Sunday 2 September 2012

Re: [wanabidii] BARUA YA WAZI KWA RAIS WA DOLA YA ZANZIBAR DR. ALI MUHAMMED SHEIN

Dear Nd. Mngonge,
Japokuwa sisi wengine ni Wapagani lakini huwezi kuitenganisha au kuitofautisha dini ya kiislamu na siasa.
Dini ya kiislamu na siasa ni kitu kimoja. Labda kwanza tujiulize nini siasa? Siasa sio kutukanana, kuoneana wivu au kuoneshana bastola.
Simply tunasema siasa ni those activities associated with the governance or running of a country. Islam does encompass a set of beliefs or principles on how to run a country, though these are very tough. 
Kwahivyo, usistaajabu Waislamu wanapochanganya siasa na dini, kwasababu huo ndio uislamu na hii ndio maana tunazo Islamic States.
Pia, ndio maana hapa ukumbini wengine walikuwa wakipiga kelele kuwa hawa ndugu zetu wanataka kuigeuza nchi yetu kuwa an Islamic State. Sasa watawezaje kufanya hivyo ikiwa siasa na dini yao ni vitu viwili tofauti? 
Kwahivyo, Kaka  Mngonge, advice yako kwa Shk Farid  kuwa ajitahidi kutofautisha siasa na mambo ya Mwenzi Mungu haina mashiko!
Kila la kheri / Nkumba.
 
From: mngonge <mngonge@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, September 2, 2012 4:42:14 AM
Subject: Re: [wanabidii] BARUA YA WAZI KWA RAIS WA DOLA YA ZANZIBAR DR. ALI MUHAMMED SHEIN

Amir mkuu Farid Hadi Ahmed, tafadhali jitahidi kutofautisha siasa na
mambo ya Mwenyezi Mungu, inaelekea munataka kuufanya uislamu kuwa
chama cha siasa cha kuikomboa Zanzibar toka utumwani wa serikali ya
Tanzania. Naomba nitofautiane na wewe na kama nitakosea naomba
kusahihishwa. Nijuavyo mimi Zanzbar haikupata uhuru kwa sababu ya
Uislam bali ni kwa mapigano yaliyotokana na msukumo wa kisiasa, sina
uhakika kama wote waliohusika kuleta mapinduzi walikuwa waislamu. Pia
sina uhakika ni asilimia ngapi ya wazanzbar wanaokuunga mkono juu ya
hoja hiyo. Ni vyema ukawa na takwimu hizo tofauti na hapo inawezekana
nyinyi ni kundi dogo sana na munalolitaka nyinyi ndo lilazimishwe kwa
wazanzbar wote. Bado tume ya kukusanya maoni ya kurekebisha katiba
inaendelea na kazi hiyo hivyo wasiliana nao juu ya hoja zenu, wazipime
na ikibidi ziingizwe kwenye katiba ijayo

2012/9/1 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>:
> BARUA YA WAZI KWA RAIS WA DOLA YA ZANZIBAR DR. ALI MUHAMMED SHEIN
>
> BISMILLAHI 'RRAHMANI 'RRAHIM
>
> Kila sifa njema zinamstahikia Allah, Subhanah wa Taala, isofichika
> kwake dhulma wala harudishi dua ya mwenye kudhulumiwa. Rehma na amani
> zimshukie Mtume Muhmmad (s.a.w) kipenzi chake na cha umma, mtetezi wa
> waliodhulimiwa hata kabla ya kupewa Utume.
>
> Mhishimiwa Rais,
>
> Kwa mapenzi makubwa, baada ya kuisoma kwa utulivu khutuba yako ya siku
> tukufu ya Iddil Alfitri, nimelazimika kuandika barua hii kufuatana na
> kauli mbiu ya Mtume Muhammad (s.a.w) inayosema:
>
> "…Dini ni nasaha…nasaha kwa Allah (S.w.T) na ni nasaha kwa Mtume
> (s.a.w.) na kwa viongozi wa Waislamu na kwa watu wote…"
>
> Mh. Rais;
> Ni kweli nchi yeti ya Zanzibar imechafuliwa jina lake kuwa ni nchi ya
> amani kama ilivyogeuzwa nchi yetu na ndugu zetu na kufanywa kuwa ni
> koloni lao baada ya mkoloni Mwingereza kutupa uhuru mwaka 1963 na kuwa
> na kiti chetu Umoja wa Mataifa huku walimwengu wote wakishuhudia; kiti
> ambacho kwa uwezo wake Allah atakirejesha karibuni na wewe ukiwa rais
> wa Zanzibar au uliyemwakilisha kuweza kuketi juu yake Insha'allah na
> sisi wananchi wako wa Zanzibar tukifurahikia jambo hilo adhimu.
>
> Mh.Rais;
> Ni kweli nchi yetu inatiwa dosari lakini si kweli kuwa wananchi wa
> Zanzibar ndio wanaosababisha dosari hiyo na doa hilo la uvunjifu wa
> amani; ushahidi wa maneno haya tutaupata tukirejea na kutizama kwa
> jicho la uadilifu na insafu katika matukio tafauti. Kwa hakika
> tukifanya hivyo tutagundua bila ya taabu kuwa Jeshi la Polisi la
> Tanzania ndio wahusika wakuu na waanzilishi wa vurugu na uvunjifu wa
> amani ya nchi yetu ya Zanzibar kwa mara zote tatu, nikimaanisha
> machafuko yaliyotokea tarehe 25-26/5/2012 mjini Zanzibar na yale ya
> kuhujumu waumini na kunajisi misiskiti tarehe 17/6/2012, Donge,
> Mahonda na Mkokotoni pamoja na hujuma ya tarehe 20/7/2012 msikitini
> pia dhidi ya Waislamu walokusanyika msikiti wa Mbuyuni kuwasalia ndugu
> zao waliofariki kwa ajali ya meli ya Mv. Skaget. Waislamu tulihujumiwa
> ndani ya msikiti. Jeshi la polisi halikusita hapo bali liliwaingilia
> wananchi wanyonge mpaka ndani ya nyumba zao na kuwatendea matendo
> haramiya ya chuki na uhuni na katika waliotendewa matendo hayo maovu
> walikuwa wanawake na watoto wachanga. Polisi hao wakhalifu wa sharia
> waharibifu wa amani walifika hadi ya kutupa mabomu ya madawa makali
> ndani ya majumba ya raia bila ya kujali athari zitakazowasibu watoto
> wachanga na wanawake wenye kunyonyesha. Iwapo jeshi la polisi
> lililopewa jukumu la kulinda sharia, kuweka amani na kuwahami wananchi
> na mali zao ndio wenye kuvunja shariakwa kuwahujumu watu bila ya
> sababu, wananchi na haki zao zitalindwa na nani?
>
> Mh.Rais;
> Matokeo ya ukiukwaji wa sharia na haki za binadamu yaliyopelekea
> kuiharibia nchi yetu ya Zanzibar sifa yake ya amani na utulivu
> yamesababishwa na jeshi la polisi la Tanzania lililoacha kutekeleza
> wajibu wake wa kutunza amani ya nchi yetu Zanzibar . La kusikitisha
> zaidi ni kuwepo baadhi ya watendaji wako wa karibu wanaopotosha ukweli
> na kuifanyia khiyana nchi yetu ya Zanzibar kwa kufikisha kwako taarifa
> za uongo zilizopelekea kuitia doa na kuiharibu khutuba yako ilojaa
> maneno matukufu ya Allah Subhanah wa Taala pamoja na mafunzo kutoka
> Sunna za Mtume (s.a.w), khutuba ambayo ilitarajiwa kukemea dhulma za
> jeshi la polisi dhidi ya Waiislam na nyumba tukufu za Allah (S.w.T)
> iliyohujumiwa pamoja na wanawake na watoto wachanga ndani ya majumba
> kama ulivotetea makanisa na kubainisha hatari na ubaya wa walioyachoma
> makanisa hayo kwa lengo la kutaka kuanzisha fitna baina ya Waislam na
> jirani zao Wakristo waliokaribishwa nchini Zanzibar na kuishi pamoja
> nao miaka mingi kwa amani kiasi ambacho haijawahi kutokea Muislamu
> kulitusi kanisa licha kulichoma moto, kwani hayo ni kinyume na mafunzo
> ya dini yetu tukufu ya Kiislamu.
>
> Mh.Rais;
> Watu wanaokuwa karibu na Rais ni watu muhimu sana katika kufanikisha
> dhana ya uadilifu na utawala bora na wa haki usioogopa kukemea maovu
> hata kama walotenda au kuteleza ni Jeshi la Polisi kwani pia wao ni
> binaadamu siajabu kutenda makosa kwa maksudi seuze kuteleza, Allah
> Sbhanah wa Taala anatwambia: "…Enyi mloamini kuweni wasimamizi wa
> Allah wenye kushuhudia ukweli hata kama ni dhidi ya nafsi zenu…" Kwa
> hivyo, kosa kubwa zaidi ni kuuficha ukweli au kumpotosha kiongozi wa
> nchi hadi kufikia kuwashushia sifa wasiostahiki, wahuni ambao
> waliwatendea ya uhuni na dhulma kubwa hata wanawake na watoto. Ni
> khatari wadhulumiwa wanapofikishwa kumshtakia Mfalme wa Mbingu na
> Ardhi juu ya dhulma wanazotendewa. Isitoshe, khiyana ya watu kamaa hao
> wa karibu na viongozi kila inapojikariri khiyana hiyo inajenga hisiya
> kwa wenyeji wa nchi hii ambao wengi wao ni Waislamu kuwa wanabaguliwa,
> na sio wao tu bali hata kudharauliwa nyumba zao tukufu za ibada na
> kuthaminiwa makanisa peke yake. Sisi Waislamu hatutaki nyumba zozote
> za ibada zidharauliwe. Nyumba zote za ibada lazima ziwekewe hishima
> zinazostahiki.
>
> Mh.Rais;
> Kwa heshma zote naomba zichunguzwe sana sifa mbili kwa watu wote wa
> karibu na viongozi, sifa mbazo ni hatari kuzikosa tena zinaweza
> kuiangamiza nchi yetu tukufu ya Zanzibar . Sifa hizo si nyengine illa
> ni ukweli na uaminifu ambazo ni kinyume na uwongo na khiyana.
>
> Yarabbi Muumba Mbingu na Ardhi, usieshindwa na jambo, tunakuomba
> muhifadhi Rais wetu, turejeshee nchi yetu kwa salama na amani, DOLA
> HURU YA ZANZIBAR, wastiri wanawake na watoto wachanga majumbani na
> Wazanzibari wote tunaodhulumiwa kwa kudai uhuru wa nchi yetu ya
> Zanzibar uloporwa na jirani zetu, ndugu zetu baada ya kutoka kwa
> wakoloni.
>
> Amir Mkuu, Jumuiya ya Maimamu Zanzibar
> Farid Hadi Ahmed
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




0 comments:

Post a Comment