Friday 7 September 2012

Re: [wanabidii] Ansbert Na Wengine...Yahusu wanahabari kugomea kufanya kazi na polisi.

Yona,

Inakuwaje, unakataa kujadili swala lililoundiwa tume na wewe mwenyewe unajadili kwa kueleza kuwa kugoma ni kujiumiza kwasababu siku hizi kuna njia nyingi za kusambaza habari! Kama ndivyo acha waliogoma waendelee kujiumiza, si wameamua?

Tume unazosema ni njia ya kuwaziba watu midomo, tume gani zisizo na matokeo na hata kukiwapo matokeo ni ineffective! Unafurahi sana kudanganywa. Acha watu waseme maana hizo tume zako ni sawa na kutokuwa na tume. Lakini kwa namna yako ya michango, wala si ajabu kutoa mchango Kama huo.


On Thursday, September 6, 2012, Yona Maro wrote:
Kwanza hili suala limeundiwa tume na tume imeanza kazi , bora muache kwanza tume imalize kazi yake ndio hatua zaidi zichukuliwe .

Mkigoma mnajiumiza wenyewe sikuhizi kuna  njia nyingi za watu kupata habari au kuhabarishana kwahiyo njia hizo zitatumika kupeleka habari zaidi kwa watu kuliko nyie ambao mmeonekana kuangusha fani ya habari nchini kwa siku za karibuni .

2012/9/6 Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
Journalists of Tanzania UNITE, you have nothing to lose but your golden chains!! Maggid, umeambiwa kuwa mgomo una matatizo yake, lakini mwisho wa siku utapata unachotafuta. Huu si mgomo wa kudumu, ni wa muda tu! Jiunge na wenzio ili kieleweke.

Mara ngapi watu wamevamiwa na kwenda polisi au kupiga simu bila kupata msaada?? Hapa tulipofikia, polisi hawatusaidii, hawana maana; kwa hivyo usipoandika habari zao kwa muda, wala hakuna jamii itakayoathirika!! LKK
 



From: mngonge <mngonge@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, September 6, 2012 11:25 AM
Subject: Re: [wanabidii] Ansbert Na Wengine...Yahusu wanahabari kugomea kufanya kazi na polisi.

Kama ni kuripoti uovu watakaoendelea kuufanya kwa umma nafikiri hilo
wanahabari wataliandika na kulitangaza kwa sababu litakuwa linagusa
jamii nyingine pia. Lakini kama ni mambo mengine ukienda kuwauliuliza
nenda wewe yakupate ya marehemu Mwangosi

2012/9/6 maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>:
> Ansbert na wengine,
>
>
>
> Ahsanteni kwa mitazamo yenu. Katika hili yawezekana tukawa na mitazamo
> tofauti, ni hali ya kibinadamu. Kwangu mimi, kwa wanahabari huu si wakati wa
> kutangaza mgomo wa kuripoti habari za kipolisi, kinyume chake, ni wakati wa
> kushambulia kwa pamoja kwa kuwakabili polisi na wahusika wengine kwa maswali
> yenye kuhitaji majibu.
>
> Huu ni wakati wa jeshi la  wanahabari  kuishambualia polisi kama taasisi
> muhimu ya dola ili ipate majibu ya maswali ambayo jamii inataka majibu yake.
> Mbali ya  tukio la mauaji ya mwandishi mwenzetu Daud Mwangosi, hatuwezi
> kuacha kufanya kazi na polisi kupata majibu ya matukio mengine ya kihalifu
> yanayotokea katika jamii kwa vile tu tuna mgogoro na polisi.
>
> Naamini, tofauti na kugoma, kuna njia nyingine za kuishinikiza Serikali na
> hata taasisi ya polisi kuchukua hatua katika yanayotokea. Na moja ya njia
> hiyo ni kila linapotokea tukio, kwa  wanahabari kwa uwingi wetu,  ' kuvamia'
> ofisi za wenye kuhusika na kutoa majibu ya maswali ambayo jamii inataka
> majibu yake.
>
> Msimamo wangu huu unaeleweka hata na baadhi ya viongozi wa juu wa Iringa
> Press Club ambao nina ushirikiano nao mzuri.  Na jema katika hili  ni kuwa,
> ushauri wangu wa namna ya kwenda mbele umepokelewa vema na Makamu Mwenyekiti
> ( Francis Godwin) na Katibu  Mkuu wa IPC ( Frank Leonard) ambao kimsingi
> nimefanya mazungumzo nao  na  wanaufanyia kazi ushauri wangu.
>
> Vinginevyo, naelewa hasira na jazba tuliyo nayo  wanahabari wengi kutokana
> na  kilichotokea. Hata hivyo, hata katika hali kama hii, tuwe na ujasiri wa
> kumeza vipande vya barafu. Tutangulize hekima na busara. Ndio, tutulie na
> kupanga mikakati ya pamoja itakayohakikisha jamii tunayoitumikia hainyimwi
> haki yake ya kimsingi ya kupata habari ikiwamo habari za kipolisi. Na hata
> katika hili, jamii ina mengi inayoyahoji kupitia wanahabari. Wenye
> kuhitajika kuhojiwa ndio hao tunaofikiria kuwagomea. Naam, tuna lazima ya
> kuwahoji wahusika. Ni kazi yetu.
>
> Ndio, mikakati hiyo ituhakikishie wenye kuhusika na  kutoa majibu ya unyama
> uliomtokea mwanahabari mwenzetu hawapati muda wa kupumua. Hii ni pamoja na
> sisi tulio mstari wa mbele kuhakikisha kila kukicha wahusika wanatukuta nje
> ya  milango ya ofisi zao tukisubiri majibu ya maswali ambayo jamii
> inayauliza.
>
>
> Kwamba matukio kama ya mauaji ya Daud Mwangosi kamwe yasiwe ni ' Upepo tu
> unaopita'- Kwa wanahabari kugomea kuwakabili polisi  kwa maswali ni  namna
> moja au nyingine ya kutengeneza mazingira ya kuruhusu

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment