Saturday, 3 January 2015

[wanabidii] Re: MAONI YANGU KUHUSU TATIZO LA PANYA ROAD

Jana tarehe 02/10/2015 kulikuwa na tafrani kubwa sana katika maeneo mengi ya jiji la dar es salaam. Tafrani hii ilisababishwa na kikundi cha vijana wanaojiita panya road ambao ni genge la uhalifu linalovamia watu na kupora mali kwa kutumia silaha mbalimbali ambazo sio za moto.

Hofu ya uvamizi wa vijana hao kwa jana ilisambaa kwa kasi sana kwenye maeneo mengi ya dar. Uvamizi ulifanyika maeneo machache ila athari za hofu zilisambaa kwenye maeneo mengi na kuleta matatizo mengi.
Katika eneo ninalokaa, tabata, hofu hii ilifika kwa kasi sana na watu walianza kukimbia hovyo, maduka na bar zilifungwa na bara bara zilibaki nyeupe. Waendesha pikipiki maarufu kama boda boda walikuwa mshari wa mbele kusambaza hofu hii. Kwani walikuwa wanapita mitaani wakikimbiza piki piki na kuwaambia panya road wako karibu na wanakuja.

Kwa kweli lilikuwa ni tukio la ajabu sana hasa ukiangalia wingi, nguvu na hata silaha wanazotumia vijana hawa na jinsi hofu hii ilivyowaathiri wengi.

Najua kila mmoja sasa hivi analaani kitendo hiki, kila mmoja analaumu jeshi la polisi kwa uzembe na kila mmoja anajiuliza serikali inashindwaje kudhibiti kikundo cha vijana wanaotumia mapanga, visu, nyembe na mawe.
Wakati hayo yakiwa ya msingi kufikiria, mimi nimejifunza mambo machache kutokana na tukio hili na mambo haya nashawishika kwamba yatatufanya tuendelee kuwa masikini kwa miaka mingi ijayo.

Jambo la kwanza; Watu ni waoga sana na hofu ni mbaya mno.
Wakati tunapata taarifa hizi watu walikuwa wanakimbia hovyo, maduka na bar vinafungwa na kila mtu alikuwa na heka heka. Muda kidogo tukapata taarifa maeneo mengine kama matano hali ni hiyo hiyo. Sasa nikafikiria hawa vijana wako wangapi kiasi kwamba waweze kuteka magomeni mpaka ubungo mpaka mabibo mpaka tabata kwa wakati mmoja. Kikubwa kilichokuwa kinaendelea ni hofu.

Nilishuhudia mama mmoja anaacha gari na kukimbia kwa miguu, hapo hakuna aliyeona sura ya hao panya road bali ni taarifa tu za uwepo wao.

Hofu hii tuliyoishuhudia kwenye sakata hili la panya road ndio inatufanya tuendelee kuwa masikini. Ni hofu hii inawafanya wengi kuendelea kufanya kazi ambazo hawazipendi na haziwapatii kipato cha kutosha ila kwa hofu kwamba nikiacha kazi hii nitafanya nini wanajikuta wanakubali kuwa watumwa.

Ni hofu hii ambayo inawafanya watu kuogopa kujarimu mambo mapya, kuogopa kuzijaribu fursa mpya zilizopo mbele yao na kung'ang'ania kufanya kile walichozoea kila siku ambacho hakiwazalishii kiasi cha kutosha.
Ni hofu hii hii ambayo inatufanya tuogope kudai haki zetu hata pale zinapovunjwa wazi wazi. Tukiamini kwamba iko siku mambo yatakuwa mazuri na hatimaye maisha yetu kuwa hovyo kila siku zinavyokwenda.

Jambo la pili; Watu ni wabinafsi sana.
Katika sakata hili nilishuhudia kitu kimoja ambacho kiliniumiza sana. Kuna wamama ambao walijifungia saluni na wakati huo akaja mtoto mwenye umri kama wa miaka sita amembeba mdogo wake mgongozi. Mtoto yule akawa anawaomba wamama wale wamfungulie aingie lakini hawakudhubutu kufanya hivyo. Mtoto alibaki nje akilia kwa hofu kubwa iliyokuwa imetanda.

Kama watu wote waliokuwa wanakimbia hovyo wangeacha kujiangalia wao binafsi na wakakaa pamoja sidhani kama kikundi hiki kingeweza kuleta tafrani kubwa kiasi hiki. Kitendo cha kila mtu kujijali yeye zaidi kilitoa nafasi kubwa ya hofu kuendelea kusambaa kwa wengine.

Ubinafsi huu kama taifa unatufanya tuendelee kuwa masikini kwa kipindi kirefu kijacho. Ni ubinafsi huu unasababisha watu wachache kuwa mafisadi wakubwa. Ni ubinafsi huu unaotumika kuwagawa wanaopigania haki na hatimaye kushindwa.

Tunahitaji kupambana na matatizo haya makubwa mawili, hii inahitaji kuanzia kwa kila mwananchi mpaka kwa viongozi.
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz



On Friday, January 2, 2015 10:49:18 PM UTC+3, mchung...@gmail.com wrote:
Chanzo cha panya road kuvamia jiji nzima leo ni kwamba kuna mwanachama mwenzao aliuawa na sungusungu majuzi walipokwenda kuiba.kwa hiyo jana walipitisha michango na leo mida ya saa kumi jioni walikusanyika magomeni kagera.karibu na friends corner hotel kwa ajili ya mazishi.kwa macho yangu nilishuhudia ni kundi kubwa kama la vijana miatano wanasubiri kwenda kuzika kumbe wote hao ni panya road fikiria.kumbe kuanzia jana wamepeana taarifa jiji nzima waje wakimaliza kuzika waanze kulipa kisasi jiji nzima.ilipofika muda wa kwenda kuzika walifunga barabara na kuanza kuwapora makonda na kuelekea makaburini ktk makaburi ya kagera mikoroshini,kipindi hicho polisi walipata taarifa na wakidhani wanaenda kuzika ktk makaburini ya mburahati wakawa wanawasubiri kule kumbe sivyo.makaburini maiti ilizikwa kwa amri uku mashee wakishurutishwa na mapanga.walipotoka kuzika ikawa balaha wakarudi morogoro road nakuanza uporaji hadi polisi walipofika na kupiga mabomu, na kuanza kuwakimbiza na kufanikiwa kuwakamata wawili.lile kundi baada ya kutawanyika basi wale wanaoenda mbaghala njia nzima wanapora,wa buguruni tabata na gongolamboto nao walikuwa napora na na kundi la mwananyama ndilo lilirudi tena usiku huu na kufukuzana na polisi hadi mida hii morogoro road nyeupe hata bodaboda ni shida kuipata.uzembe mkubwa ni polisi hawakujipanga kwani walijua kila kitu nau vijana waliwaona sasa sijajua intelejisia yao imekaa vipi kukabili hawa vijana wadogo ukiwatazama umri ni miaka 14-23

On Friday, January 2, 2015 8:46:50 PM UTC+3, Yona Fares Maro wrote:
Maduka kuanzia Makumbusho , Sinza , Ubongo na maeneo ya Jirani yamefungwa kutokana na vitisho vya kukundi kinachoitwa PANYA ROAD .

Hapa ninavyoandika ujumbe huu nimeongea na IGP kasema wanashugulikia tatizo hilo , baadaye nikasoma sehemu kwamba kuna askari wengi wameonekana kwenye magari na silaha kwa ajili ya Kupambana na vijana hawa , halafu nikapata ujumbe kwamba vijana waliteka eneo moja huko mwananyamala kwa muda mrefu na muda huu wanaelekea kinondoni studio .

Ushauri wangu 
Hawa vijana wasiuwawe wala kuumizwa wanapokamatwa wanatakiwa wakamatwe wakiwa hai katika hali ya kuwaida ili waweze kuhojiwa  vizuri na baadaye mtandao wao uvunjwe vizuri kutokana na taarifa sahihi .

Kwa mfano tunatakiwa kujua kiongozi wao ni nani ? hawa vijana hawawezi kujiendeshea mapambano wenyewe lazima wana viongozi au watu wanaowaongoza , kina nani wanawapa mafunzo na silaha ndogo ndogo ? nani wanawapa taarifa na maelezo mengine kwa mfano sehemu ambazo polisi hawapo ili wavamie au wafanye vurugu ? hizi ndio taarifa tunazotaka .
Maeneo mengi duniani vijana kama hawa wanatumika na majasusi na watu wengine kutafuta sababu za kuleta machafuko na hujuma za aina nyingine dhidi ya watu au makundi wanayodhani ni pinzani dhidi yao , na moja ya jukumu kubwa la JASUSI ni kutumia fursa ya machafuko karika jamii fulani kupigania maslahi yake , tumeona hali ya NIGERIA sasa hivi , SOMALIA , Afrika ya Kati , Mali – Chanzo ni vikundi kama hivi vya PANYA ROAD .

 Tumesomesha watu wengi kwa kodi zetu kuanzia usalama wa taifa , Jeshi la Polisi na vyombo vingine hili ndio jukumu na kazi yao lazima watupe majibu ya matatizo kama haya .

Jukumu lengine la wananchi kwenye suala hili ni kuhakikisha kama wanaweza ni kuwapiga picha haswa sura zao au kukamata hawa vijana kama wanaweza wasiwaumize wapelekwe kwenye vyombo vinavyohusika ili waweze kuhojiwa na hatua nyingine zichukuliwe .

PANYA ROAD tunaishi nao mitaani , tunawaona wanavyojidai sehemu mbalimbali , kwahiyo tunaweza kuwataja au kutoa taarifa zinazoweza kusaidia kuwamaliza mitaani kwetu .

Namba za Polisi ni 0787668306 Makao Makuu , 0684111111 Mkuu wa Polisi Kinondoni 


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment