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na chombo kitakachopewa mamlaka na Katiba hii, na vilevile, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitapata mamlaka kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka chini ya Katiba zao.
(2) Serikali za Nchi Washirika, katika kutekeleza mamlaka zao, zitawajibika kustawisha mamlaka ya wananchi kwa kugatua madaraka kwa serikali za mitaa zitakazoanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika au Katiba ya Zanzibar, kama itakavyokuwa.


69.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia kwa mujibu wa Katiba hii, viongozi wakuu wenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano waliotajwa katika ibara ndogo ya (3) watawajibika, kila mmoja wao katika kutekeleza madaraka waliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii au Katiba za Nchi Washirika kuhakikisha kuwa analinda, kuimarisha na kudumisha Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1), kila mmojawapo wa viongozi wakuu waliotajwa katika ibara ndogo ya (3), kabla ya kushika madaraka yake ataapa kuutetea na kuudumisha Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni: (a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano; (c) Rais wa Tanganyika; na
(d) Rais wa Zanzibar.
 


SURA YA SABA
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO


SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI, RAIS, MAKAMU WA RAIS NA BARAZA LA MAWAZIRI

 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
 
(a) Serikali

70.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itaundwa na Rais, Makamu wa Rais na Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengine ambayo yameainishwa katika sheria za nchi.
(3) Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa na Rais mwenyewe, au kwa kukasimu madaraka hayo kwa Makamu wa Rais au watu wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(4) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Ibara hii hayatahesabiwa kwamba:

- 26 -
 


(a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au mamlaka yoyote ambayo si Rais;
(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya kisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlaka nyingine yoyote ambayo si Rais; au
(c) yanazuia Mahakama kukabidhi madaraka yoyote ya kisheria kwa mtu au watu wenye madaraka katika Mahakama za Jamhuri ya Muungano.

(b) Rais

 

Rais wa Jamhuri ya
Muungano.







Madaraka na majukumu ya Rais.
 
71.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu na:
(a) atakuwa alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake;
(b) atakuwa alama ya umoja, uhuru wa nchi na mamlaka yake; na (c) atakuwa na dhamana ya kukuza na kuhifadhi umoja wa
kitaifa.


72.-(1) Rais, katika nafasi ya madaraka ya Mkuu wa Nchi, atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:
(a) kuisimamia na kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano; (b) kulinda utaifa wa Jamhuri ya Muungano;
(c) kuhutubia na kufungua rasmi Bunge Jipya na kulivunja Bunge baada ya kumaliza muda wake;
(d) kuhutubia na kufungua rasmi Kalenda ya Mwaka ya Mahakama;
(e) kuidhinisha uwasilishaji Bungeni wa makisio ya mapato na matumizi ya Serikali, Bunge na Mahakama katika mwaka wa fedha;
(f) kuweka saini katika Muswada wa Sheria uliyopitishwa na Bunge;
(g) kutunuku nishani za heshima kwa niaba ya Watu wa Jamhuri ya Muungano kwa ujumla;
(h) kuteua mabalozi, watu watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wawakilishi wa nchi katika taasisi mbalimbali za kimataifa;
(i) kupokea hati za utambulisho za Mabalozi wa nchi za nje nchini;
(j) kutoa msamaha kwa mtu yeyote anayetumikia adhabu iliyotolewa na Mahakama kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(k) kuidhinisha utekelezaji wa adhabu ya kifo iliyotolewa kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Rais, katika nafasi ya madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu, atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:
(a) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa; (b) kuamuru Majeshi ya Ulinzi kwenda vitani au kusitisha vita; (c) kutia saini makubaliano ya amani au kusitisha vita;
 


- 27 -
 




(d) kutangaza hali ya hatari au hali ya kuzingirwa eneo fulani la Jamhuri ya Muungano;
(e) kuteua Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
(f) kuwapandisha vyeo maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama katika ngazi mbalimbali na kutoa kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi.
(3) Rais, katika nafasi ya madaraka ya Kiongozi wa Serikali, atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo:
(a) kuongoza vikao vya Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano;
(b) kupanga, kuelekeza, kusimamia na kuratibu majukumu ya wizara na taasisi za serikali;
(c) kuwateua Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(d) kumteua Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu;
(e) kumteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na
(f) kuwateua Wenyeviti, Makamu Wenyeviti, Wajumbe na Makamishna wa Tume mbalimbali zilizoanzishwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(4) Katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ibara hii, Rais ataepuka kujinasibisha, kwa namna yoyote ile, na chama chochote cha siasa au kundi lolote kwa namna ambayo inaathiri umoja wa wananchi.
(5) Rais atakuwa na mamlaka ya kutekeleza majukumu mengine ambayo kwa asili yake yanatekelezwa na Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu au Kiongozi wa Serikali, ambayo hayakuainishwa katika Ibara hii na ambayo hayakiuki Katiba hii na sheria za nchi.


 

Utekelezaji wa madaraka ya Rais.
 
73.-(1) Katika utekelezaji wa madaraka ya Rais kwa mujibu wa Sura hii na kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (3), Rais ana mamlaka ya kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Katika utekelezaji wa madaraka kama ilivyoainishwa katika ibara ndogo ya (1) na (2), Rais atazingatia masharti kuhusu uthibitisho wa Bunge katika nafasi za madaraka na vile vile ushauri wa mamlaka za Serikali, Bunge au Mahakama zilizopewa madaraka ya kumshauri katika kufanya uteuzi, kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali.
(4) Mamlaka ya kuwateua watu wengine wote wasiokuwa viongozi wala watendaji wakuu kushika nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na mamlaka ya kuwapandisha vyeo watu hao, kuwaondoa katika madaraka, kuwafukuza
 


- 28 -
 


kazi, kuwasimamisha kazi na mamlaka ya kudhibiti nidhamu ya watu waliokabidhiwa madaraka, yatakuwa mikononi mwa Tume za Utumishi na mamlaka za nchi zilizotajwa na kupewa mamlaka hayo na sheria za nchi.
(5) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) hayazuii Rais kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya watumishi na utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.


 

Rais kuzingatia ushauri.








Rais kushindwa kumudu majukumu yake.
















Utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais kabla ya kumaliza muda wake.
 
74.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za nchi, Rais atakuwa na wajibu wa kufuata na kuzingatia ushauri atakaopewa na mamlaka za nchi, na endapo hakubaliani na ushauri aliopewa, sharti atoe sababu katika Baraza la Mawaziri kuhusu sababu ya kutokubaliana na ushauri aliopewa.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Rais hatalazimika kufuata ushauri aliopewa ambao unakwenda kinyume au kukiuka masharti ya Katiba hii au sheria za nchi.


75.-(1) Endapo Baraza la Mawaziri litaridhika kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi, linaweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi, hawezi kumudu kazi zake.
(2) Baada ya kupokea azimio lililowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1), Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ambayo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu ipasavyo.
(3) Jaji Mkuu anaweza, baada ya kutafakari ushauri na ushahidi wa kitabibu, kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba kutokana na maradhi, Rais ameshindwa kumudu kazi zake, na iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha hati hiyo ndani ya siku saba kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesabiwa kwamba nafasi ya madaraka ya Rais iko wazi, na masharti yaliyomo katika Ibara ya 76 yatatumika.
(4) Bodi ya utabibu itakayoteuliwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) itajumuisha watu wasiopungua watatu watakaoteuliwa kutoka miongoni mwa madaktari bingwa wanaotambuliwa na sheria za nchi.


76.-(1) Endapo nafasi ya madaraka ya Rais itakuwa wazi kutokana na:
(a) Rais kufariki dunia; (b) Rais kujiuzulu;
(c) Rais kupoteza sifa za uchaguzi katika nafasi ya madaraka ya Rais;
(d) Rais kutomudu kazi zake kutokana na maradhi;
(e) Rais kushtakiwa Bungeni na kuondolewa katika madaraka kwa mujibu wa Katiba hii,
basi Makamu wa Rais ataapishwa na kushika madaraka ya Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoainishwa katika Ibara ya 80.
(2) Mara tu baada ya Rais kuapishwa na kushika madaraka kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1), au kwa vyovyote vile ndani ya kipindi kisichozidi siku kumi na nne tangu alipoapishwa:
 


- 29 -
 


(a) kwa Rais aliyepatikana kwa kupendekezwa na chama cha siasa, baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka; au
(b) kwa Rais aliyepatikana kwa utaratibu wa mgombea huru, baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa,
atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zaidi ya asilimia hamsini ya Wabunge wote.

 

Utekelezaji wa majukumu ya Rais akiwa hayupo.
 
77.-(1) Ikitokea kwamba nafasi ya madaraka ya Rais iko wazi kutokana na:
(a) masharti yaliyomo katika Ibara ya 75; (b) masharti yaliyomo katika Ibara ya 88;
(c) kutokuwepo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo wa wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa -
(i) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iko wazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa, basi;
(ii) Waziri Mwandamizi; au
(iii)kama Waziri Mwandamizi nafasi yake iko wazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa, basi Waziri mwingine yeyote atakayeteuliwa na Baraza la Mawaziri.
(2) Endapo mtu yeyote aliyetajwa katika ibara ndogo ya (1) atatekeleza kazi na shughuli za Rais kutokana na sababu kwamba mtu mwingine anayemtangulia katika orodha hiyo hayupo, basi mtu huyo ataacha kutekeleza kazi na shughuli hizo mara tu mtu huyo mwingine anayemtangulia atakaporejea na mtu huyo ataanza kutekeleza kazi na shughuli za Rais.
(3) Mtu yeyote atakayekaimu nafasi ya madaraka ya Rais, kwa namna yoyote ile, hatakuwa na madaraka katika mambo yafuatayo:
(a) kuteua au kumuondoa madarakani kiongozi yeyote yule aliyeteuliwa na Rais kwa mujibu wa Katiba hii; au
(b) jambo jingine lolote kama litakavyoainishwa na Rais katika hati ya kukasimu madaraka yake.
(4) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (2) na (3), Rais atakasimu madaraka yake kwa hati maalum aliyotia saini yake.
 


(c) Uchaguzi wa Rais


 

Uchaguzi wa Rais.





Sifa za Rais.
 
78.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Nafasi ya madaraka ya Rais itakuwa wazi na uchaguzi wa Rais utafanyika baada ya Rais kumaliza muda wake wa kuwa madarakani kwa mujibu wa Katiba hii.


79.-(1) Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii na sheria za nchi;
 


- 30 -
 



(b) ni mwenye akili timamu;
(c) wazazi wake wote wawili ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini;
(e) anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(f) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa au mgombea huru;
(g) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa Taifa kwa misingi ya ukabila, dini, rangi au jinsi; na
(h) ni mwadilifu, anayeheshimu haki za binadamu, asiyedharau wala kubagua watu kwa misingi ya kabila, dini, jinsi, maumbile au hali zao katika jamii na anafuata maadili ya viongozi na mwenendo wake hautiliwi shaka na jamii.
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea nafasi ya Urais ikiwa -(a) mtu huyo ana maslahi yoyote katika mkataba wa Serikali wa
aina yoyote aliyowekewa miiko maalum kwa mujibu wa sheria za nchi, na iwapo amekiuka miiko hiyo;
(b) kwa mujibu wa sheria ya nchi inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguzi wa aina yoyote, mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha kama mpiga kura au kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu; au
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi amewahi kutiwa hatiani katika mahakama kwa kosa la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali au makosa yanayohusu kukosa uaminifu.


 

Utaratibu wa Uchaguzi wa Rais.
 
80.-(1) Katika Uchaguzi wa Rais, kila chama cha siasa kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha kwa Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano, kwa mujibu wa sheria za nchi, jina la mwanachama mmoja anayependekezwa kwa nafasi ya madaraka ya Rais.
(2) Endapo ni Mgombea huru, kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa katika Katiba hii, atawasilisha jina lake kwenye Tume Huru ya Uchaguzi.
(3) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa Rais yatawasilishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi katika siku na kwa utaratibu uliyoainishwa katika sheria za nchi.
(4) Endapo itafika siku na saa iliyotajwa kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea mmoja tu ambaye anapendekezwa kuwa halali, Tume Huru ya Uchaguzi itawasilisha jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au kumkataa kwa mujibu wa masharti yaliyoainishwa katika Katiba hii na sheria za nchi.
(5) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanyika siku itakayoteuliwa na Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria za nchi.
(6) Mgombea wa nafasi ya madaraka ya Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo atapata kura zinazozidi asilimia hamsini ya kura zote halali kwa nafasi ya madaraka ya Rais.
 



- 31 -
 


(7) Endapo katika Uchaguzi wa Rais hakuna mgombea aliyekidhi masharti ya ibara ndogo ya (6), basi uchaguzi utarudiwa ndani ya siku sitini kwa wagombea walioshika nafasi ya kwanza na ya pili.


 

Malalamiko kuhusu uhalali wa Uchaguzi wa Rais.





















Kiapo cha Rais na muda wa kushika madaraka.

















Haki ya kuchaguliwa tena.
 
81.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), endapo mtu yeyote aliyeshiriki kama mgombea katika nafasi ya madaraka ya Rais katika Uchaguzi wa Rais hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo, anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
(2) Malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais yatawasilishwa Mahakama ya Juu ndani ya muda uliowekwa na sheria ya nchi baada ya siku ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa Rais.
(3) Mahakama ya Juu itasikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais ndani ya muda utakaoainishwa na sheria ya nchi tangu kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) na uamuzi huo utakuwa wa mwisho.
(4) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (3), Mahakama ya Juu inaweza kutoa uamuzi bila kutoa sababu za uamuzi na sababu hizo zikatolewa ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini tangu siku ya kutoa uamuzi.
(5) Iwapo Mahakama ya Juu itaamua kuwa matokeo ya Uchaguzi wa Rais si halali, Uchaguzi wa Rais utarudiwa ndani ya siku sitini baada ya uamuzi kutolewa.


82.-(1) Rais Mteule ataapishwa na Jaji Mkuu na atashika nafasi ya madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote, hatashika madaraka kabla ya kupita siku thelathini kutoka siku matokeo ya Uchaguzi wa Rais yalipotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi au siku ya kuthibitishwa na Mahakama ya Juu.
(2) Isipokuwa kama ataacha kushika nafasi ya madaraka ya Rais mapema zaidi, Rais atashika nafasi ya madaraka ya Rais kwa muda wa miaka mitano tangu siku alipoapishwa kuwa Rais.
(3) Rais atashika nafasi ya madaraka ya Rais hadi -
(a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika nafasi ya madaraka ya Rais;
(b) siku ambapo atafariki dunia; (c) siku atakapojiuzulu; au
(d) atakapoacha kushika nafasi ya madaraka ya Rais kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.


83.-(1) Mtu ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika nafasi ya madaraka ya Rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

(2) Mtu hatakuwa na sifa ya kugombea na kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili katika nafasi ya madaraka ya Rais.
 



- 32 -
 


(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Tanganyika au Zanzibar hatapoteza sifa za kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa sababu aliwahi kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Tanganyika au Rais wa Zanzibar.
(4) Endapo Makamu wa Rais atashika nafasi ya madaraka ya Rais kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 76 kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais kwa vipindi viwili, lakini kama atashika nafasi ya madaraka ya Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya madaraka ya Rais kwa kipindi kimoja tu.


(d) Masharti Mahsusi kuhusu Mamlaka ya Rais


 

Madaraka ya kutangaza vita.














Madaraka ya Rais kutangaza hali ya hatari.
 
84.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara hii, Rais atakuwa na mamlaka ya kutangaza kuwepo kwa vita kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi nyingine au kundi lolote lile baada ya kupata idhini ya Bunge.
(2) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), endapo Jamhuri ya Muungano itakuwa imevamiwa au kundi lolote limeanzisha vita ndani ya Jamhuri ya Muungano basi, Rais anaweza, baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, kutangaza kuwepo kwa vita katika Jamhuri ya Muungano.
(3) Baada ya kutoa tangazo kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2), Rais atalitaarifu Bunge kwa kupeleka nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya tangazo, ataitisha Mkutano wa Bunge ili kulijulisha Bunge kuhusu tangazo lililotolewa na Rais.


85.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria za nchi, Rais anaweza, baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa, kutangaza hali ya hatari au hali ya kuzingirwa kwa eneo fulani la Jamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.
(2) Rais anaweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo -(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita;
(b) kuna hatari ya dhahiri kwamba Jamhuri ya Muungano inakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita;
(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani katika jamii au kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amani na usalama;
(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani katika jamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote ambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumia mamlaka ya pekee;
(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au janga la kimazingira ambalo linatishia jamii au sehemu ya jamii katika Jamhuri ya Muungano; au
(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri ni tishio kwa usalama wa nchi.
 




- 33 -
 



(3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano au eneo lolote la Jamhuri ya Muungano, Rais atawasilisha nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, ndani ya siku zisizozidi kumi na nne tangu kutolewa kwa tangazo hilo, ataitisha mkutano wa Bunge ili kulijulisha juu ya taarifa ya hali ya hatari iliyotangazwa na Rais.
(4) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti kuhusu nyakati na taratibu ambazo zitawawezesha baadhi ya watu wenye kusimamia utekelezaji wa mamlaka ya Serikali katika sehemu mahsusi za Jamhuri ya Muungano kumuomba Rais kutumia madaraka aliyopewa na Ibara hii kuhusiana na yoyote kati ya sehemu hizo endapo katika sehemu hizo, kunatokea lolote kati ya hali zilizotajwa katika aya ya (c), (d) na (e) za ibara ndogo ya (2) na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemu hizo, na pia, kwa ajili ya kufafanua utekelezaji wa mamlaka ya Serikali wakati wa hali ya hatari.
(5) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais kwa mujibu wa Ibara hii litakoma kutumika iwapo litafutwa na Rais.
(6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi au utekelezaji wa masharti ya Ibara hii, masharti ya utangazaji wa hali ya hatari kama ilivyotajwa katika Ibara hii, yatatumika tu katika sehemu ya Jamhuri ya Muungano ambapo hali hiyo ya hatari imetangazwa.


 

Mamlaka ya Rais kutoa msamaha.























Kinga ya mashtaka dhidi ya Rais.
 
86.-(1) Rais kwa mamlaka ya Mkuu wa Nchi, anaweza -
(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia kwa kosa lolote mbele ya Mahakama dhidi ya Jamhuri ya Muungano kwa masharti maalum kama yatakavyoainishwa katika sheria za nchi; au
(b) kubadilisha adhabu ya kifo kuwa adhabu ya kifungo cha maisha.
(2) Masharti ya Ibara hii yatatumika kwa mtu aliyehukumiwa na kuadhibiwa akiwa Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa Zanzibar kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge inayotumika Zanzibar, hali kadhalika, masharti hayo yatatumika kwa mtu aliyehukumiwa na kuadhibiwa Tanganyika kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge inayotumika Tanganyika.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii, kutakuwa na Kamati ya Taifa ya Ushauri ambayo itakuwa na wajibu wa kumshauri Rais kuhusu kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mahakamani na anatumikia adhabu.
(4) Utaratibu wa namna ya utekelezaji wa madaraka kwa mujibu wa Ibara hii, muundo, majukumu na utendaji kazi wa chombo kinachohusika na masuala ya msamaha wa wafungwa utaainishwa na sheria za nchi.


87.-(1) Wakati Rais akiwa madarakani, hatashitakiwa wala mtu yeyote hataendesha mashtaka ya aina yoyote dhidi yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
 



- 34 -
 



(2) Wakati Rais ameshika madaraka kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri la madai kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais atapewa au ametumiwa taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa analodai.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na kuondolewa madarakani na Bunge, haitakuwa halali kwa mtu kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la madai dhidi ya mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo alilofanya wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais.


 

Bunge kumshtaki Rais.
 
88.-(1) Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama itadaiwa kwamba Rais ametenda mojawapo ya makosa yafuatayo:
(a) ukiukwaji mkubwa wa masharti ya Katiba hii; (b) makosa makubwa ya jinai;
(c) kuzuia kwa namna yoyote ile yeye kuchunguzwa kwa mujibu wa Ibara hii;
(d) uhaini; (e) rushwa;
(f) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(g) kupuuza au kukataa kutekeleza uamuzi au amri halali ya Mahakama; au
(h) amefanya kitendo ambacho kinakiuka kanuni za maadili au miiko ya uongozi.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama-
(a) hoja ya namna hiyo itatolewa baada ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge; na
(b) taarifa ya maandishi, iliyotiwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini na tano ya Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku kumi na nne kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni.
(4) Taarifa itakayowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (3)(b) itafafanua makosa aliyoyatenda Rais, na itapendekeza kuwa Tume ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze tuhuma zilizotolewa dhidi ya Rais.
 




- 35 -
 


(5) Wakati wowote baada ya kupokea taarifa iliyotiwa saini na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuwasilisha hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha mbele ya Bunge na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati ya Uchunguzi.
(6) Endapo hoja ya kuunda Kamati ya Uchunguzi itaungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia sabini na tano ya Wabunge wote, Spika atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati ya Uchunguzi.
(7) Kamati ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya Ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanganyika; (c) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na
(d) Wabunge sita kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano, watatu kutoka kila upande wa Nchi Washirika watakaoteuliwa na Spika.
(8) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini na madaraka ya Rais yatatekelezwa na Makamu wa Rais hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya Azimio la Bunge kuhusiana na mashtaka yaliyotolewa dhidi yake.
(9) Ndani ya siku saba baada ya Kamati ya Uchunguzi kuundwa, itachunguza na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Kudumu za Bunge.
(10) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.
(11) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Kudumu za Bunge.
(12) Baada ya taarifa ya Kamati ya Uchunguzi kuwasilishwa, Bunge litaijadili taarifa hiyo na kutoa fursa kwa Rais kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua asilimia sabini na tano ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais ama yamethibitika au hayakuthibitika.
(13) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika nafasi ya madaraka ya Rais, Spika atamfahamisha Rais juu ya Azimio la Bunge na Rais atakuwa ameondolewa madarakani na Makamu wa Rais ataapishwa mara moja kushika nafasi ya madaraka ya Rais.
(14) Endapo Rais ataacha kushika nafasi ya madaraka ya Rais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika hatakuwa na haki ya:
(a) kushika nafasi ya madaraka ya Rais, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Tanganyika au Rais wa Zanzibar; na
(b) kupata malipo yoyote ya uzeeni, posho wala kupata haki au nafuu nyingine anazopewa Rais au mtu aliyekuwa Rais kwa mujibu wa Katiba au sheria za nchi.


- 36 -
 



 

Maslahi ya Rais.
 
89.-(1) Rais atalipwa mshahara na malipo mengineyo kama yatakavyoainishwa na Tume ya Utumishi wa Umma na atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni na stahili nyingine kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina.
(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais hayatapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii.
 

(e) Makamu wa Rais

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.













Upatikanaji wa Makamu wa Rais.













Sifa za Makamu wa Rais.
 
90.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla na:
(a) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(b) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayupo kazini au yupo nje ya nchi; na
(c) atakuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali.
(2) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Makamu wa Rais atatekeleza au atawezesha au kusimamia utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.
(3) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, Makamu wa Rais atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa majukumu yake.


91.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 76, Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake au mgombea huru wakati ule ule anapopendekezwa mgombea wa nafasi ya madaraka ya Rais na watapigiwa kura kwa pamoja.
(2) Endapo mgombea wa nafasi ya madaraka ya Rais atachaguliwa basi na Makamu wa Rais atakuwa amechaguliwa.
(3) Mtu atateuliwa kugombea nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo mgombea wa nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.


92.-(1) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama anazo sifa za kuchaguliwa kuwa Rais.
(2) Chama cha siasa chochote au mtu yeyote anayekusudia kugombea nafasi ya madaraka ya Rais, akiwa mgombea huru, hatazuiwa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mgombea nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais kwa sababu tu kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa Zanzibar au Rais wa Tanganyika.
(3) Endapo mtu ambaye ni Rais wa Tanganyika au Rais wa Zanzibar anateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha nafasi ya madaraka ya Rais wa Tanganyika au ya Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.
 


- 37 -
 



 

Kiapo cha Makamu wa Rais.



Wakati wa Makamu wa Rais kushika madaraka.















Bunge kumshtaki Makamu wa Rais.
 
93. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake ataapishwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

94.-(1) Makamu wa Rais atashika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais siku hiyo hiyo Rais anaposhika madaraka.
(2) Makamu wa Rais atashika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais hadi -
(a) muda wake utakapokwisha;
(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka; (c) atakapojiuzulu;
(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya nafasi ya madaraka ya Rais kuwa wazi;
(e) atakapoapishwa Rais mwingine kushika nafasi ya madaraka ya Rais pamoja na Makamu wake;
(f) atakapoondolewa madarakani baada ya kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii; au
(g) atakapoacha kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais vinginevyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

95.-(1) Bunge litakuwa na mamlaka ya kumshtaki na kumuondoa Makamu wa Rais madarakani kwa utaratibu unaotumika kumshtaki Rais kwa mujibu wa Katiba hii, isipokuwa kwamba, hoja yoyote ya kumshtaki Makamu wa Rais itatolewa tu iwapo:
(a) Rais amewasilisha hati kwa Spika inayoeleza kwamba Makamu wa Rais ameacha au ameshindwa kutekeleza kazi za madaraka ya Makamu wa Rais;
(b) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au kiti cha Makamu wa Rais; au
(c) anadaiwa kutenda kosa lolote kati ya makosa yanayoweza kusababisha Rais kushtakiwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba hii,
isipokuwa kwamba, haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
(2) Masharti mengine kuhusu utaratibu wa kumshtaki Rais yatatumika wakati wa kumuondoa madarakani Makamu wa Rais.
(3) Masharti mengine yote ya Ibara ya 87 yatatumika pia kwa Makamu wa Rais isipokuwa tu kwamba Makamu wa Rais aliyeondolewa madarakani chini ya ibara ndogo ya (1), hatakuwa na sifa tena za kushika nafasi ya Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Tanganyika au Rais wa Zanzibar.
(4) Endapo Makamu wa Rais ataacha kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya uzeeni, posho wala kupata haki au nafuu nyinginezo anazopewa Makamu wa Rais au mtu aliyekuwa Makamu wa Rais kwa mujibu wa Katiba hii au sheria za nchi.
 



- 38 -
 


 

Upatikanaji wa Makamu wa Rais wakati nafasi hiyo inapokuwa wazi.
 
96. Endapo nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais iko wazi kutokana na masharti yaliyomo katika Ibara ya 94 na 95, basi mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile ndani ya siku zisizozidi kumi na nne tokea kifo au baada ya kuachia madaraka, Rais atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura za Wabunge zaidi ya asilimia hamsini ya Wabunge wote.
 

SEHEMU YA PILI
BARAZA LA MAWAZIRI LA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

(a) Baraza la Mawaziri

 

Kuundwa kwa Baraza la Mawaziri.


















Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri.












Waziri Mwanda-mizi.
 
97.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano litakalokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano; na
(b) Waziri Mwandamizi na Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais ataongoza mikutano ya Baraza la Mawaziri, na endapo Rais hayupo, mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili, Rais na Makamu wa Rais hawapo, Waziri Mwandamizi ataongoza Mikutano hiyo.
(3) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria vikao vya Baraza la Mawaziri lakini hatakuwa na haki ya kupiga kura.
(4) Baraza la Mawaziri ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais kuhusu mambo yanayohusu utekelezaji wa madaraka na matumizi ya mamlaka ya Rais.
(5) Bunge na Mahakama hazitakuwa na uwezo wa kisheria kuchunguza kama ushauri wowote au ushauri wa aina gani ulitolewa na Baraza la Mawaziri kwa Rais.


98.-(1) Kutakuwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano watakaoteuliwa na Rais kwa kushauriana na Makamu wa Rais na baadaye kuthibitishwa na Bunge.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), idadi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano haitazidi kumi na tano.
(3) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na Wizara kwa kuzingatia mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa Katiba hii.
(4) Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano utazingatia uwakilishi wa Nchi Washirika.
(5) Majukumu ya Waziri na Naibu Waziri yatakuwa kama yatakavyoainishwa na Rais kwenye Hati ya Uteuzi.


99.-(1) Kutakuwa na Waziri Mwandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge.

(2) Waziri Mwandamizi kabla ya kushika madaraka yake, ataapa mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kama itakavyoelezwa na sheria za nchi.
(3) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Waziri Mwandamizi endapo atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 101.
 


- 39 -
 


(4) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mwandamizi atashika madaraka ya Waziri Mwandamizi hadi:
(c) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika madaraka ya Urais; au
(d) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au (e) siku atakapojiuzulu; au
(f) siku ambapo Rais atakapomteua mtu mwingine kushika madaraka ya Waziri Mwandamizi.


 

Kazi na mamlaka ya Waziri Mwanda-mizi.



Sifa za Mawaziri na Naibu Mawaziri.














Kiapo, muda na masharti ya kazi ya Waziri na Naibu Waziri.














Utekelezaji wa shughuli za Serikali Bungeni.
 
100.-(1) Waziri Mwandamizi atakuwa na madaraka ya udhibiti na usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za Serikali za siku hadi siku.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mwandamizi atatekeleza majukumu yote atakayoelekezwa na Rais, na katika utekelezaji wa majukumu yake atawajibika kwa Rais.


101.-(1) Mtu atateuliwa kuwa Waziri au Naibu Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(c) ana uweledi na uzoefu.
(2) Watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa Mawaziri au Naibu Mawaziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano:
(a) Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa Bunge la Tanganyika, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar au madiwani katika Nchi Washirika;
(b) mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu wa mali za umma, ama katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika.

102.-(1) Waziri au Naibu Waziri hatashika nafasi ya madaraka hadi awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa na sheria za nchi.
(2) Muda wa kushika nafasi ya madaraka ya Waziri au Naibu Waziri utaanza tarehe ambayo Waziri au Naibu Waziri anayehusika ataapishwa.
(3) Kila Waziri anawajibika binafsi na kwa pamoja kwa Rais katika utekelezaji wa majukumu na katika kutumia nafasi ya madaraka ya Waziri.
(4) Waziri au Naibu Waziri atashika nafasi ya madaraka kwa muda wote isipokuwa kama:
(a) atajiuzulu au kufariki;
(b) Rais atatengua uteuzi wake; au
(c) zimebaki saa ishirini na nne kabla ya Rais mteule kushika madaraka ya Rais.

103.-(1) Mawaziri na Naibu Mawaziri hawatakuwa na haki ya kuhudhuria vikao vya Bunge isipokuwa tu:
 


- 40 -
 


(a) endapo kutakuwa na hoja mahsusi ambayo Bunge linahitaji ufafanuzi kwa Waziri husika; au
(b) endapo Serikali au Waziri ataomba na kuruhusiwa kuwasilisha au kuitolea ufafanuzi hoja yoyote Bungeni.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Waziri atakayeruhusiwa kuhudhuria kikao cha Bunge anaweza kulihutubia Bunge.
(3) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera za Serikali kwa jumla.
(4) Kila Waziri atahudhuria vikao vya Kamati za Bunge kila atakapohitajika na kutoa maelezo au ufafanuzi wa suala lolote linalohusu utendaji katika nafasi ya madaraka yake.
(5) Kwa kuzingatia masharti mengine ya jumla ya Katiba hii, Mawaziri watatoa maelezo au taarifa ambazo zinahitajika kutolewa Bungeni kwa mujibu wa sheria za nchi.


(b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali


 

Mwana-sheria Mkuu wa Serikali.
 
104.-(1) Kutakuwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambaye katika Katiba hii ataitwa kwa kifupi kama "Mwanasheria Mkuu" ambaye atateuliwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge.
(2) Mtu anayestahili kuwa Mwanasheria Mkuu atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe na shahada ya sheria ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(c) awe ni mweledi na mwenye sifa ya uwakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar au Mahakama Kuu ya Tanganyika;
(d) awe ni mtumishi mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika;
(e) awe ni mtu ambaye amedumu na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano; na
(f) ana tabia njema na mwenendo usiotiliwa shaka na jamii.
(3) Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo, atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili au kuhusiana na sheria zitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza.
(4) Mwanasheria Mkuu atatekeleza kazi au shughuli nyingine zilizokabidhiwa kwake na Katiba hii au sheria za nchi.
(5) Katika kutekeleza kazi yake, Mwanasheria Mkuu atakuwa na haki ya kuhudhuria na kusikilizwa na Mahakama katika Jamhuri ya Muungano na Mahakama Kuu za Nchi Washirika.
(6) Mwanasheria Mkuu hatashika nafasi ya madaraka ya Mwanasheria Mkuu hadi awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha utii na uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusu utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
 


- 41 -
 


(7) Mwanasheria Mkuu, isipokuwa kama ataacha kushika nafasi ya madaraka yake mapema zaidi, ataendelea kushika madaraka hadi Rais atakapomteua Mwanasheria Mkuu mwingine.

(c) Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu

 

Katibu Mkuu Kiongozi.

































Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.
 
105.-(1) Kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi watatu katika utumishi wa umma watakaopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma na kuthibitishwa na Bunge.
(2) Katibu Mkuu Kiongozi atakuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu, Katibu wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa na Mkuu wa Utumishi wa Umma.
(3) Katika wadhifa wake wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi atakuwa Mtendaji Mkuu katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri, na atatekeleza shughuli zifuatazo kwa kufuata maagizo ya jumla au maalum atakayopewa na Rais, yaani:
(a) kuandaa ratiba ya mikutano na kutayarisha orodha ya shughuli za Baraza la Mawaziri;
(b) kuandika na kuweka kumbukumbu za mikutano;
(c) kutoa taarifa na maelezo ya uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa kila mtu au chombo cha umma kinachohusika na uamuzi uliotolewa; na
(d) kutekeleza kazi na shughuli nyingine zozote ambazo Rais ameagiza.
(4) Akiwa Mkuu wa Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi atakuwa na mamlaka ya kutoa maelekezo ya mara kwa mara kuhusiana na masuala ya utumishi wa umma.
(5) Katika nafasi ya madaraka ya Katibu wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa, Katibu Mkuu Kiongozi atakuwa Mkuu na Mratibu wa Sekretarieti ya Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa.
(6) Katibu Mkuu Kiongozi hatashika madaraka yake hadi awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha utii na uaminifu au kiapo kingine chochote kinachohusu utendaji wa kazi zake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

106.-(1) Kutakuwa na Makatibu Wakuu watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi katika utumishi wa umma kama watakavyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma.
(2) Kila Katibu Mkuu atakuwa kiongozi na Mtendaji Mkuu wa Wizara ya Serikali aliyopangiwa na Rais na atashika nafasi ya madaraka ya Katibu Mkuu na kutekeleza majukumu yake kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.
(3) Rais anaweza, kwa mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma, kumteua mtumishi mwandamizi katika Utumishi wa Umma kuwa Naibu Katibu Mkuu.
(4) Kila Katibu Mkuu atakuwa mshauri wa mwisho kwa Waziri kwa masuala yote ya utendaji na atatoa ushauri kwa Baraza la Mawaziri katika vikao na Kamati zitakazoitishwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri.
 

- 42 -
 


(5) Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu hatashika madaraka yake hadi awe ameapa mbele ya Rais kiapo cha utii na uaminifu au kiapo kingine chochote kinachohusu utendaji wa kazi zake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.


(d) Utekelezaji wa Shughuli za Baraza la Mawaziri


 

Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu.





Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.
 
107. Kutakuwa na Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu itakayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi ambayo itakuwa na majukumu ya kuchambua na kulishauri Baraza la Mawaziri juu ya masuala mbalimbali kabla ya kuwasilishwa na kufanyiwa uamuzi na Baraza hilo na itatekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa na Baraza la Mawaziri.


108.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri ambayo itakuwa na jukumu la kuhudumia Baraza la Mawaziri, Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu na kutekeleza majukumu mengine kama itakavyopangiwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri.
(2) Bunge linaweza kutunga sheria kuhusu utaratibu na utekelezaji wa shughuli za Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.
 


SURA YA NANE UHUSIANO NA URATIBU WA SERIKALI


 

Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali.














Malengo ya Tume.
 
109.-(1) Kutakuwa na Tume ya kusimamia na kuratibu mahusiano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika na kusimamia na kuratibu uhusiano baina ya Serikali za Nchi Washirika, ambayo itajulikana kwa kifupi kama "Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali".
(2) Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mwenyekiti;
(b) Rais wa Tanganyika; (c) Rais wa Zanzibar; (d) Mawaziri Wakaazi;
(e) Waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.


110. Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakuwa na malengo yafuatayo:
(a) kuweka utaratibu bora na endelevu wa kushauriana na kushirikiana baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika;
(b) kukuza na kuwezesha uratibu na ushirikiano miongoni mwa Nchi Washirika kuhusu mambo yasiyo ya Muungano kwa lengo la kuwezesha kufanana kwa kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wote;
 



- 43 -
 


(c) kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika kujadili utekelezaji wa mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano kwa manufaa na ustawi wa wananchi wote; na
(d) kuweka mazingira mazuri ya utatuzi wa migogoro baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Nchi Washirika au baina ya Nchi Washirika.


 

Majukumu ya Tume.






































Sekretarieti ya Tume.
 
111.-(1) Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakuwa na jukumu maalum la kuwezesha uratibu na ushirikiano katika kutekeleza masharti ya Katiba hii, sera, sheria, mipango na mikakati baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika na baina ya Serikali za Nchi Washirika na pia itakuwa chombo maalum kwa ajili ya:
(a) kushauriana na kushirikiana baina ya -
(i) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika; na
(ii) Serikali za Nchi Washirika zenyewe katika masuala yasiyo ya Muungano;
(b) kusimamia, kuratibu na kuhakikisha kwamba kuna kuwiana kwa sera na sheria za Nchi Washirika katika mambo yasiyo ya Muungano;
(c) kushauriana na kushirikiana baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na taasisi za kimataifa kwa niaba ya Nchi Washirika;
(d) usimamizi na ukuzaji wa masuala yenye maslahi kwa Taifa; (e) usuluhishi na utatuzi wa migogoro baina ya -
(i) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika; na
(ii) Serikali za Nchi Washirika katika mambo yasiyo ya Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1)(e), endapo upande wowote katika mgogoro hautaridhika na uamuzi wa Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali, unaweza kulipeleka suala hilo katika Mahakama ya Juu na uamuzi wa Mahakama hiyo utakuwa ni wa mwisho.
(3) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya -
(a) kusimamia uhusiano na uratibu baina ya Serikali za Nchi Washirika na kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika; na
(b) kuweka utaratibu wa utatuzi wa migogoro kwa mujibu wa Ibara hii.


112.-(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakayoongozwa na Katibu akisaidiwa na Naibu Katibu ambao watateuliwa na Rais.
(2) Mtu atateuliwa kuwa Katibu au Naibu Katibu ikiwa ana sifa zifuatazo:
(a) ni mtumishi mwandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika;
 


- 44 -
 


(b) ana shahada kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(c) ana mwenendo usiotiliwa shaka na jamii.
(3) Katibu na Naibu Katibu watawajibika kwa Tume na watafanya kazi na kutekeleza majukumu ya Sekretarieti.
(4) Uteuzi wa Katibu na Naibu Katibu wa Tume utafanywa kwa kuzingatia msingi kwamba endapo Katibu atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Naibu Katibu atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.


SURA YA TISA
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO


SEHEMU YA KWANZA
KUUNDWA NA MADARAKA YA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO


 

Kuundwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.













Muda wa Bunge.








Madaraka ya Bunge.
 
113.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano. (2) Wajumbe wa Bunge watakuwa wa aina zifuatazo:
(a) Wabunge sabini wa kuchaguliwa kupitia majimbo ya uchaguzi yatakayotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi, hamsini kutoka Tanganyika na ishirini kutoka Zanzibar; na
(b) Wabunge watano wenye ulemavu watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwakilishi wa Nchi Washirika na jinsi.
(3) Katika kila Jimbo la Uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme.
(4) Wabunge kutoka kila Jimbo la Uchaguzi watapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria inayoweka utaratibu kuhusu mambo ya uchaguzi.


114.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), maneno "maisha ya Bunge" maana yake ni muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge Jipya litaitishwa ili kukutana kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa wabunge na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha uchaguzi mwingine kufanyika.


115.-(1) Bunge ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano chenye madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Bunge litakuwa na madaraka yafuatayo:
(a) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kutungiwa sheria;
(b) kujadili na kutoa ushauri katika mambo yote yenye maslahi kwa taifa na umma wa Watanzania;
 


- 45 -
 


 






















Mipaka ya Bunge katika kutumia madaraka yake.









Madaraka ya
Bunge kutunga sheria.
 
(c) kumuuliza Waziri yeyote suala lolote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
(d) kujadili mgawanyo na kuidhinisha matumizi ya fedha kwa Wizara, taasisi na mashirika ya Serikali;
(e) kujadili utekelezaji wa majukumu ya kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(f) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu, muda wa kati au muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali katika Jamhuri ya Muungano;
(g) kujadili na kuridhia mikataba ya kimataifa inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa; na
(h) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusisha rasilimali zinazosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Bunge litaisimamia Serikali kwa kuangalia mwenendo wa utendaji wa Rais, Makamu wa Rais, Mawaziri na watendaji wakuu katika utumishi wa umma.

116.-(1) Katika kutekeleza madaraka ya kuisimamia Serikali kwa mujibu wa Katiba hii, wajibu wa Bunge utakuwa ni kuishauri Serikali na endapo Bunge halitaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika utekelezaji wa suala lililotolewa ushauri, basi Bunge litakuwa na haki ya kuiwajibisha Serikali kwa mujibu wa madaraka lililopewa katika Katiba hii.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Bunge halitachukua hatua yoyote ya kiutendaji ambayo, kwa desturi ni shughuli za Serikali, na halitatoa maagizo yoyote ya kiutendaji kwa Serikali na watumishi wa umma, isipokuwa kwamba, Bunge litashauri kuhusu suala lolote lililo katika dhamana ya Waziri anayehusika.

117.-(1) Madaraka ya kutunga sheria kwa mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(2) Madaraka ya kutunga sheria katika Tanganyika kwa mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge la Tanganyika na madaraka ya kutunga sheria katika Zanzibar kwa mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
(3) Endapo sheria iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge la Tanganyika au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili na itatenguka.
(4) Endapo sheria iliyotungwa na Bunge la Tanganyika au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, sheria hiyo itakuwa batili na itatenguka.
(5) Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri ya Muungano kwa mambo yanayohusu Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, basi sheria hiyo nyingine, kwa kiasi kinachokiuka Katiba hii, itakuwa batili.
 

- 46 -
 


 

Utaratibu wa kubadilisha Katiba.










Utaratibu wa kubadili-sha masharti mahsusi.













Utaratibu wa kutunga sheria.



















Utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha.
 
118.-(1) Bunge linaweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii.
(2) Muswada wa sheria wa kubadili Katiba utahesabiwa kuwa umepitishwa na Bunge iwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanganyika na wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Zanzibar.
(3) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (1) kubadilisha masharti ya Katiba hii maana yake ni pamoja na kurekebisha au kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti mengine badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya masharti hayo.

119. Bunge halitaweza kufanya mabadiliko ya Katiba kuhusu:
(a) masharti yaliyomo katika Sura ya Kwanza, Sura ya Pili na Sura ya Nne;
(b) masharti ya Ibara ya 60; (c) masharti ya Ibara ya 79;
(d) kuongeza au kupunguza jambo lolote la Muungano; (e) uwepo wa Jamhuri ya Muungano;
(f) masharti ya Ibara hii,
hadi kwanza mabadiliko hayo yaungwe mkono na theluthi mbili ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano kwa Kura ya Maoni itakayoendeshwa na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa sheria za nchi.

120.-(1) Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ambao utawekwa saini na Rais.
(2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (3), Muswada wa Sheria unaweza kuandikwa na Serikali, Kamati ya Bunge au kikundi cha Wabunge.
(3) Wakati wa kuandaa Muswada wa Sheria kuhusu jambo lolote la Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kwamba inawashirikisha wananchi kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo juu ya muswada huo.
(4) Muswada wa sheria utahesabiwa kuwa umepitishwa na Bunge iwapo utaungwa mkono kwa kura za wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanganyika na wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Zanzibar.
(5) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (4), Bunge litatunga Kanuni za Kudumu zitakazoweka utaratibu wa -
(a) kuwasilisha, kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria; na (b) utekelezaji bora wa masharti ya ibara ndogo ya (3).

121.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo yanayohusika na Ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Rais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri.
 


- 47 -
 


(2) Mambo yanayohusika na Ibara hii ni yafuatayo:
(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya jambo lolote kati ya mambo yafuatayo:
(i) kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza;
(ii) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina au mfuko mwingine wowote wa Serikali au kubadilisha kiwango hicho na namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza;
(b) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina au mfuko mwingine wowote wa Serikali wakati ikifahamika kwamba fedha iliyomo katika mifuko hiyo haikupangiwa itolewe kwa ajili ya malipo au matumizi hayo, au kuagiza kwamba malipo au matumizi yanayofanywa kutokana na mifuko hiyo yaongezwe;
(c) kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwa lilipwe kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au
(d) hoja au mabadiliko yoyote ya hoja kwa ajili ya lolote kati ya mambo yaliyoelezwa katika aya ya (a) ya Ibara hii ndogo.


 

Madaraka ya Mkuu wa Nchi kuhusu Muswada wa Sheria.
 
122.-(1) Muswada wa Sheria uliopitishwa na Bunge sharti kupata saini ya Rais, ili kuthibitisha kukubaliwa kwake na Rais.
(2) Muswada wa Sheria uliyowasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali utawekewa saini na Rais ndani ya siku zisizozidi thelathini kutoka siku ambayo Muswada huo uliwasilishwa na kupokelewa na Katibu wa Baraza la Mawaziri.
(3) Baada ya Muswada wa Sheria kuwasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake, Rais anaweza kukubali au kukataa Muswada huo, na iwapo Rais atakataa kuukubali Muswada huo basi ataurudisha Bungeni pamoja na maelezo ya sababu za kukataa Muswada huo.
(4) Baada ya Muswada wa Sheria kurudishwa Bungeni na Rais kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii, Muswada huo hautapelekwa tena kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake kabla ya kumalizika muda wa siku sitini tangu uliporudishwa Bungeni.
(5) Endapo katika kujadiliwa tena Bungeni kabla haujapelekwa tena kwa Rais, Muswada uliorudishwa Bungeni na Rais umeungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote, basi Muswada huo unaweza kuwasilishwa mapema zaidi kwa Rais.
(6) Iwapo Muswada uliorudishwa Bungeni na Rais na katika kuujadili ukaungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote na kupelekwa tena kwa Rais kwa ajili ya kupata kibali chake, basi Rais atatakiwa kuukubali Muswada husika kabla ya kumalizika muda wa siku sitini, na endapo siku sitini zitapita tangu Muswada huo ulipopelekwa tena kwa Rais pasipo Rais kuukubali, basi Katibu wa Bunge ataandika Hati kuthibitisha kuwa Muswada huo umekuwa sheria.
 





- 48 -
 


 

Kupitishwa kwa hoja za Serikali.
 
123.-(1) Endapo Bunge halitaridhishwa na mchanganuo au mgawanyo wa hoja ya Bajeti ya Serikali, Bunge linaweza kurudisha hoja ya Bajeti ya Serikali pamoja na mapendekezo mahsusi kuhusiana na upungufu uliobainika.
(2) Serikali itawajibika kuyafanyia kazi mapendekezo ya Bunge kwa kadri itakavyowezekana na kisha kuwasilisha tena Bungeni hoja husika pamoja na maelezo ya utekelezaji wa maelekezo ya Bunge na endapo Bunge litakataa kwa mara ya pili hoja kuhusu Bajeti ya Serikali, basi hoja hiyo itahesabika kuwa imepitishwa na Bunge.
 


SEHEMU YA PILI

WABUNGE

(a) Uchaguzi wa Wabunge


 

Uchaguzi wa Wabunge.



























Sifa za kuchagu-liwa kuwa Mbunge.
 
124.-(1) Kila baada ya Bunge kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka mitano, kutakuwa na uchaguzi wa Wabunge katika Majimbo ya uchaguzi kama itakavyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi utakaofanyika kwa mujibu wa sheria za nchi.
(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la uchaguzi ikiwa kiti cha Mbunge aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo la uchaguzi kwa utaratibu wa mgombea huru, kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na Bunge kumaliza muda wake.
(3) Endapo tarehe ya Bunge kumaliza muda wake imetangazwa au inafahamika, hakutakuwa na uchaguzi mdogo wa mbunge kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) ndani ya kipindi cha miezi kumi na minane kabla ya tarehe hiyo.
(4) Endapo Mbunge anayetokana na chama cha siasa atapoteza sifa za kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyokuwa ya Bunge kumaliza muda wake, Tume Huru ya Uchaguzi, kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na sheria za nchi kwa ajili hiyo, itamteua na kumtangaza kuwa Mbunge mtu mwingine kutoka kwenye orodha ya majina ya wagombea iliyowasilishwa na chama hicho kwa mujibu wa ibara ndogo ya (5).
(5) Orodha ya majina ya wagombea kutoka kila chama cha siasa iliyowasilishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu ndiyo itakayotumiwa na Tume Huru ya Uchaguzi baada ya kushauriana na chama cha siasa kinachohusika, kwa madhumuni ya kujaza nafasi ya Mbunge inapotokea kuwa wazi, wakati wowote wa Maisha ya Bunge.


125.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika Ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo:
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja wakati wa kugombea;
(b) anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au Kiingereza na ana elimu isiyopungua kidato cha nne;
(c) ni mwanachama aliyependekezwa na chama cha siasa au mgombea huru;
 


- 49 -
 


(d) ni mwadilifu na anayeheshimu haki za binadamu na asiyedharau wala kubagua watu kwa misingi ya kabila, dini, jinsi, maumbile au hali zao katika jamii; na
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea kuchaguliwa kuwa Mbunge ikiwa -
(a) mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka mitano; au
(b) imethibitishwa rasmi kwamba mtu huyo ana ugonjwa wa akili; (c) mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa
gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kosa lolote;
(d) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na kukosa uaminifu au kwa kuvunja sheria inayohusiana na Maadili ya Uongozi;
(e) mtu huyo ana maslahi yoyote katika mkataba wa Serikali wa aina yoyote aliyowekewa miiko maalum kwa mujibu wa sheria za nchi, na iwapo amekiuka miiko hiyo; au
(f) mtu huyo anashika madaraka ya ofisa mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Nchi Washirika;
(g) kwa mujibu wa sheria ya nchi inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguzi wa aina yoyote, mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha kama mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi wa Wabunge; au
(h) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi amewahi kutiwa hatiani katika mahakama kwa kosa la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali au makosa yanayohusu kukosa uaminifu.
(3) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti yatakayomzuia mtu asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha Jimbo la Uchaguzi ikiwa mtu huyo ni mwenye madaraka yanayohusika na shughuli za kuongoza au kusimamia uchaguzi wa Wabunge au shughuli za uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge.
(4) Katika aya ya (e) ya ibara ndogo ya (2) ya Ibara hii "mkataba wa Serikali" maana yake ni mapatano yoyote ya mkataba ambayo mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Serikali ya Tanganyika, Idara au Taasisi yoyote ya Serikali yoyote kati ya hizo au mtumishi yeyote wa Serikali aliyeshiriki katika majadiliano ya mkataba husika kwa niaba ya Serikali yoyote miongoni mwa hizo.
(5) Watu wenye nyadhifa zifuatazo katika Utumishi wa Umma hawatakuwa na sifa ya kuwa Wabunge:
(a) Rais na Makamu wa Rais;
(b) Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar na Makamu wao;
(c) Spika na Naibu Spika wa Bunge; (d) Waziri na Naibu Waziri;
(e) Mwanasheria Mkuu wa Serikali;



- 50 -
 


(f) Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu;
(g) Viongozi na watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; (h) mtu ambaye ameajiriwa katika vyombo vya dola kama
askari;
(i) Jaji Mkuu, Jaji au Hakimu wa Mahakama, Wakili wa Serikali na Ofisa Sheria Katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Washirika;
(j) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; (k) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi; na
(l) mtu yeyote aliyeajiriwa, kuteuliwa au kuchaguliwa katika utumishi wa umma.
(6) Kwa madhumuni ya kutoa fursa ya kukata rufani kwa mtu yeyote:
(a) aliyethibitishwa rasmi kisheria kuwa ana ugonjwa wa akili; (b) aliyehukumiwa na kupewa adhabu ya kifo au kifungo; au
(c) aliyepatikana na hatia ya kosa lolote lililotajwa katika sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2),
mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria kwa ajili ya kuweka masharti kwamba hukumu inayopingwa haitakuwa na nguvu kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya ibara ndogo ya (2) hadi upite muda uliotajwa katika sheria hiyo.

 

Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge.





Kiapo na masharti ya kazi ya Ubunge.








Kupoteza sifa za Ubunge.
 
126.-(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi watachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na sheria za nchi kwa mujibu wa Katiba hii, inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabunge.
(2) Wagombea uchaguzi katika majimbo ya Uchaguzi watatakiwa kuwasilisha majina yao kwa Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na sheria za nchi.


127.-(1) Kila Mbunge ataapishwa kiapo cha uaminifu na Spika katika Bunge kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge, lakini Mbunge anaweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa.
(2) Mbunge atashika madaraka kwa mujibu wa Katiba hii, na atalipwa mshahara, posho na malipo mengine kama yatakavyopangwa na Tume ya Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria za nchi.
(3) Wakati wowote wa madaraka yake, Mbunge atawajibika moja kwa moja kwa wapiga kura wake.

128.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge ikiwa litatokea lolote kati ya mambo yafuatayo:
(a) tukio lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe au apoteze sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(b) atakosa kuhudhuria Mikutano ya Bunge miwili mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;
(c) itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
 


- 51 -
 


(d) atashindwa kufanya kazi za Mbunge kwa muda wa miezi sita mfululizo kutokana na maradhi au kizuizi ndani ya gereza;
(e) atashindwa kutoa tamko rasmi kuhusu sifa za kuwa Mbunge au taarifa rasmi kuhusu mali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii katika muda uliowekwa mahsusi na sheria za nchi;
(f) atajiuzulu ubunge;
(g) kwa ridhaa yake atajiondoa au kujivua uanachama wa chama chake cha siasa, atafukuzwa au kuvuliwa uanachama na chama chake cha siasa;
(h) ataondolewa madarakani kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(i) kufariki dunia.
(2) Mbunge anaweza kukata rufani mahakamani kupinga hukumu ya kuthibitishwa kwake kuwa ana maradhi au kupinga adhabu ya kufungwa gerezani, au kupinga kupatikana kwake na hatia kwa kosa la aina iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1).


 

Haki ya wapiga kura kumwaji-bisha Mbunge.













Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge.
 
129.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, wananchi watakuwa na haki ya kumuondoa Mbunge wao madarakani, endapo Mbunge atafanya moja wapo au zaidi ya mambo yafuatayo:
(a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya wapiga kura au kinyume na maslahi ya Taifa;
(b) kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapiga kura wake;
(c) kuacha kuishi au kuhamisha makaazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi; au
(d) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya nchi. (2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya kuendesha
uchunguzi kwa Mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapiga kura wake na utaratibu wa kumuondoa katika Ubunge.


130.-(1) Kila shauri kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala -(a) kama uchaguzi wa Mbunge ulikuwa halali au sivyo; au
(b) kama Mbunge amekoma kuwa Mbunge na nafasi ya madaraka ya Ubunge iko wazi au hapana,
litafunguliwa na kusikilizwa kwanza katika Mahakama Kuu.

(2) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo:
(a) watu wanaoweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu kwa ajili ya kupata uamuzi juu ya suala lolote kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii;
(b) sababu na nyakati za kufungua shauri la namna hiyo, utaratibu wa kufungua shauri na masharti yanayotakiwa yatimizwe kwa kila shauri kama hilo; na
(c) kutaja mamlaka ya Mahakama Kuu juu ya shauri kama hilo na
kueleza utaratibu wa kusikiliza shauri lenyewe.
 




- 52 -
 


 

Tamko rasmi la Wabunge kuhusu Maadili ya Uongozi.
 
131.-(1) Kila Mbunge kabla ya kumalizika siku thelathini tangu aapishwe kushika nafasi ya madaraka ya Mbunge sharti awasilishe kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji nakala mbili za tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za kuwa mbunge kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(2) Tamko rasmi lililotajwa katika ibara ndogo ya (1), litatolewa katika fomu maalum itakayoandaliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
 


SEHEMU YA TATU UONGOZI WA BUNGE

(a) Spika na Naibu Spika


 

Spika na mamlaka ya Spika.













Ukomo wa Spika.
 
132.-(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge na atakuwa ndiye Kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.
(2) Waziri, Naibu Waziri, Mbunge au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na sheria za nchi kwa madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.
(3) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika atatakiwa, kabla ya kumaliza siku thelathini tangu kuchaguliwa kwake, kuwasilisha kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, tamko hilo litatolewa katika fomu maalum itakayoandaliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

133.-(1) Spika atakoma kushika nafasi ya madaraka ya Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:
(a) atachaguliwa kuwa Mbunge;
(b) kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika, lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa Spika;
(c) ataondolewa kwenye madaraka ya Spika kwa Azimio la Bunge lililoungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote;
(d) atashindwa kuwasilisha tamko rasmi kuhusiana na mali na madeni yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(e) atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa habari za uongo, kwa kiapo kinyume cha sheria kuhusu tamko rasmi lolote lililotolewa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(f) atashindwa kuwasilisha taarifa ya mali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa kwa ajili hiyo;
(g) itathibitika kuwa amevunja masharti ya sheria inayohusu maadili ya uongozi wa umma; au
(h) kufariki dunia.
(2) Isipokuwa shughuli ya kumchagua Spika, hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge wakati wowote ambao nafasi ya madaraka ya Spika itakuwa wazi.
 


- 53 -
 


 

Naibu Spika.


















Sifa za mtu kuchagu-liwa kuwa Spika au Naibu Spika.















Utaratibu wa Uchaguzi na kiapo cha Spika na Naibu Spika.
 
134.-(1) Kutakuwa na Naibu Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge.
(2) Waziri, Naibu Waziri, Mbunge au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na sheria za nchi kwa madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Naibu Spika.
(3) Wabunge watamchagua Naibu Spika nyakati zifuatazo:
(a) Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu au mapema iwezekanavyo baada ya wakati huo; na
(b) katika kikao cha kwanza cha Bunge baada ya nafasi ya madaraka ya Naibu Spika, kuwa wazi kwa sababu yoyote isiyohusika na Bunge kuvunjwa au mapema iwezekanavyo baada ya kikao hicho.
(4) Naibu Spika atakoma kushika nafasi ya madaraka ya Naibu Spika litokeapo lolote kati ya mambo yaliyoainishwa katika Ibara ya 133(1).


135.(1) Mtu atastahili kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika endapo atakuwa na sifa zifuatazo -
(a) angalau awe na elimu ya shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi;
(b) wakati wa kugombea, awe mwenye umri usiopungua miaka arobaini;
(c) bila ya kuathiri masharti ya aya ya (a) na (b), awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mbunge; na
(d) asiwe kiongozi au amewahi kuwa kiongozi wa juu wa chama cha siasa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya kuomba kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Spika au Naibu Spika.
(2) Kwa madhumuni ya aya ya (d), kiongozi wa juu wa chama cha siasa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu au Mjumbe wa chombo chochote cha kitaifa chenye mamlaka katika chama cha siasa.


136.-(1) Kutakuwa na uchaguzi wa Spika katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya, na katika kikao cha kwanza chochote mara baada ya kutokea nafasi ya madaraka ya Spika kuwa wazi.
(2) Kutakuwa na uchaguzi wa Naibu Spika wakati wowote katika Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya na vile vile katika kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofuata mara baada ya kutokea nafasi ya madaraka ya Naibu Spika kuwa wazi.
(3) Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika, utafanywa kwa kura ya siri, na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.
(4) Spika na Naibu Spika watachaguliwa kwa misingi kwamba, endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Naibu Spika atatoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
 




- 54 -
 


(5) Isipokuwa kama ataacha madaraka yake, Spika na Naibu Spika watakaa madarakani kwa vipindi visivyozidi viwili vya miaka mitano.
(6) Mtu yeyote atakayechaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake, kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu.


(a) Ofisi ya Bunge


 

Katibu wa Bunge.








Sekretarieti ya Bunge.
 
137.-(1) Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa majina matatu ya watu wenye madaraka ya juu katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma.
(2) Katibu wa Bunge atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Bunge na atawajibika kwa utendaji bora wa shughuli za Bunge kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na sheria za nchi.


138.(1) Kutakuwa na Sekretarieti ya Bunge itakayokuwa na watumishi kutoka pande zote za Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ngazi za utumishi kwa mujibu wa mahitaji ya shughuli za Bunge kama itakavyoamuliwa na Tume ya Utumishi ya Bunge.
(2) Sekretarieti ya Bunge chini ya uongozi wa Katibu wa Bunge, itatekeleza kazi na shughuli zote zilizowekwa au zitakazokuwa ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji bora wa shughuli za Bunge, Wabunge na madaraka ya Bunge.
 


SEHEMU YA NNE

UTARATIBU WA SHUGHULI ZA BUNGE


 

Kanuni za Kudumu za Bunge.








Rais kulihutubia Bunge.





Mikutano ya Bunge.
 
139.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Bunge linaweza kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.
(2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa Ibara hii, zinaweza kuweka utaratibu wa Mawaziri kuiwakilisha Serikali ndani ya Bunge, kusimamia utekelezaji wa shughuli za Sekretarieti ya Bunge, utekelezaji wa Shughuli za Bunge ndani ya Bunge, Kamati na Kamati Ndogo za Bunge.


140.-(1) Rais atalihutubia Bunge Jipya katika Mkutano wa Kwanza na kulifungua rasmi.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), Rais anaweza wakati wowote kulihutubia Bunge au kupeleka kwenye Bunge taarifa ambayo itasomwa na Waziri Mwandamizi.


141.-(1) Bunge litafanya mikutano yake mahali ambapo ni desturi kufanya Mikutano hiyo au mahali pengine popote katika Jamhuri ya Muungano patakapotajwa na Spika kwa ajili hiyo.
 



- 55 -
 


(2) Mkutano wa Kwanza wa Bunge Jipya katika Maisha ya Bunge utaitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano na utaanza siku ile ambayo Bunge limeagizwa kukutana, na kila Mkutano unaofuata utaanza siku yoyote itakayopangwa na Bunge au siku yoyote itakayopangwa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.
(3) Rais anaweza kuitisha Mkutano wa Bunge wakati wowote kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.


 

Uongozi na vikao vya Bunge.






Akidi ya vikao vya Bunge.






Kamati za Bunge.
 
142. Kila kikao cha Bunge kitaongozwa na mmoja wapo wa watu wafuatao:
(a) Spika;
(b) ikiwa Spika hayupo, Naibu Spika; au
(c) ikiwa Spika na Naibu Spika wote hawapo, Mbunge yeyote aliyechaguliwa na Bunge kwa ajili hiyo.


143.-(1) Akidi ya kila kikao cha Bunge ni nusu ya Wabunge wote, isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo katika Katiba hii.
(2) Kila suala litakalowasilishwa kwa ajili ya kupata uamuzi wa Bunge litaamuliwa kwa kufuata wingi wa kura za Wabunge waliohudhuria na kupiga kura, isipokuwa kwa masuala yaliyowekewa masharti mahsusi chini ya Katiba hii.


144.-(1) Bunge linaweza kuunda Kamati za Bunge za aina mbalimbali kadri litakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa madaraka yake.
(2) Kanuni za Bunge zinaweza kufafanua muundo na shughuli za Kamati za Bunge zitakazoundwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii.
 


SEHEMU YA TANO MADARAKA NA HAKI ZA BUNGE


 

Uhuru wa majadiliano Bungeni.















Mipaka ya majadiliano Bungeni.
 
145.-(1) Wabunge wakiwa Bungeni, watakuwa na uhuru wa kutoa mawazo, maoni na majadiliano na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali pengine nje ya Bunge.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote, Bunge litakuwa na uhuru wa maoni na Mbunge yeyote akiwa Bungeni kwa vyovyote itakavyokuwa, hatatakiwa kutoa kauli za uongo, kuudhi au kumuumiza Mbunge au mtu mwingine yeyote katika jamii.
(3) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), Mbunge yeyote hatashtakiwa kwa kosa la jinai au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema ndani ya Bunge.
(4) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuwezesha mahakama na sheria kuhifadhi na kutilia nguvu uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu wa shughuli katika Bunge.


146.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku kusema uongo Bungeni na kwa sababu hiyo, Mbunge anapozungumza
 


- 56 -
 


ndani ya Bunge ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha.
(2) Mbunge anapokuwa akizungumza Bungeni hatahesabika wala kutafsiriwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo lililotangazwa au lililoandikwa na vyombo vya habari au nyaraka nyingine yoyote ambayo chanzo chake kinafahamika au kitaelezwa na Mbunge huyo.

SEHEMU YA SITA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE

(a) Tume ya Utumishi wa Bunge

 

Tume ya Utumishi wa Bunge.
















Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Bunge.
 
147.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Bunge ambayo itakuwa na Wajumbe wafuatao:
(a) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mwenyekiti;
(b) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti;
(c) Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, mmoja kutoka kila upande wa Jamhuri ya Muungano;
(d) Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni; na (e) Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
(2) Katibu wa Bunge atakuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Bunge.
(3) Tume inaweza kumualika mtu mwingine yeyote mwenye utaalam mahsusi kushiriki kikao chochote cha Tume, isipokuwa mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura.

148.-(1) Tume ya Utumishi wa Bunge itakuwa na wajibu wa kuendeleza, kuwezesha na kuhakikisha utekelezaji wa kazi na shughuli za Bunge, kwa ufanisi na uwazi.
(2) Tume ya Utumishi wa Bunge itatekeleza majukumu yafuatayo:
(a) kuajiri, kuthibitisha kazini, kupandisha vyeo na kusimamia nidhamu za watumishi wa Bunge na kupokea malalamiko dhidi yao kwa mujibu wa sheria za nchi;
(b) kuandaa na kutekeleza mipango ya kujiendeleza kielimu kwa Watumishi wa Bunge;
(c) kuandaa na kupendekeza viwango vya mishahara, posho na marupurupu mengine kwa Wabunge na Watumishi wa Bunge kwa chombo chenye jukumu la kusimamia maslahi ya Watumishi wa Umma;
(d) kupendekeza Serikalini maboresho ya Taasisi ya Bunge ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya kikatiba ya Bunge;
(e) kutekeleza majukumu yoyote yatakayowekwa kwa mujibu wa Katiba hii au sheria nyingine.
(3) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Bunge.
 

- 57 -
 



(b) Mfuko wa Bunge


 

Mfuko wa Bunge.
 
149.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambao utakuwa chini ya usimamizi wa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(2) Mfuko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano utatumika kwa ajili ya kugharamia shughuli za uendeshaji, pamoja na shughuli nyingine muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(3) Serikali itahakikisha kwamba, katika kila bajeti ya mwaka wa fedha wa Serikali, inatenga kwa kiwango kinachotosha, fedha ambazo zitaingizwa katika Mfuko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu uendeshaji wa Mfuko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
 


SURA YA KUMI
MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO


SEHEMU YA KWANZA
MISINGI YA UTOAJI HAKI NA UHURU WA MAHAKAMA


 
Kuanzishwa kwa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.




Misingi ya utoaji haki.














Uhuru wa Mahakama.
 
150.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano kupitia Katiba hii, itakuwa na mamlaka kutoka kwa wananchi na itatekeleza mamlaka yake kupitia Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani.

(3) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano itakuwa ni chombo chenye mamlaka ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano.


151. Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria, Mahakama ya Jamhuri ya Muungano itafuata kanuni zifuatazo, yaani:
(a) kutenda haki kwa wote bila kujali hali ya mtu kijamii, kisiasa, kiutamaduni au kiuchumi;
(b) kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;
(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria za nchi zilizotungwa mahususi kwa ajili hiyo;
(d) kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro; na
(e) kutenda haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi.


152.-(1) Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, Mahakama ya Jamhuri ya Muungano itaongozwa na masharti ya Katiba hii na haitaingiliwa ama kwa kudhibitiwa, kushinikizwa au kupewa maelekezo na mtu au chombo chochote.
(2) Nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu au Mahakama ya Rufani haitafutwa wakati wowote ule ikiwa kuna mtu ambaye kwa wakati huo anashikilia nafasi hiyo.
 


- 58 -
 


(3) Mishahara na malipo mengine ya Majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani yatalipwa kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina.
(4) Mshahara na malipo mengine yanayolipwa kwa Jaji wa Mahakama ya Juu au wa Mahakama ya Rufani hayatabadilishwa kwa maana ya kumuondolea faida Jaji husika.
(5) Malipo ya mafao ya kustaafu ya Jaji wa Mahakama ya Juu au Jaji wa Mahakama ya Rufani hayatabadilishwa kwa maana ya kumuondolea faida Jaji husika wakati wote wa uhai wake.
(6) Jaji wa Mahakama ya Juu au Jaji wa Mahakama ya Rufani hatoshtakiwa kwa jambo lolote alilolifanya au kutolifanya kwa nia njema katika utekelezaji wa shughuli ya utoaji haki kwa mujibu wa sheria za nchi.


SEHEMU YA PILI MUUNDO WA MAHAKAMA

(a) Mahakama za Jamhuri ya Muungano


 

Muundo wa Mahakama.
 
153.-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote yaliyotangulia katika Sehemu hii, kutakuwa na Muundo wa Mahakama katika Jamhuri ya Muungano utakaokuwa kama ifuatavyo:
(a) Mahakama ya Juu; na (b) Mahakama ya Rufani.
(2) Mahakama Kuu ya Tanganyika na Mahakama Kuu ya Zanzibar zitakuwa na mamlaka sawa ya kusikiliza katika ngazi ya awali, mashauri ya madai na jinai kuhusu Mambo ya Muungano katika maeneo ya utawala ya Nchi Washirika.
 


(b) Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano


 

Mahakama ya Juu.












Akidi ya vikao vya Mahakama ya Juu.
 
154.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano au kwa kifupi itaitwa "Mahakama ya Juu" ambayo itakuwa na:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Rais wa Mahakama ya Juu;
(b) Naibu Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Makamu wa Rais wa Mahakama ya Juu; na
(c) Majaji wengine wa Mahakama ya Juu wasiopungua saba.
(2) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu utazingatia sifa zitakazoainishwa katika Katiba hii na uwakilishi wa sehemu mbili za Jamhuri ya Muungano.


155.-(1) Akidi ya kikao cha Mahakama ya Juu itakuwa ni Majaji wa Mahakama ya Juu watano.
(2) Akidi ya Majaji katika vikao vya Mahakama ya Juu kwa madhumuni ya kusikiliza shauri linalohusu masuala yaliyoainishwa katika Ibara ya 156(1) (a), (b), (c) na (e) itazingatia uwakilishi wa sehemu mbili za Jamhuri ya Muungano.
 



- 59 -
 


(3) Kila shauri na rufani inayohitaji uamuzi wa Mahakama ya Juu itaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa Mahakama ya Juu waliosikiliza shauri au rufani hiyo.

 

Mamlaka ya Mahakama ya Juu.

























Madaraka ya Majaji wa Mahakama ya Juu.
 
156.-(1) Mahakama ya Juu itakuwa ni ngazi ya mwisho ya rufani katika Jamhuri ya Muungano na itakuwa na madaraka ya:
(a) pekee na ya awali ya kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) kusikiliza na kuamua mashauri yatakayowasilishwa na wananchi, Serikali au Serikali za Nchi Washirika kuhusu tafsiri au utekelezaji wa Katiba hii;
(c) kusikiliza na kuamua migogoro baina ya Nchi Washirika au baina ya Nchi Mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(d) kusikiliza na kuamua rufani kutoka Mahakama ya Rufani;
(e) kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika, pale itakapoombwa; na
(f) kusikiliza na kuamua shauri lolote litakalowasilishwa mbele yake kwa mujibu wa Katiba hii au sheria nyingine yoyote itakayoipa Mahakama hiyo mamlaka.
(2) Mahakama ya Rufani pamoja na mahakama za Nchi Washirika, isipokuwa Mahakama ya Juu, zitalazimika kufuata maamuzi ya Mahakama ya Juu.
(3) Mahakama ya Juu itaandaa Kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa mamlaka yake.
(4) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti zaidi kuhusu uendeshaji wa Mahakama ya Juu.

157.-(1) Jaji wa Mahakama ya Juu atakuwa na madaraka ya kusikiliza na kuamua shauri lolote katika Mahakama ya Juu.
(2) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), iwapo Jaji wa Mahakama ya Juu, kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu ya Nchi Washirika, Jaji huyo anaweza kuendelea kufanya kazi zake katika Mahakama aliyotoka hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu.
(3) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), itakuwa ni halali kwa Jaji wa Mahakama ya Juu kutoa hukumu au uamuzi mwingine wowote unaohusika kwa kutumia na kutaja nafasi ya madaraka aliyokuwa akishika kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu na endapo hukumu hiyo au uamuzi huo utapingwa kwa njia ya rufani itakayofikishwa mbele ya Mahakama ya Juu, Jaji huyo hatakuwa na madaraka ya kusikiliza rufani hiyo.
 

(c) Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu

 

Uteuzi wa Jaji Mkuu.
 
158.-(1) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.
 


- 60 -
 


(2) Jaji Mkuu ndiye atakuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama katika Jamhuri ya Muungano.
(3) Mtu ataweza kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka arobaini na tano au zaidi na mwenye sifa ya uadilifu, tabia njema, uaminifu na:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye sifa ya uadilifu, tabia njema na uaminifu;
(b) awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika Jamhuri ya Muungano; na
(c) awe:
(i) amefanya kazi ya ujaji katika Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu za Nchi Washirika; au
(ii) amefanya kazi ya utumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano au uanataaluma akiwa na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka ishirini.


 

Uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu.










Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Juu.















Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Juu.
 
159.-(1) Naibu Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.
(2) Mtu atateuliwa kuwa Naibu Jaji Mkuu endapo atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 158 na kwa kufuata msingi kwamba endapo Jaji Mkuu atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Naibu Jaji Mkuu atatoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Naibu Jaji Mkuu atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Jaji Mkuu katika utekelezaji wa majukumu yake.


160.-(1) Majaji wa Mahakama ya Juu watateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

(2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu endapo atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye tabia njema, uadilifu na uaminifu;
(b) awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika Jamhuri ya Muungano; na
(i) awe amefanya kazi ya ujaji katika Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu za Nchi Washirika; au
(ii) awe wakili, mtumishi wa umma au mwanataaluma akiwa na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.


161. Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu au Jaji wa Mahakama ya Juu atashika madaraka yake mara tu atakapokuwa ameapishwa na Rais kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
 



- 61 -
 


 

Muda wa kuwa madara-kani kwa Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Majaji wa Mahakama ya Juu.














Utaratibu wa kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu.
 
162.-(1) Jaji Mkuu atashika nafasi ya madaraka ya Jaji Mkuu hadi atakapofikisha umri wa miaka sabini, isipokuwa tu kama:
(a) atajiuzulu;
(b) atashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na maradhi; (c) kufariki dunia; au
(d) atavuliwa madaraka ya Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba hii. (2) Masharti ya ibara ndogo ya (1) yatatumika pia kwa Naibu Jaji
Mkuu na Jaji wa Mahakama ya Juu.
(3) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Jaji wa Mahakama ya Juu aliyetimiza umri wa kustaafu atalazimika kuendelea kufanya kazi baada ya kutimiza umri huo hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajatimiza umri wa kustaafu.
(4) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (3), Jaji Mkuu au Naibu Jaji Mkuu aliyetimiza umri wa kustaafu, ataachia nafasi ya madaraka yake, isipokuwa ataendelea kutekeleza shughuli ambazo hajazikamilisha akiwa katika nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu hadi atakapokamilisha shughuli hizo.

163.-(1) Iwapo itatokea kwamba -

(a) nafasi ya madaraka ya Jaji Mkuu itakuwa wazi;
(b) Jaji Mkuu hayupo katika Jamhuri ya Muungano; au
(c) Jaji Mkuu atashindwa kumudu kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote iliyoainishwa katika Katiba hii,
Naibu Jaji Mkuu atatekeleza kazi za Jaji Mkuu hadi atakapoteuliwa Jaji Mkuu mwingine au hadi Jaji Mkuu ambaye alikuwa hayupo au alikuwa hamudu kazi zake atakaporejea kazini.
(2) Ikitokea kwamba nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu itakuwa wazi au endapo Jaji wa Mahakama ya Juu yeyote ameteuliwa kutekeleza kazi za Naibu Jaji Mkuu au kama Jaji wa Mahakama ya Juu atashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, au Jaji Mkuu atamshauri Rais kuwa kazi za Mahakama ya Juu zilivyo kwa wakati huo zinahitaji ateuliwe Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu, basi Rais anaweza kumteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Juu watakaopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(3) Mtu atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu atafanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu kwa muda wote utakaotajwa kwenye hati ya kuteuliwa kwake.
(4) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), mtu aliyeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi amalize shughuli nyingine yoyote inayohusika na rufani au mashauri mengine ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya muda wake wa uteuzi haujamalizika au uteuzi wake haujafutwa.
(5) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Mahakama ya Juu na atatekeleza kazi zote za Jaji wa Mahakama ya Juu na kwamba idadi ya Majaji wa Mahakama ya Juu iliyotajwa katika Ibara ya 155
 


- 62 -
 


haitaathirika kwa sababu tu mmoja au zaidi ya Majaji wa Mahakama ya Juu katika kikao chochote ni Kaimu Jaji wa Mahakama ya Juu.


 

Utaratibu wa kushu-ghulikia nidhamu ya Majaji wa Mahakama ya Juu.
 
164.-(1) Jaji wa Mahakama ya Juu ataondolewa katika nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu kwa sababu ya kushindwa kutekeleza madaraka yake ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya inayoathiri maadili ya kazi ya Jaji au sheria inayohusu maadili ya uongozi wa umma, na hataondolewa madarakani isipokuwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2).
(2) Endapo Rais anaona kuwa suala la kumuondoa Jaji madarakani linahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:
(a) Rais anaweza, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kumsimamisha kazi Jaji huyo;
(b) Rais atateua Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili na angalau nusu ya wajumbe hao wawe ni Majaji wa Mahakama ya Juu au Mahakama ya Rufani kutoka nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola; na
(c) Tume hiyo itachunguza shauri lote kisha itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri hilo na itamshauri Rais kama Jaji huyo anayehusika aondolewe madarakani kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii kwa sababu ya kushindwa kufanyakazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.
(3) Jaji aliyesimamishwa kazi kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2), ataendelea kulipwa mshahara na maslahi yake mengine hadi Jaji huyo atakapoondolewa kazini na Rais chini ya masharti ya ibara ndogo ya (4).
(4) Endapo Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye mwenendo wake umechunguzwa na Tume hiyo aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, Rais atamuondoa kazini Jaji huyo na utumishi wake utakuwa umekoma.
(5) Endapo Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) itamshauri Rais kwamba Jaji ambaye mwenendo wake umechunguzwa na Tume hiyo asiondolewe, Rais atafuta uamuzi wa kumsimamisha kazi na utumishi wa Jaji huyo utaendelea.
(6) Masharti ya Ibara hii hayatawahusu watu walioteuliwa kukaimu nafasi ya Ujaji.
 


(d) Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano


 

Mahakama ya Rufani.
 
165.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano, itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama ya Rufani" na ambayo itakuwa na:
(a) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani;
(b) Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani; na (c) Majaji wengine wasiopungua kumi na saba.
 


- 63 -
 


(2) Majaji wa Mahakama ya Rufani watateuliwa kwa kuzingatia sifa zitakazoainishwa katika Katiba hii na uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Sheria zitakazotungwa kwa mujibu wa Katiba za Nchi Washirika zitaweka masharti kuhusu utaratibu wa kuwasilisha rufani mbele ya Mahakama ya Rufani.


 

Akidi ya vikao vya Mahakama ya Rufani.




Mamlaka ya Mahakama ya Rufani.


















Madaraka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.
 
166.-(1) Akidi ya kila kikao cha Mahakama ya Rufani itakuwa ni Majaji wa Mahakama ya Rufani watatu.
(2) Kila shauri na rufani inayohitaji uamuzi wa Mahakama ya Rufani itaamuliwa kwa kufuata kauli ya walio wengi kati ya Majaji wa Mahakama ya Rufani waliosikiliza shauri au rufani husika.


167.-(1) Mahakama ya Rufani itakuwa na mamlaka ya -

(a) kusikiliza na kuamua juu ya kila rufani inayowasilishwa mbele ya Mahakama ya Rufani kutokana na hukumu au uamuzi wowote wa Mahakama Kuu za Nchi Washirika au Mahakama yoyote ya chini iliyopewa mamlaka maalum ya kusikiliza mashauri ambayo kwa kawaida husikilizwa na Mahakama Kuu;
(b) kufanya mapitio ya maamuzi ya Mahakama Kuu za Nchi Washirika au mahakama yoyote ya chini iliyopewa mamlaka maalum ya kusikiliza mashauri ambayo kwa kawaida husikilizwa na Mahakama Kuu; na
(c) kufanya jambo jingine kama itakavyoainishwa kwenye sheria za nchi.
(2) Mahakama ya Rufani itaandaa kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa mamlaka yake.
(3) Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti zaidi kuhusu uendeshaji wa Mahakama ya Rufani.


168.-(1) Jaji wa Mahakama ya Rufani atakuwa na madaraka ya kusikiliza na kuamua shauri lolote katika Mahakama ya Rufani.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), iwapo Jaji wa Mahakama ya Rufani kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Nchi Washirika, Jaji huyo anaweza kuendelea kufanya kazi katika mahakama aliyotoka hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
(3) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2), itakuwa ni halali kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoa hukumu au uamuzi mwingine wowote unaohusika kwa kutumia na kutaja nafasi ya madaraka aliyokuwa akishika kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani na endapo hukumu hiyo au uamuzi huo utapingwa kwa njia ya rufani itakayowasilishwa mbele ya Mahakama ya Rufani, Jaji huyo hatakuwa na mamlaka ya kusikiliza rufani hiyo.
 





- 64 -
 



(e)Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani


 

Uteuzi wa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani.




















Uteuzi wa Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani.








Uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani.




Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Rufani.
 
169.-(1) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atateuliwa na Rais kutoka orodha ya majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(2) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atakuwa ndiye Mkuu wa Mahakama ya Rufani na msaidizi wa Jaji Mkuu katika utendaji wa kazi katika Mahakama ya Rufani, na katika madaraka hayo, Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atatekeleza kazi na shughuli atakazopangiwa mara kwa mara na Jaji Mkuu.
(3) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani endapo atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye tabia njema, uadilifu na uaminifu;
(b) awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika Jamhuri ya Muungano; na
(i) awe amefanya kazi ya ujaji katika Mahakama Kuu za Nchi Washirika; au
(ii) awe wakili, mtumishi wa umma au mwanataaluma akiwa na sifa ya kusajiliwa kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.


170.-(1) Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atateuliwa na Rais kutoka katika orodha ya majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani.
(2) Mtu atateuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani endapo atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 169(3).
(3) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani utafanywa kwa msingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.


171.-(1) Majaji wa Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

(2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani endapo atakuwa na sifa zilizoainishwa katika Ibara ya 169(3).


172. Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Makamu Mwenyekiti na Jaji wa Mahakama ya Rufani atashika madaraka yake mara tu atakapoapishwa na Rais kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
 





- 65 -
 



 

Muda wa kuwa madarakani kwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Majaji wa Mahakama ya Rufani.
























Utaratibu wa kukaimu nafasi ya Mwenye-kiti wa Mahakama ya Rufani.
 
173.-(1) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani atashika nafasi ya madaraka ya Ofisi ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani hadi atakapofikisha umri wa miaka sabini, isipokuwa kama:
(a) atajiuzulu;
(b) atashindwa kumudu kazi kutokana na maradhi;
(c) ataondolewa katika nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani kwa mujibu wa Katiba hii; au
(d) atafariki dunia.
(2) Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani au Jaji wa Mahakama ya Rufani atashika madaraka hadi atakapotimiza umri wa miaka sabini, isipokuwa kama:
(a) atajiuzulu;
(b) atashindwa kumudu kazi kutokana na maradhi;
(c) ataondolewa katika nafasi ya madaraka ya Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani kwa mujibu wa Katiba hii; au
(d) atafariki dunia.
(3) Jaji aliyetimiza umri wa kustaafu atalazimika kuendelea kufanya kazi baada ya kutimiza umri huo hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi akamilishe shughuli nyingine yoyote inayohusika na mashauri ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla hajatimiza umri wa kustaafu.
(4) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (3), Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani aliyetimiza umri wa kustaafu, ataachia nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, isipokuwa ataendelea kutekeleza shughuli ambazo hajazikamilisha akiwa katika nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Rufani hadi atakapokamilisha shughuli hizo.


174.-(1) Iwapo itatokea kwamba -
(a) nafasi ya madaraka ya Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ipo wazi;
(b) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani hayupo katika Jamhuri ya Muungano;
(c) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ameshindwa kutekeleza kazi kwa mujibu wa Katiba hii,
Makamu Mwenyekiti atatekeleza kazi za Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani hadi atakapoteuliwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani mwingine au hadi Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani ambaye alikuwa hayupo nchini au alikuwa hawezi kumudu kazi zake kutokana na maradhi atakaporejea kazini.
(2) Endapo ufanisi wa kazi za Mahakama ya Rufani utahitaji ateuliwe Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu atamshauri Rais kumteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani.
(3) Endapo Rais ataridhika na ushauri wa Jaji Mkuu, atamteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
 




- 66 -
 


(4) Mtu atakayeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani atafanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa muda wote utakaotajwa wakati wa kuteuliwa kwake, au kama muda haukutajwa, basi hadi uteuzi utakapofutwa na Rais.
(5) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (4), mtu aliyeteuliwa kuwa Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani ataendelea kufanya kazi kama Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani hadi amalize kutayarisha na kutoa hukumu au hadi amalize shughuli nyingine yoyote inayohusika na rufani au mashauri mengine ambayo alikwishaanza kuyasikiliza kabla ya muda wake wa kazi haujamalizika au uteuzi wake haujafutwa.
(6) Kwa madhumuni ya Ibara hii, Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani atakuwa na mamlaka kamili ya Jaji wa Mahakama ya Rufani na atatekeleza kazi zote za Jaji wa Mahakama ya Rufani.


 

Utaratibu wa kushughu-likia nidhamu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.
 
175.-(1) Jaji wa Mahakama ya Rufani anaweza kuondolewa katika nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi yake kutokana na:
(a) maradhi;
(b) kukiuka kanuni za maadili ya Majaji wa Mahakama ya Rufani; (c) kutokuwa na uwezo wa kumudu kazi za Jaji; au
(d) tabia mbaya au mwenendo unaokiuka maadili ya uongozi wa umma.
(2) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani au Jaji wa Mahakama ya Rufani anaweza kuondolewa katika nafasi ya madaraka ya Jaji kwa kufuata utaratibu unaofanana na ule uliowekwa kwa ajili ya kumuondoa kazini Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu au Jaji wa Mahakama ya Juu kama ilivyoelezwa.
 


(f)Usimamizi wa Shughuli za Mahakama


 

Msajili Mkuu wa Mahakama.
 
176.-(1) Kutakuwa na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano atakayeitwa "Msajili Mkuu wa Mahakama", atakayeteuliwa na Rais kufuatia mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama endapo atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano mwenye sifa ya uadilifu, tabia njema na uaminifu;
(b) awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika Jamhuri ya Muungano; na
(i) awe amefanya kazi ya uhakimu katika Mahakama za Nchi Washirika; au
(ii) amekuwa mtumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano,
na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.
 






- 67 -
 


 

Majukumu ya Msajili Mkuu wa Mahakama.






Mtendaji Mkuu wa Mahakama.











Majukumu ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama.
 
177.-(1) Msajili Mkuu wa Mahakama atakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kusimamia utekelezaji wa shughuli za kimahakama; (b) kuratibu masuala ya kimahakama; na
(c) majukumu mengine atakayopangiwa na Jaji Mkuu.
(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Msajili Mkuu wa Mahakama atawajibika kwa Jaji Mkuu.

178.-(1) Kutakuwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama atakayeteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi wa umma kufuatia mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma na kuidhinishwa na Bunge.
(2) Mtu hatateuliwa kushika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama isipokuwa tu kama ni:
(a) mtumishi mwandamizi wa umma;
(b) mwenye uweledi na uzoefu katika masuala ya utawala na mambo ya fedha; na
(c) mwadilifu na mwenye tabia na mwenendo usiotiliwa shaka na jamii.

179.-(1) Mtendaji Mkuu wa Mahakama atakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama; (b) Ofisa Masuuli wa Mahakama;
(c) msimamizi mkuu wa Mfuko wa Mahakama;
(d) msimamizi wa masuala ya utawala ya Mahakama; na (e) kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na Jaji Mkuu.
(2) Katika kutekeleza majukumu yake, Mtendaji Mkuu wa Mahakama atawajibika kwa Jaji Mkuu.
 

SEHEMU YA TATU
TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA NA MFUKO WA MAHAKAMA

 


Tume ya Utumishi wa Mahakama.
 
(a) Tume ya Utumishi wa Mahakama

180.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo itakuwa na wajumbe nane watakaoteuliwa na Rais kama ifuatavyo:
(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu; (d) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani;
(e) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika; (f) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Zanzibar;

(g) Wawakilishi wawili wa vitivo vya sheria kutoka vyuo vikuu, mmoja kutoka Tanganyika na mmoja kutoka Zanzibar watakaopendekezwa na vyuo vya elimu ya juu husika; na
(h) Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye atakuwa Katibu.
(2) Tume inaweza kumualika mtu mwingine yeyote mwenye utaalamu mahsusi kushiriki katika kikao chochote cha Tume, isipokuwa mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura.
(3) Tume itaweka utaratibu wa kuendesha vikao vyake.
 



- 68 -
 


 

Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama.









































Uanacha-ma katika vyama vya siasa.
 
181.-(1) Tume ya Utumishi wa Mahakama itakuwa na wajibu wa kuendeleza na kuwezesha uhuru na uwajibikaji wa Mahakama na utoaji haki wenye ufanisi, mafanikio na uwazi.
(2) Tume ya Utumishi wa Mahakama itakuwa na wajibu wa:
(a) kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu, Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani;
(b) kupitia na kupendekeza masharti ya utumishi wa Majaji na watumishi wengine wa mahakama ikiwemo masuala yanayohusu nidhamu na maslahi yao;
(c) kuteua wasajili na kuajiri watumishi wengine wa Mahakama, kupokea malalamiko dhidi yao na kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za nchi;
(d) kuandaa na kutekeleza mipango ya kujiendeleza kielimu kwa Majaji na watumishi wengine wa Mahakama;
(e) kupendekeza Serikalini hatua za kuimarisha Mahakama ili kuongeza ufanisi katika utoaji haki;
(f) kutoa fursa ya majadiliano kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na hivyo kumsaidia Jaji Mkuu katika kutekeleza majukumu yake kwa malengo ya kuleta ufanisi na mafanikio katika utoaji haki; na
(g) kutekeleza majukumu yoyote itakayopewa kwa mujibu wa Katiba hii au sheria za nchi.
(3) Katika kutekeleza majukumu yake, Tume itazingatia:
(a) uwazi katika mchakato wa uteuzi wa Majaji na ajira ya watumishi wengine wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano;
(b) uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano; na (c) uwakilishi wa kijinsia.
(4) Katika kutekeleza majukumu yake, Tume inaweza kukasimu madaraka yake kwa kamati mbalimbali zitakazoundwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
(5) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2)(b), mapendekezo ya maslahi kwa Majaji na watumishi wengine wa Mahakama yatawasilishwa kwenye chombo chenye jukumu la kusimamia maslahi ya watumishi wa umma.
(6) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti ya utekelezaji wa majukumu ya Tume.


182. Itakuwa ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Juu, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Msajili Mkuu wa Mahakama, Msajili wa ngazi yoyote na Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, isipokuwa atakuwa na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi katika vyombo vya uwakilishi.
 


(b) Mfuko wa Mahakama


 

Mfuko wa Mahakama
 
183.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano ambao utakuwa chini ya usimamizi wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama.
 


- 69 -
 



(2) Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano utatumika kwa ajili ya kugharamia shughuli za utawala na uendeshaji wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na shughuli nyingine muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya Mahakama.
(3) Serikali itahakikisha kwamba katika kila bajeti ya mwaka wa fedha wa Serikali, inatenga kwa kiwango kinachotosha fedha ambazo zitaingizwa katika Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(4) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu uendeshaji wa Mfuko wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.


SURA YA KUMI NA MOJA
UTUMISHI WA UMMA KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO


 

Misingi mikuu ya Utumishi wa Umma.
































Ajira na uteuzi wa Viongozi wa taasisi katika Serikali.
 
184.-(1) Kutakuwa na utumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano utakaozingatia misingi na kanuni zifuatazo:
(a) kwamba utumishi wa umma ni dhamana kutoka kwa wananchi na hivyo mtumishi anatakiwa kutumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na unyenyekevu;
(b) umuhimu wa kudumisha na kukuza viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma;
(c) umuhimu wa kuzingatia matumizi bora na yenye tija ya rasilimali;
(d) kutoa huduma kwa umma kwa njia ya haki, usawa na bila upendeleo;
(e) kuhamasisha wananchi kushiriki katika maandalizi ya sera mbalimbali za nchi;
(f) kuitikia matakwa na mahitaji ya watu kwa haraka na kwa wakati unaofaa;
(g) kujitolea katika utekelezaji wa sera na mipango ya kitaifa;
(h) uwajibikaji wa viongozi kwa makosa yanayofanyika chini yao; (i) kuhamasisha na kutekeleza sera ya uwazi katika kutoa habari za
kweli kwa umma na kwa wakati unaofaa; na
(j) kuhakikisha kwamba uteuzi na uajiri katika nafasi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, maarifa, ujuzi na uzoefu wao katika eneo husika.
(2) Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma zilizoainishwa katika Ibara hii zitazingatiwa na kutumika katika uteuzi wa kushika nafasi za madaraka ya uongozi katika:
(a) mamlaka katika mihimili ya dola; (b) taasisi na idara zote za Serikali; na
(c) mashirika, makampuni na wakala wa Serikali.
(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya utekelezaji wa misingi ya utumishi iliyoainishwa katika ibara ndogo ya (1).


185.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, ajira katika utumishi wa umma na uteuzi katika nafasi za madaraka ya uongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano na taasisi zake, itatolewa na kufanyika kwa kuzingatia:
 


- 70 -
 



(a) taaluma na uweledi; na
(b) uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), uteuzi wa viongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano utafanyika kwa kuzingatia ushiriki wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.


 

Tume ya Utumishi wa Umma.

















Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.






Mamlaka na Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma.
 
186.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Umma itakayokuwa na Mwenyekiti na wajumbe wengine sita watakaoteuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge.
(2) Katika kuteua wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma, Rais atazingatia Kanuni za Utumishi wa Umma zilizoainishwa katika Katiba hii.
(3) Sifa za Mwenyekiti na Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi;
(c) awe na uzoefu wa utumishi wa umma, upeo mkubwa katika mambo ya utumishi, utawala na mambo ya jamii kwa kipindi kisichopungua miaka kumi; na
(d) awe na heshima, uweledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii.


187.-(1) Kutakuwa na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali za Nchi Washirika baada ya kuidhinishwa na Bunge.
(2) Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma atakuwa ndiye Mkuu wa Sekretarieti ya Utumishi wa Umma, Mtendaji Mkuu na mtekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Tume.


188.-(1) Tume ya Utumishi wa Umma itakuwa ni chombo cha juu katika utumishi wa umma chenye mamlaka ya kusimamia na kuratibu mambo yote kuhusu utumishi wa umma.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma yatakuwa ni:
(a) kumshauri Rais juu ya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbalimbali kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) kutoa miongozo mbalimbali na kusimamia mchakato wa ajira katika utumishi wa umma kwa kuzingatia vigezo stahiki;
(c) kuteua watu kuhudumu au kushikilia ofisi kwa muda katika utumishi wa umma, kuidhinisha uteuzi na kudhibiti nidhamu na kuwaondoa watumishi wanaohudumu au kushikilia ofisi hizo;
(d) kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa misingi na kanuni za utumishi katika sekta zote za utumishi wa umma;
(e) kushughulikia rufani zinazowasilishwa na watumishi wa umma dhidi ya uamuzi wa mamlaka mbalimbali za nidhamu katika utumishi wa umma;
 



- 71 -
 



(f) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama yatakavyoainishwa katika sheria za nchi juu ya masuala ya utumishi wa umma na sheria nyingine za nchi;
(g) kuunda na kupanga ngazi za mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma, ikiwemo, viongozi wa kisiasa, watumishi katika Utumishi wa Serikali, Utumishi wa Bunge na Utumishi wa Mahakama; na
(h) kudurusu na kusawazisha mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma ikiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi katika Utumishi wa Serikali, Utumishi wa Bunge na Utumishi wa Mahakama.


SURA YA KUMI NA MBILI UCHAGUZI KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI
NA VYAMA VYA SIASA


SEHEMU YA KWANZA UWAKILISHI WA WANANCHI


 

Ushiriki katika uchaguzi na kura ya maoni.
 
189.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano mwenye umri wa miaka kumi na nane au zaidi mwenye akili timamu ana haki ya kupiga kura na haki ya kuandikishwa na kushiriki kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), mamlaka ya kusimamia uchaguzi itazingatia misingi kwamba:
(a) wananchi wanatumia haki ya kisiasa kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) watu wenye ulemavu wanapewa fursa za uwakilishi;
(c) kunakuwa na haki ya kila raia kupiga kura moja kufuatana na utashi wa uwakilishi na kura sawa; na
(d) uchaguzi unakuwa huru na wa haki ambao -(i) ni wa kura ya siri;
(ii) hauna matumizi ya nguvu, vitisho, vishawishi wala rushwa;
(iii) hauna matamshi au vitendo vinavyoashiria ukabila, ukanda, udini, dharau na kashfa kwa jinsi au unyanyapaa kwa walemavu au makundi madogo katika jamii;
(iv) unaendeshwa na kusimamiwa na chombo huru; na
(v) unaendeshwa bila upendeleo au kuegemea upande wowote, ulio makini na unaoonyesha uwajibikaji wa watendaji.
(3) Katika kutekeleza masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:
(a) mamlaka zinazosimamia uchaguzi kutangaza majimbo kwa madhumuni ya uchaguzi wa wabunge;
(b) uteuzi wa wagombea;
(c) uandikishaji wa wapiga kura;
(d) kuendesha na kusimamia uchaguzi na kura ya maoni;
 


- 72 -
 



(e) kuweka utaratibu wa kuandikisha raia wa Jamhuri ya Muungano wanaoishi nje kuweza kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni; na
(f) utaratibu wa kufanya uchaguzi kuwa mwepesi, wazi na unaozingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum.
(4) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (2) na kwa kuzingatia masharti kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, kila mpiga kura ana haki ya kufungua shauri Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi, anayoamini yamekiuka masharti ya Katiba hii au sheria za nchi.

SEHEMU YA PILI TUME HURU YA UCHAGUZI

(a) Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi

 

Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
 
190.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano itakayoitwa "Tume Huru ya Uchaguzi".
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuthibitishwa na Bunge.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(5) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi watakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu aliyewahi kushika nafasi ya madaraka ya Jaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu na ameshika nafasi ya madaraka hayo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano;
(c) awe ni mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa shaka na jamii;
(d) awe ni mtu ambaye, hajawahi kushika nafasi ya madaraka katika chama cha siasa; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusiana na uaminifu.
(6) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo usiotiliwa shaka na jamii;
 



- 73 -
 


(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka yoyote katika chama cha siasa;
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusu kukosa uaminifu.
(7) Kwa madhumuni ya Ibara hii, watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi:
(a) Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mbunge wa Bunge la Tanganyika, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi au Diwani katika Serikali ya Tanganyika au Zanzibar; au
(b) mtu ambaye ni mtumishi wa umma.
(8) Uteuzi wa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi utazingatia uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.


 

Kamati ya Uteuzi.
 
191.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi itakayokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti;
(c) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; (d) Spika wa Bunge la Tanganyika;
(e) Jaji Mkuu wa Tanganyika; (f) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na
(g) Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji. (2) Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi atakuwa Katibu wa
Kamati ya Uteuzi.
(3) Kamati ya Uteuzi itakuwa na jukumu la kupokea na kuchambua majina ya watu walioomba na waliopendekezwa kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa utaratibu utakaoainishwa na sheria za nchi.
(4) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (3), Kamati ya Uteuzi mara baada ya kuchambua majina ya watu walioomba na waliopendekezwa kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi, itapendekeza kwa Rais majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
(5) Rais atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kutoka miongoni mwa majina yaliyowasilishwa na Kamati ya Uteuzi na atawasilisha majina hayo Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.
(6) Kwa madhumuni ya Ibara hii, asasi za kiraia na zisizo za kiserikali zinaweza kupendekeza majina ya watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
(7) Bunge litatunga Sheria ambayo pamoja na mambo mengine itaweka masharti kuhusu kiapo cha Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Tume Huru ya Uchaguzi.
 



- 74 -
 



 

Ukomo wa kushika nafasi ya madaraka ya Tume Huru ya Uchaguzi.




































Wajibu wa Tume Huru ya Uchaguzi.
 
192.-(1) Mjumbe wa Tume atashika nafasi ya madaraka kwa kipindi cha miaka mitano na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja cha miaka mitano.
(2) Mtu atakoma kuwa mjumbe wa Tume endapo litatokea tukio lolote kati ya matukio yafuatayo:
(a) kujiuzulu;
(b) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya maradhi;
(c) kuondolewa kwa makosa ya kukiuka Kanuni za Maadili ya Uongozi wa Umma;
(d) kutiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifungo gerezani kwa muda unaozidi siku saba;
(e) kupoteza sifa ya kuteuliwa kuwa mjumbe; au (f) kufariki dunia.
(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu ya Tume, kutakuwa na kanuni za maadili kama zitakavyoainishwa na sheria za nchi.
(4) Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ambaye atakiuka masharti ya kanuni za maadili atapoteza sifa za kuendelea kuwa mjumbe.
(5) Endapo suala la kumuondoa Mjumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kwa kukiuka kanuni za maadili litajitokeza, Rais atateua Kamati itakayoundwa na:
(a) Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu;
(c) Mjumbe wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji; na (d) Mawakili, mmoja kutoka Tanganyika na mmoja kutoka
Zanzibar watakaopendekezwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika na Chama cha Wanasheria Zanzibar,
na Kamati hiyo itafanya uchunguzi wa suala hilo na kisha kutoa mapendekezo kwa Rais.
(6) Endapo, baada ya uchunguzi, Kamati itapendekeza kuwa mjumbe huyo aondolewe madarakani, Rais atamuondoa mjumbe huyo madarakani na endapo Kamati itapendekeza kuwa mjumbe huyo asiondolewe, suala la kumuondoa mjumbe huyo litakoma.
(7) Kamati itaweka utaratibu wa kufanya uchunguzi.


193.-(1) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na wajibu wa:
(a) kusimamia na kuendesha shughuli zote za uchaguzi wa Wabunge na Rais katika Jamhuri ya Muungano;
(b) kusimamia na kuendesha kura ya maoni;
(c) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika Jamhuri ya Muungano; na
(d) kugawa na kutangaza majimbo ya uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa pia na wajibu wa kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi au kura ya maoni na kuratibu utoaji wa elimu ya uraia kuhusu uchaguzi na kusimamia asasi za kiraia, taasisi, jumuiya au makundi ya watu yatakaotoa elimu hiyo.
 



- 75 -
 


(3) Tume Huru ya Uchaguzi pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwepo kwa:
(a) uhuru wa wananchi katika kutumia haki ya uchaguzi na kuchaguliwa kupitia vyama vya siasa au mgombea huru;
(b) uwakilishi unaozingatia jinsi;
(c) uwakilishi wa watu wenye ulemavu au mahitaji maalum katika jamii;
(d) uzingatiaji wa misingi ya upigaji kura wa mtu mmoja kura moja kwa kuzingatia uwakilishi wenye usawa; na
(e) uchaguzi huru na wa haki.
(4) Tume Huru ya Uchaguzi inaweza kutekeleza shughuli zake bila kujali kwamba kuna nafasi ya madaraka ya mjumbe iliyo wazi miongoni mwa wajumbe au kwamba Mjumbe yeyote hayupo, lakini kila uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi kati ya idadi ya Wajumbe wote wa Tume Huru ya Uchaguzi.
(5) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, Tume Huru ya Uchaguzi haitalazimika kufuata amri, maagizo au maoni ya mtu yeyote, mamlaka yoyote ya Serikali, chama cha siasa, taasisi au asasi yoyote.
(6) Katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, Tume Huru ya Uchaguzi itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya Tanganyika na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
(7) Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi au kura ya maoni.
(8) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (7), watu wanaohusika na uchaguzi au kura ya maoni ni -
(a) Mwenyekiti wa Tume;
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume; (c) Wajumbe wote wa Tume;
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume; na
(e) wasimamizi wote wa uchaguzi.


 

Malalamiko kuhusu uchaguzi.
 
194.-(1) Tume Huru ya Uchaguzi itasimamia na kutatua mapema iwezekanavyo malalamiko yanayohusu kuteuliwa kwa mgombea katika uchaguzi.
(2) Kesi za malalamiko kuhusu uchaguzi wa Wabunge zitafunguliwa Mahakama Kuu mapema iwezekanavyo baada ya Tume Huru ya Uchaguzi kutangaza matokeo na kwa vyovyote vile si zaidi ya muda ulioainishwa katika sheria za nchi.
 


(b) Mkurugenzi wa Uchaguzi


 

Uteuzi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
 
195.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma na kuthibitishwa na Bunge.
 




- 76 -
 


(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu, na mwenye mwenendo usiotiliwa shaka na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka yoyote katika chama cha kisiasa;
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusu kukosa uaminifu.


 

Majukumu ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.
 
196.-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa ndiye msimamizi na mtekelezaji mkuu wa majukumu ya kila siku ya Tume Huru ya Uchaguzi kuhusiana na masuala ya uchaguzi, uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa kura ya maoni.
(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kufuata utaratibu ulioainishwa na sheria za nchi kuhusu masuala ya uchaguzi na kura ya maoni.
(3) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yake kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni watumishi wa umma kwa kadri ya idadi inayohitajika.
(4) Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurugenzi wa Uchaguzi atawajibika kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
 


SEHEMU YA TATU
USAJILI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA SIASA


(a) Vyama vya Siasa


 

Usajili wa vyama vya siasa.
 
197.-(1) Chama cha siasa kinaweza kufanya shughuli za siasa endapo kitasajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

(2) Haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kusajiliwa ambacho kutokana na Katiba au sera yake -
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya -(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila, pahala watu watokeapo, rangi au jinsi;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano;
(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa;
(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano; au
(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia.
 




- 77 -
 



(3) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au kwa chama cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.
(4) Bunge linaweza kutunga sheria inayoweka masharti yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.
(5) Mambo yote yanayohusu uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.


(b) Msajili wa Vyama vya Siasa


 

Uteuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa.











Wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa.
 
198.-(1) Kutakuwa na Msajili wa Vyama vya Siasa atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma na kuthibitishwa na Bunge.
(2) Msajili wa Vyama vya Siasa atakuwa na sifa zifuatazo: (a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) awe ni mtu mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa shaka na jamii;
(c) awe ni mtu ambaye hajawahi kushika nafasi ya madaraka yoyote katika chama cha siasa; na
(d) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.


199.-(1) Msajili wa Vyama vya Siasa atakuwa na wajibu wa:
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji na shughuli za vyama vya siasa kwa mujibu wa masharti ya Katiba na sheria za nchi;
(b) kutayarisha na kuchapisha taarifa za kila mwaka kuhusu ripoti za ukaguzi wa fedha kwa kila chama cha siasa; na
(c) kusimamia fedha za vyama vya siasa.
(2) Msajili wa Vyama vya Siasa atatekeleza majukumu yake kwa kufuata utaratibu ulioainishwa na sheria za nchi.
 


SURA YA KUMI NA TATU TAASISI ZA UWAJIBIKAJI


SEHEMU YA KWANZA
TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI


 

Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.
 
200.-(1) Kutakuwa na Tume ambayo itaitwa "Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji" itakuwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine wasiozidi saba.

(2) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati Maalum ya Uteuzi.
 



- 78 -
 


(3) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume utafanywa kwa kuzingatia msingi kwamba endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka baada ya kuthibitishwa na Bunge.
(5) Sifa za Mwenyekiti wa Tume zitakuwa kama ifuatavyo: (a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi;
(c) mtu mwenye uzoefu katika utumishi wa umma kwa kipindi kisichopungua miaka kumi na tano;
(d) mtu mwenye heshima, uweledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii; na
(e) awe ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusu kukosa uaminifu.
(6) Sifa za Makamu Mwenyekiti zitakuwa kama zilivyoainishwa katika ibara ndogo ya (5).


 
Uteuzi na sifa za Wajumbe.













Kamati Maalum ya Uteuzi.










Majukumu ya jumla ya Tume.
 
201.-(1) Wajumbe wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati Maalum ya Uteuzi.
(2) Sifa za Wajumbe wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi;
(c) mtu mwenye uzoefu kwenye uongozi kwa kipindi kisichopungua miaka kumi;
(d) mtu mwenye heshima, uweledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii.


202. Kutakuwa na Kamati Maalum ya Uteuzi ambayo itakuwa na Wajumbe wafuatao:

(a) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano; (b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(c) Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanganyika; (d) Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar; (e) Spika wa Bunge la Tanganyika;
(f) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na (g) Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


203.-(1) Majukumu ya jumla ya Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji yatakuwa ni kufuatilia na kuchunguza tabia na mwenendo wa viongozi wa umma na watumishi wa umma kwa madhumuni ya kusimamia na kuhakikisha kuwa Maadili na Miiko ya Uongozi wa Umma inazingatiwa, inalindwa na kuheshimiwa katika utumishi wa Serikali, Bunge, Mahakama, taasisi na idara nyingine zote za umma.
 



- 79 -
 



(2) Bila ya kuathiri masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1), majukumu mahsusi ya Tume yatakuwa ni:
(a) kusimamia maadili na uwajibikaji katika utumishi wa umma; (b) kufanya upekuzi kwa kushirikiana na taasisi nyingine;
(c) kuchunguza tabia na mwenendo wa mtumishi au kiongozi wa umma na kuchukua hatua pale inapostahili, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria watumishi watakaobainika kukiuka maadili na miiko ya uongozi;
(d) kusimamia sheria za nchi kuhusu maadili na uwajibikaji wa viongozi wa umma na watumishi wa umma;
(e) kutoa ushauri juu ya masuala ya ubadhirifu wa fedha kwa mamlaka husika;
(f) kufanya upekuzi kwa kiongozi wa umma anayepewa dhamana kabla ya kuingia madarakani;
(g) kutoa elimu kwa umma kuhusu maadili na miiko ya viongozi wa umma;
(h) kufanya uchunguzi kwa maamuzi yake yenyewe, au baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mtu yeyote, kutokana na kutenda au kutokutenda kwa kiongozi wa umma au mtumishi yeyote wa umma, au wakala wa serikali, ikiwa kitendo kilichotendwa au kutokutendwa ni kinyume cha maadili ya umma;
(i) kumwelekeza, baada ya kupata malalamiko au itakapoona inafaa, kiongozi wa umma au mtumishi wa umma, taasisi au wakala wa serikali au chombo chochote cha umma kufanya jambo lolote linalotakiwa na sheria, kuacha, kuzuia au kusahihisha utendaji mbaya au usio sahihi wa majukumu yake;
(j) kutoa ushauri kuhusu kuchukuliwa hatua kiongozi wa umma au mtumishi wa umma;
(k) kumwelekeza kiongozi wa umma au mtumishi wa umma, kwa mujibu wa sheria za nchi, kutoa nyaraka zinazohusiana na matumizi ya ofisi, matumizi ya fedha au mali za umma, au kutoa taarifa ya matumizi mabaya kwa Tume, kwa hatua stahiki;
(l) kuomba msaada au taarifa muhimu kutoka kwa mamlaka yoyote ya serikali au binafsi katika kutekeleza wajibu wake, na kukagua kumbukumbu muhimu na nyaraka husika;
(m)kwa kuzingatia sheria, kutangaza kwa umma, mambo yote yanayohusiana na uchunguzi uliofanywa na Tume, iwapo mazingira yanaruhusu;
(n) kuchunguza jambo au mazingira yoyote yanayokiuka au kusababisha ukiukaji wa maadili; na
(o) kuandaa kanuni za taratibu na matumizi ya mamlaka au utekelezaji wa kazi na majukumu ya Tume kama itakavyoelekezwa na sheria za nchi.





- 80 -
 


 

Muda wa kukaa madarakani kwa Mjumbe wa Tume.












Kuondolewa madarakani kwa Mjumbe wa Tume.






















Uhuru wa Tume.









Uwezeshaji wa nyenzo na rasilimali.
 
204.-(1) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine wote kila mmoja atashika madaraka yake kwa kipindi cha miaka mitatu au kipindi kingine cha chini ya miaka mitatu kama itakavyoainishwa katika barua ya uteuzi, ikizingatiwa kwamba uteuzi wa Wajumbe wa Tume utafanywa kwa namna ambayo Wajumbe wa Tume hawataanza au kumaliza muda wao kwa wakati mmoja.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe wa Tume anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja tu cha miaka mitatu au vinginevyo vyovyote itakavyokuwa.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wakati watakapokuwa madarakani hawataruhusiwa kuteuliwa, kuchaguliwa au kushika nafasi ya madaraka nyingine yoyote.


205.-(1) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe wa Tume anaweza kuondolewa madarakani kwa:
(a) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya maradhi;
(b) kukiuka kanuni za maadili ya uongozi wa umma; (c) kukiuka Miiko ya Uongozi wa Umma;
(d) kukosa uweledi; au (e) utovu wa nidhamu.
(2) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe wa Tume anaweza kuondolewa madarakani kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma au malalamiko ya mtu yeyote kwa Tume ya Utumishi wa Umma, kwa masharti kwamba:
(a) mapendekezo au malalamiko yawe kwa maandishi; na
(b) yaainishe masuala yanayopendekezwa au yanayolalamikiwa. (3) Baada ya kupokea mapendekezo au malalamiko, Rais ataunda
Kamati Maalum itakayofanya uchunguzi kuhusu malalamiko hayo.
(4) Baada ya kukamilisha uchunguzi, Kamati Maalum itapeleka mapendekezo kwa Rais kwa uamuzi.
(5) Masuala yanayohusu idadi na sifa za wajumbe, muda na utaratibu wa kufanya kazi wa Kamati Maalum yatakuwa kama itakavyoamuliwa na Rais.


206.-(1) Tume itakuwa huru na kwa mantiki hiyo haitaingiliwa na mtu au mamlaka yoyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu: (a) utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya Tume;
(b) utayarishaji na utoaji wa taarifa za Tume;
(c) utaratibu wa utoaji wa mapendekezo na maamuzi ya Tume; (d) watumishi wa Tume; na
(e) masuala mengine muhimu yanayoihusu Tume.


207. Serikali itahakikisha kuwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ya kutosha kadri hali itakavyoruhusu ili kutekeleza kazi na wajibu wake kwa ufanisi.
 




- 81 -
 


SEHEMU YA PILI TUME YA HAKI ZA BINADAMU


 
Tume ya Haki za Binadamu.







































Kamati ya Uteuzi.
 
208.-(1) Kutakuwa na Tume itakayoitwa "Tume ya Haki za Binadamu" itakayokuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wasiozidi saba.
(2) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu utafanywa kwa kuzingatia msingi kwamba endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti watashika madaraka baada ya kuthibitishwa na Bunge.
(5) Sifa za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume zitakuwa kama ifuatavyo:
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;
(b) mtu mwenye shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na sheria za nchi;
(c) mtu mwenye kuheshimu haki za binadamu;
(d) mtu mwenye uzoefu wa utumishi wa umma, upeo mkubwa katika mambo ya haki za binadamu, utawala na mambo ya jamii kwa kipindi kisichopungua miaka kumi; na
(e) mtu mwenye heshima, uweledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii.
(6) Sifa za Makamishna wa Tume zitakuwa kama ifuatavyo: (a) awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano;
(b) mtu mwenye kuheshimu haki za binadamu;
(c) mtu mwenye uzoefu usiopungua miaka kumi ikiwa angalau ana sifa ya masuala ya sheria, haki za binadamu, utawala, siasa na mambo ya jamii;
(d) mtu mwenye heshima, uweledi, uaminifu, uadilifu na asiye na tabia au mwenendo wenye kutiliwa shaka na jamii;
(e) mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na sheria za nchi.


209.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu itakayokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti;
(c) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; (d) Spika wa Bunge la Tanganyika;
(e) Jaji Mkuu wa Tanganyika; (f) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na
(g) Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.
 


- 82 -
 



(2) Katibu wa Tume ya Haki za Binadamu atakuwa Katibu wa Kamati ya Uteuzi.
(3) Kamati ya Uteuzi itakuwa na jukumu la kupokea na kuchambua majina ya watu walioomba na waliopendekezwa kuwa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu kwa mujibu wa utaratibu utakaoainishwa na sheria za nchi.
(4) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (3), Kamati ya Uteuzi mara baada ya kuchambua majina ya watu walioomba na waliopendekezwa kuwa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu, itapendekeza kwa Rais majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu.
(5) Rais atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu kutoka miongoni mwa majina yaliyowasilishwa na Kamati ya Uteuzi na atawasilisha majina hayo Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.
(6) Kwa madhumuni ya Ibara hii, asasi za kiraia na zisizo za kiserikali zinaweza kupendekeza majina ya watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu.
(7) Kutakuwa na Sekretarieti ya Tume ya Haki za Binadamu itakayoongozwa na Katibu atakayeteuliwa na Rais kutokana na orodha ya majina ya watu watatu waliopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma.
(8) Bunge litatunga sheria ambayo pamoja na mambo mengine itaweka masharti kuhusu kiapo cha Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu.


 

Kazi na majukumu ya Tume.
 
210.-(1) Kazi na majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu yatakuwa kama ifuatavyo:
(a) kuhamasisha hifadhi ya haki za binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi;
(b) kupokea malalamiko juu ya uvunjaji wa haki za binadamu kwa ujumla;
(c) kuchunguza uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
(d) kufanya utafiti na kutoa elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
(e) kufungua mashauri Mahakamani ili kuzuia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu au kurekebisha haki inayotokana na uvunjwaji huo wa haki za binadamu au ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
(f) kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika au taasisi yoyote inayohusika na masharti ya Ibara hii katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake au utekelezaji unaokiuka madaraka hayo;
(g) kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na vya sekta binafsi kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
 




- 83 -
 


(h) kuchukua hatua zinazostahiki kwa ajili ya kukuza na kuendeleza usuluhishi miongoni mwa watu na taasisi mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbele ya Tume;
(i) kutembelea magereza, vituo vya polisi au mahali pengine popote ambapo mtu au watu wanazuiliwa kwa madhumuni ya kutathmini na kukagua hali za watu wanaozuiliwa katika sehemu hizo na kutoa mapendekezo yatakayowezesha kurekebisha kasoro zilizopo;
(j) kutoa mapendekezo yanayohusiana na sheria iliyokwishatungwa au inayokusudiwa kutungwa, kanuni, au mambo ya kiutawala ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa na kikanda vya haki za binadamu;
(k) kuwasilisha taarifa na maoni huru kwenye vyombo na taasisi za kimataifa na za kikanda kuhusu hali ya haki za binadamu nchini pale inapobidi;
(l) kuihamasisha Serikali kutia saini na kuridhia mikataba au makubaliano ya kimataifa yanayohusu haki za binadamu, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa haki za binadamu zilizomo kwa mujibu wa Katiba hii, Katiba za Nchi Washirika, sheria za nchi na mikataba au makubaliano ya kimataifa ambayo Jamhuri ya Muungano inawajibika nayo; na
(m) kwa kupitia Serikalini, kushirikiana na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Nchi za Afrika, Jumuiya ya Madola na taasisi nyingine zenye mahusiano baina yao, miongoni mwao au ya kikanda na taasisi za nchi nyingine katika maeneo ya hifadhi na ukuzaji wa haki za binadamu.
(2) Tume ya Haki za Binadamu itakuwa na mamlaka maalum kama ifuatavyo:
(a) kumuita mtu yeyote mbele ya Tume na kumtaka awasilishe mbele yake nyaraka zozote, kumbukumbu au kitu chochote kilicho katika mamlaka yake kinachohusiana na jambo linalochunguzwa na Tume;
(b) kumtaka mtu yeyote kutoa taarifa anayoifahamu kwa Tume juu ya jambo linalochunguzwa na Tume;
(c) kusababisha mtu yeyote anayekiuka maagizo au taratibu za Tume kufunguliwa mashtaka ya jinai mahakamani.


 

Muda wa kukaa madarakani kwa Kamishna wa Tume.
 
211.-(1) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Kamishna wa Tume kila mmoja atashika madaraka yake kwa kipindi cha miaka mitatu au kipindi kingine cha chini ya miaka mitatu kama itakavyoainishwa katika barua ya uteuzi, ikizingatiwa kwamba uteuzi wa Makamishna wa Tume utafanywa kwa namna ambayo hawataanza au kumaliza muda wao kwa wakati mmoja.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Kamishna wa Tume anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja tu cha miaka mitatu au vinginevyo vyovyote itakavyokuwa.
 



- 84 -
 


(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Kamishna wa Tume wakati watakapokuwa madarakani hawataruhusiwa kuteuliwa, kuchaguliwa au kushika nafasi ya madaraka nyingine.


 

Kuondolewa madarakani kwa Kamishna wa Tume.

























Uhuru wa Tume.









Uwezeshaji wa nyenzo na rasilimali.




Uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
 
212.-(1) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Kamishna wa Tume anaweza kuondolewa madarakani kwa:
(a) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya maradhi;
(b) kukiuka kanuni za maadili ya uongozi wa umma; (c) kukiuka Miiko ya Uongozi wa Umma;
(d) kukosa uweledi; au (e) utovu wa nidhamu.
(2) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Kamishna wa Tume anaweza kuondolewa madarakani kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma au kutokana na malalamiko ya mtu yeyote kwa Tume ya Utumishi wa Umma, kwa masharti kwamba:
(a) mapendekezo au malalamiko hayo yawe kwa maandishi; na (b) yaainishe masuala yanayopendekezwa au yanayolalamikiwa. (3) Baada ya kupokea mapendekezo au malalamiko, Tume ya
Utumishi wa Umma itaunda Kamati Maalum kufanya uchunguzi kuhusu mapendekezo au malalamiko hayo.
(4) Baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum, Tume ya Utumishi wa Umma itapeleka mapendekezo ya Kamati Maalum kwa Rais kwa uamuzi.
(5) Rais atachukua hatua kama atakavyoshauriwa na Kamati Maalum.
(6) Masuala yanayohusu idadi na sifa za wajumbe, muda na utaratibu wa kufanya kazi wa Kamati Maalum yatakuwa kama itakavyoamuliwa na Tume ya Utumishi wa Umma.

213.-(1) Tume itakuwa huru na haitaingiliwa na mtu au mamlaka yoyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu: (a) utaratibu wa utekelezaji wa majukumu ya Tume;
(b) utayarishaji na utoaji wa taarifa za Tume;
(c) utaratibu wa utoaji wa mapendekezo na maamuzi ya Tume; (d) watumishi wa Tume; na
(e) masuala mengine muhimu yanayoihusu Tume.

214. Serikali itahakikisha kuwa Tume ya Haki za Binadamu inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ya kutosha kadri hali itakavyoruhusu ili kutekeleza kazi na wajibu wake kwa ufanisi.

SEHEMU YA TATU
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

215.-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambaye atateuliwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atashika nafasi ya madaraka yake baada ya kuapishwa na Rais.
 


- 85 -
 



 

Sifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.












Kazi na majukumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
 
216.-(1) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atateuliwa kutoka katika orodha ya majina matatu ya watumishi wa umma yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma.
(2) Mtu anaweza kuteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ikiwa ana sifa zifuatazo:
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano;
(b) amefuzu mafunzo ya juu ya uhasibu na kusajiliwa na mamlaka husika;
(c) ana uzoefu usiopungua miaka kumi na tano katika masuala yanayohusu ukaguzi wa hesabu za Serikali;
(d) ni mtu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusu kukosa uaminifu; na
(e) ni mtu mwenye heshima, uweledi, uaminifu, uadilifu na asiye na mwenendo unaotiliwa shaka na jamii.


217.-(1) Kazi na majukumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yatakuwa ni:
(a) kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina matumizi yake yameidhinishwa na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe;
(b) kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina au fedha ambazo matumizi yake yameidhinishwa na sheria za nchi, na kwamba zimetumika kwa ajili ya shughuli zilizohusika na matumizi ya fedha hizo na matumizi hayo yamefanywa kwa kufuata idhini iliyotolewa kuhusu matumizi hayo;
(c) angalau mara moja kila mwaka, kufanya ukaguzi na kutoa taarifa kuhusu -
(i) hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(ii) hesabu zinazosimamiwa na taasisi na wakala wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(iii)hesabu za Mahakama ya Jamhuri ya Muungaano; na (iv)hesabu za Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atakuwa huru katika utekelezaji wa kazi na majukumu yake na hataingiliwa na mtu au mamlaka yoyote katika utekelezaji wa kazi zake.
(3) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali au mtu yeyote aliyeruhusiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atakuwa na haki ya kuchunguza vitabu, kumbukumbu, hati nyinginezo zote zinazohusika na hesabu za aina yoyote iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1).
(4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
 



- 86 -
 



(5) Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile ulipoanza Mkutano huo, na iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika, basi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atawasilisha taarifa hiyo kwa Spika, ambaye atawasilisha taarifa hiyo kwenye Bunge.
(6) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atakuwa pia na jukumu la kutekeleza kazi na shughuli nyingine, na atakuwa na madaraka mengine ya namna mbalimbali, kama itakavyoelezwa na sheria kuhusu hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, hesabu za vyombo vya umma au hesabu za mashirika.
(7) Katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (1), (3), (4) na (5) ya Ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ametekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au sivyo.
(8) Bunge linaweza kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, matumizi ya mamlaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.


 
Muda wa kukaa madarakani kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.


Kuondolewa madarakani kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
 
218.-(1) Muda wa kukaa madarakani kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali utakuwa ni kipindi kimoja cha miaka saba mfululizo.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza kujiuzulu nafasi ya madaraka yake kwa kutoa taarifa ya siku thelathini kwa Rais.


219.-(1) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza kuondolewa madarakani kwa:
(a) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya maradhi;
(b) kukiuka kanuni za maadili ya uongozi wa umma; (c) kukiuka Miiko ya Uongozi wa Umma;
(d) kukosa weledi; au (e) utovu wa nidhamu.
(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hataweza kuondolewa kazini isipokuwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) na (4).

(3) Endapo Rais ataridhika kwamba suala la kumuondoa madarakani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali linahitaji kuchunguzwa:
 





- 87 -
 


(a) atateua Kamati Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na wajumbe wengine wasiopungua wawili na angalau nusu ya wajumbe hao wawe ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu za Nchi Washirika;
(b) Kamati Maalum itachunguza shauri na kutoa taarifa kwa Rais na itamshauri Rais kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aondolewe madarakani au la.
(4) Endapo Kamati Maalum itamshauri Rais kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aondolewe madarakani, basi Rais atamuondoa madarakani.
(5) Wakati suala la kumuondoa madarakani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali limepelekwa kwenye Kamati Maalum kwa ajili ya uchunguzi, Rais atamsimamisha kazi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
(6) Rais atafuta uamuzi wa kumsimamisha kazi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali endapo Kamati Maalum itamshauri Rais kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali asiondolewe madarakani.

 

Uwezeshaji wa nyenzo na rasilimali.
 
220. Serikali itahakikisha kuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inapatiwa fedha, nyenzo na rasilimali watu ya kutosha ili kulinda uhuru wake katika kutekeleza kazi na majukumu yake kwa ufanisi.
 

SURA YA KUMI NA NNE
MASHARTI KUHUSU FEDHA ZA JAMHURI YA MUUNGANO

 



Mfuko Mkuu wa Hazina.









Masharti ya kutoa fedha za matumizi katika Mfuko Mkuu wa Hazina.
 
(a) Mfuko Mkuu wa Hazina na Fedha za Jamhuri ya Muungano

221. Kutakuwa na Mfuko Mkuu wa Hazina wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano utakaoitwa "Mfuko Mkuu wa Hazina" ambamo fedha zote zitakazopatikana kwa njia mbalimbali zitawekwa, isipokuwa:
(a) fedha ambazo zimetajwa katika sheria kuwa zitumike kwa shughuli maalum au ziwekwe katika mfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum; au
(b) fedha ambazo kwa mujibu wa sheria za nchi, taasisi za Serikali zimeruhusiwa kukusanya na kubaki nazo kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa taasisi hizo.

222.-(1) Fedha zinaweza kutolewa kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ajili ya matumizi, kwa kuzingatia masharti yafuatayo:
(a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa kuwa yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina na idhini hiyo iwe imetolewa kwa mujibu wa Katiba hii au sheria za nchi; na
(b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa ama na Sheria ya Matumizi ya Serikali iliyotungwa mahsusi na Bunge au sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge.
 


- 88 -
 


(2) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (1), fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina zitatolewa kutoka Mfuko huo kwa ajili ya matumizi kwa kuzingatia masharti kuwa matumizi hayo yawe yameidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
(3) Fedha zilizomo katika mfuko maalum wowote wa Serikali, isipokuwa Mfuko Mkuu wa Hazina, hazitatolewa kutoka mfuko huo kwa ajili ya matumizi isipokuwa kwa mujibu wa sheria inayoidhinisha matumizi hayo.


 

Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina.





























Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali kuanza kutumika.
 
223.-(1) Rais atatoa maagizo kwa wahusika kutayarisha na kuwasilisha kwenye Bunge, katika kila mwaka wa fedha wa Serikali, makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kipindi cha mwaka wa fedha wa Serikali unaofuata.
(2) Baada ya Bunge kuyakubali makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1), Serikali itawasilisha kwenye Bunge Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali, kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina zitakazogharamia shughuli mbalimbali za Serikali zinazohusu makadirio hayo.
(3) Ikiwa katika mwaka wa fedha wowote inaonekana kwamba:
(a) fedha za matumizi zilizoidhinishwa na Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali kwa ajili ya kugharamia shughuli mahsusi hazitoshi;
(b) imekuwa lazima kulipa gharama za shughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibu wa sheria za nchi;
(c) kuna fedha ambazo zimetumiwa kwa ajili ya shughuli mahsusi kwa kiasi kinachozidi kiwango cha matumizi kilichoidhinishwa na Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali kuhusu shughuli hiyo;
(d) fedha zimetumiwa kulipia gharama za shughuli ambayo haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibu wa sheria za nchi,
kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio ya matumizi ya nyongeza au, kadri itakavyokuwa, maelezo ya matumizi ya ziada, na baada ya Bunge kuyakubali makadirio ya matumizi ya nyongeza au maelezo ya matumizi ya ziada, kutawasilishwa kwenye Bunge Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali au Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Nyongeza ya Fedha za Serikali kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina, na fedha hizo zitagharamia shughuli zinazohusika na makadirio au maelezo hayo.

224.-(1) Iwapo mwaka wa fedha wa Serikali umeanza na Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali inayohusika na mwaka huo haijaanza kutumika, Rais anaweza kuidhinisha fedha zitolewe kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ajili ya kugharamia shughuli za lazima za Serikali, na fedha hizo zitatumiwa ndani ya miezi minne tangu mwanzo wa mwaka wa fedha wa Serikali hadi Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali itakapoanza kutumika, kutegemea na lipi kati ya mambo hayo litatokea mapema zaidi.
 


- 89 -
 



(2) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa kufuata utaratibu ulioelezwa katika ibara ndogo ya (1).


 

Mfuko wa Matumizi ya Dharura.

























Mishahara ya baadhi ya watumishi kudhami-niwa na Mfuko Mkuu wa Hazina.
 
225.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa Matumizi ya Dharura ambao matumizi yake yatawekewa masharti katika sheria za nchi.
(2) Sheria iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1) itaruhusu Rais au Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, pale anaporidhika kuwa kuna:
(a) jambo la haraka na la dharura na ambalo halikutazamiwa kutokea na ambalo halikupangiwa fedha, kuazima fedha kutoka Mfuko wa Matumizi ya Dharura kwa ajili ya kugharamia jambo hilo; au
(b) jambo la haraka na la dharura kama ilivyoelezwa katika aya (a) ya ibara ndogo ya (2), kutumia fedha zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya kugharamia shughuli fulani kulipia gharama za jambo hilo.
(3) Iwapo fedha zimeazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi ya Dharura au fedha zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli fulani zimetumiwa kugharamia jambo la haraka na la dharura, basi kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio ya matumizi ya nyongeza, na baada ya Bunge kuyakubali makadirio hayo Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali utakaowasilishwa kwenye Bunge kwa ajili ya kuidhinisha matumizi hayo utahakikisha kwamba fedha zozote zilizoazimwa kwenye Mfuko wa Matumizi ya Dharura zitarudishwa kwenye Mfuko huo kutoka katika fedha za matumizi yatakayoidhinishwa na Muswada huo.


226.-(1) Watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wanaohusika na masharti ya Ibara hii watalipwa mishahara na posho kama itakavyoelezwa na sheria za nchi.
(2) Fedha za malipo ya mishahara na posho za watumishi wa Serikali wanaohusika na masharti ya Ibara hii pamoja na fedha za malipo ya uzeeni na kiinua mgongo, zitatolewa kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina.
(3) Mshahara anaolipwa mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya Ibara hii pamoja na masharti yake ya kazi havitabadilishwa kwa jinsi ambayo itapunguza maslahi ya mtumishi huyo baada ya kuteuliwa, isipokuwa kwamba masharti haya hayahusiki na posho anayolipwa mtumishi huyo.
(4) Endapo mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya Ibara hii ana hiyari ya kuchagua kima cha mshahara au aina ya masharti ya kazi, basi kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (3), mshahara wa kima hicho atakaochagua na aina hiyo ya masharti ya kazi atakayochagua vitahesabiwa kuwa vina maslahi zaidi kwake kuliko kima cha mshahara kingine chochote ambacho anaweza kuchagua au aina ya masharti ya kazi nyingine yoyote ambayo angeweza kuchagua.
 




- 90 -
 


(5) Masharti ya Ibara hii yatatumika kwa Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu, Jaji wa Mahakama ya Juu, Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na watumishi wengine watakaoainishwa katika sheria za nchi.


(b) Deni la Taifa na Mikopo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano


 

Deni la Taifa.




Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kukopa.














Mamlaka ya Serikali za Nchi Washirika kukopa.
 
227.-(1) Deni la Taifa litadhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina. (2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa Ibara hii, deni la Taifa
litajumuisha deni la Serikali ya Jamhuri ya Muungano pamoja na deni lolote litakalodhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.


228.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya kukopa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kugharamia shughuli zilizo chini ya mamlaka yake.
(2) Bunge linaweza kutunga sheria ambayo:
(a) itaweka masharti ya kuzingatiwa na Serikali wakati wa kukopa; (b) itaweka ukomo wa deni la Taifa na madhumuni ya deni hilo; na (c) itaweka utaratibu wa Serikali kutoa taarifa kwenye Bunge
kuhusu mikopo na deni la Taifa.
(3) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2)(b), taarifa itakayowasilishwa Bungeni pamoja na mambo mengine itaeleza:
(a) kiasi cha deni lililopo na riba yake;
(b) matumizi yaliyofanywa au yatakayofanywa kutokana na fedha za mkopo husika;
(c) utaratibu uliowekwa wa kulipa deni husika; na (d) hatua iliyofikiwa katika kulipa deni husika.


229.-(1) Serikali ya Nchi Mshirika itakuwa na mamlaka ya kukopa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kugharamia shughuli zilizo chini ya mamlaka yake.
(2) Endapo mkopo utahitaji dhamana, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, baada ya kushauriana na kukubaliana na Serikali ya Nchi Mshirika, inaweza kutoa dhamana kwa mkopo unaoombwa.
(3) Bunge litatunga sheria itakayoweka utaratibu wa Serikali kudhamini mikopo ya Serikali za Nchi Washirika.
(4) Katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa mwaka wa fedha wa Serikali, Serikali itachapisha Taarifa katika Gazeti la Serikali itakayoelezea mikopo iliyodhaminiwa na Serikali katika mwaka wa fedha wa Serikali uliopita.
 





- 91 -
 



 

Masharti ya kutoza kodi.
 
230. Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa na mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
 

(c) Vyanzo vya Mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Ununuzi wa Umma


 

Vyanzo vya mapato vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.





Ununuzi wa umma.
 
231. Vyanzo vya mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano vitakuwa:
(a) ushuru wa bidhaa;
(b) mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na taasisi za Muungano; (c) mchango kutoka kwa Nchi Washirika;
(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano; na (e) mapato mengine.


232.-(1) Katika kufanya ununuzi wa umma, Serikali na taasisi zote za umma zitatakiwa kutumia mfumo na utaratibu utakaozingatia haki, uwazi, maslahi ya umma, uwajibikaji, ushindani na thamani halisi ya fedha.
(2) Katika kufanya ununuzi wa umma, Serikali na taasisi zake zitatakiwa kutumia au kuweka mfumo ambao utazingatia kununua bidhaa zinazozalishwa au huduma zinazotolewa nchini kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika Ibara hii na sheria za nchi.
(3) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti ya usimamizi na udhibiti wa manunuzi ya umma.
 


(d) Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano


 
Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano.













Benki za Serikali za Nchi Washirika.
 
233.-(1) Kutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano itakayojulikana kuwa "Benki Kuu" ambayo itakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kutoa sarafu, kudhibiti na kusimamia mzunguko wa sarafu;
(b) kuandaa na kusimamia sera na mipango inayohusiana na sarafu; (c) kudhibiti na kusimamia masuala ya fedha za kigeni; na
(d) kusimamia Benki za Nchi Washirika.
(2) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Benki Kuu itakuwa huru na haitaingiliwa ama kwa kupewa maelekezo au kudhibitiwa na mtu au mamlaka yoyote.
(3) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo wa Benki Kuu utakaozingatia uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano, mamlaka, shughuli na utendaji wa Benki Kuu.


234. Serikali za Nchi Washirika zitakuwa na Benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti ya fedha za Serikali ya Nchi Mshirika husika, kusimamia sera za kifedha na benki za biashara katika mamlaka zao.
 






- 92 -
 


SURA YA KUMI NA TANO
ULINZI NA USALAMA WA JAMHURI YA MUUNGANO


(a) Ulinzi na Usalama wa Taifa

 

Usalama wa Taifa.

















Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Taifa.
 
235.-(1) Jukumu la ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano ni la kila raia.
(2) Usalama wa Jamhuri ya Muungano unahusu ulinzi wa mipaka yote ya eneo la Jamhuri ya Muungano ikiwa ni pamoja na ardhi, anga na bahari kuu, watu wake, mali zao, haki, uhuru na maslahi mengine ya kitaifa dhidi ya vitisho vya ndani na nje ya nchi.
(3) Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano utaimarishwa kulingana na kanuni zifuatazo:
(a) ulinzi na usalama wa Taifa unaongozwa kwa mamlaka ya Katiba hii;
(b) ulinzi na usalama wa Taifa utatekelezwa kwa kuzingatia sheria za nchi na sheria za kimataifa, na kwa kuheshimu kikamilifu utawala wa sheria na haki za binadamu; na
(c) taasisi za ulinzi na usalama wa Taifa zitaheshimu utamaduni wa aina mbalimbali wa jamii katika kutekeleza majukumu yao.


236.-(1) Vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa vitakuwa ni: (a) Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania;
(b) Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano; na (c) Idara ya Usalama wa Taifa.
(2) Wajibu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa na mfumo wa usalama ni kulinda mipaka ya Jamhuri ya Muungano, maslahi ya raia na watu wengine, mali zao, haki na uhuru, mamlaka za nchi, amani na umoja wa kitaifa.
(3) Katika utekelezaji wa majukumu yao, vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa na kila mtumishi wa vyombo hivyo hataruhusiwa -
(a) kuwa na upendeleo kwa njia yoyote;
(b) kuendeleza maslahi ya chama chochote cha siasa au sera zake; (c) kuhujumu maslahi ya kisiasa au mpango wa kisiasa ambao ni
halali chini ya Katiba hii;
(d) kutishia, kudhulumu au kuwatendea ukatili raia na watu wengine; na
(e) kutii amri yoyote isiyokuwa halali.
(4) Mtu hataruhusiwa kuanzisha taasisi, kampuni, jumuiya au shirika linalohusiana na ulinzi na usalama wa Taifa au ushirika wa kijeshi, isipokuwa kama inavyoruhusiwa na Katiba hii au sheria za nchi.
(5) Vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa vitakuwa chini ya mamlaka ya Rais.
(6) Rais anaweza kuunda chombo cha ulinzi na usalama kwa kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.
(7) Bunge litatunga sheria kuweka masharti kuhusu utekelezaji wa majukumu, utaratibu na usimamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa.
 




- 93 -
 


 
Kuanzishwa kwa Baraza la Ulinzi na Usalama
la Taifa.



























Majukumu ya Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.
 
237.-(1) Kutakuwa na Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa litakalokuwa na wajumbe wafuatao -
(a) Makamu wa Rais; (b) Rais wa Tanganyika; (c) Rais wa Zanzibar;
(d) Waziri mwenye dhamana ya ulinzi;
(e) Waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani ya nchi; (f) Waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje;
(g) Waziri mwenye dhamana ya usalama wa taifa; (h) Waziri mwenye dhamana ya fedha;
(i) Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
(j) Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania;
(k) Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa;
(l) Mkuu wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na
(m) Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
(2) Mwenyekiti anaweza kumualika mtu yeyote kushiriki katika kikao cha Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.
(3) Kutakuwa na Sekretarieti ya Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa itakayoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi.
(4) Vikao vya Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa vitaongozwa na Rais.
(5) Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa litaweka utaratibu wa mwenendo wa vikao vyake.
(6) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.


238.-(1) Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa litakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kuunganisha sera za ndani, sera za nchi za nje na za kijeshi kuhusiana na usalama wa Taifa ili kuwezesha taasisi za ulinzi na usalama wa Taifa kushirikiana kikamilifu;
(b) kupokea, kutathmini na kuchunguza taarifa kutoka katika vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Taifa na taasisi za Serikali kuhusiana na usalama wa nchi;
(c) kutoa maelekezo mahsusi kuhusiana na masuala ya ulinzi na usalama wa Taifa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Nchi Washirika na Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Taifa;
(d) kuanzisha sera kuhusu maslahi ya pamoja ya kiusalama ya vyombo vya usalama na kudhibiti usimamizi vyombo hivyo; na
(e) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama Rais atakavyoagiza.
(2) Rais atatoa taarifa kwenye Bunge kila mwaka kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Muungano.
 






- 94 -
 


(b) Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania


 

Kuanzishwa kwa Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.


Uteuzi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.


Madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu.































Tume ya Utumishi ya
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
 
239.-(1) Kutakuwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania litakalokuwa na jukumu la kulinda uhuru na mipaka ya Jamhuri ya Muungano na kusimamia ulinzi na usalama wa wananchi.
(2) Rais anaweza kuanzisha vikosi vingine vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kama atakavyoona inafaa.


240. Kutakuwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ambaye atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.



241.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria za nchi, Rais kwa nafasi ya madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu atakuwa na mamlaka ya kuyaamuru majeshi ya nchi:

(a) kutenda mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya Muungano;
(b) kuokoa maisha na mali za watu katika hali ya hatari;
(c) kusaidia na kushirikiana na mamlaka nyingine wakati wa dharura au maafa;
(d) kusaidia mamlaka au uongozi wa Serikali kutuliza ghasia, fujo au kurejesha hali ya utulivu;
(e) kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika ulinzi wa amani pale itakapoonekana inafaa; na
(f) kutenda mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu ataona inahitajika,
na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu anaweza kuyaamuru majeshi hayo yatekeleze mambo hayo ndani au nje ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Katika utekelezaji wa masharti ya Ibara hii na kwa kuzingatia sheria za nchi, madaraka juu ya mambo yafuatayo yatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu -
(a) kuwateua viongozi katika majeshi ya ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(b) kuwateua wanajeshi watakaoongoza vikosi mbali mbali vya majeshi ya ulinzi;
(c) kumwamuru mwanajeshi yeyote asitumie madaraka yoyote aliyokabidhiwa na ambayo yanaambatana na kuwa kwake mwanajeshi; na
(d) kulinda uhuru na mipaka ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii, jambo lolote atakalotenda mwanajeshi kinyume cha amri ya Amiri Jeshi Mkuu litakuwa batili.


242.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo, majukumu na mambo mengine yanayohusu Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
 




- 95 -
 


(c) Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano


 

Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano




Misingi ya utendaji wa Jeshi la Polisi.









Uteuzi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi.


Uhuru wa Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi.
 
243.-(1) Kutakuwa na Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litakalokuwa na jukumu la ulinzi na usalama wa watu na mali zao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya utekelezaji wa kazi na majukumu ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia haki za kiraia na sheria za kimataifa.


244.-(1) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litazingatia -
(a) viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake;
(b) ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu; (c) kanuni za uwazi na uwajibikaji; na
(d) kukuza mahusiano na jamii.
(2) Jeshi la Polisi, katika kutekeleza majukumu yake, litashirikiana na vyombo vinavyohusika na kupambana na uhalifu vya Nchi Washirika katika kufanya uchunguzi na kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi.


245. Kutakuwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano ambaye atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa.


246. Mkuu wa Jeshi la Polisi atatekeleza kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi.


247.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itakayokuwa na jukumu la kusimamia utumishi wa Jeshi la Polisi.
(2) Katika uajiri wa askari wa Jeshi la Polisi, Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itazingatia kanuni na misingi ya utumishi iliyoainishwa katika Katiba hii.
(3) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya muundo na utekelezaji wa kazi na majukumu ya Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi.
 


(d) Idara ya Usalama wa Taifa ya Jamhuri ya Muungano

 

Kuanzish-wa kwa Idara ya Usalama wa Taifa.




Uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.
 
248.-(1) Kutakuwa na Idara ya Usalama wa Taifa ya Jamhuri ya Muungano itakayoitwa "Idara ya Usalama wa Taifa".
(2) Idara ya Usalama wa Taifa itahusika na shughuli za kuimarisha usalama wa Jamhuri ya Muungano na kulinda Katiba hii, maslahi ya Taifa na ya watu wake na itatekeleza majukumu mengine kama yatakavyoainishwa na sheria za nchi.


249. Rais atamteua Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa baada ya kushauriana na Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa.
 



- 96 -
 


 

Usalama katika Nchi Washirika.
 
250.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sura hii, Wakuu wa Nchi Washirika wanaweza kumuagiza kiongozi yeyote wa Jeshi la Polisi au Idara ya Usalama wa Taifa kuchukua hatua yoyote ambayo ni muhimu kwa ajili ya kulinda au kuimarisha usalama wa eneo lolote la Nchi Mshirika husika.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoainisha masharti yanayohusu namna bora ya utekelezaji wa ibara ndogo ya (1).
 


SURA YA KUMI NA SITA MENGINEYO


 

Utaratibu wa kujiuzulu katika Utumishi wa Umma.





























Masharti kuhusu kukabidhi madaraka.
 
251.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii anaweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiwa saini kwa mkono wake, kwa kufuata masharti yafuatayo:
(a) iwapo mtu huyo aliteuliwa au kuchaguliwa na mtu mmoja, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa mtu huyo aliyemteua au aliyemchagua, au iwapo aliteuliwa au kuchaguliwa na kikao cha watu, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye kikao hicho;
(b) iwapo mtu huyo ni Rais, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika;
(c) iwapo mtu huyo ni Makamu wa Rais, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Rais;
(d) iwapo mtu huyo ni Spika au Naibu Spika wa Bunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwenye Bunge; na
(e) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika.
(2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (1), atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku ile ambayo taarifa yake ya kujiuzulu itakapopokelewa na mtu anayehusika au kikao kinachohusika au itakapopokelewa na mtu yeyote aliyeruhusiwa kuipokea taarifa hiyo na mtu anayehusika au kikao kinachohusika, lakini kama taarifa hiyo ya kujiuzulu imeeleza kwamba mtu huyo atajiuzulu tangu siku nyingine baada ya taarifa hiyo kupokelewa na mtu anayehusika au kikao kinachohusika, basi mtu huyo atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku hiyo nyingine ya baadaye.
(3) Endapo mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii amejiuzulu, ikiwa anazo sifa zote zinazohitajika na kwa kila hali anastahili, anaweza kuteuliwa au kuchaguliwa tena kushika madaraka ya kazi hiyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.


252.-(1) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya Katiba hii kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, mtu yeyote mwenye mamlaka, kwa mujibu wa Katiba hii, ya kumteua mtu mwingine kushika madaraka pia atakuwa na uwezo wa kumteua kaimu au mtu ambaye atashika kwa muda na kutekeleza madaraka hayo.
(2) Kanuni zifuatazo zitatumika pia kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya Katiba hii kuhusu utaratibu wa kukabidhiana madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano:
 



- 97 -
 


(a) iwapo kuna mtu mwenye madaraka aliyokabidhiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na mtu huyo yupo likizo na wakati huo huo anasubiri kuacha madaraka hayo, basi anaweza kuteuliwa mtu mwingine na kukabidhiwa madaraka hayo, bila ya kujali kuwepo kwa yule mtu anayesubiri kuacha madaraka hayo;
(b) iwapo kuna watu wawili au zaidi ambao kwa wakati mmoja wote wanashika madaraka kutokana na uteuzi wao uliofanywa kwa mujibu wa Kanuni iliyoelezwa katika aya ya (a), basi katika hali hiyo kukitokea umuhimu wa kutekeleza shughuli yoyote inayohusika na madaraka hayo yule mtu wa mwisho kuteuliwa ndiye atakayehesabiwa kuwa mtu pekee mwenye dhamana ya madaraka hayo; na
(c) iwapo mtu ameteuliwa, kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, kuwa kaimu au kushikilia madaraka wakati mtu aliyeteuliwa kushika nafasi ya madaraka hayo ameshindwa kutekeleza shughuli zinazohusika na madaraka hayo, basi haitaruhusiwa kufanya uchunguzi wowote au kutoa hoja yoyote juu ya uteuzi wa huyo kaimu kwa sababu mtu aliyeteuliwa kushika nafasi ya madaraka hayo ameshindwa kutelekeza shughuli zinazohusika na mmadaraka hayo.


 

Baadhi ya watumishi wa umma kutoshika nafasi za kisiasa.
 
253.-(1) Watumishi wafuatao hawatakuwa na haki ya kugombea, kuchaguliwa au kuteuliwa katika nafasi ya kisiasa hadi utakapopita muda wa miaka mitatu tokea kuacha au kustaafu nafasi ya madaraka aliyokuwa akiishikilia:
(a) Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Jaji wa Mahakama ya Juu wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano; (d) Spika na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; (e) Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama;
(f) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(g) Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano; (h) Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na
(i) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Uchaguzi;
(j) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu;
(k) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji;
(l) Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma; (m) Msajili wa Vyama vya Siasa.
(2) Bunge linaweza kutunga sheria kuhusu aina nyingine ya watumishi wa umma ambao hawataruhusiwa kushika nafasi za madaraka ya kisiasa kwa mujibu wa Ibara hii.
 




- 98 -
 


Ufafanuzi. 254.-(1) Katika Katiba hii, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo: "chama cha siasa" maana yake ni chama cha siasa kilichoandikishwa kwa
mujibu wa sheria za nchi;
"Jamhuri ya Muungano" maana yake ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
"Jaji Mkuu" maana yake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano;
"Jeshi" maana yake ni Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano pamoja na chombo chochote kilichoundwa kwa mujibu wa Katiba hii au sheria za nchi na kinachotawaliwa kwa amri ya jeshi;
"nafasi ya madaraka" maana yake ni wadhifa, cheo, hadhi, madaraka ya uongozi au mamlaka ya utendaji katika utumishi wa umma;
"Mahakama" maana yake ni Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani; "Mahakama Kuu" maana yake ni Mahakama Kuu za Nchi Washirika; "mtumishi wa umma" maana yake ni mtu aliyeajiriwa katika Utumishi wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Utumishi wa Mahakama, Utumishi wa Bunge, wakala wa Serikali, utumishi katika taasisi zinazojitegemea ambazo zinafanya kazi za Serikali au zinazomilikiwa na Serikali isipokuwa haitajumuisha utumishi wa kisiasa;
"Mwanasheria Mkuu" maaana yake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
"Naibu Waziri" maana yake ni mtu aliyeteuliwa na kukabidhiwa madaraka ya kazi ya Naibu Waziri;
"Nchi Washirika" maana yake ni Tanganyika na Zanzibar;
"Serikali" maana yake ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na mtu yeyote anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali;
"Uchaguzi Mkuu" maana yake ni uchaguzi wa Rais na uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi unaofanywa baada ya Bunge kumaliza muda wake;
"Waziri" maana yake ni mtu aliyeteuliwa kushika nafasi ya madaraka ya Waziri na wadhifa wa "Naibu Waziri" utatafsiriwa kwa muktadha huo"
"Waziri Mwandamizi" maana yake ni mtu aliyeteuliwa kushika nafasi ya madaraka ya Waziri Mwandamizi kwa mujibu wa Katiba hii;
"Waziri Mkaazi" maana yake ni Waziri aliyeteuliwa na Serikali ya Nchi Mshirika kushika nafasi ya madaraka ya Waziri Mkaazi;
(2) Kanuni zifuatazo zitatumika kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya Katiba hii:
(a) kila yanapotajwa madaraka ya Rais, ifahamike kuwa madaraka yanayohusika ni pamoja na mamlaka ya kutekeleza shughuli za kazi mbalimbali na vile vile wajibu wa kutekeleza shughuli na kazi mbali mbali kama Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na pia mamlaka mengine kama hayo au wajibu mwingine kama huo ikiwa imeelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote kwamba mamlaka hayo mengine ni ya Rais au kwamba wajibu huo mwingine ni wa Rais;
(b) kila yanapotajwa madaraka ya kazi katika utumishi wa Serikali, ifahamike kuwa kazi inayohusika ni kazi katika Utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Mungano isipokuwa kama imeelezwa


- 99 -
 


vingine, na kila inapotajwa Idara ya Serikali ifahamike kuwa idara inayohusika ni idara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa kama imeelezwa vingine;
(c) iwapo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii kuna jambo lolote linalotakiwa litekelezwe au lishughulikiwe na chama chochote cha siasa, basi, jambo hilo litatekelezwa au litashughulikiwa na chama hicho kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na chama hicho kwa ajili hiyo, na pia kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii au sheria ya nchi iliyotungwa kwa ajili hiyo;
(d) mtu hatahesabiwa kuwa ana madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa sababu tu kwamba anapokea malipo ya uzeeni au malipo mengine ya aina hiyo kwa ajili ya utumishi wake wa zamani katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya zamani ya Zanzibar, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano na Idara ya Usalama wa Taifa au;
(e) isipokuwa kama muktadha utaelekeza vinginevyo, kila anapotajwa mtu mwenye dhamana ya madaraka kwa kutaja madaraka yake, mtu anayehusika atakuwa ni pamoja na mtu yeyote ambaye ni Kaimu au aliyeteuliwa kihalali kushikilia dhamana ya madaraka hayo;
(f) kila yalipotajwa mamlaka ya kumwondoa mtu katika nafasi ya madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, mamlaka yanayohusika ni pamoja na mamlaka yaliyotolewa kwa mujibu wa masharti ya sheria yoyote yanayomtaka mtu huyo au yanayomruhusu mtu huyo kustaafu:
Isipokuwa kwamba masharti haya hayatamhusu Jaji wa Mahakama ya Juu, Jaji wa Mahakama ya Rufani au Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; na
(g) kila ilipotajwa sheria ambayo inabadilisha au kufuta sheria nyingine, ifahamike kuwa sheria inayohusika ni pamoja na sheria ambayo inarekebisha sheria hiyo nyingine au ambayo inaendeleza kutumika kwa hiyo sheria nyingine, ama bila mabadiliko au baada ya kubadilishwa au kurekebishwa; au sheria ambayo inaweka masharti mapya katika sheria nyingine.


 
Jina la Katiba na kuanza kutumika.



Kufutwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Sura ya 2.
 
255.-(1) Katiba hii itaitwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.
(2) Katiba hii itaanza kutumika itakapozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


256. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inafutwa na, isipokuwa kwa masuala yaliyoelekezwa katika Masharti Yatokanayo, Masharti ya Mpito na Masharti ya Muda, haitakuwa na nguvu ya kisheria mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii.
 





- 100 -
 


SURA YA KUMI NA SABA

MASHARTI YATOKANAYO NA MASHARTI YA MPITO

SEHEMU YA KWANZA

MASHARTI YATOKANAYO

 

Matumizi ya baadhi ya masharti ya katiba
Sura ya 2.
 
257.-(1) Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito yaliyoainishwa katika Sura hii ya Katiba yataanza kutumika tarehe ambayo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 itakapoanza kutumika.
(2) Kwa kuondoa shaka, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 itakuwa imefutwa na, isipokuwa kwa masuala yaliyoainishwa katika Sehemu ya Pili ya Sura hii, haitakuwa na nguvu ya sheria kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.
 


SEHEMU YA PILI

MASHARTI YA KIKATIBA NA SHERIA ZA NCHI


 

Kuendelea kutumika masharti ya Katiba.











Kuendelea kutumika sheria za nchi.
 
258.-(1) Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito katika Sura hii ya Katiba na yale yaliyowekwa katika Mabadiliko ya "Sheria Maalum" ambayo bado yanaendelea kutumika katika Katiba zilizoainishwa katika Ibara hii, yataendelea kutumika.
(2) Kwa madhumuni ya Ibara hii, "Sheria Maalum" maana yake ni "the Republic of Tanganyika (Consequential, Transitional and Temporary Provisions) Act, 1962, the Interim Constitution (Consequential, Transition and Temporary Provisions) Act, 1965, the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary Provisions) Act, 1977, the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary Provisions) Act, 1984 na "the Constitution (Consequential, Transitional and Temporary Provisions) Act, 1992".


259.-(1) Masharti ya sheria zilizoainishwa katika ibara ndogo ya (2) na ambazo zinatumika kabla ya tarehe ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 zitaendelea kutumika kwa namna ambayo imeelekezwa katika Ibara hii.
(2) Sheria za nchi ambazo:
(a) zimetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 zitaendelea kutumika kwa madhumuni ya masuala yaliyoelekezwa katika sheria hizo; na
(b) zimetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania Bara zitaendelea kutumika Tanganyika kwa madhumuni ya masuala yaliyoelekezwa katika sheria hizo.
(3) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (2) wakati na baada ya Muda wa Mpito:
(a) sheria zote zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania Bara na Zanzibar na kwa kuzingatia marekebisho yatakayohitajika, zitakuwa sheria za nchi ambazo zitatumika katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano;
 


- 101 -
 


(b) kwa kuzingatia mgawanyo wa Mambo ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano yaliyoelekezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014, sheria zote zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania Bara na Zanzibar, kwa kuzingatia marekebisho yatakayohitajika, zitatumika Tanganyika na Zanzibar kwa mambo yasiyo ya Muungano hadi hapo Tanganyika au Zanzibar itakapotunga sheria kuhusu mambo hayo; na
(c) sheria zote zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambazo zinatumika Tanzania Bara na kwa kuzingatia marekebisho yatakayohitajika, zitakuwa sheria za nchi ambazo zitatumika Tanganyika.
(4) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (3), Bunge la Jamhuri ya Muungano linaweza kutunga sheria yoyote kuhusu mambo ya Muungano na mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanganyika hadi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakapoundwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.


SEHEMU YA TATU

UTUMISHI WA UMMA

(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano

 

Kuendelea kuwepo kwa Rais madarakani.




Kuendelea kuwepo kwa Makamu wa Rais madarakani.



Kuendelea kwa Waziri Mkuu, Mawaziri na Naibu Mawaziri.







Kuendelea kwa utumishi wa umma.
 
260. Mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, ataendelea kushika nafasi ya madaraka ya Rais kwa masharti ya Katiba hii hadi mtu mwingine atakapochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kushika nafasi ya madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.


261. Mtu aliyekuwa anashika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, ataendelea kushika nafasi ya madaraka ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa masharti ya Katiba hii hadi Rais wa Jamhuri ya Muungano atakapochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.


262.-(1) Mtu anayeshika nafasi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ataendelea kuwa katika nafasi ya madaraka hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 utakapofanyika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshika madaraka.
(2) Mtu anayeshika nafasi ya madaraka ya Waziri au Naibu Waziri ataendelea kushika nafasi hiyo ya madaraka hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 utakapofanyika na nafasi hiyo ya madaraka itakoma saa ishirini na nne kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuapishwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais.
(b) Watumishi wa Umma

263.-(1) Kila mtu aliyeshika au kukaimu nafasi ya madaraka ya utumishi wa umma katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano au Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano kabla ya tarehe ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
 


- 102 -
 


2014, ataendelea na atatambuliwa kuwa amechaguliwa, kuteuliwa au kuajiriwa kushika au kukaimu nafasi ya madaraka ya utumishi wa umma katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano au Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na kwamba masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014 au sheria za nchi kuhusiana na kuchaguliwa, uteuzi, ajira na kula kiapo au yamini yamezingatiwa na kutekelezwa.
(2) Kila mtu ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 au sheria za nchi, atahitajika kuondoka katika nafasi ya madaraka baada ya muda maalum kupita au atakapotimiza umri wa
Sura ya 2 kustaafu ataacha kushika nafasi ya madaraka katika utumishi wa umma baada ya kufika mwisho wa muda maalum au atakapofika umri wa kustaafu.
(3) Masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2), hayatatafsiriwa kwamba yanaondoa au kufifisha madaraka aliyonayo mtu au mamlaka imepewa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 au sheria za nchi kufuta nafasi ya madaraka na kumvua madaraka au kumwachisha kazi mtu anayeshika au kukaimu nafasi ya madaraka au kumtaka mtumishi wa umma kujiuzulu.
(4) Kwa madhumuni ya malipo ya kiinua mgongo au malipo mengine ya uzeeni, muda wa utumishi wa mtumishi wa umma anayehusika na masharti ya Ibara hii, utahesabika kuwa ni pamoja na muda wa utumishi aliokuwa nao kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.
(5) Isipokuwa kama itaelekezwa vinginevyo, masharti ya kazi ya mtumishi wa umma ambaye masharti ya Ibara hii yanamhusu hayatakuwa duni au hafifu ukiliganisha na masharti ya kazi aliyokuwa nayo kabla ya kuanza kutumika kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 au sheria za nchi zitakazotungwa kwa ajili hiyo.


SEHEMU YA NNE
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO


 

Kuendelea kwa Ubunge na Uongozi wa Bunge.




Sura ya 2 na 343





Kuvunjwa kwa Bunge.

Sura ya 2
 
264.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (2) na sheria za nchi kuhusu masuala ya uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na uchaguzi wa Spika, Naibu Spika na Viongozi wa Kamati za Bunge, Spika, Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge na Wabunge wataendelea kuwa Spika, Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge na Wabunge, hadi Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
(2) Masharti ya Ibara ndogo ya (1) hayatatafsiriwa kwamba yanazuia kuondolewa kwa Spika, Naibu Spika, Viongozi wa Kamati za Bunge au Mbunge, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, Sheria ya Uchaguzi wa Taifa na Kanuni za Kudumu za Bunge.


265.-(1) Endapo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 au sheria za nchi, jambo au suala lolote linahitaji kufanyika au linaweza kufanyika, jambo au suala hilo linaweza kufanyika kutokana au kufuatia kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(2) Ikiwa umuhimu wa kuliitisha Bunge utatokea kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu ambao utafanyika baada ya kuvunjwa Bunge la Jamhuri ya Muungano:
 

- 103 -
 


 
(a)





Sura ya 2 (b)
 
kwa madhumuni ya kuliitisha Bunge, Spika, Naibu Spika na Wabunge waliochaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, sheria za nchi na Kanuni za Bunge wanaweza kuitwa na watakuwa Spika, Naibu Spika na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano litakaloitishwa;
kwa madhumuni ya uteuzi katika nafasi ya madaraka wakati Bunge limevunjwa, mtu anayeweza kuteuliwa sharti awe Mbunge, uteuzi unaweza kufanywa wa mtu ambaye alikuwa Mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria za nchi zinazohusika.
 

SEHEMU YA TANO

MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO

 

Kuendelea kwa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu.

Sura ya 2




Kuendelea kwa mashauri yaliyopo Mahakamani.

Sura ya 2
 
266.-(1) Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Kuu ya Tanzania Bara zitaendelea na zitakuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri na kutoa uamuzi au amri kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na sheria za nchi.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu watakuwa na madaraka ya kusikiliza mashauri, kutoa hukumu au amri kutokana na mashauri yaliyofunguliwa au yatakayofunguliwa katika Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu.


267.-(1) Shauri lolote ambalo halijakamilika au limekamilika katika Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu litaendelea kusikilizwa hadi kukamilika; na hukumu, hati ya kukazia hukumu na amri iliyotolewa au itakayotolewa katika shauri hilo inaweza kutolewa na kutekelezwa na Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), kila hukumu, hati ya kukazia hukumu na amri iliyotolewa na Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu ambayo haijatekelezwa kikamilifu kabla ya kufutwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaweza kutekelezwa kikamilifu baada ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.
(3) Uamuzi wowote wa Mahakama ya Rufani uliotolewa kuhusu shauri lolote lililofunguliwa kabla ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014, hautakatiwa rufani katika Mahakama ya Juu.
 


SEHEMU YA SITA MASHARTI YA MPITO

 

Muda wa Mpito.



Utekelezaji wa masharti ya Katiba Mpya.
 
268. Muda wa Mpito utakuwa muda wote kuanzia tarehe ya kuanza kutumika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 hadi tarehe 31 Disemba, 2018.


269.-(1) Mambo yafuatayo yatafanyika na kukamilika katika Muda wa Mpito:
(a) kutungwa kwa Katiba ya Tanganyika;
 


- 104 -
 


(b) kurekebisha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ili kuwiana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014;
(c) mgawanyo wa rasilimali baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika;
(d) kutunga na kurekebisha sheria mbalimbali za Nchi Washirika ili kuwiana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014;
(e) mgawanyo wa watumishi wa umma baina ya Serikali za Muungano na Serikali za Nchi Washirika;
(f) mgawanyo wa madeni baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Nchi Washirika;
(g) kuundwa kwa Tume na taasisi za kikatiba zilizoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 na kwa kuzingatia masharti ya Katiba hiyo;
(h) kufanya uteuzi katika nafasi za madaraka kwa utaratibu ulioainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014;
(i) kufanya maandalizi na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014; na
(j) kufanya maandalizi na mambo yote muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.
(2) Maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba yaliyotumika kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014 yanaweza kutumika katika kuandika Rasimu ya Katiba ya Tanganyika.


 

Kamati ya kusimamia muda wa Mpito.













Kufutwa kwa Masharti Yatokanayo na Masharti ya Mpito.
 
270.-(1) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa masuala yanayohitaji kufanyiwa kazi na kukamilishwa katika Muda wa Mpito, Rais atateua Kamati ya Utekelezaji wa Katiba katika Muda wa Mpito.

(2) Kamati ya Utekelezaji wa Katiba itakuwa na: (a) Mwenyekiti; na
(b) Wajumbe wengine wanane.

(3) Sekretarieti ya Kamati ya Utekelezaji itaongozwa na Katibu na itakuwa na watumishi wa idadi inayotosha katika utekelezaji wa kazi ya kamati kwa ufanisi.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti, Wajumbe na watumishi wa sekretarieti utazingatia uwakilishi wa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.


271. Baada ya kumalizika kwa Muda wa Mpito, masharti ya Sura ya Kumi na Saba yatakoma na hayatakuwa na nguvu ya kisheria.
 





- 105 -
 

________________


NYONGEZA [Imetajwa katika Ibara ya 63]
Mambo ya Muungano ________________


1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 3. Uraia na Uhamiaji.
4. Sarafu na Benki Kuu. 5. Mambo ya Nje.
6. Usajili wa Vyama vya Siasa.
7. Ushuru wa Bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.


On Monday, December 30, 2013 6:13:44 PM UTC+3, soleapril26 wrote:

Asante Mwinjilisti Mndeme

On Dec 31, 2013 1:30 AM, "Mathew Mndeme" <mathew...@gmail.com> wrote:
Pakua Kiambatanisho

MM

--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment