Thursday 6 September 2012

Re: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...

Mjengwa, kuna njia za kutafuta utatuzi kutegemeana na utamaduni pamoja na mazoea ya watu, au mahali.
Njia unayoisema ni nzuri, lakini ni mara ngapi mwandishi wa Tanzania, alipotaka habari kwa polisi ali ipata, zaidi ni kuwa wao wanapo kuwa na habari zao na kutaka kuuza sura, anhaaaa hapo utawaona na wanaweza kuwapa hata nauli ya kurudia walipotoka.
 
Labda kwakuwa mimi si mwandishi wa habari, ningeshauri kuwa, yale ambayo mwayajua juu ya jeshi la polisi, mabaya yote ( najua yapo ingawa mnawalindia heshima) , kashfa za makamanda wakorofi wote, picha za polisi wakichukua rushwa zitoeni kwa wingi sana sasa hivi. Hawawezi kuwakamata kwakuwa wanajua wataunganishiwa na habari za kuwawinda kwa makusudi.

--- On Wed, 9/5/12, maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, September 5, 2012, 11:51 PM

Ansbert na wengine,

Yahusu wanahabari kugomea kufanya kazi na polisi.

Ahsanteni kwa mitazamo yenu. Katika hili yawezekana tukawa na mitazamo tofauti, ni hali ya kibinadamu. Kwangu mimi, kwa wanahabari huu si wakati wa kutangaza mgomo wa kuripoti habari za kipolisi, kinyume chake, ni wakati wa kushambulia kwa pamoja kwa kuwakabili polisi na wahusika wengine kwa maswali yenye kuhitaji majibu.

Huu ni wakati wa jeshi la  wanahabari  kuishambualia polisi kama taasisi muhimu ya dola ili ipate majibu ya maswali ambayo jamii inataka majibu yake. Mbali ya  tukio la mauaji ya mwandishi mwenzetu Daud Mwangosi, hatuwezi kuacha kufanya kazi na polisi kupata majibu ya matukio mengine ya kihalifu yanayotokea katika jamii kwa vile tu tuna mgogoro na polisi.

Naamini, tofauti na kugoma, kuna njia nyingine za kuishinikiza Serikali na hata taasisi ya polisi kuchukua hatua katika yanayotokea. Na moja ya njia hiyo ni kila linapotokea tukio, kwa  wanahabari kwa uwingi wetu,  ' kuvamia' ofisi za wenye kuhusika na kutoa majibu ya maswali ambayo jamii inataka majibu yake.

Msimamo wangu huu unaeleweka hata na baadhi ya viongozi wa juu wa Iringa Press Club ambao nina ushirikiano nao mzuri.  Na jema katika hili  ni kuwa,  ushauri wangu wa namna ya kwenda mbele umepokelewa vema na Makamu Mwenyekiti ( Francis Godwin) na Katibu  Mkuu wa IPC ( Frank Leonard) ambao kimsingi nimefanya mazungumzo nao  na  wanaufanyia kazi ushauri wangu.

Vinginevyo, naelewa hasira na jazba tuliyo nayo  wanahabari wengi kutokana na  kilichotokea. Hata hivyo, hata katika hali kama hii, tuwe na ujasiri wa kumeza vipande vya barafu. Tutangulize hekima na busara. Ndio, tutulie na kupanga mikakati ya pamoja itakayohakikisha jamii tunayoitumikia hainyimwi haki yake ya kimsingi ya kupata habari ikiwamo habari za kipolisi. Na hata katika hili, jamii ina mengi inayoyahoji kupitia wanahabari. Wenye kuhitajika kuhojiwa ndio hao tunaofikiria kuwagomea. Naam, tuna lazima ya kuwahoji wahusika. Ni kazi yetu.

Ndio, mikakati hiyo ituhakikishie wenye kuhusika na  kutoa majibu ya unyama uliomtokea mwanahabari mwenzetu hawapati muda wa kupumua. Hii ni pamoja na sisi tulio mstari wa mbele kuhakikisha kila kukicha wahusika wanatukuta nje ya  milango ya ofisi zao tukisubiri majibu ya maswali ambayo jamii inayauliza.

Kwamba matukio kama ya mauaji ya Daud Mwangosi kamwe yasiwe ni ' Upepo tu unaopita'- Kwa wanahabari kugomea kuwakabili polisi  kwa maswali ni  namna moja au nyingine ya kutengeneza mazingira ya kuruhusu ' Upepo upite'.

Kufanya hivyo ni kulisaliti jukumu letu la msingi- Kuitumikia Jamii ya Watanzania.

Maggid Mjengwa
Iringa
0788 111 765
http://mjengwablog.com

2012/9/6 Ansbert Ngurumo <ansbertn@yahoo.com>

Mjengwa,

Wasikilize kwanza waandishi wenzio, si polisi. Usiwavunje moyo, an usiwe mgumu kuguswa na hili linalotusibu. Katika hali hii ya msiba huu mbichi kabisa, kukejeli au kupuuza waandishi wale wale ambao mwenzao kauawa juzi eti kwa kuwa alikuwa "anauliza uliza maswali sana" ni dhambi kubwa; na harakati wanazofanya waandishi zinakuhusu, na zinalenga kukunusuru, hata wewe.

Kumbuka, hata waandishi ni sehemu ya jamii. Lakini hawataki kutumiwa kama mifereji ya kupitisha propaganda chafu za polisi katika mazingira ambao polisi wenyewe wanataka kutumia fursa hiyo kunyanyasa jamii. Wewe andika, lakini ujue kuwa huitendei haki jamii hiyo hiyo unayoizungumzia.

Ansbert Ngurumo
Deputy Managing Editor
Free Media

P.O. Box 15261
Dar es Salaam
Tanzania

Mobile      .+255 719 001 001
                  +255 767 172 665

--- On Thu, 9/6/12, maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:

From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, September 6, 2012, 1:16 AM

Mubelwa,
Nakushukuru kwa kunielewa, na umeliweka vizuri hasa unapoandika; " Huwezi kumkomoa mtu kwa kutenda kile asichojali".

2012/9/5 Mubelwa Bandio <changamoto@gmail.com>
Salaam Mwenyekiti.
Waliogomea kuandika habari za kiPolisi wanaamini kuwa POLISI HAWAJALI KUHUSU JAMII.
LABDA NI KWELI.
Na...Ni kwa sababu hiyohiyo naamini kuwa kwa kuwa habari za kipolisi haziwanufaishi polisi bali jamii, kugoma kuandika ni kuipa adhabu ya pili jamii.
Huwezi kumkomoa mtu kwa kutenda kile asichojali

Nakuunga mkono.
ANDIKA TU....KWA MANUFAA YA JAMII

On Wednesday, September 5, 2012 6:04:33 PM UTC-4, maggid mjengwa wrote:
Ndugu zangu,

Kufuatia mauaji ya kutisha na ya kusikitisha ya mwandishi Daudi Mwangosi ambapo askari wa Jeshi la  polisi wanatuhumiwa kuhusika, kumekuwa na mitazamo na mikakati tofauti miongoni mwa wanahabari ikiwamo kugomea kuripoti  habari zinazotoka kwenye  jeshi la polisi.

Mjengwablog, kama chombo cha habari na mawasiliano ya kijamii,  ina mtazamo wa kuendelea kuripoti habari za kipolisi, za kutoka ndani na nje ya jeshi hilo  ikiwamo taarifa za kichambuzi.

Tunafanya hivyo tukiamini, kuwa habari za kipolisi kwa kiasi kikubwa ni habari zenye kuihusu jamii.

Maggid Mjengwa,
Mwenyekiti Mtendaji,
Mjengwablog.
Iringa
0788 111 765
http://mjengwablog.com
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment