Friday, 30 January 2015

Re: [wanabidii] 'WELI SPANA ' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI

Hongera hapo kwa kutumia uhuru wako kujieleza na kueleza hisia zako .

Usikubali mtu akunyamazishe hata hata , hata babako akikosea unamwambia , unaandika , unatoa mawazo yako .

Kama tunataka kupiga hatua kwenye maendeleo na mambo mengine mbalimbali lazima tukubali mawazo ya wengi lazima tukubali maoni na chochote ambacho anaandika mwingine .

Hongera tena na tena hilo tatizo la herufi , lugha na mengine ni mambo ya kawaida watu hujifunza kila siku .

Endelea kujifunza naamini siku moja hawa wanakushambulia utawapiku na kuwaacha mbali kwa sababu hawatoi mawazo yao tuwasikie na kuwasoma kazi yao ni kushambulia watu binafsi badala ya hoja .

On Friday, January 30, 2015 at 10:11:07 AM UTC+3, Reuben Mwandumbya wrote:
Mwambapa;
Happy hajui kuna kesho,upeo wake unaishia leo.
Hapa jukwaani nina imani kuna maelfu ya wanajukwaa na wana nafasi tofauti katika kila fani hapa duniani.
Wanapata kumjua hata bila ya kumuona,hivyo hata siku ukikutana naye kama ni issue ya kutoa maamuzi juu yake unakuwa huna kazi kubwa ya kufanya.
 
Reuben


On Thursday, January 29, 2015 9:37 PM, Adam Mwambapa <adammwambapa@ymail.com> wrote:


Pengine ningempongeza mwanangu Happness Katabazi, kutokana na jinsi alivyotumia uhuru na haki yake ya Kikatiba kuongea. Hilo kwa kweli amejitahidi sana kulifanikisha.
Isipokuwa ningemwomba kama ataupata ujumbe wangu huu, na kama alimsikia vizuri sana Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Mhe. James Mbatia, ambaye alikuwa ni mtoa hoja namna alivyohitimisha kwa umahiri mkubwa sana hoja yake.

Hii ilionesha jinsi ambavyo Mbatia ni mweledi na mjuvi wa mambo. Moja ya point ambazo Mbatia alizitoa kwa wote wanaonekana kushabikia kupigwa kwa Prof. Ibrahimu Lipumba, kama afanyavyo leo Happness kushangilia na kuona ndivyo inavyopaswa iwe.

Alisema kuwa, inawapasa wote hao ambao wanashangilia na kushabikia waelewe kuwa wanashabikia na kushangilia kutokana na nafasi walizonazo sasa. Ambazo zinawawekea kinga kwa namna fulani ya kutopatwa na adha pamoja na kadhia ya namna hii. Lakini wakumbuke kuwa pindi watakapoondoka na kuwa mbali na nyadhifa zao walizonazo leo, na wao watakuwa ni raia wa kawaida ndipo watakumbana na haya wanayokumbana nayo Watanzania walioko huku.

Hivyo basi kwa pointi kama hii, nisingetegemea Happness kushabikia matukio ya uvunjifu wa amani kama haya kwa kuwa tu wanaofanya ni sehemu ya mahali alikokuwa na ajira. Je, ni kwa kuwa ndugu zake, jirani zake na watu wake wa karibu hawakukumbwa na kipigo hiki au ni sababu gani?

Pointi nyingine ni ile ya Mhe. Nasari aliyosema kuwa, askari wakumbuke kuwa wananchi ndiyo wanaoishi na wake zao, watoto zao na ndugu zao huko uraiani wakati wao wapo kazini. Sasa isingekuwa vema kuwatendea mabaya watu wengine wakati familia na watu wengine kwenye makazi yako, wapo kwenye uangalizi wa jamii hiyo hiyo ambayo wewe unaifanyia unyama na ukatili wa kutisha kiasi hicho. Je, na wao waamue kuwatendea vivyo familia na nduguzo uliowaacha nyumba? Kwa maana hiyo nchi hii hatakalika.

Happness, leo uko kwenye ajira ambayo kwa kiasi kikubwa imefanikishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Na kwa maana hiyo umekuwa ukisifia hata lisilohitaji sifa, na kutumia mwanya huo kuandika kwa nyodo na kiburi kwa kutusi upinzani. Kumbuka kuwa ajira ni dhamana tu!

Mwisho wa siku utajikuta unarudi na kujiunga na hawahawa kwenye masuala fulani ya kufanikisha shughuli zako za kikazi na zile za kijamii wakati fulani.




On Thursday, January 29, 2015 5:35 PM, "'allanlawa@yahoo.co.uk' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Am so sorry for the vulgar language Happiness has been using against MPs from the opposition particularly lately against Hon. Mbatia following the motion he moved in parliament after Prof. Lipumba was battered by police. She is an ambarrasment to Bagamoyo.UNiversity. For some of us who know the genesis of UB, Mbatia is one of those who agitated for its establishment. For Happines to disparage him is like bitting the hand which feeds her. UB, take note that your public affairs officer has disengaged from her emisary work of promoting a positive image of the college to spoilling the integrity the college had already built.


From: 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
To: WANABIDII <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: [wanabidii] 'WELI SPANA ' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI
Sent: Thu, Jan 29, 2015 2:11:52 PM


'WELI SPANA ' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI

* MBUNGE LUSINDE MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU
Na Happiness Katabazi
LEO nimepata fursa ya kutaza tena Kipindi cha Bunge kilipoanza hadi kumalizika mchana kupitia Televisheni ya Taifa TBC 1 nakuona michango mbalimbali ya maoni kuhusu Hoja ya Dharula iliyawasilisha na Mbunge wa kuteuliwa watoto wa mjini wanawaita ni wabunge wa kuteuliwa ni ' Wabunge wa Lifti', James Mbatia.

Awali ya yote na kwa moyo mkunjufu napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mbunge wa Mtera ,Livingstone Lusinde kwa mchango wake alioutoa Leo bungeni asubuhi  Kwani umejaa ukweli mchungu kwa wa wakorofi ,wazushi na wanasiasa uchwara wa vyama baadhi ya vyama Vya upinzani ambao ni wazi wamefirisika kiajenda na walikuwa wamekusudia kuigeuza Kesi inayomkabili Ya Jinai Na. 25/2015 .

Iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi wa CUF, Jana Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, Kuwa ni Gia ya kujipatia Umaarufu wa kisiasa, kutaka kufanya jaribio la kumuundia mtego mwingine Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili ang'olewe madarakani Kama walivyozoea lakini  jaribio Hilo Leo tena limekufa  kifo cha Mende mapema kabisa.

Ama kweli Ngoma ya kitoto yaani 'Ngoma ya wapinzani' ,Na kweli Ngoma ilivyoanzishwa na wapinzani Jana bungeni na Kuzusha tafrani hadi Bunge likaairishwa haijakesha ,hoja ya Mbatia aliyoianzisha kwa mbwembwe imemalizwa na Chikawe, Masaju,Lusinde, Said Mkumba ,Henri Shekifu , Sadifa Hamis Juma 'kilainiii Kama wana nawaa'

Nilimtazama na kumsikiliza Tundu Lissu na baadhi ya wabunge wenzake wa upinzani ,kwanza wakati wakachangia mada zao walikuwa wakionekana Kuwa na jazba Hali iliyosababisha kushindwa kujadili kwa vielezo kinzani taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani , Mathias Chikawe.

Hali iliyosabisha taarifa hiyo ya Chikawe ambaye ni msomi wa sheria na alishawahi kuwa Mwanasheria wa Serikali kama alivyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju ambaye naye aliwahi kuwa Mwanasheria mzuri tu wa serikali na kazi alizozifanya na kusaidia serikali kushinda kesi kubwa Si za Kutafuta, zipo wazi.

Taarifa yake kubaki Kama ilivyo kwasababu walioleta hoja ya dharula na wachangiaji wa vyama ya upinzani wameshindwa kuilarua kwa vielezo taarifa hiyo ya Chikawe ambaye Profesa Ibrahim Lipumba yeye upenda kumuita Chikawe Kuwa ni ' Cheki Bob'.

Licha Lissu ambaye alikuwa ni mchangiaji wa kwanza alifanikiwa kumtikisa Spika Makinda kuhusu suala la uchache wa muda na Makinda akatikisa na Akaamua kuufuta uamuzi wake wa awali wa kuwapatia dakika Tatu kila mbunge kuchangia,badala ya Lissu Kumtikisa ndiyo Akaamua Kusema kila mbunge atachangia dakika Kumi .

Huo ni ushindi kwa msomi Lissu ambaye ujasiri wake siyo tu ni wa kuzaliwa nao pia una changiwa na fani ya Sheria aliyosoma pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Hongera Lissu kwa ujasiri huo Kwani katika Hilo ulikumbuka Kanuni inasema je na ukainukuu.Wasomi wa Sheria tunasema ulifanya 'citation'.

Nilichojifunza kwa kwa wabunge wachache wa upinzani Leo kupitia michango Yao kwanza Wengi wao wanapenda kukuza jambo dogo lionekane kubwa, Kutenda matendo ambayo yanazidi kuporomosha heshima ya viongozi wa upinzani na upinzani kwa ujumla, uongo na unafki na kushindwa kujadili mada iliyopo mezani na kuamua kuingiza mada ambazo siyo mada iliyokuwa imepangwa kujadiliwa Leo.

Baadhi ya wabunge wa upinzani Leo waliochangia Walijikuta kujitolea Mifano Yao binafsi Kuwa wamewahi kupigwa na kubambikiwa Kesi na Polisi na kuzungumzia kifo cha Mwanahabai Daud Mwangosi.

Kwa hiyo  ni wazi hawa Tayari wanaupande(bias). Na wakasahau taarifa ya waziri Chikawe ilikuwa ikielezea tukio Moja tu la Temeke lilitokea Januari 27 Mwaka huu ,lilomuusisha Lipumba na Si vinginevyo.

Mfano mzuri Mbowe alipokuwa akichangia pamoja na Kusema alikaa muda mrefu Polisi Central Dar es Salaam, kuakikisha Lipumba anapata dhamana alitumia muda mwingi kueleza eti na yeye alishawahi kupigwa na Bomu, mashine gun na Hao Hao Polisi.

Sasa watu wenye akili timamu tunajiuliza HIvi kweli MTu upigwe na silaha zote hizo nzito yaani Bomu, Mashine Gun halafu uendelee Kuwa mzima tu?Huu sio uongo Mkuu jamani ?

Si ni Mbowe huyu huyu Bunge lilopita baada ya Bunge Hilo kutaja maazimio ya Bunge kuhusu Sakata la Escrow , Mbowe alisimama Bungeni na kumtaka waziri Mkuu Pinda azidishe Ukali maana eti Pinda amezidi Kuwa mpole ndiyo mAana mambo yanavurugika.

Haya tusaidieni Tushike la Mwenyekiti wa Chadema,Mbowe aliyemtaka Pinda awe Mkali au Tushike Mwanasheria wa Chadema, Lissu anayetaka kwa Nguvu zote Pinda aachie ngazi?

Pia Nilichojifunza wabunge wa upinzani wengine ni wasahaulifu akiwemo Lissu.Wametaka Pinda ajiuzuru kwasababu Juni 20 mwaka 2013  ,Pinda alisema ndani ya Bunge wale wote watakao kaidi sheia za nchi watapigwa  na kwamba kauli hiyo eti Ndiyo maana polisi wanaendelea kupiga watu na kwa sababu hiyo Pinda ajiuzuru.Ni aibu ya aina yake.

Kwa faida yenu Nyie wabunge wasahaulifu na msiotaka kufanya utafiti Kabla ya kuzungumza .

Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),  Chama cha Wanasheria Tanganyika, Agosti Mosi Mwaka 2013 kulifungua Kesi ya Kikatiba Na.24/2013 Katika Mahakama Kuu Kandaya Dar es Salaam, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Pinda

Juni 6 Mwaka 2014 , jopo la majaji watatu Dk.Fauz Twaibu, Augustine Mwarija na Fakhi Junfu, walitoa uamuzi wa awali wa Kesi hiyo ambapo jopo hilo lilikubaliana na pingamizi la awali lilokuwa limewasilishwa na Wakili wa wadaiwa ambaye alikuwa ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye kwa sasa ndiye Mwanasheria Mkuu wa serikali Masaju Kuwa walalamikaji walikuwa hawana haki ya kuwashitaki washitakiwa , waliokuwa wanahaki ya kumshitaki Pinda na Mwanasheria Mkuu kuhusu Kauli hiyo ya Pinda ni wanachi na siyo Taasisi hizo  (Legal Person) .

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu kuhusu Kauli hiyo ya Pinda upo na hadi sasa naandika makala hii bado Mahakama ya Rufaa haijatengua uamuzi huo hivyo bado ni uamuzi halali na Unatakiwa uwafuatwe na sisi wasomi wa Sheria tunautumia Kama 'refence'.

Sasa nashangaa sana wabunge wetu Hao wanaotaka  Pinda  ajiuzuru wakati Mahakama Kuu ilishatoa uamuzi wa Kesi hiyo na Kesi ile ilifutwa Katika Hatua za awali.

Kweli sasa nalazimika kuamini maneno ambayo yamekuwa yalisemwa na Pinda  aka ' Mchawi' ,Kuwa anaandamwa kwa uzushi na kuchafuliwa kwasababu tu ametangaza kimya kimya Kugombea urais.

Maana misioni 'connection' ya hoja ya dharula ya Mbatia hapa na wabunge wa upinzani kulazimisha Pinda, ajiuzuru.

Kupitia michango hiyo ni wazi kabisa kuna baadhi ya wanasiasa wanamchukia Pinda.Haiwasaidii na ni dhambi kumchukia binadamu mwenzako.

Jana Bungeni wabunge wa upinzani walichukua muda mwingi kuleta tafrani bungeni hadi bunge likaairishwa , tukajua leo watakuja na michango kabambe kumbe hakuna kitu ,wameshindwa kujadili taarifa ya waziri Chikawe.

Na matokeo yake mbunge mmoja wa CUf akaishia kuligeuza Bunge Hilo lisijui ni Kanisa Ka ufufuo na uzima wa kufufua marehemu waliokufa na kuanza kusoma Majina aliyedaiwa ni ya marehemu waliouwawa Unguja na Pemba.

Minajiuliza kuna ufufuo wa marehemu pale Bungeni?  Hayo Majina ya marehemu ingekuwa ni vyema angeyaleka kwenye makanisa yanayofufua wafu Kama yapo lakini siyo bungeni.

Mbunge Habib Mnyaa amesema Lipumba alishasemehe Mauji yale ya Unguja na Pemba, haya Nyie baadhi ya wabunge wa CUF Kama siyo kiherehere cha kujadili bungeni Mauji ya marehemu yake na kuyataja Majina ya marehemu wale ni kitu gani?

Ni kiherehere na Kufirisika Kiajenda .Maana Mwenyekiti wa Chama chenu cha CUF Lipumba, alishasemehe Mauji Yale, kilichowawasha kitu gani Kuja kujadili Mauji yake bungeni kitu gani?

Nafahamu nitawakera sana wale watu wanaopenda ukorofi na wasiyoaka kutii sheria bila shuruti na ambayo kutwa wamekuwa wakishitiki maandamano haramu.Mtanisamehe sana.

Leo katika makala hii namuomba sana Waziri Chikawe katika bajeti ijayo aliombee jeshi ka polisi fedha za kununulia Weel Spana nyingi sana ili zianze kutumiwa na jeshi ka polisi kuwarekebisha akili wananchi wakorofi ambao wameonekana ngozi,akili zao kuwa ngumu sana kama gari aina ya Fiati hali inayosababisha wakipigwa virungu ,virungu vinavunjika.

Weel Spana Katika zama hizi hasa kuelekea Katika wakati wa kupiga kura za maoni ya Katiba Pendekezwa Aprili 30 na uchaguzi Mkuu Mwaka huu unatarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu, Polisi wa zitumie sana Katika kurekebisha akili za wananchi wakorofi ambao wamekuwa wagumu kutii Sheria Kama shuruti na Miili Yao imekuwa ni migumu Kama Gari aina ya Fiati hivyo Weel Spana ni matumizi sahihi kabisa kwa watu waina hiyo.

Polisi msitumie tena silaha za Moto wala virungu,tumieni Weel Spana kurekebisha akili za hawa wavunja Sheria za nchi kwa makusudi Hali inayo sababisha wananchi wasiyo na hatia na mali zao kuumizwa , wananchi kuishi na wasiwasi na shughuli za uchumi kwenda kwa kusuasua kwasababu ya wapumbavu wachache wenye Malengo ya kujipatia Mtani wa kisiasa kwa kuvunja Sheria za nchini.

Mtu ambaye siyo mkorofi, na havunji Sheria ni Nadra sana kukutana na Weel Spana wala virungu Vya Polisi.

Kumbukeni hata Katiba ya Nchi inatoa haki na inamtaka aliyepewa haki hiyo ambaye ni Mwananchi kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria.

Katiba inasema kila Mwananchi anajukumu la kulinda Sheria za nchi zisivunjwe.Pia Mhimili wa serikali upo pale kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na kamwe haiwezi kumuona Mwananchi anafungwa Sheria kwa makusudi halafu imuache bila kumchukulia Hatua.

Kwa maoni yangu Matumizi ya Weel Spana kwa Jeshi la Polisi HIvi sasa ni muhimu sana ili Weel Spana ziweze kurekebisha akili za hawa wananchi ,wanasiasa wakorofi na wavunja Sheria za nchi.

Baadhi ya wapinzani  wanajifanya hawana akili wanaovunja Sheria makusudi hivyo basi Weel span zikitumiwa kwenye Miili Yao Sitasaidia sana kurekebisha akili zao zikae sawa.

Naheshimu mchango wa vyama Vya upinzani nchini ,ila nawashauri kadri siku zinavyozidi kwenda waanze Kujenga tabia ya Kuwa na subira, Kuwa wa kweli Katika baadhi ya mambo mnayo ya jadili Bunge Kwani watu wengine wanaowaaminiwa sana kila macho sema sasa inapotokea kiongozi wa upinzani  nayeye Kusema uongo watu watapoteza Imani na Nyie Kama baadhi ya wananchi walivyopoteza Imani na viongozi wa CCM na serikali.

Binafsi Lissu namheshimu sana lakini kwa kitendo alichokifanya Leo cha kusimama ndani ya Bunge na Kusema uongo Kuwa eti TBC  wamezima Matangazo Yao ili umma usiangalie kinachojadiliwa Bunge wakati sisi tulikuwa tu naendelea kutazama Bunge na kumuona yeye kupitia Televisheni jinsi anavyosema uongo wa wazi ambao umemshushia asilimia Fulani ya uaminifu  kwa wafuasi wake Leo, siyo tabia nzuri.

Lissu msomi wa Sheria ni lazima alisoma somo la Legal Research wakati akisoma shahada ya Sheria ambalo somo Hilo linamtaka msomi yoyote wa Sheria anapojadili jambo lazima awe amelifanyia utafiti.

Sasa Leo Lissu kaka yangu uliteleza kwa kwa Kusema Bila kufanya utafiti Kuwa TBC imezima matangazo yake wakati TBC hadi kufanya hivyo.

Nguvu nyingi na vitendo Vya Fedha Jana wapunge wa upinzani mlevi fanya bungeni kushinikiza Jana hoja ya Mbatia ijadiliwe lakini hao kujadiliwa ikajadiliwa Leo na Leo yenyewe Nyie mliojifanya mnauchungu wa kuijadili Wengi wenu mlitoka nje ya mada.

Matokeo yake Spika Makinda kamaliza kwa Kusema Bunge lake lina Ruhusu Kesi inayomkabili Lipumba iendelee na anamshukuru wabunge waliochangia hawajaingilia Mwenendo wa Kesi.

Hivyo Lipumba watoto wa mjini kwa hitimisho Hilo la Bunge kuhusu hoja ya Mbatia iliyokuwa ikikuhusu wewe ni kwamba ' hadithi yetu imeishaa hapo'.

Kashda ,na vibweka vyote Vya wana UKAWA wenzio bungeni vikijaribu kukunusuru wewe vimegonga mwambwa, na hivyo unaendelea kuangaika na Kesi hiyo ya jinai inayokukabili ,Mbatia na Mbowe na wabunge wengine waliokuwa wanajaribu kukusemea bungeni Jana na Leo muda Si mrefu hutawaona Jijini Dar es Salaam, watakuwa kwenye kampeni Katika majimbo yao yanafanya kampeni, hutawaona tena wakikusindikiza Katika Mahakama ya Kisutu. Hiyo inaitwa kila Mtu atabeba  msalaba wake Mwenyewe.

Nasisitiza tena Weli Spana ni kifaha muhimu sana HIvi sasa kutumiwa na Polisi  kurekebisha akili za wapinzani wakorofi na wavunja Sheria za nchi.

Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Januari 29 Mwaka 2015



Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment