Friday 7 September 2012

RE: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...

Kibanda/Ngurumo na wanahabari wenzangu,

  1. Kwanza naungana na wanahabari wenzangu kutoa pole kwa kifo cha Mpiganaji Daudi Mwangosi, damu yake haitapotea bure bali itakuwa chachu ya ukombozi kwa tasnia nzima ya habari.
  2. Mjengwa is right, huwezi kususia habari za kipolisi kwa sababu ni habari za jamii, unaweza kususa kuwataja polisi lakini bado ukaitendea haki jamii kwa kutoinyima haki yake ya kupata habari, bora hiyo "media services bill ipite" ili kuondoa huu uongo wa kutishiana kususa.
  3. Kisuso cha baadhi ya waandishi kususia habari za kipolisi sio kisuso cha kweli, ni kisuso cha hasira za muda tuu kutokana na uchungu wa kifo cha kusikitisha na kuhuzunisha cha Daudi Mwangosi, lakini siku zikipita, uchungu utapungua, hasira zitapungua na kwa ma RPC waandishi watakwenda, wataripoti na ma editors mtazitumia tuu hizo stories kwa sababu hazikwepeki!.
  4. Ili dhana ya kususa iweze kutekelezeka, lazima kwanza kuwepo na "independence" of the "media", na "indepedence of individual journalist". Wengi wa waandishi tulionao ni watumwa tuu,( nimetumia "watumwa" kwa maana ya "watu wa kutumwa tuu" na sio kujituma) hawafanyi kazi kwa utashi wao bali hufanya kwa utashi wa anayewatuma, awe ni editor au mmiliki ( rejea pressures shapping the news). Kama waandishi ni watu wa kutumwa tuu, hawana huo uwezo wa kususia habari za polisi kwa sababu wataendelea ama kutumwa na ma editors wao, au kutumwa na trend of events.
  5.  Editors nao akiwemo Kibanda na Ngurumo, ambao sio wamiliki wa vyombo vyao, nao pia ni watumwa tuu wa wamiliki, au waajiri wao, hivyo japo wanatekeleza majukumu yao kwa "editorial independence" ya kifkra tuu, ukweli halisi, nao hawafanyi kazi kwa utashi wao bali utashi wa wamiliki wa vyombo vyao, "he who pays the piper may call the tune"!.
  6. Waandishi pekee wenye uwezo na jeuri ya kususia habari za kipolisi, ni waandishi wa kujitegemea ambalo nalo nila sehemu mbili
  7. (1) Kada ya kwanza ya waandishi wa kujitegemea ni hawa "freelance journalist", hawa wanaandika to survive na kuitegemea hiyo habari ndio imlipe, kama ili asurvive, story iliyopo ni ya polisi, hana jeuri ya kuisusa, ataindika tuu!
  8. (2) Kada ya pili ya waandishi wa kujitegemea ni "independent journalists", kada hii inahusisha waandishi ambao wako huru, na kuandika just for the love of it, hawa wanaandika "to inform" "not to survive" na wengi wa kada hii ndio waandishi ambao wako huru kuandika chochote, au kususia chochote kwa sababu hawa hawatumwi na yoyote, wala hawamtegemei yoyote, japo nao stories zao au makala zao zinategemea huruma ya editors ili zitoke. 
  9. Kama watekelezaji wa azimio la kususia habari za polisi, ndio hili kundi la mwisho, then kususa huku kunawazekana, lakini ili kususa ili kuwe na maana, lazima kuwe focus ni malengo gani tunataka to achieve kwa kuwasusia polisi!.
  10. Mwisho, kama kweli tasnia ya habari, tumedhamiria kususia habari za kipolisi, lazima tuweke miongozo au embargo kuwa jeshi la polisi lisitajwe popote wala kamanda yotote ili kutowapa promo, lakini taarifa muhimu bado zikaifikia jamii kwa kuripoti kwa angle ya jamii, ila iwe isiwe, waandishi kwa RPC lazima watie timu, chini ya hapo ni kujidanganya!.

Asante.

Pascal Mayalla
(Independent Journalist)
Press & Public Relations (PPR)
+255 784 270403

--- On Fri, 7/9/12, absalom Kibanda <absakib@yahoo.com> wrote:

From: absalom Kibanda <absakib@yahoo.com>
Subject: RE: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 7 September, 2012, 11:02






Ndugu zangu wanabidii

Siungi mkono hoja zote za pande mbili, ile ya Mjengwa na ile ya wanabidii wenzangu ambao mnapendekeza wana habari kususia shughuli na habari zote zinazohusu Jeshi la Polisi.

Thamani ya maisha ya watu wote wanaouawa katika mikono ya polisi kama ilivyotokea kwa mwanahabari Daudi Mwangosi ni kubwa kuliko kususa. Mwangosi na wenzetu wengine kadhaa wamepokonywa haki ya kikatiba ya kuishi. Mwangosi na muuza magazeti wa Morogoro kwa mfano wote wameuawa wakiwa kazini na wale waliowaua walikuwa kazini pia.

Kwa mtazamo wangu hoja ya msingi ingekuwa ni kuwajibika kwa viongozi wa juu wa Jeshi la Polisi na wale wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Period. Uamuzi huu unapaswa kuwagusa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, RPC wa Iringa, IGP na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Wanapaswa kuwajibika si kwa sababu wao wamehusika kuua la hasha bali kuonyesha kwao kuguswa na matukio haya yanayolifedhehesha Jeshi la Polisi na Serikali, Lakini wanawajibika kwa sababu pia utakuwa msingi bora wa uwajibikaji kwa polisi wengine na viongozi katika siku zijazo.

Huu ndiyo msimamo ambao nilitarajia kuusikia kutoka kwa wanabidii na wana habari. Wanahabari.

Nawasilisha












Absalom Kibanda
Managing Editor
Free Media Ltd
Chairman Tanzania Editors Forum
P.o. Box 77343
Dar es Salaam
Cell:+255754001010,+2550652114422

--- On Thu, 9/6/12, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Subject: RE: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...
To: "Wanabidii googlegroups" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, September 6, 2012, 11:08 AM

Mollel,
 
Nagusia suala lako la haki za mwandishi anapokufa kazini iwapo ama wakati hakuwa mwajiriwa:
 
1. Si lazima mwandishi awe mwajiriwa na ndivyo ilivyo duniani kote. Anaweza kuwa kitu kingine kwa mujibu wa makubaliano.
 
2. Ajira ni utamaduni uliozoeleka Tanzania lakini ajira si kila kitu maishani, kwa hiyo tusilazimishe ajira kwenye kila kitu.
 
3. Mtu anaweza kupata haki zake hata bila kuajiriwa ili mradi kuwe na mkataba wa kazi unaojulikana kisheria na sheria za nchi zinazoheshimiwa hata kama mkataba haupo.
 
4. Pale ambapo mtu hana mkataba wa kisheria, bado ana haki zake nje ya kazi, mfano hakuna anayezuiwa kuwa na bima ya maisha. Hili sasa ni suala la utamaduni na ufahamu wa mambo au tuseme maendeleo ya jamii yetu wenyewe. Kwani itakuwaje iwapo mtu hutaki kuajiriwa au kuwa chini ya mkataba wenye masharti?
 
5. Kwa tukio la kifo cha Daudi Mwangosi Channel Ten inawajibika kisheria kuilipa fidia familia yake bila kujali alikuwa na hadhi gani ya ajira kwa kuwa amekufa akiitumikia Channel Ten. Hili ni suala la kwenda mahakamani na kupata hukumu na halikwepeki duniani pote.
 
6. Kwa kuwa Mwangosi ameuawa na Jeshi la Polisi, basi inatakiwa familia ya marehemu na ikibidi hata na Channel Ten yenyewe waende mahakamani kudai haki na hili nalo ni la kawaida kabisa. Familia ya Lt. Jen Imrani Kombe ilishinda kesi mahakamani na ililipwa.
 
Ni suala la kuzijua haki zilizopo kisheria. Familia ya marehemu huyu ina haki zake zimekaa mahali tuli zinasubiri kuchukuliwa.
 
Asante kwa udadisi wako,
 
Matinyi.
 
 
 

 
> Date: Wed, 5 Sep 2012 23:55:59 -0700
> From: aramakurias@yahoo.com
> Subject: Re: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
>
> Mjengwa kwa hili ni usaliti wa kifani. Hv mfano mh mjengwa ungekua ww ndo ulotumbuliwa utumbo ungejisikiaje huko akhera kuona wenzako wanaendelea tu bila hata kukutetea! Kusimama aside eti ww na blogu yako utaendelea kureport habari za kipolisi ni usaliti. Hz habari utareport vp wakati tayar kuna uhasama kati yao na cc! Huoni kua hz habari ni za utetezi tu hao mapolisi, ili mambo yaende lazima walazimishwe kujua umuhimu wanahabari, that we depend each other,bila wanahabari polisi cant perform their duties properly, sasa hata kama wao hawajaua kwanini washindwe kutuprotect! Kuna haja ya kugomea kureport habar zao. Mjengwa kama vp nae atengwe tu make hes like betraying, hafu jamani wapi press clubs zetu, wapi journalist associations, kwa hili ilikua na kutoa tamko la pamoja kutoshiriki tena shughuli zozote za kipolisi bw. But its seem kuna gap hapa. We need to think big jamani na tujitetee make 2015 bado hatujafika na cjui itakuaje, nahisi waandishi
> wataogopa na kuhama fani. Lingine nimeambiwa daud hakua na mkataba rasmi na channel tena, this is another gap, hv umoja wa wanahabari, au jukwaa la wahariri kwanini msilazimishe moat watu waajiriwe jamani. Embu chek sasa david kafia kazini who will pay his family, na itakuaje? Watoto wake wataishije, hakuna insurance yoyote! This is another gap. Eh taabu tupu hapa
> ------------------------------
> On Thu, Sep 6, 2012 2:26 AM EDT martin pius wrote:
>
> >Ukweli ni kuwa,
> >
> >Katika migomo huwa wapo watu wachache ambao hawaoni sababu ya kufanya hivyo na huwa wana sababu nzuri zinazowaridhisha wao kufanya hivyo. Ila nilichojifunza ni kuwa wanakuwa wanajitoa kwenye jamii au kundi lao taratibu na kwa uhakika! Siku yakiwakuta wao wanajikuta wako peke yao.
> >
> >
> >
> >--- On Thu, 6/9/12, Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com> wrote:
> >
> >From: Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
> >Subject: Re: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...
> >To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> >Date: Thursday, 6 September, 2012, 9:05
> >
> >Mjengwa kwenda kinyume na maazimio ya wanahabari wenzako ni usaliti wa hali ya juu. Kama ulikuwa na hoja ya msingi ulistahili kuijenga hoja hiyo kwenye kikao cha maamuzi na kuweza kuwashawishi wanahabari wenzako juu ya kila unachokiona kuwa ni sahihi; namna nyingine yeyote kwa maelezo yoyote yale, hakuna maelezo mazuri zaidi kuwa utakuwa ni msaliti wa wanahabari wenzako.
> > 
> >Siku zote ni Umoja unaoleta mabadiliko.
> > 
> >Nakubaliana na Matinyi kuwa mgomo ni lazima ukuumize wewe kwanza kabla ya kumwumiza unayemgomea, na ndipo mafanikio yapatikane. Mjengwa hujanishawishi bado kuweza kuamini kuwa uamuzi wako wewe mmoja ni wa busara kuliko uamuzi wa wanahabari wenzako wote kwa pamoja.
> > 
> >Bart
> >
> > 
> >
> >From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
> >To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
> >Sent: Thursday, September 6, 2012 8:49 AM
> >Subject: RE: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >
> >Mgomo una sifa moja, kwamba yule anayegoma ni lazima aumie kwa upande fulani lakini mwisho wa siku anakipata kile anachokitaka.  
> >
> >
> >Date: Wed, 5 Sep 2012 22:38:24 -0700 From: ansbertn@yahoo.com Subject: Re: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi... To: wanabidii@googlegroups.com
> >
> >
> >
> >
> >Mjengwa,
> >
> >Wasikilize kwanza waandishi wenzio, si polisi. Usiwavunje moyo, an usiwe mgumu kuguswa na hili linalotusibu. Katika hali hii ya msiba huu mbichi kabisa, kukejeli au kupuuza waandishi wale wale ambao mwenzao kauawa juzi eti kwa kuwa alikuwa "anauliza uliza maswali sana" ni dhambi kubwa; na harakati wanazofanya waandishi zinakuhusu, na zinalenga kukunusuru, hata wewe.
> >
> >Kumbuka, hata waandishi ni sehemu ya jamii. Lakini hawataki kutumiwa kama mifereji ya kupitisha propaganda chafu za polisi katika mazingira ambao polisi wenyewe wanataka kutumia fursa hiyo kunyanyasa jamii. Wewe andika, lakini ujue kuwa huitendei haki jamii hiyo hiyo unayoizungumzia.
> >
> >
> >Ansbert Ngurumo
> >Deputy Managing Editor
> >Free Media
> >
> >P.O. Box 15261
> >Dar es Salaam
> >Tanzania
> >
> >Mobile      .+255 719 001 001
> >                  +255 767 172 665
> >http://www.freemedia.co.tz/
> >http://www.voxmediatz.com/
> >http://www.ngurumo.wordpress.com/
> >http://www.ngurumo.blogspot.com/
> >
> >
> >
> >
> >--- On Thu, 9/6/12, maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> >
> >
> >From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
> >Subject: Re: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...
> >To: wanabidii@googlegroups.com
> >Date: Thursday, September 6, 2012, 1:16 AM
> >
> >
> >Mubelwa, Nakushukuru kwa kunielewa, na umeliweka vizuri hasa unapoandika; " Huwezi kumkomoa mtu kwa kutenda kile asichojali".
> >2012/9/5 Mubelwa Bandio <changamoto@gmail.com>
> >Salaam Mwenyekiti.
> >Waliogomea kuandika habari za kiPolisi wanaamini kuwa POLISI HAWAJALI KUHUSU JAMII.
> >LABDA NI KWELI.
> >Na...Ni kwa sababu hiyohiyo naamini kuwa kwa kuwa habari za kipolisi haziwanufaishi polisi bali jamii, kugoma kuandika ni kuipa adhabu ya pili jamii.
> >Huwezi kumkomoa mtu kwa kutenda kile asichojali
> >
> >Nakuunga mkono.
> >ANDIKA TU....KWA MANUFAA YA JAMII
> >
> > On Wednesday, September 5, 2012 6:04:33 PM UTC-4, maggid mjengwa wrote:
> >
> >Ndugu zangu,
> >
> >
> >Kufuatia mauaji ya kutisha na ya kusikitisha ya mwandishi Daudi Mwangosi ambapo askari wa Jeshi la  polisi wanatuhumiwa kuhusika, kumekuwa na mitazamo na mikakati tofauti miongoni mwa wanahabari ikiwamo kugomea kuripoti  habari zinazotoka kwenye  jeshi la polisi.
> >
> >
> >Mjengwablog, kama chombo cha habari na mawasiliano ya kijamii,  ina mtazamo wa kuendelea kuripoti habari za kipolisi, za kutoka ndani na nje ya jeshi hilo  ikiwamo taarifa za kichambuzi.
> >
> >
> >Tunafanya hivyo tukiamini, kuwa habari za kipolisi kwa kiasi kikubwa ni habari zenye kuihusu jamii.
> >
> >
> >Maggid Mjengwa,
> >Mwenyekiti Mtendaji,
> >Mjengwablog.
> >Iringa0788 111 765
> >http://mjengwablog.com
> >--
> >Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
> >Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
> >Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
> > 
> >Kujiondoa Tuma Email kwenda
> >wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
> > 
> >Disclaimer:
> >Everyone posting to this Forum bears the
> > sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> > 
> > 
> > -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and
> > Guidelines.     -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.     -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    
> >
> >
> >
> >--
> >
> >Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> >
> >Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> >
> >Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
> >
> > 
> >
> >Kujiondoa Tuma Email kwenda
> >
> >wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
> >
> > 
> >
> >Disclaimer:
> >
> >Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> >
> > 
> >
> > 
> >
> >--
> >Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> >Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> >Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
> >
> >Kujiondoa Tuma Email kwenda
> >wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
> >
> >Disclaimer:
> >Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> >
> >
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment