Wednesday, 3 July 2013

Re: [Mabadiliko] Re: [wanabidii] Angalia Tofauti Hii KUBWA Kati Ya Marekani Na Tanzania...!

sikumbuki bush kuwahi kugombea na obama, sasa waasuguane kwa lipi Maggid? bush alipiga ya minane, kaondoka kulingana na katiba yao


2013/7/3 Patty <magubira@gmail.com>
Duuu, shikamoo Makene! Pokea            usiogope, ni heshima tu tokana
na uchambuzi wako. nimeukubali!

On 03/07/2013, Tumaini Makene <makene_84@yahoo.com> wrote:
>
> Maggid
>
> I have my reservations.
>
> Kwa miaka kadhaa sasa, hasa kabla (kidogo), wakati na baada ya uchaguzi mkuu
> wa mwaka 2010, nafikiri nimekuwa nikimsoma Maggid Mjengwa mwingine, si yule
> niliyekuwa nikimsoma, nikimwelewa, wakati niko shule ya msingi, nikiiba
> shilingi 200 kununua nakala ya Gazeti la RAI la enzi za miaka ya 90 hadi
> mapema 2006 hivi.
>
> Huyu wa sasa, ni Maggid Mjengwa mwingine. Si yule. Maggid wa sasa anafikiria
> siasa ni uchaguzi na uchaguzi ni siasa. Ni kujifungu kwenye boksi la
> 'demokrasia ya uchaguzi'. Uchaguzi ukiisha, watu warudi wafanye kazi, as if
> wakati wa uchaguzi wanakuwa mapumzikoni. Uchaguzi si kazi.
>
> Maggid wa sasa, anakubaliana na maoni ya Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama,
> ambaye amenukuliwa kwenye Ripoti ya Kamati ya Nchimbi juu ya kifo cha Daudi
> Mwangosi, akisema hivi;
>
> "Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama, alishauri kufanyiwa marekebisho kwenye
> sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya mwaka 1992 itakayoweka wazi shughuli za
> vyama vya siasa baada ya Uchaguzi Mkuu. Alisisitiza kuwa shughuli za siasa
> baada ya Uchaguzi Mkuu zihamie bungeni kwa wanasiasa kuhoji mipango ya
> maendeleo ya serikali na matumizi ya rasilimali za nchi na wananchi waachwe
> wachape kazi zao za maendeleo."
>
> Mawazo ya ajabu kweli kweli. Ndiyo mawazo ambayo CCM kupitia kwa Msajili wa
> Vyama, John Tendwa (anakalia ofisi kinyume cha sheria) wanataka kuyatungia
> sheria. Kudhibiti siasa. Wanataka kudhibiti maisha ya kila siku ya
> mwanadamu. Pamoja na uajabu wake, yanatupeleka kwenye nadharia ya siasa
> (siasa ni nini?) kama inavyozungumziwa na Plato kwenye kazi yake ya 'The
> Republic'. Naam what is politics?
>
> Maggid wa sasa ni yule anayeweza kuandika such a generalized argument
> "kelele za vyama", kama ninavyoweza kumnukuu kwa kirefu hapa chini!
>
> "Kwa kweli ujio wa Obama umetusaidia Watanzania kupumzika na kelele za
> vyama, maana, kwa siku kadhaa, kabla na wakati wa ujio wa Obama, Watanzania
> tumepata kupumzika na kusikia habari za vyama vya siasa na malumbano yasio
> na hoja za msingi, mara nyingi yasio na tija kwa nchi na maendeleo yake.
>
> "Picha hiyo hapo juu ina mengi ya kutufundisha; kuwa siasa si uhasama.
> Uchaguzi ukiisha watu mnarudi kwenye kufanya kazi. Kupigania maslahi ya
> taifa. Si kuendeleza migogoro ya kisiasa na hata kuwepo kwa vurugu. Hayo
> hayana tija kwa nchi."
>
> Wakati Obama fever ikiingia, nchi nzima ilikuwa na kelele fever juu ya
> mauaji na majeruhi yaliyotokea kwenye mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa
> hadhara wa CHADEMA, kwako kuzungumzia 'mjadala' wa nani kahusika, wengine
> wanasema CHADEMA wamejilipua, wengine wanahoji mbona serikali ya CCM inahofu
> sana kila inapotakiwa kuunda tume huru ya kijaji/kimahakama kumaliza kadhia
> za namna hii, kwa nini polisi wanafanya operesheni ya 'kuficha' ushahidi wa
> bomu la Arusha, badala ya kupata wahusika, ni kelele za vyama hizo.
> Tupumzike nazo, au siyo!
>
> Kabla ya Obama fever, tulikuwa na by election fever. Uchaguzi wa madiwani
> kata 26, maeneo mbalimbali ya nchi. Moja ya chaguzi za hovyo kabisa kuwahi
> kufanyika. Watu wamepigwa mapanga, watu wamepigwa mashoka, watu wamepigwa
> kwenye vituo vya kura, mbele ya polisi.  Watu wametekwa nyara na kuwekewa
> chupa sehemu ya haja kubwa. Vijana, akina baba, akina mama, wametekwa na
> kuteswa, kwa amri ya viongozi wa serikali na chama tawala, wakiwemo wabunge.
> Hadharani. na ushahidi upo.
>
> Polisi wamepelekewa mashtaka, hakuna hatua wanayochukua. Hayo ni makelele ya
> vyama vya siasa. Tumpumzike nayo!
>
> Kabla ya Obama fever, tulikuwa na bajeti fever. Mahali ambapo wananchi
> wameenda kuongezewa ukali wa maisha, kwa serikali kuendelea kuwatoza na
> kuwakamua kodi zisizo na idadi Watanzania maskini, huku wakubwa wakiachwa na
> misamaha ya kodi inayofikia takriban asilimia 2 ya pato la taifa. Bajeti
> imepingwa hadharani, lakini hayo ni makelele ya vyama. Tumpuzike nayo!
>
> Bodaboda na bajaji ni politics kwa sasa utake usitake Maggid. Serikali ya
> CCM ikaamua kucheza mchezo kama ilivyo ada. Inasema imewaondolea kodi ili
> wapate nafuu! Uongo.
>
> Homa ya mijadala ya ufisadi haijawahi kupoa tangu ilipofumuliwa kwa kasi
> kubwa mwaka 2007 pale Mwembeyanga, List of Shame. Watawala wameendelea
> kukawapua na kuchukua. Tunaendelea kushuhudia Primitive Accumulation of
> Capital, ambayo si kwamba inahusisha tu plundering and looting, bali kupiga
> na kuua watu wetu hadharani (kama Nyamongo, Mtwara na kwingineko ambako
> ardhi inapiganiwa), sasa tumefika hadi awamu ya mabilioni ya Uswisi! Je hizi
> ni kelele za vyama vya siasa? Tupumzike nazo.
>
> Watapata wapi nafuu wakati bei ya mafuta ya petroli na diseli, imepandishwa!
> Wapi umeona mafuta yanapandishwa kisha maisha yanabaki bile yalivyokuwa,
> gharama za vitu vingine visipande. Kwani si watalazimika kuongeza nauli,
> atakayelipa nauli ni nani? Je abiria wangapi watamudu kulipa nauli mpya? Je
> mwendesha boda boda au bajaji sasa atalazimika kufanya nini kwa sababu
> hesabu ya bosi wake (ambaye kiuhalisia ndiye kapewa msamaha, si mwendeshaji)
> iko pale pale? Huu ni mfano mdogo tu. Hizi ni kelele za vyama, tumpuzike
> nazo, au siyo Maggid.
>
> Kabla ya Obama fever, ambayo Maggid umejitahidi kweli kweli kuipatia postive
> coverage kadri ya uwezo wako wote (sijasema ni vibaya) tulikuwa na homa
> nyingine kali na bado inaendelea, Mtwara fever, kuna makelele kweli kweli
> juu ya hali inayoendelea Mtwara. Govt against its own people! When the state
> arsons...torturing, brutalizing, with serious allegations of raping, hukan
> being and natural resources, not listening. Hayo ni makelele ya vyama vya
> siasa, tumpuzike nayo.
>
> Lakini kama hiyo haitoshi, kabla ya Obama fever, tulikuwa na homa nyingine
> kali zaidi, Katiba Mpya. Yapo makelele mengi kweli kweli katika jambo hili
> nyeti. Lakini nayo inaonekana ni kelele za vyama vya siasa, tumpumzike nazo,
> au siyo!
>
> Tangu uchaguzi mkuu, kumekuwa na makelele mengi kweli kweli ya vyama vya
> siasa. Ni makelele hayo (ikiwemo yale ya kumsusia Rais Kikwete wakati
> akizindua bunge na kutaka uchunguzi huru wa uchaguzi mkuu, malipo ya Dowans,
> watu wametekwa nyara, wameteswa, watu wameuwawa na vyombo vya dola, hakuna
> uwajibikaji, ufisadi umeongezeka zaidi kuliko wakati wa list of shame,
> hakuna uwajibikaji) ndiyo yametufikisha sasa tunajadili katiba mpya na sasa
> hivi tumefikia hata hatua ya rasimu ya katiba mpya. Lakini si yalikuwa
> makelele ya vyama baada ya uchaguzi mkuu. Tulipaswa kumpuzika nayo!
>
> Hakuna tatizo na mantiki ya Maggid kuhusu siasa za hovyo hovyo. Lakini mbona
> 'kaificha'. Ni kweli hazihitajiki. Tuzipinge kwa nguvu zote. Zitatuangamiza
> sote. Ubaya unakuja kwenye mantiki ya jumla jumla sana ambayo imewekwa wazi
> wazi kweli iliyo katika andiko hili.  Siasa za hovyo ni ni zipi hizo,
> zikoje, zinafanyikaje? Tumefikaje hapo. Tunaondokaje.
>
> Tutaendelea kujificha katika generalization hadi lini? Tukiyasema haya mambo
> kwa ujumla jumla wake, haitatusaidia. Hatutawasaidia. Tukiyaweka specific,
> tutakemea, kuonya, kurekebisha na kufundisha. Lakini pia mjadala hunoga na
> tunapata fursa ya kujua ukweli na uhalisia ni upi. Tunahitaji tuyazungumze
> haya mambo kama yalivyo. Specifically.
>
>
>
>
>
>
>
>
> Tumaini Makene
> CHADEMA Senior Information(Press) Officer
> 0752 691569/ 0688 595831
>
> Sent from my iPad
>
> On Jul 3, 2013, at 8:00 AM, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
>
>>
>> Ndugu zangu,
>>
>> Katika saa 20 na zaidi Rais Obama alipokuwa katika ardhi ya Tanzania,
>> sikusikia mahali popote akitamka jina la chama chake cha Democrat. Obama
>> ametamka ' AMERICA!' mara zisizohesabika.
>>
>> Kwa kweli ujio wa Obama umetusaidia Watanzania kupumzika na kelele za
>> vyama, maana, kwa siku kadhaa, kabla na wakati wa ujio wa Obama,
>> Watanzania tumepata kupumzika na kusikia habari za vyama vya siasa na
>> malumbano yasio na hoja za msingi, mara nyingi yasio na tija kwa nchi na
>> maendeleo yake.
>>
>> Hakika, siasa ni kitu kizuri sana kwa nchi. Lakini siasa za ' ovyo ovyo'
>> ni kitu kibaya kwa nchi. Na mara nyingi, siasa za ' ovyo ovyo' ni kitu cha
>> hatari kwa nchi na mustakabali wake.
>>
>> Picha hiyo hapo juu ina mengi ya kutufundisha; kuwa siasa si uhasama.
>> Uchaguzi ukiisha watu mnarudi kwenye kufanya kazi. Kupigania maslahi ya
>> taifa. Si kuendeleza migogoro ya kisiasa na hata kuwepo kwa vurugu. Hayo
>> hayana tija kwa nchi.
>>
>> Unapomwangalia Obama na Bush kwenye picha ya pamoja wakiwa Dar na kwenye
>> kutoa heshima kwa wahanga wa ugaidi kwenye mlipuko ulitokea kwenye Ubalozi
>> wao mwaka 1998, inadhihirisha ukomavu wa kisiasa.
>>
>> Unachotumainia hapa, kuwa ifike siku, hata hapa kwetu Tanzania, kwa Rais
>> aliye madarakani na Rais Mstaafu kutoka vyama viwili tofauti, tuone picha
>> yao wakiwa wamesimama pamoja kwenye makaburi ya kumbukumbu ya mashujaa
>> wetu wa Vita Vya Kagera kule Uganda.
>>
>> Ndio, picha hiyo hapo juu ni somo kwetu. Hawa wawili; Bush na Obama, ndio
>> tuliowaona kwenye kampeni zao wakipambana kiasi huwezi kufikiri wanaweza
>> kusimama pamoja kama ndugu wa taifa moja.
>>
>> Lakini, kwa wenzetu Marekani, siasa si uhasama wala mambo ya kuwindana.
>> Wanachogombania kwenye siasa ni kupewa heshima ya kuitumikia Marekani.
>>
>> Na heshima hiyo akipata mpinzani wako, basi, kwa wenzetu wanachofanya ni
>> kuungana mkono kwenye kazi ya maslahi ya Marekani bila kujali tofauti zao
>> za kiitikadi. Na ndicho tunachofundishwa kwenye picha hiyo.
>>
>> Swali linabaki, Watanzania tuko tayari kubadilika kifikra kwa maslahi ya
>> taifa letu?
>>
>> Maggid,
>> Iringa.
>> 0754 678 252
>> http://mjengwablog.com
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
>  http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>


--
Sincerely Patty,
Cell: +255 713 474 155
        +255 767 474 155
E-mail:magubira@gmail.com,
          pmagubira@aol.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.

TEMBELEA Facebook yetu:
 http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl

For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en

---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment