Sunday 23 September 2012

Re: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela

Matinyi,
Penda usipende kaka, huo ndo mradi na Mtaji wa kisiasa kwa sasa. Tumeona viongozi wastaafu baada ya kuona waliowaachia madaraka hawa wajali waliingia na kujikita makanisani! Makanisani ndo mahala pa kujificha na kubebwa. Ndio siasa zetu zinakoenda huko.

Ukwasi ulioko kanisani unatisha, hakuna auditor huo,hakuna bodi, hakuna mtu wa kuueleza umma fedha zile tunachanga kanisani zinatumikaje.

Hao viongozi wa dini kazi Yao kuchangisha fedha kwa anayeweza fanya hivo, fedha chafu, waumini wachafu ukichangia tu fedha wewe unapewa kiti cha Mbele, unatukuzwa. Mambo ya ajabu!

Kanisani sasa hivi ni Kama saccos, wako busy wanachangishana fedha,hawafanyi kazi ya injili, muda mwingi ni michango, sasa watakataaje wanasiasa?

From LR

On 23 Sep 2012, at 18:26, "Mobhare Matinyi" <matinyi@hotmail.com> wrote:

.... lakini sipendi tabia ya wanasiasa na viongozi wengine wa kijamii kujibanzabanza kwenye nyumba za ibada kama ninavyoichukia hii tabia iliyoibuka siku hizi ya wanasiasa kutoa salamu hii:
 
...Asalamu Aleikumu, Bwana asifiwe.
 
Tunazidi kuwa taifa la kijinga.
 
Sipendi uunganishaji wa siasa na dini; sipendi viongozi wa dini kuabudiwa. Nasema sipendi.
 
 
******************************
 
> Subject: [wanabidii] Sherehe za Dr. Harrison Mwakyembe za kumshukuru Mungu - Nduli, Ikolo, Kyela
> To: wanabidii@googlegroups.com
> From: hkigwangalla@gmail.com
> Date: Sun, 23 Sep 2012 14:31:17 +0000
>
> Tuko hapa nduli kanisani, Ikolo, Kyela kumuunga mkono Dr. Mwakyembe wakati akimshukuru Mungu kwa kumponya. Ameamua kujenga kanisa na kituo cha chekechea na biashara za akinamama kama sadaka yake kwa Mungu. Sisi tumekuja kumsindikiza. Bravo Komredi! Walikuwpo watu wngi akiwemo S Sitta, Tizeba, Mulugo, Maige, Kilufi, Zambi, Mtutura, Mwambalaswa, Mwandosya, Ngoye, Lembeli etc bila kuwasahau Ndg. Mboka - kijana aliyemuokota Dr. Mwakyembe kwenye ajali ya Ihemi Iringa, inayosadikiwa kuwa ilelenga kuondoa uhai wake, pia Ndg Paul Makonda, Rais wa TAHLISO na ambaye anagombea Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM, Ndg. Eng Chambo
> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment