Sunday 2 September 2012

RE: [wanabidii] Nilipopokea Taarifa Za Kuuawa Kwa Mwenzetu Daud Mwangosi Nikiwa Hapa Iringa...

Jamani Jamani nchi hii inapelekwa wapi? Polisi kuuwa watu imekuwa kama vile wanuwa kuku?
 Kwanini wanatumia silaha za moto kwa wananchi wasiokuwa na silaha?
Lazima serikali ifanyie kazi jambo hili. Mzaha mzaha hutumbua usahaa.
Poleni wote walioguswa na msiba huu familia, wana Habari na wapenda Amani wote wa Tanzania.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Daud Mwangosi mahali pema
peponi . Amina
 

Subject: Re: [wanabidii] Nilipopokea Taarifa Za Kuuawa Kwa Mwenzetu Daud Mwangosi Nikiwa Hapa Iringa...
To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
From: manonga2003@yahoo.com
Date: Sun, 2 Sep 2012 17:36:45 +0000

Majid,
Binafsi nimesikitishwa na kuhuzunishwa na kupigwa risasi kwa marehemu Daudi. Nimepata wasiwasi kwamba huenda askari wetu wamepata mafunzo ya shabaha za voda fasta! Ama sivyo ni hujuma. Kamwe askari waliopata mafunzo hawawezi kupiga risasi watu wasio na silaha including waandishi wa habari. Rais Kikwete ashtuke huenda kuna watu ndani ya Jeshi la Polisi wanaohujumu serikali yake.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 2 Sep 2012 18:17:35 +0100
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Nilipopokea Taarifa Za Kuuawa Kwa Mwenzetu Daud Mwangosi Nikiwa Hapa Iringa...

Ndugu zangu,

Jioni ya leo nikiwa katikati ya kufundisha soka ya vijana hapa Iringa nilipigiwa simu na ndugu yangu Allen,  Katibu Wa CHADEMA , Iringa,  akinitaarifu tukio la vurugu zilizotokea Nyololo, Mufindi na hata kifo cha Mwanahabari mwenzetu, mpiganaji  Daud Mwangosi ambaye pia  ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari hapa Iringa. Kuondoka kwake kutaacha pengo kubwa. Inasikitisha sana.  Ni juzi tu nilikutana na kusalimiana nae nje ya ofisi zake kwenye jengo la Mwamoto.

Pole zangu binafsi kwa familia yake ya karibu na mbali.  Tuko nao katika wakati huu mgumu kwao.
Chini hapa ni baadhi ya picha nilizopata kumpiga Daud Mwangosi katika uhai wake.
Maggid Mjengwa,
Iringa

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment