Monday 3 September 2012

Re: [wanabidii] Majibu ya Samwel Sitta Kuhusu Tuhuma alizozushiwa na Dr Slaa

Hakuna hata mara moja CHADEMA imeua au kumwaga damu isiyo na hatia
wala damu yeny hatia,ni kutotaka kufikiri kutaka kuaminisha Dunia kuwa
eti Operesheni za CHADEMA zinasababisha vurugu
Hili la vurugu lipo wazi ni polisi ndio wanaoua Raia,polisi ndio
wanamwaga damu,nguvu kubwa inayotumiwa kupambana na CHADEMA,ingetumiwa
kupambana na ujambazi nchi hii isingekuwa na jambazi hata mmoja,polisi
hawataki kushirikisha akili zao katika maamuzi,wanatii amri za
watawala wasiotaka mabadiliko,wanafikiri wingi wa Silaha utazuia
mabadiliko,wanafikri kuua viongozi wote wa CHADEMA kutazuia
mabadiliko,kimsingi mabadiliko haya hayazuiliki,mabadiliko ya
kiuchumi,kisiasa,na kijamii,wakati umefika na hakuna atakayezuia
mabadiliko

On 9/4/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
> Ndugu Felix nimekwishakushauri kupima hoja zako na kuangalia wengi
> wanasemaje acha kuprolytise uCCM. Unawatiaje hatiani Chedema kabla ya
> kuwalaani polisi?
> Inaoneka polisi sasa wamegeuka majambazi ya kuua watu kwa maslahi ya
> wachache na
>
> 2012/9/4 Nickson ngajilo <nngajilo@yahoo.com>
>
>> Matanda
>>
>> Wewe kweli ni mtanzania
>> Nini kazi ya polisi?
>> Nakujibia:kulinda amani
>> Nani alivuuga amani ya nyororo jibu POLISI wa kikwete.
>> Siasa ni haki ya kila mtanzania.
>> ukisema chadema ni inaleta fujo unapotoka sana.
>>
>> kikwete na mwema lazima wajue kuwa wamepewa dhamana ya kulinda amani ya
>> nchi na watanzania kwa ujumla
>>
>>
>> --- On *Mon, 9/3/12, cngaswaga@yahoo.com <cngaswaga@yahoo.com>* wrote:
>>
>>
>> From: cngaswaga@yahoo.com <cngaswaga@yahoo.com>
>>
>> Subject: Re: [wanabidii] Majibu ya Samwel Sitta Kuhusu Tuhuma
>> alizozushiwa
>> na Dr Slaa
>> To: wanabidii@googlegroups.com
>> Date: Monday, September 3, 2012, 6:01 AM
>>
>>
>> Dr Slaa alipoleta hoja ya epa , alikuwa ni mheshimiwa Sitta aliyesema
>> kuwa
>> ushahidi wa Dr ni wa hovyo hovyo eti wa internet ambao mtu yeyote anaweza
>> kutengeneza , pia alitishia kumpeleka Dr kwenye kamati ya maadili.Hivyo
>> jamani ansadi si zipo?kwa nini zisitolewe tu ile watu wamwelewe sitta
>> halisi..mzee wa opportunities.Ni Sitta pia aliyefunga mjadala wa Richmond
>> kibabe bungeni.Mheshimiwa hatujasahau...wewe sio mkweli ni mtu wa
>> kuangalia
>> maslahi.Ni wewe pia uliyesupport wabunge kulipwa zaidi kwa hoja dhaifu
>> kuwa
>> tuwe kama wenzetu wa nchi jirani..ni kweli hata ukatibu kata usingefaa.
>> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom
>> ------------------------------
>> *From: * denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
>> *Sender: * wanabidii@googlegroups.com
>> *Date: *Mon, 3 Sep 2012 15:50:53 +0300
>> *To: *<wanabidii@googlegroups.com>
>> *ReplyTo: * wanabidii@googlegroups.com
>> *Subject: *Re: [wanabidii] Majibu ya Samwel Sitta Kuhusu Tuhuma
>> alizozushiwa na Dr Slaa
>>
>> Kaka Mwakyembe umepotoka kabisa. Hamna justification yoyote ya kufanya
>> hiki kilichotokea! HAMNA...................
>>
>> 2012/9/3 Felix Mwakyembe
>> <fkyembe@gmail.com<http://mc/compose?to=fkyembe@gmail.com>
>> >
>>
>> CHADEMA pokeeni na upande wa pili wa shilingi yenu, msipende kusifiwa tu
>> mtashindwa kujitathmini.
>>
>> Leo kelele za ufisadi zimelekezwa CCM lakini katika Bunge lililopita
>> tumeshuhudia baadhi ya wabunge wa CHADEMA wakitajwa kwenye ufisadi kwenye
>> sakata la TANESCO, kwa hiyo hamjawa malaika nanyi ni binadamu wa kawaida,
>> kuna mapungufu mengi tu.
>>
>> Leo kwenye hiyo M4C, zinatokea vurugu, sijasikia kiongozi wa CDM
>> akikamatwa or kuawa, bali ni wananchi wasio na hatia, tena wasiohusika,
>> nanyi mnaendelea pasipo kuijihoji kuhusu movement yenu na maisha ya
>> wananchi wasio na hatia yanayopotea.
>>
>> Hata kama ni polisi ndio wenye kuua, lkn chanzo ni M4C!!
>>
>>
>> Kubalini kukosolewa mtafika mnakotaka kwenda,sifa ndizo zilizoifikisha
>> CCM
>> hapo ICU ilipo.
>>
>> Ni mtazamo tu!
>>
>> Felix
>>
>>
>> 2012/9/3 mngonge
>> <mngonge@gmail.com<http://mc/compose?to=mngonge@gmail.com>
>> >
>>
>> Mzee Sitta tumekupata vilivyo kwanza nikushukuru kwa kujitokeza
>> waziwazi kutoa maoni yako hadharani. Nakubaliana na wewe mambo kadhaa
>> lakini pia natofautiana na wewe kama nitakavyoeleza hapo chini. Mambo
>> hayo ni pale unaposisitiza kwamba Chadema wanayo safu nyembamba ya
>> uongozi na kwamba hawana uwezo wa kubuni mikakati ya kuinua uchumi,
>> hivyo wasikabidhiwe nchi. Ninasema maoni yako ni ya juu juu tu
>> ukichambua mambo hayo kwa undani hadithi inakuwa kinyume kwa sababu
>> zifuatazo:
>> 1. Safu ya uongozi nyembamba- Ni kweli ukiangalia safu ya uongozi wa
>> Chadema haina watu wengi wenye CVs (vyeti) zinazotisha, wengi ni watu
>> wa kawaida sana. Na hilo ndo linaifanya Chadema kukubalika kwa watu,
>> ebu mzee jikumbushe kilichotokea katika chaguzi ndogo za ubunge huko
>> Igunga na Arumeru . Hao viongozi waliopo CCM wenye CVs kubwa
>> kimaandishi ndio hao waliotufikisha tulipo, mzee Sitta usifikiri
>> wananchi hawako objective, wanaelewa wanachokitaka na ata
>> wanachikifanya. Viongozi wenye CVs ni watu wanaoishi dunia nyingine
>> tofauti na ya wapiga kura. Naomba nimuelimishe Mzee Sitta kwamba
>> watanzania wengi wenye CVs ni woga wa kujiunga na siasa wazi wazi kwa
>> vile mfumo uliopo unaonyesha kwamba mtu akijiunga na opposition
>> parties kuna favours na mambo kadha wa kadha atayakosa na ata
>> kufukuzwa kazi au kunyimwa fursa za kibiashara. Hivyo wanabaki kuwa
>> neutral au kujiunga na CCM si kwa mapenzi yao bali kuweza kufanikisha
>> malengo yao kiuchumi pengine ata mzee Sitta yuko kundi hilo.
>>
>> Mzee Sitta naomba ukumbuke kwamba wataalamu wa nyanja zote wanaofanya
>> kazi serikalini si mali ya CCM. Hawa ni waajiriwa wa serikali na ata
>> kama Chadema kitakuwa madarakani bado wataendelea kuwepo kazini. Labda
>> kama kwenye sera za Chadema kuna hilo la kuvunja mikataba na
>> wafanyakazi wote hapo nitaomba kuelimishwa. Hao ndo watu
>> wanaofanyakazi zote za kuinua uchumi na maendeleo ya jamii nchini
>> kwetu siyo kwa sababu wako CCM. Kinachotakiwa ni wanasiasa wachache tu
>> wenye uzalendo na akili ya kuwatumia vizuri hao waajiriwa wa serikali.
>>
>> Sera zote zinazotumika katika wizara, idara na mashirika ya serikali
>> zimetengenezwa na wataalam ambao ni waajiriwa wa serikali wala siyo
>> CCM. CCM inachokifanya ni kusimamia tu na ata wakati mwingine
>> kukologa. Kwa vyovyote vile nchi zote zilizoendelea si kwa sababu ya
>> safu kubwa ya wanasiasa bali ni kwa sababu ya wataalamu katika nyanja
>> mbalimbali ( wachumi, wahandisi, walimu, madaktari, mafundi, wakulima
>> wakubwa nk). Kama ni utaalamu wa mambo ya siasa basi ata hao walio
>> CCM siku Chadema kikichukua madaraka wengi wao watakuwa upande wa
>> Chadema. Naomba nikutoe wasiwasi huo kwamba swala la safu ya uongozi
>> kuwa nyembamba si tatizo kama wananchi wataamua kuipa madaraka
>> Chadema.
>>
>> 2. Dr.Slaa kuwa dikteita
>> Ni kweli inawezekana Dr.Slaa kama binadamu akawa dikteita kwa hulka
>> yake lakini ata Mlm Nyerere alikuwa na kaelement ka udkiteita ili
>> mambo yaende na kwa manufaa ya taifa. Kama kiongozi atakuwa na
>> udikteita kwa manufaa ya wengi nasema huyo anatufaa. Ukitaka kumuua
>> nyani usimtazame usoni, mambo ya kumtazama mtu usoni ndiyo
>> yaliyotufikisha hapa tulipo. Kwa vile watu tumepigia kelele juu ya
>> kupunguza madaraka ya rais basi ni vyema tukaliangalia vizuri swala
>> hilo wakati wa kurekebisha katiba, ili tukimuona kiongozi an
>> udikteita usiyo kuwa na manufaa ya wengi tumuondoe madarakani.
>>
>> 3. Chadema hawana sera bali wanatembea nchi nzima kueneza chuki dhidi
>> ya serikali
>> Binafsi siamini maneno hayo kwa vile watu wanakuja wenyewe kwenye
>> mikutano ya Chadema na kusikiliza. Kama wanaeneza chuki ni vyema
>> serikali ikawapeleka mahakamani lakini kama yanayosemwa yapo hizo si
>> chuki bali ni ukweli. Siku zote ukweli unauma.
>> 4. Hawaonyeshi vyanzo vya mapato
>> Mzee Sitta hivi mtu kama wewe unahitaji kuelezwa ni vyanzo vipi vya
>> mapato tulivyonavyo Tanzania? Binafsi ninachojua ata bila ya kubuni
>> vyanzo vipya mtu akasimamia vile ambavyo tunavyo sasa maisha ya
>> mtanzania lazima yataboreka.
>> Ninaposema hivyo nina maana kwamba kila sehemu ya kazi inayosimamiwa
>> na serikali moja kwa moja wawekwe watu wenye uwezo na sifa za
>> kusimamia bila upendeleo. Bila kujali ni dini gani, kabila gani,
>> mwanachama wa chama gani nk. Bila kusahau kukomesha rushwa na hasa kwa
>> kuanza na viongozi wa juu. Kuwa na idara ya usalama wa taifa
>> itakayowezeshwa na kusimamia maslahi ya taifa vilivyo
>>
>> Nahitimisha kwa kusema kama wananchi wataona Chadema ndo chama cha
>> kuwaletea maendeleo tuheshimu uamuzi wao. CCM kama munataka kuendelea
>> kushika hatamu jitahidi kuleta maendeleo ya kweli siyo ya mdomoni.
>> Watanzania wa leo wanayo akili ya kuchambua pumba na mchele.
>> Tusiangalie maendeleo ya familia zetu tu tukahisi na wenzetu wa kima
>> cha chini wanaridhika na hali zao.
>>
>> Mchana mwema
>>
>> 2012/9/3 denis Matanda
>> <denis.matanda@gmail.com<http://mc/compose?to=denis.matanda@gmail.com>
>> >:
>> > Kuzushiwa?
>> >
>> >
>> > 2012/9/2 Pata Habari
>> > <patahabari@gmail.com<http://mc/compose?to=patahabari@gmail.com>
>> >
>> >>
>> >> Nimesikitishwa na kauli za jazba na mwangwi wa kiwewe za Mhe Dr W
>> >> Slaa alipokuwa Iringa juzi hadi kuniita mnafiki, mwongo, mtu wa hatari
>> >> n.k
>> >>
>> >> Hali hii inatia mashaka juu ya uwezo wa kiongozi huyo wa kisiasa
>> >> kuhimili kukosolewa ambayo ni sifa muhimu ya maisha ya mwanasiasa
>> >> yeyote hususani anapojinadi kuwa anaweza kuchukua madaraka ya
>> >> kuiongoza nchi.
>> >>
>> >> Kauli zisizo na staha alizozitoa Dr Slaa dhidi yangu kama vile sifai
>> >> hata uongozi wa kata zinadhihirisha mambo mawili:
>> >>
>> >> Dr Slaa ni dicteta. Hana uvumilivu. Ana hulka ya kujiskia kwamba
>> >> mawazo yake hayapingwi.
>> >> Ni mzushi asiyeogopa kusema na kupindisha mantiki ya jambo ili tu
>> >> kushinda hoja. Iweje mtu aliyenibembeleza nigombee uraisi kupitia
>> >> chama chake mwaka juzi leo aseme sifai kuongoza hata kata kwasababu tu
>> >> nimetamka ukweli juu ya udhaifu wa chama chake cha siasa?
>> >>
>> >> Niliyoyasema pale Karagwe majuzi katika uchambuzi wangu wa vyama vya
>> >> siasa nchini ni kwamba CHADEMA wamekuwa hodari wa kukosoa na
>> >> kuishambulia CCM na serikali zake lakini wanasau kuwa ili wawe mbadala
>> >> kwa kuiongoza nchi hawana budi kurutubisha safu yao ya uongozi nawe na
>> >> watu wakutosha kuweza kushika madaraka ya ngazi mbalimbali za uongozi
>> >> wa Taifa. Kuukataa ukweli kwamba safu ya uongozi wa CHADEMA ni
>> >> nyembamba ni kujidanganya tu.Kupita mikoani kutangaza kwamba matatizo
>> >> yote ya wananchi yanatokana na CCM ni kazi rahisi na ina mvuto wake
>> >> kisiasa lakini mwanasiasa makini hana budi kwenda mbele zaidi ya
>> >> hapo.
>> >> Hana budi kutuambia wapiga kura mipango ya chama chake inayoeleweka na
>> >> inayotekelezeka na iliyo makini kukabiliana na changamoto mbalimbali
>> >> za maendeleo ya nchi. Ahadi za alinacha za tiba bure, elimu bure bila
>> >> kuonyesha vyanzo halisi vya mapato ni porojo tu. Kusema kwamba
>> >> raslimali za nchi kama vile gesi asilia, madini, makaa ya mawe, utalii
>> >> zinatosha kuondoa umaskini ni nadharia tupu ambayo uhalisia wake hauna
>> >> budi kubainishwa kwa mikakati dhahiri na thabiti ya kiutawala
>> >> (uendeshaji) inayoweza kuchuma utajiri huo kwa ufanisi, kwa uendelevu
>> >> na kwa faida ya wengi1. Kuhusu mwenyekiti Mh Mbowe – MB
>> >>
>> >> Katika hotuba yangu sikukejeli uzoefu wa Mhe Mbowe, wala sijasema Mhe
>> >> Mbowe ni mcheza disko. Niliuchambua wasifu wa viongozi wa CHADEMA na
>> >> kutamka uzoefu wa Mhe Mbowe katika vitega uchumi vya burudani hii
>> >> siyo kudharau bali ni kutamka ukweli tu.Huwezi kuuelezea wasifu wa Mhe
>> >> Mbowe bila kuelezea mchango wake mkubwa katika tasnia ya
>> >> burudani.Mmoja wa maraisi maarufu wa marekani (USA)alikuwa ni mcheza
>> >> sinema Ronald Reagan.Na hapa Tanzania tulikuwa na mzee R. Kawawa
>> >> ambaye alianzia katika tasnia ya uigizaji, kwa hiyo Mhe Mbowe au Dr.W.
>> >> Slaa anaweza akawa Rais wetu kwa maana ya kupigiwa kura za uchaguzi wa
>> >> demokrasia.Kumudu au kutoyamudu madaraka hayo ni suala tofauti.
>> >> Tathmini yangu ilihusu safu nzima ya uongozi wa CHADEMA kwa ujumla
>> >> wao.Ni safu nyembamba mno.2. Kujiunga na CHADEMA
>> >>
>> >> Kama alivyosema Dr. Slaa Chadema walifanya jitihada ya kunishawishi
>> >> niingie CHADEMA 2010 na niwe mgombea wao wa Urais. Jambo hili
>> >> nililitafakari na kutafuta ushauri kwa watu wangu wa karibu na
>> >> nikabaini kwamba:-
>> >>
>> >> CHADEMA wana migawanyiko yao ya uongozi tena ni ya hatari
>> >> kwasababu ni ya kikanda za nchi – yaani nani anatoka wapi.
>> >>
>> >> Kutokana na yaliomo katika ilani yao ya uchaguzi 2010 – 2015
>> >> nilibaini mambo ya kiitikadi ambayo siyakubali kama vile sera ya
>> >> majimbo. Sera ya majimbo inawezekana katika nchi ambazo ni tajiri na
>> >> pia isiyo na tofauti kubwa ya hali ya maisha baina ya kanda mbalimbali
>> >> za nchi kama vile Marekani (USA). Kuleta majimbo Tanzania ambako kuna
>> >> tofauti kubwa za kimaendeleo baina ya Kaskazini, Mashariki, kati,
>> >> Kusini na Magharibi ni kusababisha nchi ichanike vipande vipande.
>> >>
>> >> Huduma bure za elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na huduma
>> >> bure za afya kwa wote ni ndoto na ni ghilba kwa wananchi. Isitoshe
>> >> siamini kwamba kazi ya Serikali yoyote Duniani ni kuwalea Wananchi kwa
>> >> umaskini huku ukiwaahidi huduma za bure badala ya kuwaendeleza
>> >> wajitume na waongeze kipato ili wamudu gharama za maisha. Kwa hiyo
>> >> nisingeweza kuwa mgombea Uraisi ndani ya chama ambacho itikadi zake za
>> >> msingi sikubaliani nazo.
>> >>
>> >> Baada ya hapo nisingeweza eti baada ya uchaguzi Mkuu niombe kugombea
>> >> Uspika kupitia chama cha CHADEMA.3. Kuhusu CCJ
>> >>
>> >> Kama ilivyo kawaida kwa vyama vya siasa kutafuta wagombea bora, CCJ ni
>> >> miongoni mwa vyama vilivyonifuata mimi na baadhi ya wanasiasa wakati
>> >> wa maandilizi ya uchaguzi mkuu. jambo hili si la siri wala la ajabu na
>> >> Nimelizungumza hili mara nyingi. Isitokee katika mfumo wa vyama vingi
>> >> vya siasa mtu kutoka chama kumoja cha siasa na kujiunga na chama
>> >> kingine haiwezi kusemwa kuwa ni uhaini. Na kama Ningeridhika na mambo
>> >> yao ningejiunga na CCJ mwaka 2010 lakini sikufanya hivyo. Pia ni
>> >> uzushi usio na msingi kunihusisha na uanzishaji wa chama hicho.
>> >> Waanzilishi wa chama hicho cha siasa wanajulikana na wapo hai, ni haki
>> >> ya kikatiba ya kila Mtanzania kuanzisha au kujiunga Binafsi na chama
>> >> chochote cha siasa.4. Madai mengine
>> >>
>> >> Eti nilitamka kwamba ningehamia chadema na Wabunge wa CCM 55 ni porojo
>> >> za Dr. Slaa kama ulivyo usemi ningeihama CCM siku chache kabla ya
>> >> kuvunjwa Bunge la 9.
>> >>
>> >> Inashangaza kwa Dr Slaa kukejeli uendeshaji wa bunge la 9 ambalo ndilo
>> >> lililowapa fursa watu kama yeye kujulikana na kujipatia umaarufu.
>> >>
>> >> Haya madai ya mimi nikiwa Spika kukwamisha uchunguzi wa Meremeta na
>> >> Richmond ni kutokana na hisia tu za chuki. Taratibu za Kibunge
>> >> hazimwezeshi Spika kuwa Dikteta anayeamua nini kijadiliwe na nini
>> >> kisijadiliwe. Yote yapo katika kanunu za Bunge. Maamuzi ya Bunge si
>> >> lazima yawe ni ya Spika.
>> >>
>> >> Kuhusu ofisi ya Mbunge jimboni Urambo mahasimu wangu ndani ya CCM na
>> >> nje yake wameng'ang'ania kwa makusudi maalum kuiita ofisi ile kuwa ni
>> >> ya Spika. Michoro yake na gharama zake hata ukijumuisha samani
>> >> haifikii tarakimu za ajabu wanazotaja mahasimu wangu kujenga hoja
>> >> istoshe ofisi hiyo haina maslahi yeyote binafsi kwangu Aidha viongozi
>> >> wengine waliofikia hadhi za juu mathlani ya uwaziri mkuu nao
>> >> wamejengewa majimboni ofisi zinazolingana na hiyo
>> >>
>> >> Porojo nyingine binafsi kama vile kumuhusisha mke wangu kumpigia simu
>> >> Dr Slaa kumsihi anisaidie kisiasa ni upuuzi wa aina yake
>> >> unaodhihirisha umahiri wa Dr.Slaa katika siasa za kiwango cha chini.
>> >>
>> >> 5. HITIMISHO
>> >>
>> >> Mimi nikiwa mwanasiasa mzoefu na mkongwe nimetoa ushauri na
>> >> nitaendelea kutoa ushauri kwa makundi mbalimbali nchini.Kuniambia
>> >> naingilia mambo ya CHADEMA ni kichekesho.Wakiwa wao ni chama cha siasa
>> >> kinachoendesha harakati za kuwania kuchukua madaraka ya kuongoza nchi
>> >> ambayo mimi ni raia wasitazamie kuwa sisi wapiga kura tutaacha
>> >> kuwachambua.Wanalo tatizo kubwa la safu nyembamba mno ya uongozi,
>> >> Kulingana na majukumu ya kuendesha nchi.
>> >>
>> >> Kujilinganisha na safu ya uongozi ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere
>> >> ni mzaha wako wapi akina R.M Kawawa, Pauli Bomani, George Kahama, Amir
>> >> Jamal, Solomoni Eliufoo, Tewa Saidi, Tewa Abdallah, Fundikira wa
>> >> CHADEMA? Kutembea nchi nzima kuhamasisha chuki dhidi ya serikali
>> >> iliopo madarakani ni jambo jepesi lakini Watanzania walio makini
>> >> wanahitaji maelezo ya mipango mbadala ya uchumi kuinua hali za maisha
>> >> yao na kuiona safu ya uongozi itakayowezesha kwa dhati kubuni na
>> >> kusimamia mikakati endelevu ya kuondoa umaskini kujenga uchumi imara
>> >> na kuimarisha umoja wa watanzania
>> >>
>> >> --
>> >> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> >> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> >> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>> >>
>> >> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> >> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com>
>> >> Utapata Email ya kudhibitisha
>> >> ukishatuma
>> >>
>> >> Disclaimer:
>> >> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> >> consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be
>> >> presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to
>> >> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> >>
>> >>
>> >
>> >
>> >
>> > --
>> > Wasalaam
>> >
>> > Denis Matanda,
>> > Mine Supt,
>> > Nzega - Tanzania.
>> >
>> > " Low aim, not failure, is a crime"
>> >
>> > --
>> > Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> > Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> > Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>> >
>> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com>Utapata
>> > Email ya kudhibitisha
>> > ukishatuma
>> >
>> > Disclaimer:
>> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> > consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> > must
>> be
>> > presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to
>> > this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> >
>> >
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com>
>> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com<http://mc/compose?to=wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com>Utapata
>> Email ya kudhibitisha ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>>
>>
>>
>> --
>> Wasalaam
>>
>> Denis Matanda,
>> Mine Supt,
>> Nzega - Tanzania.
>>
>> *" Low aim, not failure, is a crime"*
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>


--
Ephata Nanyaro
P.o.box 15359
Arusha
+255 754 834152
Skype.nanyaro.ephata

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment