Wednesday 5 September 2012

Re: [wanabidii] Umma walaani Polisi kuua ovyo - NIPASHE

Pamoja na kutupasha mtazamo wa umma kuhusu kulaani polisi kuua ovyo,
ndani ya gazeti hilo hilo la Nipashe la jana kuna makala iliyoandikwa
na Theresia Peter kulaani Chadema katika hilo. Amewaita watanzania
kwamba wamerogwa na Chadema kwa kuwa bendera fuata upepo. Kupitia
makala hii namshauri Theresia Peter akafanye utafiti na baada ya
tafiti atueleze ni kwa nini watanzania maelfu kwa maelfu wanaunga
mkono M4C ya Chadema. Aache kulalama tu badala yake afanye utafiti
siyo kusema wamerogwa, hayo ni mawazo ya mtu ambaye hakwenda shule.

2012/9/4 Selemani Rehani <srehani@hotmail.com>:
>
>
> Umma walaani Polisi kuua ovyo
>
> Na Mwandishi wetu
>
> 4th September 2012
>
> B-pepe
>
> Chapa
>
> Maoni
>
> Aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten,
> Daudi Mwangosi
>
> Wadau wamelaani vikali kitendo cha polisi kuua Mwandishi wa Habari wa Kituo
> cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, na kutaka uchunguzi huru
> ufanyike kubainisha hasa chanzo cha kadhia hiyo.
>
> Wakati sauti hizo zikipazwa, Jukwaa la Wahariri limepingana taarifa za Jeshi
> la Polisi kuhusu mauaji ya Mwangosi, kwa kile kinachoonekana ni kama njama
> za kuficha ukweli wa tukio hilo.
>
> Hayo yakitokea, Mkuu wa Jeshi hilo, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema,
> pamoja na maofisa wengine waandamizi wa jeshi hilo, wamekutana na viongozi
> wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuzungumzia hali ya
> baadaye baada ya kutokea kwa mauaji hayo.
>
> Habari za uhakika zilizolifikia NIPASHE jana jioni zilieleza kuwa mkutano
> huo ulioitishwa na IGP Mwema, ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Upelelezi wa
> Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
> Iringa, Michael Kamuhanda.
>
> Wengine waliohudhuria mkutano huo ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Iringa,
> maofisa wengine waandamizi wa jeshi hilo pamoja na Rais wa Vyama vya
> Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Keneth Simbaya.
>
> Chadema katika mkutano huo, iliwakilishwa na Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod
> Slaa, aliyefuatana na viongozi wengine wa chama hicho.
>
> Kwa mujibu wa habari hizo, mazungumzo hayo yalichukua zaidi ya saa mbili
> kabla ya IGP Mwema kwenda wilayani Mufindi kujionea mwenyewe eneo la tukio
> hilo katika kijiji cha Nyololo.
>
> Habari hizo zinasema katika mazungumzo hayo, viongozi wa Chadema
> walimshutumu Kamanda Kamuhanda wakisema ndiye aliyesababisha vurugu.
>
> Walisema kabla ya hapo Chadema walifanya mkutano wao wa kwanza uliohudhuriwa
> na Mkuu wa Upelelezi Mkoa (RCO) bila vurugu kabla ya Kamanda Kamuhanda
> kufika na kuamuru watu kukaa chini na baadaye kuruhusu watu kupigwa mabomu.
>
> "Ni sheria gani inayoruhusu mtu, ambaye amekaa chini na wengine kukaa ndani
> ya ofisi kumpiga mabomu? Ndani ya ofisi hiyo yalipigwa mabomu zaidi ya 50.
> Kitu hicho ni cha kushangaza wakati watu walitii amri na sisi hatukufanya
> mikutano ya hadhara, bali ni mkutano wa ndani. Ni vigumu kuwaweka ndani watu
> zaidi ya 100 katika chumba kimoja. Na ndiyo maana watu walikaa nje," habari
> hizo zimemnukuu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohamed,
> akisema kwenye mkutano huo.
>
> IGP Mwema alisema pamoja na yote yaliyotokea, kikubwa ni jinsi gani
> mazungumzo yanavyoweza kuleta mwafaka na siyo kila mtu kuchukua maamuzi
> yake.
>
> Alitaka busara zitumike zaidi ili kufikia maelewano na kukiri kuwa baadhi ya
> mambo mengine yalikiukwa katika utekelezaji wa tukio hilo ambapo alisema kwa
> sasa tayari tume imeundwa kushughulikia tatizo hilo ili kubaini ukweli.
>
> Kwa upande wake, Kamishna Manumba alisema ni kitu cha busara kila mtu
> akaangalia tumetoka wapi na tunakwenda wapi na kila mmoja ni lazima akiri
> upungufu wake kama binadamu.
>
> Alisema amani ya nchi haitajengwa kwa kutumia nguvu ya risasi, mabomu ama
> kupinga sheria kwa aina yoyote ile bali pia viongozi wa vyama vya siasa
> wanao wajibu mkubwa wa kuwazuia wafuasi wao ili kuleta amani nchini.
>
> Dk. Slaa alimtaka IGP Mwema kuwaambia ni kwani nini wamekuwa wakizuia
> mikutano ya Chadema peke yake wakati vyama vingine vikiendelea kufanya
> mikutano bila kupigwa mabomu na kumkumbusha kuwa walisitisha operesheni
> Sangara kupisha zoezi la sensa kwa siku tano, lakini iweje leo waambiwe wao
> kuwa ndio wakorofi?
>
> Habari za ndani ya kikao hicho zinasema kuwa jeshi hilo lilikubaliana kuwa
> taratibu zote zifuatwe ili kuhakikisha kuwa watu waliokamatwa katika tukio
> lile wanapata huduma na taratibu za kisheria zifuatwe na kuunda timu mbili
> za Polisi na Chadema ili watu walioshuhudia tukio hilo watoe maoni yao
> katika tume ya usuluhishi.
>
> Baadhi ya viongozi wa Chadema waliokuwapo kwenye tukio hilo watatoa maoni
> yao walivyoona tukio hilo na kwa upande wa polisi, timu hiyo itaongozwa na
> Kamishna Manumba.
>
> Katika mkutano huo, polisi na Chadema walikubaliana chama hicho kiendelee na
> mikutano yake ya ndani kama kawaida na isifanye mikutano yoyote ya hadhara
> na maandamano mpaka siku zilizoongezwa za sensa zitakapoisha.
>
> Pia walikubaliana kujenga kuaminiana na kuondoa uhasama kati ya viongozi wa
> Chadema na polisi.
>
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment