Saturday 22 September 2012

Re: [wanabidii] UVAMIZI NA UNYANG'ANYI ULIOFANYWA NA POLISI HUKO KIGOMA

Nafikiri Kitendo hiki cha Polisi kufanya unyang'anyi SIO TATIZO. Ni dalili ya Tatizo.
 
1) Walimu wanagoma. Wanawekewa pingamizi wasigome. Yaani wanazuiliwa kueleza tatizo lao. Si kwamba wametatuliwa matatizo yao. La. Wanalazimishwa kunyamaza na matatizo yao. Wanadanganywa kuwa wanyamaze yanashughulikiwa.
 
2) Madaktari wanagoma. Wanawekewa Pingamizi wasigome. Si kwamba wametatuliwa matatizo yao. La. Wamezuiliwa wasieleze tatizo lao kwa jamii. Tatizo lipo. Linawaumiza na kuwauma. Hawaruhusiwi kulieleza.
 
3) Polisi wanatumia Bunduki kufanya uhalifu. Kuwakamata hao si kumaliza tatizo. La. Tatizo ni kubwa. Polisi hawa tena wao ndio balaa. Hawaruhusiwi hata kufikiri kugoma. Wao ni kufiamo MAMIGE.
 
Tunakokwenda ni kubaya zaidi japo ufumbuzi uko karibu. Lazima upatikane. Tuombe Mungu ufumbuzi huo usiwe chanzo cha safari nyingine ya matatizo.
Bado kidogo makundi haya matatu na mengine mengi yataungana na kuwa na mkakati mmoja.

Nasema tuombe Mungu kwa sababu katika mazingira tunayoelekea uimara wa kutumia njia za kikatiba ndiyo njia pekee ya kuepusha machafuko na safari nyingine ya kupitia porini kufika tunakokwenda.
 
Na njia zenyewe za kikatika ninazosema ni hizi za Operation Mchakamchaka, Operation Sangara na M4C. Tuombe na Polisi wanaotumiwa kuzidhibiti njia hizi za kikatiba wawe wamefumbuka macho. Watafanya kosa kuheshimu sheria ziinazotumiwa kuwazuia wananchi wasitumie njia za kikatiba kuelekea tunakotaka. Kama awmeanza kufanya kwa uwazi vituko kama hivi! Wao ndio hawapendi kuonekana wanajiheshimu?! Watajiheshimu na njaa zinauma huku wamezungukwa na wakubwa wao walioshiba?! Ni upumbavu kutoliona hili.
Soma mara mbili.
Elisa

--- On Fri, 9/21/12, godfred mbanyi <mbanyibg@yahoo.com> wrote:

From: godfred mbanyi <mbanyibg@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] UVAMIZI NA UNYANG'ANYI ULIOFANYWA NA POLISI HUKO KIGOMA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, September 21, 2012, 11:46 PM



Ndugu wanabidii,
 
Kama mlivyosikia na kuona kwenye vyombo vya habari, mama mmoja katika wilaya ya Kibondo huko Kigoma, amevamiwa usiku na askari polisi wanne, wakampiga sana  na kumnyang'anya shilingi milioni mbili na simu zake nne! Kwasa mama huyo amelazwa hospitali ya wilaya kutokana na kipigo hicho na askari wamekamatwa na kuwekwa selo.
Matukio ya aina hii ni mengi mkoani Kigoma yakiwamo ya vitisho na kubambizwa kesi!
 
Nawaomba wanaharakati, wanasheria, wanahabari pamoja na wadau wengine mfuatilie suala hili ili haki itendeke. La sivyo, polisi hao wataachiwa bila hata ya uchunguzi wowote!
 
Nawasilisha;
 
Mwl.Mbanyi
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment