Friday 21 September 2012

[wanabidii] Re: NILICHOSIKIA KONGAMANO LA KIISILAMU ARUSHA

On Monday, March 28, 2011 6:21:21 AM UTC-7, Henry Kaisi wrote:
> Wakati habari juu ya babu huko Loliondo zinapumzika kidogo, naomba niwape na haya niliyoyasikia kwa masikio yangu kutoka redio Imani. Hii ni redio ya Waislamu ambayo inatangaza kutokea mkoa wa Morogoro. Sijui kama husikika nchi nzima au la. Hapa kwetu Arusha kulikuwa na kongamano kubwa la Waislamu wa madhehebu yote, jana Jpili na lilianza tangu asubuhi hadi jioni. Walikuwepo watoa mada mbalimbali, lakini mimi nilifanikiwa kumsikia mmoja, pamoja na immamu wa mkoa aliyetoa maazimio ya kongamano.Bila shaka magazeti yataripoti vizuri. Nimesukumwa kuandika tena kwa urefu kwani nilisikitika sana kusikia maneno ambayo sikuwahi kuyasikia tangu nizaliwe yakiongelewa hadharani ndani ya nchi yangu. Nakumbuka nilisoma maazimio ya Mwanza, lakini hii imenistua sana. Kama tunamwomba Mungu basi tuongeze nguvu, kama hatuombi basi tuanze. Kwa mtindo huu, ninawasiwasi na amani ya Tanzania ambayo tumejivunia miaka hamsini sasa. Mliopata neema ya kupata nafasi za juu serikalini, sijui serikali inayaonaje mambo haya. Hayajaanza leo, ila imeyaachia yaendelee. Makanisa yanazidi kuchomwa, hakuna msikiti uliwahi kuchomwa kama sijakosea. Wakristo wanavamiwa na kupigwa, hakuna mhadhara wa Waislamu uliwahi kuvamiwa. Redio Imani na magazeti ya Kiislamu (mfano Al-alnuur) yanazidi kumwaga sumu ya udini, na ubaguzi, na chuki, lakini sijawahi kusikia vyombo hivi vikikemewa. Huu, ukimya wa serikali na vyombo vyake, sijui maana yake ni nini? Sumu hii ikiishapandwa kuing'oa ni kazi. Jamaa hawa walifanya mambo yao sirini tangu enzi za Mwinyi, na sasa, wameamua kuyaweka wazi na kuhamasisha Watanzania waziwazi tuuane. Haiingii akilini mwangu. Je, viongozi wetu wa dini wanazo taaarifa za kutosha kuhusu mambo haya? Wanachukua hatua gani? Je, sisi tuchukue hatua gani? Shehe Ilunga Hassan ndiye niliyeweza kumsikia. Ameongea mambo mengi, lakini yote ni ya kupandikiza chuki ndani ya Watanzania. Ameanza kwa kutoa pongezi kwa kile Waislamu walichokifanya huko Mto wa mbu (Arusha) kwa kuwapiga wachungaji, na kuwajeruhi, nk. Amesisitiza kuwa Tanzania inaongozwa na mfumo Kristo. Na sasa umefika wakati mfumo huo uondolewe na hiyo ndiyo itakuwa pona ya Waislamu. Serikali inaongozwa na maaskofu. Wao ndiyo wanaweza kumwambia rais tunataka hiki au la. Amesisitiza kuwa amani tunayoiona TZ ipo kwa gharama ya Waislamu. Umefika wakati Waislamu waseme basi kwa mfumo Kristo ili na Wakristo wabebe gharama ya amani hii. Ametoa takwimu kuwa mwaka 1992 Serikali iliingia mkataba na Wakristo, na tangu hapo imekuwa ikitoa fedha za kuwaendeleza wao huko Waislamu wakibaki nyuma. Kwa mfano, mwaka 2009, serikali imetoa bilioni 45, mwaka 2010 bilioni 54, na mwaka huu kwa miezi miwili hii na siku imekwisha toa bilioni 611, zote hizi zikiwa ni kuwaendeleza Wakristo. Wakati serikali ikifanya hayo yote, Waislamu wameachwa nyuma na watoto wao wamezidi kuwa wamachinga huku watoto wa Wakristo wakiendesha baiskeli za kizungu na kufurahia beach. Amesema ifike mahali Waislamu waamue kama walivyofanya Wahutu dhidi ya Watutsi. Ati Kikwete hawezi kuongoza nchi bila maaskofu, maana kila analotaka kufanya lazima awaone. Amesema kuwa Chama cha kususa na maandamano kipo tu kwa ajili ya maslahi ya Wakristo. Waislamu wanadanganywa wakidhani hicho chama kipo kuwatetea WaTz kumbe kipo kwa ajili ya Wakristo. Makafiri wanasaidiana wao kwa wao hivyo waislamu waamke, waungane hili kuuondoa mfumo Kristo. Amesema mfumo huu ulianza zamani,kwani hata 1964, Nyerere aliwafunga kina Chief Fundikira na wenzake kwakuwa walikuwa Waislamu. Akaendelea kuwa hata Azimio la Arusha lilikuwa kiini macho kwani liliwalenga Waislamu hata mali zilizotaifishwa zilikuwa za Waislamu Wahindi kwani wakati huo wakristo wengi walikuwa makarani na hawakuwa na chochote. Kwa hiyo Azimio lililenga kuwakandamiza Waislamu. Wakristo na mfumo wao wamekanyaga nyoka mkia, au wanamkamata ng'e mkia. Aliendelea kusema kuwa imefika sasa Waislamu kuongea lugha wanayoilewa makafiri kwani wao hawataelewa kama waislamu wataendelea kuongea kwa njia ya makongamano kama haya. Kuendelea kudai haki kwa njia hii ya mikutano na makaongamano ni kama mtu anayemwambia mbuzi lugha ya kibinadamu wakati hailewi. Mbuzi lugha yake ni kupigwa ndipo huelewa. Ndivyo walivyo makafiri. Ifike wakati waislamu waseme basi. Usilamu hauna historia ya kushindwa. Allah alikwisha wahaidi waisalamu ahela, hivyo wao wana kazi mbili tu, KUUA au KUUAWA, na ndipo watapata zawadi ya ahela. Hivyo ndivyo wanaweza kuuondoa mfumo Kristo. Akasisitiza kuwa huko Rwanda ilifika ambapo ilipotakiwa kuubadili mfumo, Mtusi na Mhutu hakuna aliyelala ndani, sasa Waislamu waseme basi. Akasema kuwa hata kama kunasemwa mabadiliko ya katiba, nayo hayatakuwa na maana kama bado kuna mfumo Kristo. Akasema kwa mfano waislamu wanabaguliwa hata kama katiba inakataza ubaguzi, hivyo, shida si katiba bali ni mfumo Kristo. Amesisitiza kuwa Waislamu hawana historia ya kushindwa hivyo hata sasa watashinda tu. Amekiponda sana chama cha kususa na maandamano akiwasihi Waislamu wasikiunge mkono. Jamani yamesemwa mengi, laiti ningekuwa mwanahabari ningeadika mengi. Kwa ufupi yule bwana amehamasisha chuki, uuaji, kuchukia CHADEMA, nk. Muda wote wafuasi walikuwa wakishangilia kwa TAKBIR! TAKBIR! Yaani kama angesema sasa tunaaza kazi nakwambia kungekuwa na balaa hasa. Ndugu zangu, inaonyesha hawa jamaa wamefanya mikutano, Dar es Salaam, Kigoma, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Singida, na sasa Arusha. Wanaendelea hadi nchi nzima wakihamasisha haya na Waislamu kuungana na kuondoa tofauti za madhehebu yao kwani mfumo huu, unawaathiri wote. Baada ya hapo alikaribishwa Imamu wa mkoa wa Arusha naye akatoa maazimio ambayo yaligawanyika katika makundi mawili. 1. MAAZIMIO YA KITAIFA i) Wanaunga mkono maazimio yote yaliyotangulia kutolewa katika mikoa mingine ii) Wanaunga mkono tamko la Immam mkuu (Shehe Issa Bin Simba)- sasa dhuluma basi iii) Wanaitaka serikali kuangalia uwiano wa kimadaraka katika ngazi zote za serikali iv) Wanaiagiza Wizara ya Elimu ifuatilie na kuhakikisha waraka wa mavazi (hijabu,nk), na ibada kwa Waislamu wanafunzi inatekelezwa. v) Wanamtaka waziri wa fedha kuthibitisha uhalali wa mkataba kati ya Wakristo na Serikali wa mwaka 1992. vi) Wanasema suala la mahakama ya kadhi si ombi ila ni lazima litekelezwe na pia TZ ijiunge na OIC vii) Wanaagiza ubalozi wa Vatican uondolewe nchini 2. MAAZIMIO YA KIMKOA i) Halmashauri ya Arusha imepewa mwezi mmoja irudishe mali za Waislamu ii) Waislamu wapewe kibali kujenga msikiti katika kiwanja cha NHC kilicho karibu na Mahali pa Kumbukumbu ya Azimio la Arusha. iii) Mahali ilipo stendi ya daladala ni mali ya Waislamu, irudishwe mara moja iv) Kwa kuwa serikali ya JK ni halali kwa mujibu wa sheria, wanaoleta chokochoko waache mara moja. v) Waislamu wanamuunga mkono Meya wa jiji la Arusha kuwa alichaguliwa kihalali, na wanamtambua kwa nguvu zote. Aachwe afanye kazi. Wao hawatakuwa tayari kuona upuuzi huo wa kumpinga. vi) Kama Chadema itaandamana kama ilivyotoa taarifa ya siku 21, basi nao watatoka ili wapambane nao ili kujihami kwani maandamano yaliyopita yaliwaathiri vii) Wanamwagiza IGP amrudishe kazini yule askari aliyesimamishwa kazi kwa kuwakamata wachungaji huko mto wa mbu. Pia mkuu wa kituo aliyehusika kumsimamisha kazi achunguzwe na kushughulikiwa. viii) Waislamu wanasema sasa dhuluma basi. Ni hayo kwa ufupi jamani. Ninaagalia uwezekano wa kupata kanda zao kama zitakuwa zimerekodiwa. Kazi kwetu kanisa. Tukumbuke: Hawa ndugu sio wa kudharauliwa, wako very systematic katika mambo yao. Walianza chinichini, wakaongeza mihadhara, wakadai OIC, wakadai mahakama ya kadhi, sasa wanatoka nje wazi wazi , sio mihadhara, bali makongamano tena ya madhehebu yao yote nchi nzima. Huko nyuma walikuwa wanabaguana, sasa wanahamasisha umoja ili wafanikiwe katika malengo yao. Na wanawatumia wasomi wao kupindisha mambo, kwa nia wanazozijua wao. Walihamasishana kuingia kwenye siasa, wakitaka kufanikisha mambo yao kwa njia hiyo, sasa wameona haitawezekana, maana chama walikojikita kinayumba sasa. Mapendekezo yangu. • Tusiwachukie, tuwapende na kuwasaidia kwa moyo wote. • Kanisa lizame katika maombi juu ya taifa hili • Kanisa lisijibizane na hawa jamaa. • Kanisa litumie vyombo halali vya serikali tena wakati huu akiwepo mwenzao ili serikali itoe msimamo • Kanisa lihakikishe kuwa linazo taarifa za kutosha kuhusu hawa jamaa. Asante.

uSIJALI, KANDA ZA MIHANDARA, MATAMKO NA MAKONGAMANO ZIPO TELE, HATA MIMI NINAZO NI HATARI KWELI. iNASHANGQAZA KUSIKIA MATAMSHI YA KUHATARISHA AMANI NA SERIKALI IPO KIMYA. kULIKONI? wATU WA bIBLIA NI JIBU WEANAZO WATAFUTE AKINA NDIMBO. wATANZANIA WOTE WAKIJIONEA WENYEWE UTAKUWA NDIYO MIWHSO WA ccm, KWA MAANA KWAMBA INALEA KIDONDA NDANI YS SERIIALI YAKE NA KUIBEBA DINI MOJA. lAKINI mUNGU YUPO NA HAWATAFAQNIKIWA, KWA VILE MPANGO HUU NI WA SHETANI NA WALA SI WA MUNGU KUTAKA KUANGAMIZA UKRISTO.mUNGU ATAWAFANYA KAMA MNARA WA BABEL, SOMA KTIKA KITABU CHA MWANZO atika biblia takatifu.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment