Kuna matangazo mengi sasa ya radioni yanayoonyesha kuwa kuna kitu kinachoitwa Islamic Banking (account na ATM) katika Bank ya NBC. Nafikiri maana ya Islamic account na ATM ni mfumo ambao hauzingatii utozaji riba kama imani ya kiislm inavyosema. Najiuliza maswali mengi,mfano,kama NBC wanaona hilo la kutotoza riba linafaa,ni mtanzania gani asiyependa kupewa huduma bure au kupata mikopo isiyo na riba?Na kama hilo linawezekana si waondoe riba na tozo kwa watu wote.Na kama haliwezekani,je mzigo wa gharama za uendeshaji account nani anaubeba?. Binafsi kwa uelewa wangu huo mdogo sifurahishwi na kitu kama hicho ndani ya Bank ya kitaifa kama ya NBC. Hizi taasisi zinazobeba watu wengi sidhani kama ni busara hata kidogo kuanza kuweka vitu ambavyo mwisho wa siku vitaishia kutugawa tu wa Tanzania. Nimeshawasikia si chini ya watu 10 ambao wamesema wanachukizwa na jambo hilo na wako tayari kufunga account zao NBC. Tunaomba maoni kama kuna mtu mwenye uelewa zaidi....na kama vipi tujue Bank hiyo ishaingiliwa na nini kifanyike. Godfrey Ngupula
0 comments:
Post a Comment