Thursday 6 September 2012

[wanabidii] TAMKO LA BAVICHA KULAANI MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI MAREHEMU DAVID MWANGOSI

BARAZA LA VIJANA CHADEMA (BAVICHA) JIMBO LA SEGEREA


TAMKO LA BAVICHA KULAANI MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI MAREHEMU DAVID
MWANGOSI.

1.UTANGULIZI

Ndugu wanahabari,BAVICHA jimbo la Segerea limewaita hapa leo
06/09/2012,ili kutoa masikitiko,kulaani na kutoa tamko juu ya vitendo
vinavyoendelea kushamiri vya mauaji dhidi ya raia wasio kuwa na
hatia.vifo hivi vyenye mashaka vinavyoendelea kutokea mbele ya uwepo
wa jeshi la polisi vimeendelea kwa muda mrefu sasa bila ya kupatiwa
ufumbuzi wa kudumu,na vinazidi kuondoa imani ya jeshi hili lenye
dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

Matukio ya mauaji ya hivi karibuni yaliyotokea mbele ya jeshi la
polisi,mkoani Morogoro (Morogoro mjini) Nyamongo mkoani Mara na tukio
la kuuwawa kwa mwandishi wa habari kijiji cha Nyololo mkoani Iringa ni
baadhi tu ya matukio mengi yenye mashaka na yanayoleta sintofahamu juu
ya utendaji kazi wa jeshi la polisi na kusababisha kutokuaminika tena
kwa watanzania.

BAVICHA jimbo la Segerea tunasikitishwa sana na mauaji ya KINYAMA ya
mwandishi wa habari,marehemu DAVID MWANGOSI yaliyotokea
02/09/2012,akitekeleza majukumu yake ya kutafuta habari kwenye tukio
la uzinduzi wa tawi la CHADEMA kijiji cha Nyololo,huku akiwa
amezungukwa na polisi wengi na wasiweze kumuokoa na kifo hicho.Je kazi
yao ilikuwa nini kama siyo kulinda usalama wa raia na kama ni kulinda
ilikuwaje DAVID alikufa amemkumbatia moja ya wanausalama hawa?huku
wengine wakimshambulia?

Tunashangazwa sana na jeshi la polisi kuzuia mikutano ya ndani
iliyokuwa ikifanywa na CHADEMA kwa kisingizio cha kupisha zoezi la
sensa ya watu na makazi,wakati likiacha mikutano ya ndani ya CCM
wakiendelea na chaguzi za viongozi wa UWT na UVCCM na mikutano ya
hadhara wakati zoezi la sensa likiendelea,kwa mfano Uzinduzi wa
kampeni za uchaguzi mdogo wa mbunge jimbo la BUBUBU UNGUJA( Uzinduzi
huo ulifanywa na Dr Mohamed Ghalib Bilal,UVCCM wilaya ya Temeke na
Kinondoni,UWT wilaya ya Temeke-Uchaguzi uliofanyikia PTA hall
sabasaba,Mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi uliofanyika jimbo
la Mchinga(Mh.Said Mtanda alihutubia),Asha Suleiman Idd(mjumbe wa
kamati ya siasa wilaya ya Kaskazini B) aliekuwa akifungua mkutano wa
UVCCM katika wilaya ya Kindunina mbunge wa Bumbuli mh.January Makamba
aliefungua mkutano wa jumuia ya wazazi CCM wilaya ya Lushoto.

Wakati matukio haya yote yakifanywa na CCM ni kipindi cha muda wa
nyongeza wa sensa ulikuwa ukiendelea.

BAVICHA jimbo la Segerea tunahoji,KATAZO LA POLISI LA KUZUIA MIKUTANO
NA SHUGHULI ZOTE ZA SIASA NI KWA CHADEMA TU? Hali hii inatoa picha
kwamba jeshi la polisi linatumika kisiasa kwa kuibeba CCM,ni kwa namna
gani wataepuka kuitwa POLISISIEMU?hata hivyo kuna dalili tosha kwamba
vyombo vya habari navyo vimeanza kujengewa hofu katika kutekeleza
majukumu yao,kwa hili la kuuwawa kwa mwandishi akiwa amezungukwa na
polisi akitafuta habari kwenye tukio la kisiasa za chadema,tunajiuliza
ni kwa vipi walishindwa kulinda usalama wake ili hali wakijua ni
mwandishi?ni nani hasa alimuua DAVID MWANGOSI?mbele ya wanausalama
waliokuwa na silaha,magari, intelijensia,radio call,kofia za
kujikinga,marungu,mabuti na vyote walivyotakiwa kuwa navyo?

Mauaji haya ya KINYAMA katikati ya polisi wengi yanatudhihirishia
kwamba wizara hii ya mambo ya ndani inayoongozwa na Emmanuel Nchimbi
pamoja na mkuu wa polisi IGP MWEMA wameshindwa kabisa kukomesha tabia
ya vifo vya raia vyenye utata na hasa pale vinapotokea mikononi mwa
polisi,na kwamba wao ni wadau halali wa kifo cha marehemu DAUD
MWANGOSI. BAVICHA SEGEREA TUNATAMKA KWAMBA

1.TUNAMTAKA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI AJIHUZULU KWA
KUSHINDWA KUZUIA VIFO VYA RAIA WASIO NA HATIA VINAVYOTOKEA MIKONONI
MWA JESHI LA POLISI ,HASA KWA MAUAJI YA MWANDISHI YALIYOTOKEA AKIWA
AMEZUNGUKWA NA POLISI WENGI TU.

2.TUNAMTAKA RAIS JK AVUNJE UKIMYA SASA JUU YA TABIA HII YA MAUAJI YA
RAIA WASIO NA HATIA KUUWAWA MBELE YA POLISI, KWA KUWAFUKUZA KAZI MARA
MOJA IGP SAID MWEMA,MKUU WA OPERATION PAUL CHAGONJA NA RPC WA IRINGA
KAMUHANDA ,NAHATA HIVYO RAIS NI MWEPESI SANA KUTOA SALAMU ZA RAMBI
RAMBI KWA MISIBA INAYOGUSA TAIFA, NI VIPI KWA KIFO CHA DAUD BADO YUKO
KIMYA?

3.POLISI KAMA WANAJIFUNZA KUUA RAIA WASIO NA HATIA BASI NASISI
TUTAHAMASISHANA KUJIFUNZA KUFA,NA HATUTAOGOPA TENA KUFA KWA KUWA
TUNAJUA TUSIPOKUFA LEO,TUTAKUFA KESHO NA TUSIPOKUFA KESHO IPO SIKU
TUTAKUFA.

4.SERIKALI YA CCM IACHE KUTUMIA NGUVU YA DOLA KUTISHA ,KULETA HOFU
WALA KUDHOOFISHA WANANCHI WASIENDELEE KUKIUNGA MKONO CHAMA CHA
CHADEMA,NA TUNA MTAKA KATIBU WA UVCCM TAIFA,MARTIN SHIGELA AACHANE NA
PROPAGANDA ZENYE LENGO LA KUPOTOSHA UMMA NA KUTISHA VIJANA WASIKIUNGE
MKONO CHADEMA.

5.BAVICHA SEGEREA TUNATANGAZA KUTOKUWA NA IMANI NA MSAJILI WA VYAMA
VYA SIASA,NA TUNAMTAKA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JOHN TENDWA AUELEZE
UMMA KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KAULI YAKE,NA KAULI YA WASIRA NA KAULI
YA WAZIRI MKUU BUNGENI(AMBAYO NI YA SERIKALI NA NI YA CCM PIA)
ILIYOLENGA KUTISHIA KUIFUTA CHADEMA,ILI HALI WAKIJUA WANAOUA WATU SIO
CHADEMA BALI NI JESHI LA POLISI? NA ATUELEZE JE TENDWA NAE ANAKOSA
AMANI KUFUATIA CHADEMA KUUNGWA MKONO NA WANANCHI HUKO VIJIJINI? NA
MAENEO MENGINE NCHINI.

6.BAVICHA JIMBO LA SEGEREA TUNATOA RAI KWA VIJANA WOTE TANZANIA
WANAOHITAJI MABADILIKO NA WENYE MTIZAMO CHANYA WA UKOMBOZI KUTOKA
MIKONONI MWA MAFISADI, KUWA TAYARI KUPAMBANA NA NAMNA YOYOTE YA
UONEVU,UKANDAMIZAJI,UDHALILISH AJI NA UBAGUZI WA NAMNA YOYOTE ILE.

Imetolewa leo na uongozi wa BAVICHA (J) SEGEREA
Daniel Raymond
M/Kiti

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment