Friday 7 September 2012

Re: [wanabidii] Kutoka Iringa : Mwandishi Francis Godwin atoweka kuhofia maisha yake

Godwin pole sana kwa ajili ya hayo.

Lakini sioni sababu ya kutoweka, kwa maana maisha yapo kwa jinsi ambavyo kifo kipo.

Unaweza kukikimbia kutoka mikononi mwa 'wasio haki' lakini ukakutana nacho kwenye mazingira magumu.

Simama katika ukweli ili hata mauti yakikukuta ndani ya ukweli, utakufa kifo chema. Usikikimbie kifo kwa mtindo huo.



--- On Thu, 9/6/12, SAID SIMON EZEKIEL <salingu@gmail.com> wrote:

From: SAID SIMON EZEKIEL <salingu@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Kutoka Iringa : Mwandishi Francis Godwin atoweka kuhofia maisha yake
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, September 6, 2012, 7:59 AM

Siku mbili baada ya kifo cha mwandishi mwenzao wa habari (Daudi
Mwangosi) aliefariki kutokana na kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa
polisi waliokuwa wanatawanya wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi
wa habari Francis Godwin ambae alikua rafiki wa marehemu
amejisalimisha polisi kufata masharti ya taarifa iliyotolewa kwa yeye
na wenzake wawili kusakwa na polisi.

Exclusive na millardayo.com namkariri Godwin akisema "kutokana na hali
halisi ya kushuhudia tukio la mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa
nyuma na gari lisilokua na namba pia nilipofika nyumbani niliambiwa
kuna watu walikuja kuniulizia lakini hawafahamiki, na taarifa zikatoka
kwamba tunasakwa"

Kuhusu kujisalimisha, Godwin amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada
ya kusikia taarifa za kusakwa kwake pamoja na waandishi wengine
wawili, jana (september 5) aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa
amesindikizwa na waandishi wa habari kama hamsini ambapo baada ya
kufika pale walikutana na kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Robert
Manumba ambae ilibidi ahoji polisi Iringa kama ni kweli wanamtafuta
Godwin na wenzake.

Namkariri Godwin akisema "baada ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa
wake kama ni kweli wanamtafuta Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae
akasema hatumtafuti, baada ya hapo waandishi wa habari tulisimama
tukaondoka kwa sababu ya kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu
taarifa ya uchunguzi ya Manumba"
Kingine kilichoendelea baada ya hapo ni Club ya waandishi wa habari
Iringa kuziomba redio mbalimbali za iringa ambazo zimekua zikirusha
matangazo ya polisi jamii kusimamisha matangazo hayo ambapo wamiliki
wa vyombo hivyo wamekubali ombi.

Francis Godwin ambae alikua karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda
mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu amesema "Nilijua kwamba mimi ni
miongoni mwa waandishi watatu wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla
ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka kwenda kumuokoa pale lakini
nilipokua namsogelea Daudi akaniambia Godwin mdogo wangu kimbia…
wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma nageuka nasikia mlipuko
mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na nilibahatika kupiga baadhi ya
picha ambapo askari waliokuwepo walipoona narudi kwenye eneo hilo
walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono juu kwamba jamani mimi
nakuja kwa heri wakaniambia potea"

Godwin amesema baada ya kugeuka na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia
ila bahati nzuri gari yake ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi
walipokwenda hospitali ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze
kutoa mabango ya wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na
kutoa namba za gari, alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari
zilikua zinamfukuzia kwa nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa
Iringa na kuingia mitaani ndio akafanikiwa kukimbia.

Kwenye sentensi ya mwisho Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja
ambae alimwambia kuhusu kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari
awengine mbapo alimuonya kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa
pamoja na ushahidi wa tukio la mauaji ndio vimefanya atafutwe.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment