Kwa vyovyote mimi naamini kuna jambo, lililojificha au malengo maalum, vinginevyo si rahisi kwa mtu aliyemsoma na kumfatilia Nyerere, leo kusema umagufuli utadumu zaidi ya unyerere. Mi nawaona sawa tu na wale waliojaribu kusema mkapa aongezwe muda, katiba irekebishwe kwa kigezo kwamba alikuwa rais bora zaidi, kuliko hata Nyerere, na wengine wakamfananisha kikwete na rais sakozy wa ufaransa na kusema ni tumaini lililorejea! Kwa nini hawajaniaminisha kuwa magufuri tayari amefanya yanayostahili kuwa kama au zaidi ya Nyerere.
1. Sijaelewa hasa dira ya magufuri kiitikadi, sijasoma andishi lake linaloonyesha Imani na undani wa vision yake kwa nchi hii zaidi ya kumsikia akisema tz ni tajiri.
2. Muda alioitumikia nchi ktk nafasi ya urais ni Mdogo mno, kujua hasa nia na uwezo wake. Tumemuona masika tu.. Ikija kiangazi je hatabadirika??
3. Yapo mengi kuhusu matumizi mabaya ya madaraka, yameshaandikwa kumhusu, wakati akiwa waziri, sijui kesho yake hasa kipindi chake cha Pili madaraka yatakapomnogea atafanya nini!
4. Tuna uzoefu sasa watatu waliomtangulia wamekuwa wakifanya vizuri kipindi cha kwanza na kulewa madaraka kipindi cha Pili, kinachofanya wengine mseme kuwa huyu jamaa ni tofauti na mkapa ni nini!!? On May 25, 2016 09:04, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Bado Magufuli ana nafasi ya kufanya masahihisho ya makosa waliyofanya watangulizi wake. Yatakayomsaidia ni haya:
> 1) Kuna makosa yaliyofanyika na watangulizi wake.
> 2) magufuli ana akili za kuyaelewa yote.
> 3) Ana nia njema na taifa hili na anajua hawezi kuyatimiza yote anayoyawaza kulielekeza taifa hili katika kipindi cha myaka 10.
> 4) haya tunayoyajadili anayasoma na ana akili ya kujua tunasema nini. Ndiyo maana tunayasema wala hatusemi kujifurahisha.
>
> --------------------------------------------
> On Wed, 5/25/16, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] POMBE MAGUFULI: Rais wa kwanza Tanzania kurithiwa na chaguo lake?
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Wednesday, May 25, 2016, 2:19 AM
>
> JKamala,Kwa sababu naijua CCM. Ilimshinda
> Nyerere mpaka akalazimika kurudisha multiparty. I am
> essentially an optimist by nature,but not like
> this. Akina Mkapa, Kikwete, Lowassa wote walilelewa na
> Nyerere, lakini walikuwa chui waliovaa ngozi za kondoo.
> Unaposemawatu walioonekana wenye vichwa
> walilazimika kumkimbia Nyerere unamaanisha the likes of
> Kambona? What did he do to show alikuwakichwa? Si
> alifika London akabaki tu kunywa pombe. Angalia watu ambao
> Magufuli anaona ni mahiri. Makonda? Na huyu waziri
> aliyefukuzwa kazi karibuni?I am an optimist who
> has been turned around by realities on the
> ground.em
> 2016-05-24 12:11 GMT-04:00
> J L Kamala <jlkamala@gmail.com>:
> Muganda.
> Kwann unaamini wasioshabikia anachokifanya Magu
> watawashinda wale wanoshabikia? Pessimistic mbaya hiyo.
> Harafu ujue kosa kubwa alilolifanya Nyerere
> nikutokuwalea watu makini wa kimrith. Wale walioonekana
> vichwa walilazimika kumkimbia Nyerere apart from Magufuri
> anayewakumbatia na kuwalea vyema wakimsaidia kutekeleza
> dhana yake ya hapa job tu
> On May 24, 2016 6:11
> PM, "Emmanuel Muganda" <emuganda@gmail.com>
> wrote:
> Elisa,Hatujawahi kuwa na rais mzuri, makini,
> mzalendo kama Julius Nyerere. Lakini hata kabla hajaodoka
> wenzake, kuanzia Mwinyi walihakikisha Unyerere unafutwa
> nakushindwa. Ndivyo hivyo itakavyokuwa na
> Magufuli. Sidhani kila mtu ndani ya CCM anashabikia
> anachofanya mheshimiwa. Hence my conclusion kwamba
> utashindwa.Nyerere alituwekea misingi kwa miaka
> 23 lakini katika kipindi cha miaka miwili tu Mwinyi alianza
> kuifuta akaja kumalizia Mkapa. Tuombe Mungu tuwepo halafu
> tuje tupimemaneno yako na ya
> kwangu.em
> 2016-05-24 7:10 GMT-04:00
> 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
> Afadhali ungesema Umagufuli
> ''unaweza kushindwa'' kuliko kusema
> ''utashindwa'. Ninatamani tuwepo wote wakati huo
> tukumbushane. Umagufuli unaweza kuendelea mpaka rais wa tatu
> kutoka kwake. Kuna sababu nyingi: Watu walichoka na kuonewa
> na watu waliokuwa ndani ya CCM. Wakafikia kuichukua CCM. CCM
> imenusulika kwa sababu ya kusambaratika upinzani. Baada ya
> hapo CCM kumpata Magufuli akainusulu. Asipopepesuka
> ataendelea kuishi baada yake. Kingine ni hiki cha kutafuta
> watu na kuanza kuwalea. Sikumuongeza Makonda kwenye orodha
> ya wanaolelewa makusudi. Magufuli akilenga kumuweka mrithi
> na akatumia njia zinazotajwa humu, basi umagufuli utaishi
> baada yake.
>
> --------------------------------------------
>
> On Tue, 5/24/16, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
> wrote:
>
>
>
> Subject: Re: [wanabidii] POMBE MAGUFULI: Rais wa kwanza
> Tanzania kurithiwa na chaguo lake?
>
> To: "wanabidii@googlegroups.com"
> <wanabidii@googlegroups.com>
>
> Date: Tuesday, May 24, 2016, 1:20 AM
>
>
>
> Ndani ya
>
> CCM hakuna linaloweza kutabirika. Unyerere ulishindwa
>
> kuendelea, Umwinyi ulishindwa na vile vile Umkapa na
>
> Ukikwete.Hata Umagufuli utashindwa
>
> tu.em
>
> 2016-05-23 16:30 GMT-04:00
>
> 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
>
> Kumbukumbu zizizo rasmi na zilizo
>
> rasmi Tanzania zinaonyesha marais wote waliotangulia
>
> walishindwa kuwaweka watu watakaorithi nafasi zao mara
> baada
>
> yao kumaliza vipindi vyao.
>
>
>
> Mwalimu Nyerere inasemekana alishindwa kuhakikisha
> chaguo
>
> lake linapita na badala yake Ndugu Ali Hasan Mwinyi
>
> akaichukua nafasi hiyo. Inasemekana chaguo la Mwalimu
>
> alikuwa Ndugu Salim Ahmed Salim.
>
>
>
> Ndugu Ali Hasan Mwinyi angalau huyo tunafahamu hakuwa
> na
>
> chaguo. Ushawishi wake uliporomoka sana na karibu
> Mwalimu
>
> Nyerere alikuwa strongman. Hotuba zake zinazotoka kila
> mara
>
> kwenye luninga zinajieleza. Mwalimu Nyerere alifanikiwa
>
> kumpigia chepuo Ndugu Mkapa kwa hiyo Mwinyi
> hakufanikiwa
>
> kumpachika chaguo lake.
>
>
>
> Wakati wa Benjamin Mkapa kung'atuka ilionekana alikuwa
> na
>
> chaguo lake japo kwa umahili wake haikuwa rais kumjua.
>
> Lakini kuna dalili kuwa Jakaya Kikwete hakuwa chaguo
> lake.
>
> Wakati wa mkutano mkuu
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment