Monday 30 December 2013

[wanabidii] Re: Tembo wanazid kuuwawa?


Nimesikikia Mheshimiwa Nyalandu... Hii hali inasiktisha kwamba pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali tunazidi kupoteza uhai wa mali asili na na maisha ya watu. Maana yake ni kwamba sisi Watanzania tumekubali kushindwa kuzuia maovu kutendeka katika hali ya kawaida, hadi tuwe na "Operesheni". Sipingi umuhimu wa kuwa na operesheni, lakini katika mazingira ya sasa sidhani kama inaweza kuwa suluhu ya kudumu. Hapa tunatakiwa kujitathimi kizalend, kimaadili..... na uchungu wa nchi na maisha ya watu. Siamini kwamba wanaongiza mifugo katika hifadhi hawajulikani kwa wananchi na viongozi wa vijiji husika. Hapa kuna uzembe au makusudi tu. Watu wanaoweka kambi ya ujangili katika hifadhi hawatoki nje ya nchi yetu na kama hivyo ndivyo kuna ushirika au ubia na watu wa ndani.. na wanajulikana  kwa viongozi wa ngazi husika.
 
Nionaavyo mimi yanayotokea katika hifadhi zetu, ambayo yamepelekea Mawaziri 4 kufikwa na mgogoro wa kiuongozi ni dalili tu za kushindwa kwa mfumo mzima wa utawala wa uwajibikaji. Udhaifu uko zaidi katika ngazi za usimamizi. Maovu  na mauaji ya aina hii yanafanyika katika kila sekta, ila tu hayajafumuka kama haya yaliyoundiwa tume.  Maana yake ni kwamba serikali haitaweza kuanzisha operesheni kila sekta na kuunda tume za kuchunguza umakini wa hizo operesheni. Tunahitaji watu wachache tu waliopewa dhamana ya kusimamia amani, usalama na utulivu wa nhci kuanzia ngazi ya vijiji/mitaa na hata taifa, na tena bila gharama  kukubali kuwa sasa imetosha. Wajitoe kusimamia na kuzuia maovu haya ya watu wachache wenye uchu na choyo kwa dhati na nidhamu, hata kama italazimu wao kuwa wahanga wa matendo yao.  
 
Mheshemiwa  Raisi, Kama ilivyokuwa katika hadithi ya Kalumekenge, angalia safu yako tena bila woga na umpate shujaa wa kushika kisu cha kumchinja mbuzi ili anywe maji, maji yazime moto na moto uchome fimbo na fimbo imchape kalumekenge apate kwenda shule.
 
Mungu Inusuru Tanzania
 
 
----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam,
TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256

0 comments:

Post a Comment