Friday 7 September 2012

[wanabidii] Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Kukagua Taasisi Zote zilizopo chini ya wizara yake

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema anapitia
taasisi zote zilizopo chini ya wizara yake ili kusikiliza mafanikio
na kujua matatizo yanazozikabili taasisi hizo ili kuweza kuboresha
huduma katika sekta ya afya nchini pamoja na kupanga mipango mizuri
katika kuendeleza taasisi hizo.

Dkt. Mwinyi amesema hayo leo kwenye ziara yake na kuzungumza na
wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Liche Tanzania (TFNC).

"Lazima tujiulize uwepo wa taasisi hii,mwanzoni taasisi hii ilikuwa
inajikita na utapiamlo, kwa sasa kuna magonjwa yasiyo ya
kuambukizwa ,alitaja mfano wa magonjwa haya ni moyo,kisukari na
mengineyo magonjwa haya mapambano yake ni kinga,na wataalamu wa kutoa
kinga ni nyinyi,hivyo masuala ya lishe ni muhimu kabla ya kuanza
kuyatibu.

Aidha Dkt. Mwinyi alisema wizara yake ina kila sababu ya kuyapa
kipaumbele masuala ya lishe nchini licha ya ufinyu wa bajeti
wanayoipata, "ipo haja ya kujipanga upya na kufanya kitu cha ziada
ili kupunguza kiwango cha utapiamlo nchini pamoja na upungufu wa
wekundu wa damu kwa wanawake wenye umri wa kuzaa ambapo inachangia
vifo vya akina mama wajawazito nah ii inachangia na akina mama wengi
kutokuwa na elimu na mafunzo juu ya lishe na hivyo nchi kuwa nyuma na
kutofikia malengo ya millennia ya kupunguza vifo vya akina mama
wajawazito nchini.

Awali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Benetict Jeje
alisema taasisi yake ina changamoto ya kuhakikisha kuwa huduma za
lishe nchini zinapanuka na kuwafikia wananchi wengi hasa waishio
vijijini , hivyo serikali kuamua kuajiri maafisa lishe katika
halmashauri 106 kati ya 168 na mikoa 11 imefanya hivyo.

"Lishe ni suala mtambuka na linalogusa maendeleo ya kijamii, kiuchumi
na maendeleo ya nchi kwa ujumla,ushiriki wa sekta mbalimbali katika
kukabliana na changamoto za lishe nchini ni jambo
lisiloepukika"alisema Jeje.

Hata hivyo alisema taasisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
zimechangia kupunguza kwa kiwango cha utapiamlo nchini kati ya mwaka
1999 na 2010.Asilimia 16 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano
wana uzito pungufu,asilimia 5 ni wakondefu na asilimia 42 wana udumavu
na upungufu wa damu unaathiri asilimia 69 ya watoto wakati upungufu wa
vitamin A ni asilimia 33

-MWISHO-


Na.
Catherine Sungura.
Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamiii

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment