Friday 7 September 2012

[wanabidii] Ughali wa umeme umeturudisha kwenye uijma

 
 
Ughali wa umeme umefanya watu turudi kwenye zama za ujima za kutumia mkaa na kuni na kuzidisha uharibifu wa mazingira.
Nimejaribu kufanya utafiti sehemu ninyoishi ambayo wakazi wake ni watu wa kipato cha kati.
Wengi wana majiko ya umeme lakini kati ya watu 10 watu wawili tuu ndio wanatumia majiko hayo, tena kwa kupikia vitu kama chai na vyakula vyepesii na sio kuchemsha nyama wala maharage. kwa hiyo majiko mengi ya umeme yamebakia kama mapambo tuu ndani ya nyumba zetu. Umeme tunautumia kuwashia taa, frige na Tv tuu.
Kwa hili jamani zama hizi za sayanai na tekinolojia tutafika kweli? Serikali iangalie upya bei za umeme ili wananchi tuondokane na ujima wa kupikia kuni na mkaa na kuharibu mazingira. Unit ya umeme ni sh. 270 nani ataweza? Gasi ndio usiseme tunaelekea wapi?
Tunarudi nyuma au tunaenda mbele? Na bado TANESCO wanang'ang'ania kupandisha tena bei.

0 comments:

Post a Comment